Beatrice Mwimbwa Ministry

Beatrice Mwimbwa Ministry Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Beatrice Mwimbwa Ministry, Religious organisation, Mjini, Mapumulo.

05/05/2026
Hellow my odience     karibuni twendeni YouTube  nimepandisha kazi   audio ya sifa  za MUNGU  NA  video ipo tayari  nipo...
07/03/2026

Hellow my odience karibuni twendeni YouTube nimepandisha kazi audio ya sifa za MUNGU
NA video ipo tayari nipo njiani kuiachia naomba nisaidie ku share sub na kulike .

20/04/2022
05/03/2021

HOJA YA SURUALI KWA WANAWAKE - Part 2
Kwa sababu ya michango yenu mizuri katika kuijadili hoja hii naomba niongeze ufafanuzi ufuatao kuhusu suruali. Kuna aina mbili za suruali zinazotajwa katika Biblia. Aina ya kwanza ni ile inayotajwa katika Kutoka 22:05 ambayo Musa aliamriwa awafanyie makuhani inayoishia mapajani ambayo kwa Kiebrania inaitwa Miknas. Na aina ya pili ni ile waliyovaa akina Shadraki, Meshaki na Abednego ambayo kwa Kiebrania inaitwa Sarbal(Dan 3:21). Sarbal ai sirwil kwa Kiarabu au suruali kwa Kiswahili ilirithiwa na waajemi yaani Wairan wa leo kutoka kwa Wasinthia mnamo karne ya 5 kabla ya Kristo. Mwanahistoria wa Kigiriki Hirotudus anawataja Wasinthia kuwa walikuwa wakivaa suruali miaka 470KK. Sarbal ilikuwa suruali ndefu k**a zetu lakini nayo ilivaliwa k**a nguo ya ndani pia. (angalia Elicotts Comentary for English readers, na Cambridge bible for schools and colleges - Dan 3:21). Katika Biblia yote Sarbal inaonekana kuvaliwa tu na akina Shadraki, Meshaki na Abednego, na wao ni kwa sababu wakati huo walikuwa uhamishoni Babeli. Suruali ya Musa (Miknas) iliyokuwa inaishia mapajani ilitumika k**a nguo ya ndani (underwear) na siyo k**a vazi kuu. Hivyo naomba kusema yafuatayo:
1. k**a tunamzuia mwanamke kuvaa suruali kwa msingi wa Torati ya Musa (kitu ambacho siyo sahihi), basi tumzuie tukijua suruali aliyoikusudia Musa ni ile inayoishia mapajani iliyotumika k**a nguo ya ndani (boxer), maana Musa mwenyewe mpaka anaondoka duniani hakuwahi kuiona suruali k**a tunavyoifahamu leo.
2. Mwanamke azuiliwe kuvaa suruali k**a katika jamii husika vazi hilo linachukuliwa k**a vazi la watu wasiojiheshimu. Hapo kuvaa suruali kutazuia injili. Lakini jamii yetu imezoea kuwaona askari wa k**e wakiwa wamevaa suruali.
3. Mwanamke azuiliwe kuvaa suruali k**a wapendwa wanakwazika;
Kwa hiyo, chakula kikimkwaza ndugu yangu, hakika sitakula nyama hata milele, nisije nikamkwaza ndugu yangu (1Kor 8:13).
Lakini tuache unafiki katika kukwazika, maana mzungu wa k**e akiingia na suruali hatukwaziki. Mkuu wa wilaya, au mbunge, au waziri wa k**e akiingia na suruali hasa kwenye harambee hatukwaziki, lakini akiingia mswahili wa k**e na suruali, hasa asiye na hela ndio mistari yote ya Biblia inakumbukwa!
4. Bunge letu lina dress code yake, hali kadhalika na vyuo mbali mbali. Hivyo sioni ubaya kwa kanisa kuwa na dress code yao. Kanisa letu pia lina dress code lakini inawahusu watumishi tu wakati wa ibada tu. Tulifanya hivyo ili dress code isizuie injili.

Address

Mjini
Mapumulo

Telephone

+255713807171

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Beatrice Mwimbwa Ministry posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share