01/06/2022
THIBITISHA UPENDO WAKO KWA KUVUNA NAFSI
Yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho (2 Wakorintho 5:19).
Wajibu wetu wa kiinjilisti ni jambo ambalo mbingu yote inalichukulia kwa uzito. Cha kusikitisha, wengi hawaelewi jinsi hili lilivyo na uzito. Kuna Wakristo ambao bado wanauliza ikiwa mtu ambaye havuni nafsi ataenda mbinguni au la. Swali la kuuliza watu k**a hao ni, “Ikiwa mtu hampendi Mungu, au kumpenda Yesu, je, mtu huyo ataenda mbinguni?” Hilo haliwezi kutokea. Biblia inasema, “…Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye” (1 Yohana 5:1). Ikiwa unampenda Baba, lazima umpende Yesu. 1 Wakorintho 16:22 inasema, “Mtu awaye yote asiyempenda Bwana, na awe amelaaniwa. Maranatha.” Maana yake, na alaaniwe. Uthibitisho wa upendo wako kwa Yesu ni kushika amri Zake—Neno Lake (Yohana 14:15). Neno Lake linasema, “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe” (Marko 16:15). Kwa hiyo unashika neno hilo kwa kuwa mvunaji nafsi. Mtu anaweza kuuliza, “Vipi kuhusu wale walioishi kabla ya Yesu kuja na hawakuwa na nafasi kabisa ya kuonyesha upendo wao Kwake?” Walikuwa na Neno la Mungu— sheria na amri Zake. Ayubu alisema, “…Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu” (Ayubu 23:12).
Yesu ni Neno (Yohana 1:14). Haleluya! Hivyo, kila mmoja wao alikuwa na nafasi ya wazi ya kuonyesha upendo wake Kwake. Alisema katika Mathayo 28:19; “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi…” Hiyo ina maana kuwafanya wale walio katika ulimwengu wako kuwa wanafunzi; wafundishe juu ya Mungu na maisha ya Ufalme; atausimamisha Ufalme Wake katika nchi.
Upendo wako na kujitolea kwako kwa Bwana lazima kuakisi kujitoa kwako kuihubiri Injili.