Efatha Church-Zanzibar

Efatha Church-Zanzibar The Official Efatha Church-Zanzibar page
YouTube: www.youtube.com/efathachurchzanzibar

Isaya 59:1-2" Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; l...
16/06/2023

Isaya 59:1-2" Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarakanisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia."

Rehema inakurudisha vigezo vya wewe kumwangalia Mungu. Uovu ukiwa ndani yako hata k**a upako ni mwingi hakuna kitakachotokea. Kazi kubwa ya uovu ni kuleta mafarakano na Mungu. Unapoinua mikono yako juu ni ishara ya kujifunia mbele za Mungu, anaona damu yako. Damu yako inanena mbele zake –nayo imefarakana naye, haipatani naye – kwa sababu ya uovu.

Kazi za uovu;1. Unakufarakanisha na kuweka uadui na Mungu 2. Kukuondoa mbele za Mungu na kukuweka mbali Yeye.
Damu yako ikikombolewa mafarakano na mali za Mungu yanakoma.

Yohana 15:2 – Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha ili lizidi kuzaa. Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. Kuhani anaweza kutamka neno juu yako – Neno la utakaso – na likatimia.

MAOMBI;
1. Amekuja na hati ya nyongeza – mambo yanahusiana na uhai na mapato; Isaya 38:1
2. Wito wa kuinua vipawa, amaekuja kuinua vipawa.
3. Amekuja kutuambia songeni mbele. Upo karibu na hatma yako, upo karibu na ndoto yako upo karibu songa mbele.
4. Bwana anakwenda kurejesha watu wake na kuwaweka kwenye mikono yenu. Yeye atawaleta. Mungu anakwenda kuleta wenye dhambi. Mungu anakwenda kuwarejesha waliokimbia
Unaenda kuwa na kibali. Kabla ya December vitu vinakwenda kutokea.

SEMINA MAALUMU YA MAANDALIZI YA MKUTANO WA MWEZI WA NANE 2023
MCHUNGAJI HERRY NELSON -ZANZIBAR

Matukio mbalimbali pichani;katika Ibada ya Semina MAALUMU ya Maandalizi ya mkutano wa mwezi wa Nane 2023      KANISA LA ...
16/06/2023

Matukio mbalimbali pichani;katika Ibada ya Semina MAALUMU ya Maandalizi ya mkutano wa mwezi wa Nane 2023

KANISA LA EFATHA SAYUNI-MOSHI KDC

IBADA YA JUMAPILI YA TAREHE 28/5/2023 – KANISA LA EFATHA MWENGE DAR ES SALAAM TANZANIA.Mungu hutazama tamanio la watu wa...
29/05/2023

IBADA YA JUMAPILI YA TAREHE 28/5/2023 – KANISA LA EFATHA MWENGE DAR ES SALAAM TANZANIA.

Mungu hutazama tamanio la watu wake na kulifuata, k**a Biblia isemavyo, “Mungu akamwambia Ibrahimu nenda mbele yangu ukae mkamilifu” Hivyo Mungu hufuata watu wake, haenda mbele yao bali huenda nyuma yao ili kuangalia wanaenenda vipi.

Yohana 4:6-24 “…… Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu k**a hao wamwabudu. Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.” Biblia inasema waabuduo wataabudu katika roho na sio mahali fulani, hivyo waabuduo wanapokusanyika kunakuwa na uwepo wa Mungu hapo wanapokusanyika.

Waabuduo halisi Mungu anawatafuta ili waje kumwabudu, hao waabuduo halisi hawapo kanisani tu bali wapo kule na kule na Mungu anawatafuta ili wapate kumwabudu Yeye. Na ndio maana anasema “Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli”
Tunapaswa tufahamu Mungu amefanya nini, Biblia inasema

“Mungu ametuumba sisi ndani yake” ndani ya nani? Ya Kristo Yesu ili tuweze kutenda matendo mema, matendo gani hayo? Tupate kumwabudu Baba wa Mbinguni. Waabuduo ni watafutaji na Mungu anawatafuta ili awapate na kuwaleta ili wapate kumwabudu Yeye.

© MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA.

MAOMBI.1. Mathayo 6:9 “Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,” hii maana yake ni kutamani mapen...
29/05/2023

MAOMBI.
1. Mathayo 6:9 “Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,” hii maana yake ni kutamani mapenzi ya Mungu yatimizwe sawa na; Waefeso 5:15 “ Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si k**a watu wasio na hekima bali k**a watu wenye hekima;”
• Mshukuru Mungu kwa kukuumba, kukuokoa na kukupa mahitaji yako.
• Mshukuru Mungu kwa ajili ya utumishi wako mbele zake ili uweze kumzalia matunda, tamani Jina la Bwana liwe ndani yako, Mungu awe ndani yako. Muombe Mungu akupe moyo wa kutii.
2. “Ufalme wako uje”, tamani ufalme wa Mungu uenee , Wafilipi 2:5-11 “Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu,………”
• Omba Injili ya Yesu ihubiriwe duniani kote, mwambie Mungu nifanye niwe sehemu ya injili yako, sehemu ya muujiza kwa watu wengi iwe asubuhi au mchana niwe muujiza unaoishi niwafanye watu wakujie wewe Bwana.
• Jitiishe kwa Bwana, kinywa chako mikono yako na kila ulichonacho ni kwa ajili ya Bwana.
3. Matayo 6:11 “Utupe leo riziki yetu.” Rejea kunako mahitaji yako, Omba kwa ajili ya mahitaji yako, sawa sawa na Wafilipi 4:4-7 “ Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini. Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu…..”.
Furahi kwamba umemueleza Baba yako wa mbinguni shida yako, furahi kwamba Baba yako wa mbinguni ameelewa hitaji lako.
MAOMBI YA MADAI.
• Mwambie Mungu kuhusu wewe na familia yako, wewe unajua familia yako inanini na unahitaji nini juu ya familia yako.
• Omba kwaajili ya ustawi wako, hapo utamueleza biashara zako, kazi zako, nyumba unayotaka shamba n.k
• Omba kwaajili ya Amani yako, Amani ya jamii yako, familia yako, nchi yako na Amani ya mazingira yako.
4. Mathayo 6:13 “Utusamehe deni zetu, k**a sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.” Zitake Rehema za Mungu, zaburi 103:1-4 “Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote. Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote, Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema,”
Kuna mambo mawili ya kutangaza hapa.

• Tangaza msamaha kwa makosa uliyofanya wewe mwenyewe na kwa wale waliokukosea.

• Tamani uponyaji wa Mungu ukujilie. Unaweza ukawa ni uponyaji kwa ajili ya mwili wako, biashara yako, familia yako n.k

• Utaelezea juu ya ukombozi wako. Tamani utoke kutoka katika milki ya kukandamizwa, milki ya kuteseka, kuonewa, kudhulumiwa, ruhusu Mungu aingilie kati.

5. Mathayo 6:13a “Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu.”Omba ili kutaka ulinzi na maongozo ya Mungu, Zaburi 91:1-7 “Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi…….”

Taka ulinzi na maongozi ya Mungu kwa maana ukilindwa na Mungu hata k**a watu watakuvizia usiku au mchana hawatakupata kamwe. "Maana umemfanya aliye juu kuwa makao yako hivyo mabaya hayatakupata wewe".

Mwana mpotevu baada ya kuzingatia moyoni mwake (baada ya kutambua kosa lake) akaamua kurejea kwa baba yake, alisema Luka...
29/05/2023

Mwana mpotevu baada ya kuzingatia moyoni mwake (baada ya kutambua kosa lake) akaamua kurejea kwa baba yake, alisema Luka 15:17-19 “Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa. Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye k**a mmoja wa watumishi wako.” Baba yake alikuwa kila siku ana wasiwasi na mtoto wake na akitamani arejee nyumbani.

Mfano kwako wewe uliye mzazi; hata k**a mtoto wako akiwa mkubwa kiasi gani akiondoka nyumbani kwako na usijue wapi ameenda na hajapiga simu au hajatokea nyumbani unakuwa na wasi wasi mara zote, mfano mtoto akiwa mdogo na akiwa hajaonekana nyumani ndipo sasa unaweza kumuona mzazi akihangaika anapiga simu kila kona ili kuuliza k**a mtoto ameonekana na atakwenda hata police ili wamsaidie kumtafuta.

Hivi ndivyo ilivyo kwa Mungu wetu, wakati wote anaangalia njiani anauliza “Anna atarudi lini, John atakuja lini?” Leo Baba wa mbinguni anakusubiri anaangalia njiani nani atakuja leo kwangu, mwana wa Mungu amua kumkaribia Baba yako.

Mfano mtoto wako anaporejea kwako baada ya kitambo kutokumuona, na ukamuona akiwa amechubuka kila mahali, anachechemea utamchukua na kumuhudumia vizuri kumpa chakula ni kwa kwa sababu ni mwanao, mwana wa Mungu, Mungu anakusubiri, Baba yako wa Mbinguni anakusubiri; haijalishi unapitia nini, haijalishi unamagonjwa au una udhaifu wa aina gani Mungu anasubiri pale utakapokubari kurejea kwake, ipo siri ya ajabu unapomkaribia Baba wa mbinguni, Yeye ana kiu na wewe, njoo leo kwa Baba yako, anakuita.

Haijalishi ulichokosea, ulichopitia, nini kilikupata lakini leo rejea kwa Baba yako wa mbinguni.

© MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA – KANISA LA EFATHA.

Mfungo ni maandalizi ya kumkaribia Mungu. Waefeso 2:18-19 “Kwa maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba...
29/05/2023

Mfungo ni maandalizi ya kumkaribia Mungu. Waefeso 2:18-19 “Kwa maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja. Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu.” Wale wanaomkaribia Bwana, wanaosogea mbele zake, waliokaribu nae, wanaotamani mapenzi yake wanaacha vyote wanamkaribia watu hao ndio anaowaita sio wapitaji wala wageni bali ni wenyeji na ni watu wa nyumbani kwake Mungu.

Mtu anayekaa nyumbani mwako anaona sura yako, anasikia sauti yako, anafurahia mema yako. Vivyo hivyo tunapo mkaribia Baba wa mbinguni ni ili tuweze kupokea vile vilivyo vya kwake, tuweze kuona uzuri wake na tuweze kushiriki mema yake.

Mtu aliye nyumbani mwako hatumii mali yake hata k**a nyumbani kwake ana kilakitu, lakini atatumia kila kitu chako. Lengo la wewe kukaribishwa kwake ni ili ufike mahali usitumie tena vya kwako, kuna siri ya kumsogelea Bwana.

Baada ya kujua kuwa nina kibali cha kumsogelea Bwana ndipo nilianza kusema kuwa mimi sio maskini na ndipo nilianza kumuona Mungu akinitunza . Mwana wa Mungu toka katika kujitahidi maana yupo anayekujali, ana ndege, samaki na wanyama porini, yupo anayekujua anayetunza uhai wako na atakuokoa. Ipo siri ya kumsogelea Mungu na Yeye anasema kuanzia sasa hautajitegemea bali utamtegemea Yeye.

Leo nataka tutoke mahali pa kujitegemea na kujilisha sisi bali kumtegemea Bwana wa mabwana.

© MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA – KANISA LA EFATHA.

IBADA YA KUFUNGA NA KUOMBA SIKU YA ISHIRINI NA SABA TAREHE 27/5/2023SOMO: MAMBO YA MSINGI KATIKA MAOMBIUnapaswa kutambua...
28/05/2023

IBADA YA KUFUNGA NA KUOMBA SIKU YA ISHIRINI NA SABA TAREHE 27/5/2023
SOMO: MAMBO YA MSINGI KATIKA MAOMBI

Unapaswa kutambua lengo au kusudi la kuomba kwako,
Mathayo 6:1 “Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya k**a hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.” Lengo la maombi yetu ni kutaka thawabu, kibali na kutaka mapenzi yake yatimie kwetu. Lengo la kuomba ni kutaka Mungu akuone na kukusikia.

Usifanye maombi ili mtu akuone kuwa unaomba, la! Bali fanya kwa sababu unataka Mungu aone, kile ulichodhamiria moyoni mwako.
Mathayo 6:2 “Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, k**a wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu.” Usitoe kwa sababu unataka watu waone kuwa umetoa, la! Bali toa kwa sababu unataka Mungu akuone umetoa. Toleo la kwanza sio fedha au mali unayotoa, bali ni wewe unavyojitoa kwake.

Usifanye kazi kanisani ili kutaka kumfurahisha kiongozi wako, la! Bali fanya kwa sababu unataka Mungu wako aone.
Mathayo 6:5 “Tena msalipo, msiwe k**a wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. ” Yesu anawachukia wanafiki kuliko hata wenye dhambi, wanafiki ni watu wa aina gani? Ni wale ambao wanajua wanachotakiwa kufanya na wanafanya ili watu waone, hawafanyi ili Mungu aone bali watu wawaone. Unapotaka kusali ingia mahali pa ibada mahali ambapo pameandaliwa kwa ajili ya ibada ongea na Mungu wako.

Lengo la kuomba sio ili nani aone umetimiza maombi au Mchungaji wako aone kuwa umekwenda ibadani, la bali ni kile unachotaka kuongea na Mungu wako na hapo ndipo unahitaji Roho wa Neema akusogeze.

Mathayo 6:6 “Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.” Maombi ni siri ya mtu, hata k**a utasikia anaongea nini lakini ni siri yake iliyojaa moyoni, anapotoa hakutolei wewe unayesikia pembeni, la! Bali anatoa kwa yule aliyemuumba na anayetaka kusikia ili asikie.

© MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA – KANISA LA EFATHA.

23/05/2023

MUNGU WETU NI MKUBWA

Kuna tabia ambazo zinaharibu wana wa Mungu walio wengi na tabia hizo tunapaswa kuziangamiza ili tuweze kusonga mbele. 1....
08/05/2023

Kuna tabia ambazo zinaharibu wana wa Mungu walio wengi na tabia hizo tunapaswa kuziangamiza ili tuweze kusonga mbele.

1. Tabia ya nguruwe; 2 Petro 2:22 “ Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni.” Watu wengi wanakwenda kanisani wanasafishwa lakini wakitoka tu kanisani wanaenda kujichafua tena, hiyo ni tabia ya nguruwe na lazima ikome.

UKIRI:
Baba katika Jina la Yesu, kila tabia ya nguruwe katika maisha yangu naiangamiza kwa Jina la Yesu, natumia Neno lako k**a shoka ninaangamiza tabia za kujichafua na kuyachafua matakatifu yako kwa Jina la Yesu kila tabia za nguruwe hazitaambatana na mimi kuanzia leo.

2. Tabia za Mbwa, Biblia inasema “Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe”
UKIRI:
Kila tabia za Mbwa ndani yangu leo naziangamiza kwa Jina la Yesu, natumia Neno lako k**a rungu ili kuangamiza kila tabia ya Mbwa katika maisha yangu.

3. Tabia ya kuku, hii ni tabia ya kuchonganisha, tabia ya maneno maneno, kulaani na kusengenya; hapa ndipo palipo na laana kwani wengi wetu tunasengenya watumishi wa Mungu.
UKIRI:
Kila tabia za kuku katika maisha yangu hazina nafasi naziangamiza kwa Jina la Yesu.

4. Tabia za bata, bata anatabia gani? Tabia ya kujikanyaga kanyaga;
UKIRI:
Kila tabia ya bata, tabia ya kujikanyaga kanyaga naiangamiza ndani yangu kwa Jina la Yesu, natumia Neno lako k**a rungu naiangamiza hii tabia siitaki kwa Jina la Yesu.

5. Tabia ya kobe, hii ni tabia ya kiburi na dharau, Biblia inasema “ajikwezaye atashushwa”
OMBI:
Mwambie Mungu akuondolee tabia hii na akupe unyenyekevu.
6. Tabia ya Faru: Hii ni tabia ya ubabe na ya kutokujali, kutokuonyesha pendo, msamaha na huruma.
OMBI:
Mwambie Mungu niondolee tabia hii ndani yangu.

7. Tabia ya nyoka, ng'e na kaa, hii ni ile ambayo anakuja kukugonga na akiondoka anakuachia sumu, ukija kutaamaki ndoa imeharibika, uchumi umeyumba na mengine mengi, tabia ya kaa ni kudidimiza.
OMBI:
Kila tabia za nyoka, nge na kaa zilizopo ndani yangu sizitaki kwa Jina la Yesu.

Bwana Yesu kila tabia katika maisha yangu isiyokupa utukufu naipeleka msalabani na kuisulubisha kwa Jina la Yesu. Kila tabia inayonichafua na kunisababisha nimkosee Mungu wangu saa hii naipeleka msalabani.

© MCHUNGAJI WOLFGANG PATRICK - KANISA LA EFATHA

Tunaposema tunafunga ni nini kinafungwa?Mwanadamu ana sehemu kuu tatu• Roho• Nafsi na • Mwili.Kwa nini tunafunga? Tunafu...
08/05/2023

Tunaposema tunafunga ni nini kinafungwa?

Mwanadamu ana sehemu kuu tatu
• Roho
• Nafsi na
• Mwili.

Kwa nini tunafunga? Tunafunga huu mwili ili kuruhusu nafsi na roho iweze kuwa na nguvu na mawasiliano na Mungu.
Mwili una mambo mengi na asili yake ni hii dunia, kwa nini tunafunga mwili? Baada ya anguko la mwanadamu ndipo mwanadamu akapoteza nafasi yake ya umiliki, na ndio maana ibilisi anatutesa kupitia mwili, kwa nini mwili? Kwa sababu mwili ni mavumbi na Biblia inasema “hapo mwanzo giza lilikuwa juu ya vilindi vya maji” hii inamaana kuwa ibilisi alikuwa anatawala mavumbi na mwili ni mavumbi kwa maana hiyo ibilisi anaweza kuutesa mwili wako kwa magonjwa, uchovu n.k. Kwa maana hiyo tunapofunga tunautiisha mwili ili roho iinuke na kukubali kuyafanya mapenzi ya Mungu.

Warumi 12:1 “ Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.”
© MCHUNGAJI WOLFGANG PATRICK - KANISA LA EFATHA

IBADA YA KUFUNGA NA KUOMBA SIKU YA NANE TAREHE 8/5/2023Wewe na mimi tumeokolewa ili tuweze kuwa sifa na utukufu kwa Mung...
08/05/2023

IBADA YA KUFUNGA NA KUOMBA SIKU YA NANE TAREHE 8/5/2023

Wewe na mimi tumeokolewa ili tuweze kuwa sifa na utukufu kwa Mungu, kuna mambo ambayo Mungu alifanya kwetu baada ya kutuokoa:-
• Alitubariki
• Akatufanya tuwe watakatifu
• Akatuchagua
• Akatufanya tuwe watoto wake kwa njia ya Kristo Yesu.

Alifanya hayo yote ili nini? Ili mimi na wewe tuweze kuwa k**a Yeye. 1 Yohana 4:17 “Katika hili pendo limekamilishwa kwetu, ili tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu; kwa kuwa, k**a yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu.”

Ili tuweze kuwa k**a Yeye kuna kazi ambayo mimi na wewe tunapaswa kuifanya, Wafilipi 2:12 “Basi, wapendwa wangu, k**a vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka.” Wewe na mimi tuna kazi ya kufanya katika wokovu wetu ili tuweze kufikia hatua ya kufanana na Yeye. Kazi hiyo ni ipi? Warumi 12:1 “ Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.” Kubali kuutoa mwili wako kwa ajili ya Utukufu wa Mungu.
© MCHUNGAJI WOLFGANG PATRICK - KANISA LA EFATHA

Address

Zanzibar
71212

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Efatha Church-Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Efatha Church-Zanzibar:

Share