Almadrasat Imani Dini Kwamtipura Zanzibar.

Almadrasat Imani Dini Kwamtipura Zanzibar. Karibu katika ukurasa wa Almadrasat Imani Dini Islamia kwamtipura zanzibar

Kuwa kiongozi sio sababu ya kuacha amri za mungu .Makamo wa kwanza wa raisi zanzibar asimamisha msafara akiwa safari kis...
03/05/2021

Kuwa kiongozi sio sababu ya kuacha amri za mungu .
Makamo wa kwanza wa raisi zanzibar asimamisha msafara akiwa safari kisiwani pemba kuelekea kijiji cha makangale na kuwaongoza wafuasi wake katika swala ya adhuhuri kisha kuendelea na msafara

01/05/2021

KUCHUNGA AHADI NA MIKATABA YA AHADI KATIKA UISLAM.
Kuchunga au kutekeleza ahadi ni miongoni mwa vipengele muhimu vya tabia ya muumini wa kweli. Utekelezaji wa ahadi pia ni matunda ya ukweli na uaminifu. Mtu mkweli na mwaminifu ni lazima awe ni mwenye kutekeleza ahadi. Tumeona katika hadith kuwa ukosefu wa uaminifu, uwongo na uvunjaji wa ahadi ni alama kuu tatu za unafiki.

Muislam hana budi kujizatiti katika kutekeleza ahadi zote alizozitoa katika kutekeleza mambo mema. Muislamu akiahidi kutekeleza jambo jema au akiapa kufanya jambo fulani jema analazimika kutekeleza ahadi hiyo au kiapo hicho. Ama kiapo au ahadi ya kufanya mambo maovu si jambo lililosahihi mbele ya Allah(sw). Kwa hiyo ahadi au kiapo cha kufanya mambo yaliyokinyume na sharia ya Allah (sw) si ahadi au kiapo kinacho tambulika mbele ya Allah na atakapodhihirika kuwa ahadi yake au kiapo chake kilikuwa nicha kutenda maovu akivunje

mara moja. Vinginevyo kila ahadi njema ni lazima itekelezwe na kuna adhabu kali mbele ya Allah kwa wavunjao ahadi. Hebu tuone msisitizo wa Allah (s.w) juu ya utekelezaji wa ahadi:

“...Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itaulizwa (siku ya Kiyama). (1 7:34)

“Na tim izeni ahadi m nazozitoa kw a jina la Mw enyezi Mungu m napoahidi, wala msivunje hizo ahadi baada ya kuzithubutisha , hali mume kweisha mfanya Mw enyezi Mungu kuw a shahidi kw enu. Hakika Mw enyezi Mungu anayajua yote mnayoyafanya. (16:91)

“Basi kwa sababu ya kuvunja kwao ahadi yao, tuliwalaani na tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu. (5:13)

Aya hizi zinatosha kutuonesha umuhimu wa kuchunga ahadi katika Uislamu. Aya zinabainisha kuwa utekelezaji wa ahadi ni amri k**a amri nyingine za Allah (sw) ambazo mja akizitekeleza hupata mafanikio mema hapa duniani na malipo makubwa humngojea huko akhera na akizivunja huhasirika katika maisha yake hapa duniani na huko akhera. Tunafahamishwa pia katika Qur’an kuwa miongoni mwa watu wema watakaofuzu mbele ya Allah ni wale watekelezao ahadi zao.

01/05/2021

NINI MAANA YA UAMINIFU KATIKA UCHUNGAJI WA AMANA .
Uaminifu ni uchungaji wa amana. Amana ni kitu chochote halali mtu alichokabidhiwa ili akihifadhi na kukirudisha kwa mwenyewe atakapokihitaji au ili akitumie inavyostahiki au akifikishe mahali palipokusudiwa. Mali uliyokabidhiwa na mtu au umma ni amana; uongozi au cheo ulichopewa na jamii ni amana.

Amana kuu aliyotunukiwa Binadamu na Mola wake Ni roho, vipaji au vipawa vyote alivyonavyo na neema zote za Allah(sw) zilizomzunguka. Binadamu ametunukiwa vitu hivi ili aweze kumuabudu Mola wake inavyostahiki na kuwa Khalifa wetu katika ardhi. Amana hii kuu anaibainisha Allah (sw) katika aya ifuatayo:

“Kwa yakini sisi tulidhihirisha amana juu ya mbigu na ardhi na milima (majabali) vikakataa kuichukua na vikaiogopa lakini mwanadamu akaichukua. Bila shaka yeye ni dhalimu mkubwa, mjinga sana. ” (33:72)

Amana iliyokataliwa na kuogopewa na mbingu, ardhi na milima (ya majabali) si nyingine bali amana ya kuwa Khalifa wa Allah(sw) kuongoza ulimwengu kwa kufuata kanuni na sheria zake.

Hivyo kila mwenye akili hanabudi kuwa na yakini kuwa chochote alicho nacho ni amana kutoka kwa mola wake Muumba ili aitumie katika kumuabudu ipasavyo na kusimamisha ukhalifa katika jamii. Allah (sw) anatukumbusha mara kwa mara juu ya amana hii na kutuamuru:

“Sema: Hakika swala yangu, na matendo yangu (ibada zangu) na uzima

wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allah. Hana mshirika wake. Na haya andiyo niliyoamrishwa, na mimi ni wa kwanza wa waliojisalimisha ”. (6:1 62-1 63).

Muislamu wakweli anatakiwa awe na msimamo huu. Awe na yakini kuwa kila alichonacho ni cha Allah (s.w)na analazimika kukitumia kwa ajili yake tu. Kinyume cha hivyo ni kumfanyia khiana Allah (s.w) na Mtume wake. Tunaonywa katika Qur-an:

“Enyi mlioamini! Msimfanyie khiana Allah na Mtume wala msikhini amana zenu na hali mnajua. Na jueni ya kwamba mali zenu na watoto ni mtihani na jueni ya kwamba kwa Mwenyezi Mungu yapo malipo makubwa. (8:27-28).

01/05/2021

UJUE UONGO NA MADHARA YA UONGO KATIKA DINI YA UISLAMU
Uwongo ni kinyume cha ukweli. Uwongo ni giza na ukweli ni nuru. Uwongo ni upotofu na ukweli ni uongofu. Ambapo ukweli ni uhakika wa asili wenye kudumu, uwongo ni uzushi ambao hutoweka mara tu ukweli unapo Simama.

“Na sema: Ukweli umefika na uwongo (batwili) umetoweka. Hakika uw ongo ndio w enye kutow eka.” (17:81)

Uongo ni uovu wenye kumuangamiza mja hapa duniani na huko akhera. Aidha uwongo ni miongoni mwa maovu makubwa mbele ya Allah (s.w) k**a inavyobainika katika Hadith zifuatazo:

Abubakar (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Nikufahamisheni juu ya madhambi makubwa katika madhambi

makubwa? Sikia! Ni kumshirikisha Allah (s.w), kutotii wazazi na kusema uwongo”. (Bukhari na Muslim).

Katika Hadithi nyingine tunafahamishwa:

Abubakar (r.a) anasimulia kuwa Mtume wa Allah aliuliza: “Je, nikufahamisheni madhambi makubwa?” Aliuliza swali hilo mara tatu. Tukamjibu: “Kwa nini usitufahamishe, Ee Mtume wa Allah?” Akaeleza “Ni kumshirikisha yeyote na Allah (s.w). “Na kusema uwongo na kutoa ushahidi wa uwongo. “Aliendelea kurudia hili mpaka tukaanza kujishauri, kuwa ingelikuwa vyema k**a tusingelimuuliza. ” (Bukhari)

Mtume (s.a.w) ametukataza kusema uwongo hata katika mazungumzo ya utani. Mtume (s.a.w) alitoa makemeo makali k**a ifu atavyo:

Kuna Kifo kw a mtu anayejihusisha na simulizi za uw ongo ili kuchekesha watu na kuna kifo kwake, kuna kuangamia kwake. (Tirmidh).

Katika Hadith nyingine Mtume (s.a.w) amesema:

Muumini hataweza kuikamilisha imani yake mpaka aache kusema uwongo katika utani na katika midahalo hata k**a ni mkweli katika mambo yote mengine. (Ahmad)

Pia katika Hadith nyingine Mtume (saw) aliulizwa;

Kuwa Mu is lamu anaweza kuwa mwoga. Akajibu “Ndiyo”. Akauliza tena, “ Je, Muis lamu anaweza kuwa bakhili?” akajibu, “Ndiyo, anaweza kuwa bakhili. ” Aliuliza tena, “Je, Muumini anaw eza kuw a mw ongo?” Alijibu, “Hapana ”. (Malik)

Ieleweke kuwa si kwamba maovu mengine yaliyotajwa katik

01/05/2021

AINA ZA UNAFIKI
Unafiki uko wa aina mbili:
(1)Unafiki wa kiitikadi. (2)Unafiki wa kimatendo.

1. Unafiki wa kiitikadi

Huu unapatikana kwa kuficha Ushirikina na Kudhihirisha Uislamu, na huu ndio uliotajwa katika Qur-ani.

2. Unafiki wa kimatendo

Huu unapatikana kwa kuyaendea kinyume maneno kwa vitendo, basi mwenye kufanya Kosa kubwa kwa kuacha lilioamrishwa au kufanya lililokatazwa atakua ni Mnafiki, mwenye kuacha Sala kwa uvivu, na Zaka kwa ubakhili, na mwenye kufanya Uzinifu, na mwenye kula Riba na mfano wa hayo, wote hao ni wanafiki.

Na kwa Ujumla Mtu akifikia ukubwa na anazo akili (Mukallafu) ima atakua ni Muumini au atakua ni Kafiri, na wala hakuna nafasi baina ya haya mawili.

﴿إِنَّا هَدَيْنَـٰهُ ٱلسَّبِيلَ إِمَّا شَاكِراً وَإِمَّا كَفُوراً﴾

﴾Hakika sisi tumemuongoza Njia ima atakua ni mwenye kushuru na ima atakua ni mwenye kukufuru﴿

[Insaan 3]

Basi Ukafiri kwa mujibu wa lugha ni kuficha na kuziba, nao kwa mujibu wa Sheria umegawika aina mbili Ukafiri wa Kishirikina, -((na Ushirikina uko aina mbili wa kukataa na kufanya usawa))-, na Ukafiri wa Neema.

Basi mwenye kufanya Kosa kubwa ambalo sio Ushirikina atakua ni Kafiri wa Ukafiri wa Neema, ni Mpotevu wa Njia anafanya lisilokua zuri.

Na Unafiki unatembea baina ya Kufuru mbili, basi huo ni Ukafiri wa Ushirikina kwa kuuficha kwake Ushirikina, na huo ni Ukafiri wa Neema kwa kuyaendea kinyume Matendo.

Na Hukumu za Wanafiki katika maisha yetu ya Kidunia ni Hukumu za Waislamu katika Kuoana na Kurithiana na Kuhifadhika Nafsi na Mali, na Allah anajua zaidi.

01/05/2021

MJUE MNAFIKI PAMOJA NA SIFA ZA NAFIKI.
Mnafiki ni yule anayeukubali Uislamu mdomoni (kwa kauli tu) lakini moyoni mwake na katika matendo yake anaukanusha. Wanafiki wanaainishwa vema katika aya zifuatayo:-

“Na katika watu wako wasemao: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho; na hali ya kuwa wao si wenye kuamini. Wanataka kumdanganya Allah na wale w alioamini, lakini hawadanganyi ila nafsi zao, nao hawatambui.” (2:8-9)

Wanafiki pamoja na kuonyesha imani ya uwongo, ni maadui wakubwa wa Allah (s.w) na Mtume wake. Hushirikiana na Makafiri na Washirikina katika kuupiga vita Uislamu. Wao ni maadui wabaya zaidi kuliko makafiri na washirikina kwa sababu wao hutoa siri za ndani za Waislamu na kuwapelekea maadui wa Uislamu ili wapate kuuhilikisha Uislamu. Hivyo Allah (s.w) amewaahidi wanafiki kuwa watapata adhabu kali k**a tunavyojifunza katika aya ifuatayo:

Bila shaka wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa katika moto. Hutamkuta kwa ajili yao msaidizi’. (4:145)

Hakuna alama au nembo maalum zinazoonekana katika sura au viwili wili vya wanafiki, bali wanafiki wanatambulika kwa matendo

yao au mienendo yao. Mwenendo wa kinafiki au sifa za wanafiki zimebainishwa kwa uwazi katika Qur-an na Hadith Sahihi. Katika Qur’an Allah (s.w) amewaelelezea wanafiki katika aya zifuatazo:

(2:8-20), (3:167-168), (4:60-63), (4 :138-145), (9:43-68), (33:12-20), (57:13), (59:11-1 7), (63:1-8).

aya hizi tunajifunza kuwa wanafiki wamesifika kwa sifa

Maneno ya wanafiki siku zote ni kinyume na matendo yao.

Wanafiki hujaribu kumdanganya Allah pamoja na Waislamu wakidhani kuwa yaliyo vifuani mwao h ayaju likan i.

SIFA ZA WANAFIKI
Siku zote wanafiki hufanya ufisadi huku wakidai kuwa wanatenda wema (wanatengeneza).
Huwaona waumini wa kweli kuwa ni wajinga kwa kufuatakwao Uislamu inavyotakikana.
Huwacheza shere Waislamu.
Wanafiki huyapendazaidi maisha ya dunia kuliko ya
Hawapendi kuhukumiwa na sheria ya Allah (s.w).
Hutumia viapo k**a kifuniko cha maovu yao.

THAMANI YA MWALIMU WA MADRASA NI NANI WA KUIREJESHA?JE NI WAZAZI?JE NI BAKWATA?JE NI WALIMU WENYEWE?JE NI MATAJIRI?JE NI...
01/05/2021

THAMANI YA MWALIMU WA MADRASA NI NANI WA KUIREJESHA?
JE NI WAZAZI?
JE NI BAKWATA?
JE NI WALIMU WENYEWE?
JE NI MATAJIRI?
JE NI JAMII?
JE NI MIMI NA WEWE?
JE NI....?

MUHESHIMIWA ANAEDHARAULIKA.

MWALIMU WA MADRASA.

Kwa mujibu wa maneno ya Mtume Muhammad saw mweshimiwa wa Watu ni yule aliejifunza Quran Kisha akaifundisha anasema Mtume saw.

ﻋﻦ ﻋﺜﻤﺎﻥ ﺑﻦ ﻋﻔﺎﻥ - ﺭﺿﻲ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻨﻪ - ﻋﻦ ﺍﻟﻨﺒﻲ - ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺳﻠﻢ - ﻗﺎﻝ : ‏« ﺧَﻴﺮُﻛُﻢ ﻣﻦ ﺗﻌﻠَّﻢَ ﺍﻟﻘﺮﺁﻥَ ﻭﻋﻠَّﻤَﻪُ ‏» .
‏[ ﺻﺤﻴﺢ . ‏] - ‏[ ﺭﻭﺍﻩ ﺍﻟﺒﺨﺎﺭﻱ . ‏

Kutoka kwa Othman ibn Affan anasema, amesema Mtume saw "Mbora (muheshimiwa) wenu ni yule mwenye kujifunza Qur'an na kufundisha" kaipokea bukhari.

Lakini kwa njama za mfumo mchafu wa kibepari wenye kuonyesha kila kitu ni lazima kiwe na maslahi ya kushikika basi wameondosha thamani ya elimu ya Qur'an. Kwakuwa inaonekana thamani yake sio ya kushikika. Na hakika ni thamani ya kiroho. Yaani jambo la kumuunganisha mwanadamu na muumba wake. Na kihakika ndio thamani bora zaidi kuliko zote.

Na Ummah wa kiislam umefikishwa na wamagharibi katika hali ya kutoithamini Qur'an kuisoma na kiutekelezaji katika Sheria zake hasa baada ya kuvunjwa kwa dola ya kiislam ya kiulimwengu Khilafah.

Na Kisha wamagharibi wakakuza thamani ya masomo mengine kwakuwa maslahi yake ni ya kushikika baada ya mtu kufikia daraja fulani ya kielelimu. Kwa maana atapa kazi au kipato kutokana na elimu hiyo. Na kwakuishusha hadhi elimu ya Qur'an basi mwalimu wa Qur'an pia ameshushwa hadhi katika jamii kubwa ya waislamu. Katika jamii mwalimu wa madrasa anaonekana katika sura hizi.

1. Mwalimu wa Madrasa/Qur'an ameonekana ni mtu anayechukuliwa asiye na thamani sana katika jamii ya Waislamu waliowengi na hata jamii nzima kiujumla.

2. Anaeonekana dhalili, na maisha yake yanaonekana ni kuombaomba na kugonga milango ya wanaojiweza (matajiri). Naam Hali hiyo sababu kubwa ni kutokuwepo kwa dola ya kiislam ya kiulimwengu Khilafah, dola ambayo inawajibu wa kusimamia mafao yao.

UFAHAMU USIKU WA CHEO (LAYLATUL QADR) NA JINSI YA KUUPATA.Siku chache zijazo waislamu In Shaa Allaah tunaingia katika ku...
01/05/2021

UFAHAMU USIKU WA CHEO (LAYLATUL QADR) NA JINSI YA KUUPATA.

Siku chache zijazo waislamu In Shaa Allaah tunaingia katika kuuwania usiku wa cheo (Laylatul Qadr) ulio ndani ya kumi la mwisho la Ramadhwaan, ‘ibaadah yoyote itakayotendwa usiku huo, ni bora kuliko ‘ibaadah za miezi elfu.

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ ﴿١﴾

Hakika Sisi Tumeiteremsha Qur-aan katika Laylatil-Qadr (usiku wa Qadar).

وَمَا أَدْرَاكَ مَا لَيْلَةُ الْقَدْرِ ﴿٢﴾

Na nini kitakachokujulisha ni nini huo Laylatul-Qadr?

لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ ﴿٣﴾

Laylatul-Qadr ni mbora kuliko miezi elfu.

تَنَزَّلُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمْرٍ ﴿٤﴾

Wanateremka humo Malaika na Ar-Ruwh (Jibriyl) kwa idhini ya Rabb wao kwa kila jambo.

سَلَامٌ هِيَ حَتَّىٰ مَطْلَعِ الْفَجْرِ ﴿٥﴾

Amani mpaka kuchomoza Alfajiri. [Al-Qadr: 1-5]

Hadiyth mbali mbali zimethibiti kuhusu fadhila za usiku huu mtukufu na jinsi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alivyokuwa katika masiku kumi ya mwisho ya Ramadhwaan.

Hesabu ya thawabu za usiku huo ni k**a ifuatavyo:

Miezi elfu moja ni sawa na miaka themanini na tatu na miezi mitatu takriban. (1000 ÷ 12 = 83.3)

Utakapokuwa umo katika ‘ibaadah usiku huo wa Laylatul-Qadr, basi utaandikiwa thawabu za miaka 83! Juu ya hivyo, ‘ibaadah ya usiku huo ni bora zaidi kuliko ‘ibaadah ya miaka themanini na tatu.

MAZINGATIO KUHUSU LAYLATUL QADR NA YAPASAYO KUTEKELEZWA.

1. MWENYE KUKOSA LAYLATUL QADR ATAKUWA MWENYE KULA HASARA.

Kwa dalili:

عَنْ أَبِي هُرَيْرَة رَضِيَ اللَّه عَنْهُ قَالَ : لَمَّا حَضَرَ رَمَضَان قَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ (( قَدْ جَاءَكُمْ شَهْرُ رَمَضَان شَهْرٌ مُبَارَكٌ اِفْتَرَضَ اللَّهُ عَلَيْكُمْ صِيَامَهُ تُفْتَح فِيهِ أَبْوَاب الْجَنَّة وَتُغْلَق فِيهِ أَبْوَابُ الْجَحِيم وَتُغَلُّ فِيهِ الشَّيَاطِين فِيهِ لَيْلَة خَيْرٌ مِنْ أَلْف شَهْر مَنْ حَرُمَ خَيْرهَا فَقَد

HISTORIA YA ABRAHA KUVUNJA AL KAABA.Mwaka wa ndovu.  Umeitwa mwaka wa Ndovu kwa sababu mwaka kulitokea kisa muhimu sana ...
01/05/2021

HISTORIA YA ABRAHA KUVUNJA AL KAABA.

Mwaka wa ndovu.

Umeitwa mwaka wa Ndovu kwa sababu mwaka kulitokea kisa muhimu sana cha kutaka kuvundwa Al-Ka'aba na mfalme wahabash.

Kisa cha mwaka wa tembo kinaanzia pale Abraha mfalme wa Habashah na Yaman alipowaona Waarabu wakihiji Makkah na ibada hii ya Hijjah ikaufanya mji wa Makkah kuwa ni kitovu cha biashara .

Abraha Mhabashi aliyekuwa gavana wa Al Najashi katika nchi ya Yemen alidhamiria kuihamisha ibada hii ya Hijjah kutoka Makkah na kuipeleka katika milki ya himaya yake ya Yaman.

Ili kuutekeleza mkakati wake huu akajenga kanisa kubwa sana katika mji wa Sana-a na kulipamba kwa mapambo ya fakhari ili watu wavutike na kuja kufanya ibada ya Hijjah hapo.

Baada ya ujenzi huo, akawaamrisha watu waje kuhiji hapo, amri hii ikawa nzito kwa Waarabu kuitekeleza na hawakuiridhia.Ili kuonyesha chuki yao dhidi ya amri hii alitoka mtu mmoja wa kabila ya bani kinaanah akaja kufanya haja kubwa ndani ya kanisa lile.

Kitendo hiki cha kulichafua kanisa kilimkasirisha sana Mfalme Abraha, hasa baada ya kugundua kwamba mhusika wa kitendo hicho ni mtu kutokea pande za Makkah.

Akaandaa jeshi kubwa idadi yake askari wapatao elfu sitini pamoja na tembo ishirini na mbili yeye mwenyewe akiwa juu ya tembo mkubwa sana, aliekuwa akiitwa (Mahmud) na kuelekea nalo Makkah kwa ajili ya kuibomoa Al-Ka’abah.

Waarabu wa Makkah waliogofya sana na jeshi lile. Jeshi la Abraha lilipofika katika viunga vya mji wa Makkah likawakuta ngamia, kondoo na mbuzi wa watu wa Makkah na wengine walikuwa ni milki ya babu yake Mtume Mzee Abdul-Mutwalib, Abraha awachukua wanyama wale wote.

Mzee Abdul-Mutwalib kiongozi wa kabila la Kikurayshi, mtumishi wa Al-Kaab na mtawala wa Makkah akamuendea Abraha na kumtaka amrejeshee wanyama wake aliowachukua Abraha akamshangaa sana Mzee Abdul – Mutwalib
akamwambia:"Mimi nilitazamia umekuja kuniomba nisiivunje Al-Kaab, kumbe umekuja kunitaka nikurudishie wanyama wako!"

Mzee Abdul – Mutwalib akamjibu:

[أنا رب الإبل وللبيت رب

30/04/2021

*HISTORIA YA BANI ISRAIL*

Nabii Musa na Harun walikuwa na kazi kubwa mbili; kwanza, kuwakomboa Bani Israil kutokana na dhuluma waliyokuwa wakifanyiwa na Firaun na Serikali yake, na pili, kuwarudisha kwenye nchi yao takatifu ya Palestina.

Nchi hii imeitwa takatifu kwa sababu ilikuwa nchi iliyo kaliwa na Mitume watukufu, Ibrahim(a.s),Is-haq(a.s) na Ya‘aquub(a.s).

Palestina pamoja na kuwa nchi iliyokaliwa na Mitume maarufu k**a hao, watu waliofuatia baadaye waliacha mafunzo yao na kuanzisha mifumo ya maisha ya kishirikina. Hivyo Bani Israil walitakiwa warudi nchini mwao wakautawalishe Uislamu juu ya mfumo ya kishirikina uliokuwemo mle.

Kutoka Misr walienda hadi Mlima Sinai. Hapa walikaa kwa muda wa mwaka mmoja ambapo Nabii Musa(a.s) alishushiwa karibu hukumu zote za Taurat.

*Musa(a.s) Kupewa Taurati*

Musa(a.s) aliitwa na Allah(s.w) katika Mlima Sinai ili apewe sharia kwa ajili ya wana wa Israili. Siku arubaini ziliteuliwa ili Mtume aweze kujiandaa mwenyewe kwa kufunga na kuswali kwa ajili ya kazi ngumu inayomsubiri ya kuwaongoza Bani Israil wakasimamishe ufalme wa Allah(s.w) katika nchi ya Palestina.

Wakati huu Mtume Musa aliwaacha Bani Israil (Mayahudi) katika sehemu ambayo sasa huitwa Wadiy-Shaikh ambayo ipo kati ya Nubi Salih na Mlima Sinai. Mlima Sinai una urefu wa futi 7,359 toka usawa wa bahari na mara nyingi huwa umefunikwa na mawingu. Kileleni mwa mlima huu lipo pango ambapo Nabii Musa (a.s) alikaa siku arobaini.

Leo hii karibu na pango hilo pana msikiti na kanisa.Habari ya kuitwa Musa katika Mlima Sinai inatajwa katika aya zifuatazo:

Na tulimuahidi Musa siku thalathini (afanye ibada, kisha tumpe Taurati) na tukazitimiza kwa kumi ikatimia miadi ya Mola wake siku arubaini. Na Musa akamwambia ndugu yake Haruni: "Shika mahali pangu katika (kuwaangalia) watu wangu na utengeneze wala usifuate njia ya waharibifu" (7:142).

K**a aya inavyobainisha, ilipotimia miadi Musa alikwenda kupokeasheria. Akasema (Mwenyezi Mungu):

30/04/2021

HISTORIA FUPI YA MTUME (S.A.W)

JINA LAKE NA NASABU YAKE.

Jina lake ni Mohammad bin Abdallah bin Abdul mutwalib bin hashim bin Abdul manaf bin Quswai bin kilaab. Na ukoo wake mtukufu unamalizikia kwa mtume Ibrahiim (A.S)

MAMA YAKE.

Mama yake ni Amina binti Wahabi bin Abdul manafi bin zuhra bin kilaab.

KUNIA YAKE NI:

Abul qaasim, pia Abuu Ibrahiim.

JINA LAKE MASHUHURI.

1- Mustafa, na anayo majina mengine mengi yaliyo pokelewa ndani ya Qur’ ani tukufu k**a:

2- Khaatamun nabiyyiin. 3- Al ummiyyi. 4- Al muzammil. 5- Al mudathir. 6- Al mubiin. 7-Al kariim.

8- An nuur. 9- An niima. 10- Ar rahmaan. 11- Ash shaahid. 12- Al mubashir.13- An nadhiir. 14- Abdur rauuf. 15- Ar rahiim. 16- Ad daai na mengine mengi.

TAREHE YA KUZALIWA KAKE.

Alizaliwa tarehe 17 mwezi wa Rabiiul awwal, mwaka wa tembo sawa na mwaka 571 H.D.kutokana na kauli iliyo mashuhuri kwa mashie, na kauli nyingine inasema ya kuwa alizaliwa tarehe 12 mwezi wa Rabiul awwal mwaka huo huo.

SEHEMU ALIPO ZALIWA.

Alizaliwa katika mji wa makkatul mukarramah ulioko katika nchi ya Saudi Arabia.

KUPEWA KWAKE UTUME.

Ali pewa rasmi utume tarehe 27 mwezi wa rajab katika mji wa makka baada ya kutimiza miaka 40 ya umri wake mtukufu.

MAFUNDISHO YAKE.

Mtume (s.a.w) alikuja na wito wa usawa kwa viumbe wote, na alikuwa akilingania udugu, na msamaha kwa kila mwenye kuingia kwenye Dini ya ki islaam, kisha aliweka sheria iliyo nyepesi, na kanuni za uadilifu alizo zipokea kutoka kwa Mwenyezi Mungu alie takasika, kisha waislaam wakazipokea kutoka kwa Mtume (s.a w).

MIUJIZA YAKE.

Muujiza wake pekee wa milele na milele ni Qur’ ani tukufu; ama miujiza yake iliyo dhihiri mwanzoni mwa uislaam ni mingi sana kwani hai hesabiki.

WITO WAKE.

Mtume (s.a.w) ali walingania watu kwenye upweke wa Mwenyezi Mungu katika mji wa makka na kwa njia ya siri kwa muda wa miaka mitatu, na baada ya kipindi cha siri ali waita watu kwa njia ya wazi kwa muda wa miaka kumi.

KUHAMA KWAKE.

Alihama kutoka katika

Address

Kwamtipura
Zanzibar City

Telephone

+255778312137

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Almadrasat Imani Dini Kwamtipura Zanzibar. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share