Kanisa la Pentecoste Zanzibar

Kanisa la Pentecoste Zanzibar Welcome to Kanisa la Pentekoste Zanzibar (KLPZ) the first Pentecostal church established and operating in Zanzibar.

KLPZ is a Christ-centered community dedicated to spreading the Gospel, building strong believers, and serving the people of Zanzibar.

29/05/2026
Asubuhi ya leo, Askofu wetu pamoja na viongozi wa kanisa na baadhi ya waumini walipata nafasi ya kufika katika Ofisi ya ...
25/05/2026

Asubuhi ya leo, Askofu wetu pamoja na viongozi wa kanisa na baadhi ya waumini walipata nafasi ya kufika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa ajili ya kufanya mazungumzo na kueleza changamoto iliyojitokeza hivi karibuni, kwa lengo la kuangalia namna bora ya kutatua hali hiyo kwa manufaa ya kanisa na jamii kwa ujumla.
Vilevile, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya alipata nafasi ya kutembelea kanisa letu ili kujionea hali halisi ya tukio lililotokea na kutoa pole kwa kanisa na waumini wote walioathirika na tukio hilo.
Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Dkt. Said Haji Mrisho, pamoja na viongozi wote wa Serikali, ikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama vya Wilaya ya Mjini, kwa ushirikiano wao mkubwa, moyo wa kutusikiliza, na kutuhakikishia kuendelea kuwepo kwa amani, utulivu na usalama katika jamii yetu.
Tunaendelea kusisitiza umuhimu wa mshik**ano, amani, na kuheshimiana katika jamii yetu huku tukiiweka imani yetu kwa Mungu.
Mungu awabariki sana. πŸ™


25/05/2026

Hii ni sehemu ya tukio lililotokea jana katika kanisa letu ambapo baadhi ya watu walionekana wakiharibu na kung’oa geti la kanisa letu. Pamoja na hali hii ya kusikitisha, tunamshukuru Mungu kwa kuwa bado tupo salama na hakuna maisha yaliyopotea. πŸ™
Kwa sasa jambo hili lipo chini ya mamlaka za kiserikali na tunaamini haki itachukua mkondo wake kwa amani na utulivu.
Tunawashukuru sana wote ambao mmeguswa na tukio hili na kuendelea kutuombea, kutupa faraja, na kuonyesha moyo wa kutushika mkono katika kipindi hiki kigumu. ❀️
Kwa yeyote anayependa kuunga mkono matengenezo na msaada wa huduma yetu, unaweza kutumia namba zifuatazo:
🏦 Account ya Benki:
National Microfinance Bank (NMB)
Account Name: Kamati ya Mipango na Maendeleo KLPZ
Account Number: 22910110206
πŸ“± Vodacom M-Pesa:
Jina: Kanisa la Pentekoste Zanzibar
Namba: 0756314354

β€œMungu ni kimbilio letu na nguvu yetu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.” β€” Zaburi 46:1


πŸ™ OMBEA KANISA LA ZANZIBAR πŸ™Siku ya leo tumepitia wakati mgumu baada ya kanisa letu kuvamiwa na watu wasioipenda Injili....
23/05/2026

πŸ™ OMBEA KANISA LA ZANZIBAR πŸ™
Siku ya leo tumepitia wakati mgumu baada ya kanisa letu kuvamiwa na watu wasioipenda Injili. Wakati vijana wetu wakiendelea kujiandaa kwa ajili ya ibada ya kesho, kundi la watu walivamia eneo la kanisa na kusababisha uharibifu wa mali, ikiwemo kuvunja geti la kanisa pamoja na maeneo mengine. Pia baadhi ya ndugu zetu wamejeruhiwa katika tukio hilo.
Pamoja na yote yaliyotokea, tunaendelea kusimama katika imani tukijua kuwa Mungu bado anatawala. Tunaomba muendelee kuliombea kanisa la Zanzibar, viongozi wetu, vijana wetu, pamoja na huduma ya Injili kisiwani Zanzibar.
β€œSilaha yoyote itakayofanyika juu yako haitafanikiwa.” β€” Isaya 54:17 πŸ™




20/05/2026
Kila jukumu unalofanya leo iwe ni kazini, nyumbani, au katika huduma ni nafasi ya kipekee ambayo Mungu amekupa ili Mungu...
10/05/2026

Kila jukumu unalofanya leo iwe ni kazini, nyumbani, au katika huduma ni nafasi ya kipekee ambayo Mungu amekupa ili Mungu apate kutukuzwa kupitia wewe.

Mungu hatafuti watu wenye uwezo mkubwa pekee, bali anatafuta wale walio tayari kutumiwa naye, watu walio Kua tayari kwenye majukumu ili Mungu apate utukufu..

Karibu KLPZ jumapilu hii tumuabudu Mungu alie Hai

"Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele." β€” Zaburi 136:1
05/05/2026

"Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele." β€” Zaburi 136:1

Karibu Jumapili hii
30/04/2026

Karibu Jumapili hii

Hakika hakuna mahali pazuri k**a kuwa mbele za uso wa Mungu.Kuna kitu kinatokea wakati watu wa Mungu wanapokusanyika na ...
27/04/2026

Hakika hakuna mahali pazuri k**a kuwa mbele za uso wa Mungu.
Kuna kitu kinatokea wakati watu wa Mungu wanapokusanyika na kuomba kwa moyo mmoja. Leo tumeuona mkono wa Bwana ukigusa maisha yetu! Leo tumepata nguvu mpya kupitia sifa na maombi. "Maana siku moja katika nyua zako ni bora kuliko siku elfu. Ningependa kuwa bawabu nyumbani mwa Mungu wangu, kuliko kukaa katika hema za uovu." β€” Zaburi 84:10

Address

Https://maps. App. Goo. Gl/3L6J46ncQrcv1Kdr7?g_st=ac
Zanzibar City

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kanisa la Pentecoste Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share