15/05/2026
MKRISTO UJUE UKWELI HUU ILI UWE SALAMA
Mambo ambayo yana upinzani kwa Wakristo walio wengi.
Nimeona niyaweke mambo haya machache ili kila mmoja ajipime na kugundua nidhamu aliyonayo kwa Mungu anayemwabudu.
Hii ni changamoto ambayo unapaswa kujipima kwayo na kijifanyia tathimini ili kujiona namna ulivyosimama kwa Mungu.
Haijalishi umri wako au cheo chako nafasi yako hii inatuhusu wote.
Sasa hebu pitia dondoo hizi hapa chini:-
1. Shauku ya kusoma Biblia.
2. Kufunga na kuomba kibinafsi.
3. ShUku ya kumtolea Mungu kwa upendo
4. Kushuhudia habari za Yesu kwa wengine.
5. Nidhamu ya kuhudhuria ibada.
6. Shauku ya maombi ndani yako.
Ili iwe rahisi kwetu kujipima naomba dondoo hizi niziwekee mfumo wa namba kuanzia 1 mpaka 5
Alama ya juu ya ubora ni 5
Kwa mtindo huu wa tathmini hakuna aliye 0 hivyo hata 1 ni namba ya ubora.
Lakini maandiko yanatutaka kupandisha thamani yetu ya utendaji mbele za Mungu namna hii.
Hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; Waefeso 4:13
Wengine walikuwa bora inawezekana hata wewe ulikuwa Bora, lakini kwa hila za shetani kiwango chako kimeshuka hata wewe unashangaaa imekuwaje.
Sasa hebu tuweke wazi ili ujipime mwenyewe k**a andiko linavyotutaka .
Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa. 2Korintho 13:3
Kwa Kila swali alama ni moja tu inaweza kuwa 1 au 2,3,4,5
Usiweke alama mbili kwenye swali moja unapojibu.
Sasa endelea
1. Shauku ya kusoma Biblia. 1. 2. 3. 4. 5
2. Kufunga na kuomba kibinafsi. 1. 2. 3. 4. 5
3. ShUku ya kumtolea Mungu kwa upendo.
1. 2. 3. 4. 5
4. Kushuhudia habari za Yesu kwa wengine.
1. 2. 3. 4. 5
5. Nidhamu ya kuhudhuria ibada. 1. 2. 3. 4. 5
6. Shauku ya maombi ndani yako.
1. 2. 3. 4. 5.
Mtindo huu utakusaidia kujua nafasi ya ubora uliyopo kwa habari za kumtumikia Mungu na kicho chako kwake.
Kutunza nidhamu yako ya utumishi mbele za Mungu ni wajibu wako, kumbuka Mungu atalipa utendaji wa mtu uwe bora au uwe wa chini. Hebu soma andiko hili kwa makini,
Basi yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe. 1Korintho 3:8
Paulo alitahadharisha aliposema
Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, k**a mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.
Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo.
Lakini k**a mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri.
Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani.
Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu.
Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni k**a kwa moto. 1Koritho 3:10-15.
Baada ya kujipima na kuona hali yako halisi usivunjike moyo bali tafuta namna ya kuberesha hali yako ya kiroho na utendaji wako mbele za Mungu.
Usivunjike moyo na kukata tamaa ukajiona hufai kwasababu ya matokeo ya chini uliyopata. Tathmini hii ikusaidie kujikagua Kisha kujigundua udhaifu wako na hatimaye ujirkebishi kibinafsi.
Nakutakia tathimini njema tena hatua kwa hatua. Ka Kisha kupandisha kiwango chako katika neema ya Yesu Mwokozi
Barikiwa
Mwl Zoeril Bukuku
0713765 777
Sauti kutoka mbali.