Efatha Church_Uyole

Efatha Church_Uyole Healing and Deliverance by blood of God
Efatha Church Uyole
Administered by pastor Evance_Msamati

Tufuatile kwenye mitandao yakijamii Facebook efatha church uyole Instagram efatha church uyole welcome JUN
01/06/2025

Tufuatile kwenye mitandao yakijamii Facebook efatha church uyole Instagram efatha church uyole welcome JUN

MATUKIO MBALIMBALI YA PICHA KATIKA IBADA YA JUMAPILI YA TAREHE 20/10/2024
20/10/2024

MATUKIO MBALIMBALI YA PICHA KATIKA IBADA YA JUMAPILI YA TAREHE 20/10/2024

USHUHUDA Felista Mwingira anapenda kumshukuru sana Mungu kwa ajili ya wokovu kwa maana kupitia wokovu huo amebarikiwa sa...
06/10/2024

USHUHUDA

Felista Mwingira anapenda kumshukuru sana Mungu kwa ajili ya wokovu kwa maana kupitia wokovu huo amebarikiwa sana. Felista aliokoka mwaka 2014 akiwa na hali duni sana, siku moja Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alitembelea kanisa la Efatha Karatu na akaongoza ibada, katika ibada ile akasema “wale wote waliotelekezwa na baba zao mimi nitakuwa baba kwao” akatuita mbele na kutuombea. Tangu wakati huo Felista aliona Mungu akibadilisha maisha yake, Felista alihudhuria kusanyiko la mwaka huo na katika lile kusanyiko Mtumishi wa Mungu alisema mtaenda kupokea baraka double double. Felista aliporejea nyumbani aliona Baraka zikimfuata, mume wake akashinda kesi ya shamba iliyodumu kwa muda wa miaka 15, wakajenga nyumba, wakanunua lori la biashara na gari la kutembelea. Felista anamshukuru sana Mungu kwa matendo yake makuu katika maisha yake.

Our joy knows no bounds today, Kwa tukio hili la leo limetuonyesha na kutudhihirishia kwamba katika msimu huu wa umiliki...
06/10/2024

Our joy knows no bounds today, Kwa tukio hili la leo limetuonyesha na kutudhihirishia kwamba katika msimu huu wa umiliki, hatumiliki vya rohoni pekee lakini tunamiliki na vya mwilini pia. Katika siku yetu ya 5 ya Kusanyiko la umiliki tumepata fursa pia ya kusherekea na wahitimu wa chuo cha Precious College katika mahafali yao ya Pili katika chuo hicho kilicho mkoa wa Pwani Kibaha.

Wahitimu wametunikiwa Stashahada za Theology, Church Administration & Management, Stashahada ya Church Administration & Management pamoja na Astashahada ya Theology, Church Administration & Management.

Tuna uhakika kwamba they have passed through rigorous training and teaching under the supervision of their mentors — Tunatoa pongezi za dhati kwa wahitimu wote, tunawaombea Neema ya Mungu iwe na wao na katika huduma zao. Tunawatakia kila la kheri wanapoenda kutimiza wito na kusudi la kiungu ndani yao kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Amen! 🎓

Neno moja la pongezi kwa ajili yao kwenye comment section!
———————————————

KUSANYIKO KUU LA KUMI NA SITA SIKU YA TANO ASUBUHI TAREHE 5/10/2024 - KANISA LA EFATHA PRECIOUS CENTRE KIBAHA. Zaburi 28...
05/10/2024

KUSANYIKO KUU LA KUMI NA SITA SIKU YA TANO ASUBUHI TAREHE 5/10/2024 - KANISA LA EFATHA PRECIOUS CENTRE KIBAHA.

Zaburi 28:6-7 "Na ahimidiwe BWANA. Maana ameisikia sauti ya dua yangu; BWANA ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru."

Zaburi 66:1-4 "Mpigie Mungu kelele za shangwe, nchi yote, Imbeni utukufu wa jina lake, Tukuzeni sifa zake. Mwambieni Mun...
05/10/2024

Zaburi 66:1-4 "Mpigie Mungu kelele za shangwe, nchi yote, Imbeni utukufu wa jina lake, Tukuzeni sifa zake. Mwambieni Mungu, Matendo yako yatisha k**a nini! Kwa ajili ya wingi wa nguvu zako, Adui zako watakuja kunyenyekea mbele zako. Nchi yote itakusujudia na kukuimbia, Naam, italiimbia jina lako."

KIINDI CHA PILIASKOFU MICHAEL KYAZZE KUTOKA UGANDA Obadia 1:17 “Bali katika mlima Sayuni watakuwako wenye kuokoka, nao u...
05/10/2024

KIINDI CHA PILI
ASKOFU MICHAEL KYAZZE KUTOKA UGANDA

Obadia 1:17 “Bali katika mlima Sayuni watakuwako wenye kuokoka, nao utakuwa mtakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki milki zao.”

Sayuni ni mahali pa ukamilifu, ni mahali pa agano jipya, ni mahali palipo kamilishwa, ni mahali pa furaha na ni mahali ambapo pana malaika wengi.

Sayuni ni mahali ambapo watu wanafanywa kuwa wakamilifu, ni mahali ambapo pana haki, wote wanaoenda katika mlima Sayuni watakuwa katika haki kwa maana Mungu yupo hapo. Sayuni ni mahali pa ujumbe wa agano jipya, ni mahali ambapo pana Damu inenayo mema; katika mlima Sayuni kuna ukombozi.

Ili uweze kumiliki milki zako ukombozi lazima utokee kabla ya kitu chochote kutokea katika maisha yako, ukombozi unawahusu wale waliyotekwa na kuonewa. Ukombozi ni kwa ajili ya:-

• Wale waliyokandamizwa na magonjwa ili wapate kuwa huru.
• Ukombozi ni kwa ajili ya wale ambao wametekwa, wale ambao wamepelekwa mahali ambapo hawakustahili kuwepo, wale ambao hawawezi kwenda mahali ambapo wanataka kwenda wala kufanya wanachotaka bali wapo kizuizini.

Ili uweze kumiliki ahadi za Mungu katika maisha yako ni lazima uwe huru kutoka katika kukandamizwa na ukombolewe.

Zaburi 100:4-5 "Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake;  kwa k...
05/10/2024

Zaburi 100:4-5 "Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake; kwa kuwa BWANA ndiye mwema; Rehema zake ni za milele; Na uaminifu wake vizazi na vizazi."

Mathayo 28:19 “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho M...
05/10/2024

Mathayo 28:19 “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;”
Yesu ametutuma sisi ulimwenguni huku, huu siyo wito bali ni wajibu ametupa katika maisha yetu na Roho Mtakatifu akija juu yetu tutapokea nguvu ya kuwa mashahidi na kutimiza wajibu huu. Huu siyo mchezo bali unapaswa kumfikia mtu mmoja tu aliyekusudiwa na bado haujamfikia, yapasa ubadilishe mtazamo wa mtu mmoja, kuna mtu anapaswa kusikia habari za Yesu kupitia kwako wewe uliyeokoka ili aweze kuokolewa. Hiki ni kipindi cha mavuno huwezi kulala kipindi cha mavuno.

Siku moja ukifika mbinguni, swali moja tu utaulizwa, je! Ulitumia vipi uhai wako ulipokuwa duniani, uliwasababisha wangapi wakaokolewa? Huu ndiyo wajibu ambao tumepewa sisi k**a wana wa Mungu; huu ni wakati wa mavuno usilale.

Huu ni wakati wa maachilio, kwa wale waliotekwa ni wakati wao wa kuwekwa huru, sheria zimevunjwa, watu watawekwa huru. Haya ni majira mapya, hatuwezi kulala katika majira haya ya mavuno.

Sisi tuliyookoka ni wana wa nuru hivyo yapaswa kupeleka nuru gizani, tukawe chumvi ulimwenguni, tupeleke uzima kwa wale wanaohitaji, Yesu anakutuma wewe na ukikubali kuwa mtendakazi pamoja na Yeye atakufanya upae k**a Tai, je! Uko tayari kuipeleka injili kwa mataifa? Wakati ni sasa usilale wakati mavuno yako tayari.

© MCHUNGAJI STEFAN ADEFORS KUTOKA SWEDEN.

Yohana 17:17 “Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.” Kweli ni Neno la Mungu, akili yako lazima iwe na Neno, ha...
05/10/2024

Yohana 17:17 “Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.”

Kweli ni Neno la Mungu, akili yako lazima iwe na Neno, hauwezi kuhubiri neno la kweli k**a hakuna Neno la Mungu ndani yako, mpaka akili yako itakapokuwa imejaa Neno ndipo utaweza kuinena kweli, ikiwa akili yako haijapata kweli hauwezi kuisema hiyo kweli.

Katika kuisema kweli kuna haya:-
1. Utakaso wa akili yako, Yohana 8:31-32 “Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.”

Mpaka akili yako itakapokuwa imepata kweli ndipo utakuwa huru vinginevyo kamwe hautakuwa huru.
• Lazima uwe mwanafunzi wa Yesu, uwe katika maisha ya kujifunza kwa sababu kweli itakuweka huru.

Nini faida ya kuwa na kweli?
a. Warumi 8:1-2 “ Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.”

K**a akili yako ina kweli ndani yake kifungo kilichokufunga katika akili yako kitakuachia na utakuwa huru.
Kweli ni nini? Ni kujua kipi ni kibaya na kipi ni kizuri, ukipata ufahamu huo hiyo ni akili ya Mungu na kwa sababu ya hiyo unakuwa mbali na hukumu ya Mungu.

b. Unakuwa mbali na hukumu ya Mungu, Zaburi 32:1-2 “Heri aliyesamehewa dhambi, Na kusitiriwa makosa yake. Heri Bwana asiyemhesabia upotovu, Ambaye rohoni mwake hamna hila.”

c. Utaishi maisha ya kumwamini Mungu sawasawa na Wafilipi 4:13 “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.” Hakuna unachokipoteza bali mara zote unapata faida na chochote ukifanyacho kinastawi.

d. Waliyo na kweli ya Mungu wanawezeshwa na silaha za Mungu kwa sababu wameibeba kweli ndani yao, Waefeso 6:17-18 “Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;…..”

Ukiwa na kweli inakusaidia kujua namna ya kufanya vitu kwa maana palipo na kweli ndipo palipo na hekima, hekima imeambatana na kweli ukijawa na hekima basi

Address

Uyole
53000

Opening Hours

Monday 04:00 - 18:00
Tuesday 05:00 - 18:00
Wednesday 04:00 - 18:00
Friday 04:00 - 18:00
Sunday 08:00 - 16:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Efatha Church_Uyole posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Efatha Church_Uyole:

Share