George ABEL Mwache

George ABEL Mwache Evangelism

04/09/2026

*JE, UNATAKA KUFANIKIWA KWENYE MAISHA YAKO KIROHO NA KIMWILI?*

BWANA YESU KRISTO APEWE SIFA 🙏

▶️▶️Jifunze Kufanya Yafuatayo;

1️⃣ Hakikisha Unamiliki ,na kutawala na kulitiiisha ANGA la mahali ulilopo!

▶️▶️Iwe ni kwenye Biashara, Huduma, Kazi,Elimu,Kukua Kiroho, ANGA ni Eneo Muhimu Sana kwako!

Kwanini??
Kwasababu;

✅Shetani anaweza Kutumia ANGA la mahali ulilopo kukuzuia Usifanikiwe kabsa!

""ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata *mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi*
(Waefeso 2:2)

✅ Shetani anaweza Kutumia ANGA la mahali ulilopo kukuzuia MAOMBI Yako!

*Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi*
(Danieli 10:13)

2️⃣ Hakikisha Unaomba MBINGU ziwe Upande wako!

✅Mbingu zinaweza kufunguka kwaajili Yako na kukuruhusu kufanikiwa

✅Lakini pia Mbingu zinaweza kufungwa kwaajili Yako!

✅K**a Mbingu zisipokuwa Upande wako kufanikiwa kwako itakuwa ni NGUMU Sana

*Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka k**a hua, akija juu yake*
(Mathayo 3:16)

*Hizo mbingu hupambwa kwa roho yake*
Mkono wake umemchoma nyoka aendaye mbio.
(Ayubu 26:13)

✅ Mbingu zikiwa Upande wako, Maana yake ni kwamba ROHO wa YESU yupo Upande wako pia!

3️⃣ Hakikisha ARDHI unayofanyia Biashara,Kazi ,Kujenga nyumba,au Huduma Iko Upande wako pia

✅ ARDHI ni Silaha Muhimu sana kwetu Katika kutusaidia kufanikiwa Kiroho na Kimwili pia

*Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake*
(Ufunuo wa Yohana 12:16)

Mungu wangu awabariki Sana Sana

SHALOM 🙏

ONLY CHRIST CAN ACCOMPLISH IT WITHIN US!
AMEN

04/09/2026

*TUMIA MAMLAKA ULIYO NAYO JUU YA SHETANI KATIKA MAGONJWA NA ONDOA VIZUIZI*

Hapo mwanzo, Adamu alikuwa na mfano wa Mungu katika utakatifu mpaka pale alipotenda dhambi kwa kutumia vibaya hiari yake ya kuchagua jambo la kufanya.

Akachagua kuliasi Neno la Mungu, tendo ambalo ndilo linaloitwa dhambi.

Kabla Adamu hajafanya dhambi, alikuwa ni MTAWALA.

Chochote katika nchi kilipaswa kumtii Adamu.

Hii ni pamoja na Shetani. Adamu alipofanya dhambi na kukubali Neno la Shetani, alipoteza mamlaka ya utawala aliyokuwa nayo na akayachukua Shetani. [MWANZO 1:26-27].

Alipokuja Yesu na kututoa katika utumwa wa dhambi, na kuzivunja kazi za Ibilisi aliyetutumikisha wote tuliozaliwa kutokana na Adamu; alifanya jambo jingine zuri.

Aliturudishia mamlaka aliyotunyang’anya Shetani. Ndiyo maana Yesu alisema *Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani baada ya kufufuka [MATHAYO 28:18]*

Sasa mamlaka hii aliyoichukua Yesu ni ile aliyokuwa ametunyang’anya Shetani. Kwa kumshinda Shetani na kazi zake zote, Yesu alimnyang’anya mamlaka Shetani na kutupa mamlaka hiyo ambayo pia inaitwa *AMRI*. Kwa mamlaka hii au *AMRI* aliyoturudishia kila mtu aliyeokoka ana uwezo wa kumkanyanga nyoka yuleyule aliyetukanyaga mwanzo. Nguvu zote za Shetani, hazina uwezo juu ya mtu aliyeokoka.

LUKA 10:18-19
*Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni k**a umeme. Tazama nimewapa AMRI ya kukanyanga nyoka na nge, na NGUVU ZOTE ZA YULE ADUI (SHETANI), wala hakuna kitu kitakachowadhuru*

Nguvu zozote za Shetani hata k**a zingekuja kwa vitisho k**a umeme, ziko chini ya *AMRI* au *MAMLAKA* ya mtu aliyeokoka. Unapolitumia Jina la Yesu kwa Mamlaka au Amri juu ya pepo wanaosababisha tatizo ulilo nalo, pepo hao watakutii na kuondoka [SOMA LUKA 10:17].

Magonjwa mengi husababishwa na pepo wa udhaifu [SOMA LUKA 13:11; MATHAYO 12:22;MARKO 9:17, 25; LUKA 11:14].

Unapokuwa umeelemewa na ugonjwa wowote iwe ni homa au ugonjwa wowote, au unapokuwa unaomba kwa ajili ya ugonjwa alio nao mwenzio; haitoshi tu kumwomba Mungu auponye ugonjwa huo, ila inakubidi pia UTUMIE MAMLAKA ULIYO NAYO JUU YA SHETANI NA KUUKEMEA UGONJWA HUO NA KUUAMURU KWA AMRI KWAMBA UHAME. [Angalia mfano katika [LUKA 4:38-39].

*MFANO WA MAMLAKA KATIKA ULIMWENGU HUU:*

Waangalie askari wa Usalama Barabarani au askari wa trafiki. Hata k**a umbo la askari ni dogo namna gani, kwa kutumia mamlaka aliyopewa na Serikali, anaponyosha mkono mtupu usio na chochote, gari kubwa lenye tela nyuma na linaloendeshwa na mtu mwenye umbo kubwa husimama pale pale. Vivyo hivyo kwa mtu aliyeokoka. Hata k**a ukiwa na umbo dogo namna gani au umeokoka leo tu au jana, unapoamuru pepo wa udhaifu au kazi yoyote ya Shetani ikuachie bila mashaka yoyote, kazi hiyo ya Shetani itahama.

Mamlaka uliyopewa na Yesu ni kubwa mno. Unapolitumia Jina la Yesu, ni kwamba unamwakilisha Yesu mwenyewe k**a jinsi ambavyo askari wa Usalama Barabarani anavyoiwakilisha Serikali. Askari wa Usalama Barabarani anaponyosha mkono kuamuru gari kusimama, huwa hana mashaka ndani yake kwamba labda gari hilo litaendelea kwenda. Ni lazima dreva huyo atatii na kulisimamisha gari. Vivyo hivyo kwako, inakupasa kutoa mashaka unapomkemea Shetani kuhama; naye lazima atakutii [LUKA 10:17].

Unapokuwa pia ukiomba, kumbuka kukemea namna zozote za vizuizi vya Shetani juu ya majibu ya maombi yako. Shetani hutumia wakuu wake wa giza walio chini yake KUCHELEWESHA MAJIBU ya Maombi ya Watakatifu [ANGALIA MFANO KATIKA DANIEL 10:12-13].

Mungu awabariki Sana Sana

SHALOM 🙏

ONLY CHRIST CAN ACCOMPLISH IT WITHIN US!
AMEN.

04/09/2026

*SIKU YA NNE LEO!*

AGENDA ZA MAOMBI 🙏

✓Kushughulika na Misingi ya Maisha yako iliyoharibika

✓Kufungua Malango yako yaliyokuwa Yamefungwa kwasababu ya Misingi yako Kuharibika

1️⃣Kushughulika na Misingi ya Maisha yako Yaliyokuwa yameharibika na kufungwa na Adui

*K**a misingi ikiharibika,*
*Mwenye haki atafanya nini?*
(Zaburi 11:3)

👉 Inawezekana Misingi ya Maisha yako Imeharibika kwasababu ya Wazazi wako Kuabudu miungu mingine,Leo tunaiponya Kwa Jina la Yesu

✓Kwa Jina la Yesu Kristo, Ninafungua Misingi yangu ya ndoa,Kazi, Biashara,Uzao, Mafanikio yaliyokuwa yameharibika,na kufungwa na Adui

✓Ninatakaza Misingi yangu,

✓Ninakomboa Misingi yangu Kwa Damu Ya Yesu

✓Ninaachilia Uponyaji wa Ki-Ungu kwenye Misingi yangu, Kimaisha, Kiroho,Kiakili, Ki-Uchumi Kwa Jina la Yesu Kristo

✓Uponyaji kwenye Misingi ya AFYA

✓Uponyaji kwenye Misingi yangu ya ndoa

✓Uponyaji kwenye Misingi yangu ya Ki-Uchumi

✓Uponyaji kwenye Misingi yangu ya Kazi/Biashara

✓Uponyaji kwenye Misingi yangu ya Mahusiano

✓Uponyaji kwenye Misingi yangu ya Mafanikio

✓Naiweka Wakfu Misingi yangu Kwa Bwana Yesu, Kwasababu hiyo *Kila nitakalolifanya litafanikiwa sawasawa na Neno lake*
(Zaburi 1:3)

2️⃣ Kufungua Malango yako yaliyokuwa Yamefungwa kwasababu ya Misingi yangu Kuharibika

*Nifungulieni malango ya haki*
*Nitaingia na kumshukuru BWANA*

*Lango hili ni la BWANA,*
*Wenye haki ndio watakaoliingia*
(Zaburi 118:19-20)

✓Ninafungua Malango yangu Yote yaliyokuwa Yamefungwa na Adui

✓Ninachilia Ukombozi kwenye Malango yangu

✓Enyi Malango yangu Funguka kwaajili yangu Kwa Jina la Yesu Kristo

✓Nitaingia na Kupita kwenye Malango yangu Yote ya Mafanikio kwako

✓Malango ya Elimu, Malango yangu ya Uzao, Malango yangu ya Kiroho, Malango yangu ya Mafanikio,Funguka kwa Jina la Yesu Kristo

👉Asante Bwana Yesu *Nitakushukuru kwa maana umenijibu*
*Nawe umekuwa wokovu wangu sawa sawa na Zaburi 118:21*

Mungu awabariki sana,mnaposhiriki haya Maombi.

SHALOM 🙏

ONLY CHRIST CAN ACCOMPLISH IT WITHIN US!
AMEN.

03/09/2026

*JE, UNATAMBUA MAMLAKA TULIYOPEWA DHIDI YA NGUVU ZA GIZA?*

BWANA YESU KRISTO APEWE SIFA 🙏

LUKA 10
19 Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.

Shambulio lolote ambalo adui atalifanya huangukia katika moja ya njia zile au mikakati 4

Mkakati anaotumia kwa waamini ni majaribu k**a tulivyoona.

Mt 26:41.
Ushawishi wa dhambi unaotokana na tamaa. Msifanye dhambi dhidi ya tamaa maana adui siku zote yupo kutujaribu.
1Yohana 2:16
Imezungumzwa hapa tamaa ya mwili, tamaa ya macho, kiburi cha uzima ambayo havitokani na Baba bali vyatokana na dunia.

1. TAMAA YA MWILI.
Tamaa yoyote inayotokana na hisia ya mwanadamu kuonja, kugusa, kunusa, kuona kwake anaweza akajaribiwa.

Yesu anasema ili uweze kushinda uwe na kukesha na maombi ili Mungu aweze kuufanya mwili wako uwe mpya siku zote hata ujaribiwapo utashinda.

WARUMI 12
2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

2.TAMAA YA MACHO
Shetani anaweza kutumia tamaa ya macho kwa kile unachokiona kwa macho yako akakunasa.
Mfalme Daudi alishawishiwa na shetani kwa kumwona mwanamke aliye kuwa anaoga hata akaanguka dhambini.
Maarifa ndani ya ufahamu wako unabadilishwa.

AYUBU 31
1 Nilifanya agano na macho yangu; Basi nawezaje kumwangalia msichana?
Kile alichokiangalia kwa macho kina athari juu ya moyo wake au nafsi yake.

MATHAYO 5
28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.

Hivyo Ayubu alijua akakiepuka baada ya ku tafakari moyo ni mwake.
Adui anaweza kutumia macho yako ili a upate moyo wako.
Macho yako ya naona nini?
Kujiingiza katika dhambi juu ya unachokiona ni sawa na kuchukua hatua juu ya dhambi hiyo unayo iona.

Tatizo linaanzia kwenye macho na kushambulia moyo wako.
Chukua hatua.
Kikiingia kwenye macho yako moyo unaitikia na kufuata unachokiona.
Shetani anakushawishi kutenda dhambi nawe unamfuata ndipo Yesu anasema mkeshe mkiomba muwe macho msiingie majaribuni.
Shetani ni mbaya sana wengi wamepotea kupitia macho yao.

3.KIBURI CHA UZIMA
Dhana aliyonayo mtu kujiona yeye ni bora kuliko watu wengine amejitenga tu na wengine.
Kujiona bora kwa vitu vya duniani kuliko Mungu akiyekuumba.
Mungu anakuwa mbali na wewe kwa kuwa umethamini vitu vya kidunia.
Mali ni moja ya vitu ambayo mtu hujivuna navyo na kumsahau Mungu maana ndipo na moyo wako ulipo.
Shetani akikushinda anakuondoa kwenye nafasi uliyopewa na Mungu k**a alivyofanikiwa kumwondoa Adamu pale Bustani ya Edeni.

1 WAKORINTHO 10
13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.
Hivyo baki kwenye imani ili Mungu akupe njia ya kutokea kwa maana hanabudi kukujia ukiisha kuwa mkristo unasajiliwa kwenye ufalme wa mbinguni. Utapambana na kutoka katika mlango ambao Mungu atakufanyia.
Mlango wa kutoka katika ugonjwa, kazi, biashara uifanyayo kuna mlango kwa ajili yako.

Tuna njia ya kushinda majaribu maana kuna mlango ambao ni neno la Mungu. Tutashinda kwa kuwa Mungu yupo pamoja nasi tukeshe na kuomba Mungu yupo pamoja nasi siku zote.

UFUNUO WA YOHANA 12
11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.
Njaa, mapepo, umaskini, ugonjwa ni mpango wa shetani na Tutashinda kwa damu ya Yesu na neno la Mungu.

Shetani alimjaribu Yesu kule jangwani lakini alimshinda kwa neno la Mungu.
Bwana Yesu asifiwe sana mtu wa Mungu neno la Mungu ni boma, silaha juu ya hila za ibilisi kataa majaribu mshinde shetani.

SHALOM 🙏

ONLY CHRIST CAN ACCOMPLISH IT WITHIN US!
AMEN.

03/09/2026

*LEO SIKU YA TATU.*

AGENDA ZA MAOMBI NA KUFUNGA.

✓Maombi Ya Toba kwa Mungu

✓Kushughulika na roho ya mauti

✓Kushughulikia Siku ya Uovu ya kipepo

✓Kushughulikia Saa ya Mamlaka ya Giza Juu yako

1️⃣ Fanya Maombi ya Toba Kwa Mungu kwaajili yako,ndugu zako, Wazazi wako nk

*nikasema, Nakusihi, Ee BWANA, Mungu wa mbinguni, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, mwenye kutimiza agano lake na rehema zake kwa hao wampendao na kuzishika amri zake;*

*tega sikio lako, macho yako yakafumbuke, upate kuyasikiliza maombi ya mtumishi wako, ninayoomba mbele zako wakati huu, mchana na usiku, kwa ajili ya wana wa Israeli, watumishi wako; hapo ninapoziungama dhambi za wana wa Israeli, tulizozifanya juu yako; naam, mimi na nyumba ya baba yangu tumefanya dhambi*

*Tumetenda maovu mengi juu yako, wala hatukuzishika amri, wala sheria, wala hukumu, ulizomwamuru Musa, mtumishi wako*

*Nakuomba, likumbuke neno lile ulilomwamuru Musa, mtumishi wako, ukisema, Mkikosa, nitawatawanya kati ya mataifa;*

*bali mkinirudia mimi, na kuzishika amri zangu na kuzitenda, watu wako waliofukuzwa wajapokuwa katika pande za mwisho za mbingu, hata hivyo nitawakusanya kutoka huko, na kuwaleta mpaka mahali pale nilipopachagua ili kuliweka jina langu hapo*
(Nehemia 1:5-9)

2️⃣Kwa Mamlaka ya Jina la Yesu,Ninakufungua wewe, Pamoja na ndugu zako,na Kazi yako au Biashara yako kwenye orodha ya waliondikiwa kufa na Mamlaka ya Giza/Wachawi

👉Nabatilisha na Kutangua roho ya mauti na kuzimu Juu yako

*Na kuwafungua walioandikiwa kufa*
(Zaburi 102:20)

👉 Kemea roho za Mauti zinazojifunua Juu yako hata Kwa Njia ya NDOTO

👉Kiri na Kusema Ahadi hii ya Mungu kwenye Neno lake;

*Sitakufa bali nitaishi*
*Nami nitayasimulia matendo ya BWANA*
(Zaburi 118:17)

3️⃣Natangua na Kubatilisha Kwa Jina la Yesu Siku ya Uovu iliyoandaliwa kwaajili yako, kwaajili ya ndoa yako, kwaajili ya watoto wako, kwaajili ya familia yenu, kwaajili ya Wazazi wako

👉Naifuta hiyo Siku ya Uovu Juu yako kwa Kutumia Damu Ya Yesu Kristo

👉Tangaza Kwa Ujasiri Kabsa, Usiogope

*mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama*
(Waefeso 6:13)

4️⃣Nabatilisha na Kutangua,na kuifuta Saa ya Mamlaka ya Giza,Iliyoandaliwa kwaajili ya kukuaibisha,Kukutegeshea Ajali, Kukurudisha nyuma,Kuiba Mafanikio yako,

*lakini hii ndiyo saa yenu, na mamlaka ya giza*
*but this is your hour, and the power of darkness*
(Luka 22:53)

👉Ibilisi nakunyanganya hiyo saa, dakika,sekunde na kuiweka Wakfu Kwa Bwana Yesu

✅Endelea kuomba usizimie moyo na Bwana atatenda Sawa Sawa na Maombi yako!

SHALOM 🙏

ONLY CHRIST CAN ACCOMPLISH IT WITHIN US!
AMEN.

02/09/2026

MWONGOZO WA MAOMBI YA KUPINGA MAGONJWA, VIFO, AJALI NA UHARIBIFU KATIKA MAISHA YAKO.

BWANA YESU KRISTO APEWE SIFA 🙏

OMBA KWA SAUTI KUHUSU HITAJI LAKO.

1. Baba, katika jina la Yesu, naangusha kila mbinu/Mikakati, harakati,mitego,sayansi,nk za kishetani zinazozuia mafanikio yangu, katika jina la Yesu.RUDIA HATA MARA 7.USINYAMAZE!

2. Nakataa na kupinga magonjwa(YATAJE KWA SAUTI CHUMBANI KWAKO UKIOMBA) ya kila aina katika nyumba yangu na familia yangu, kwa jina la Yesu.RUDIA MARA 7 .KWA MAMLAKA

3. Imeandikwa katika Zekaria 2:8 ya kwamba “Yeye anayenigusa mimi anagusa mboni ya jicho la Mungu”, hivyo, ninalisimamia Neno hili na kupinga kila nguvu inayosababisha magonjwa,Afya kuvurugwa, Huduma umekaukiwa,huoni upenyo,unaonewa Kazini, uchumba,ndoa,Mtaje K**a mmeo/mkeo, watoto,madeni yamekuk**ata,uzazi kuzuiliwa, biashara, upotevu wa fedha zangu nk katika jina la Yesu.RUDIA HIVOHIVO KWA SAUTI,ZAIDI YA MARA 7

4. Nasimama kinyume na ajali na vifo katika familia yangu na ndugu zangu katika jina la Yesu.

5. Nawafunika watu wa familia yangu, kijiji changu na nje ya kijiji kwa damu ya Yesu,Ukuta wa Moto,na malaika wawalinde na kuwaongoza kila mmoja kwa jina la Yesu.RUDIA..... KWA SAUTIII YA MAMLAKA.....

6. Ninaamuru kila kinachoharibu,kuziamtaji na biashara yangu kufa mara moja,elimu, Mahusiano,kazi,ndoa ONGZEAA WEWE MENGINE, katika jina la Yesu.RUDIA.......

7. Ninaificha fedha yangu yote,Ndoa yangu, uchumba, familia,nk ONGEZAA katika damu ya Yesu na kamwe adui hawezi kuigusa.RUDIAA.

8. Baba, katika jina la Yesu, nasimama katika Neno k**a mtoto wa Mungu niliyeketishwa mahali pa juu pamoja na Kristo, na ninatangaza kuwa mikutano ya kipepo,vikao, mijadala, Mikakati, Ratiba mbaya, ONGEZEA,juu ya maisha yangu na fedha yangu haitafanikiwa, katika jina la Yesu.RUDIAAA KWA SAUTI.

9. Namfunga mwenye Nguvu (Askari wa Kipepo) sawasawa na Mathayo 12:29,,,Soma hapo Kwa SAUTIII,mfunge Kisha AMURU atoke,,,kila anayeharibu fedha yangu nyumbani na sehemu yangu ya kazi,nk katika jina la Yesu.RUDIAAA .......ZAIDI YA MARA 7.....KWA NGUVUUU

10. Wewe pepo,MTAJE KABISA,BALISHEBE NA AHERUMI HULETA HOMA ZA MARAKWAMARAAA NA MAGONJWA YASIYOPONA,MAIMUNA NA BARADI-HUVUNJA NDOA,MURAFARI NA JOHARI WA CHUMA ULETE,HUZUIA BIASHARA ISINAWIRI, MAFANIKIO,KUIBA MALI,PESA ZAKO,JUBE NA SUMIL HULETA UTASA NA KUUA MIBA CHANGA,SUBIANI HULETA AJALI,HUNYWA DAMU SIKU ZA HEDHI UNASIKIA MAUMIVU MAKALI SANA,,MAKATA HULETA VIFO VYA GHAFLA MFULULUZO KILA MARA KWA FAMILIA,,,,,WAPO WENGI NITAWALETEA,,KAGUA ENEO LAKO UNAPOTESWAA uliyetumwa kuharibu biashara na fedha zangu, ninakufunga na kukutupa kwenye shimo la giza katika jina la Yesu.

11. Ninaamuru moto wa Roho Mtakatifu kumlamba kila mmoja aliyesimama kinyume na biashara na mafanikio yangu katika jina la Yesu.

12. Ewe mlima uharibio, ninakuangusha na nianaamuru usambaratike, katika jina la Yesu. 13. Ninaificha biashara, ofisi, fedha na miradi yangu yote katika damu ya Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliye hai. Amen.

14. Bwana, ninaomba upendeleo wako katika maisha yangu ili niweze kufanikiwa.

15. Upendeleo wako unizunguke kadiri ya Neno lako, katika jina la Yesu.

16. Bwana, naomba kuunganishwa na watu watakaonisaidia kufikia ndoto zangu kwa jina la Yesu.

17. Oh, Bwana, naomba ufanye njia kwa ajili yangu hata pale pasipo na njia katika jina la Yesu.

18. Baba, naomba niunganishe na mtu ambaye atakuwa msaada mkubwa katika kuyafikia mafanikio yangu katika jina la Yesu. 19. Baba ninaamini ya kwamba kila ninapokanyaga ninapamiliki sawasawa na na Neno lako, hivyo naomba univike vazi lako la upendeleo katika jina la Yesu.

20. Asante Bwana Yesu kwa kuwa umefanya sawasawa na nilivyokuomba katika jina la Yesu.

RUDIIIAA SANA KIPENGELE CHAKOOO MARA NYINGI TUUU HADI UMEPONAA,,,NAAMINI UMEFUNGULIWA NA UMEELEWA WAPI SHIDA YAKO ILIPO, UMEJIELEWA UNAPOTESWAA

SHALOM 🙏🙏

ONLY CHRIST CAN ACCOMPLISH IT WITHIN US!
AMEN.

02/09/2026

*HATUA MUHIMU ZA KUFUATA ILI UOMBEE IPASAVYO NDOTO ULIZOOTA UNAVYALISHWA PETE.*

BWANA YESU KRISTO APEWE SIFA 🙏

HATUA YA KWANZA

*OMBA TOBA KWA MUNGU MLANGO KUFUNGUKA NA UKAPATA HIYO SHIDA, SHIDA INAYOTOKANA NA HIYO PETE*

Biblia inakupata kibali, ukiwa kuhani kuomba Toba hata kwa dhambi usizozijua hivyo usijiulize sana maswali mengi wewe omba toba.

*Waebrania 9:7*
_“Lakini katika hema hiyo ya pili kuhani mkuu huingia peke yake, mara moja kila mwaka; wala si pasipo damu, atoayo kwa ajili ya nafsi yake na kwa dhambi za kutokujua za hao watu.”_

HATUA YA PILI
*NYUNYIZA DAMU YA YESU JUU YA ENEO ULILOLIONA LA HIYO PETE KWENYE NDOTO*

Maana hiyo ni ishara, k**a umeona kwenye kidole angalia ni kidole kipi na ushike hicho kidole kuanza kunyunyiza DAMU YA YESU.

*Waebrania 12:24*
_“na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.”_

Na unaponyunyiza jifunze kusema k**a vile Musa alivyokuwa anasema wakati ananyunyiza. Usinyunyize kawaida kawaida tu maana waweza usione matokeo uliyotarajia. Kitabu cha Waebrania kinatupa utaratibu wa kunyunyiza.

*Waebrania 9:19-22*
_“Maana kila amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa hao watu wote, k**a ilivyoamuru sheria, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu na hisopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote, *akisema, Hii ni damu ya agano mliloamriwa na Mungu.* Na ile hema nayo na vyombo vyote vya ibada *alivinyunyizia damu vivyo hivyo.* Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.”_

Alikuwa akitumia damu ya mbuzi na kondoo au ile ya ndama. Heshima ya damu hizi zilikuwa ni kwa sababu ya neno la agano la kipindi kile. Agano jipya lilipokuja ile damu ilipoteza heshima yake, ilipoteza kibali chake kwenye madhabahu ya MUNGU maana yake haiwezi kusema kwa niaba ya watu, ila kwenye nguvu za giza bado ina kibali huko. Ni DAMU YA YESU pekee iliyomwagika na ndiyo maana YESU pia alisema wakati akizungumza kwa habari ya _“kikombe hiki”_ alisema ni DAMU YA AGANO hakusema tu ni damu yangu, alihakikisha amesema neno agano kwa sababu unaiwekea hadhi kubwa inayostahili.

Kwa hiyo k**a ni kidole chako ndo kwenye hiyo pete sema: _“Nanyunyiza DAMU YA YESU YA AGANO iliyomwaga na YESU pale msalabani inenayo maneno mazuri kuliko ile ya Habili juu ya eneo hili ambalo niliona kulikuwa na pete”_

HATUA YA TATU
*NG’OA HIYO PETE KWA DAMU YA YESU*

*Yeremia 22:24*
_“K**a niishivyo mimi, asema BWANA, hata Konia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, angekuwa pete yenye muhuri katika mkono wangu wa kuume, ningekung’oa wewe hapo;”_

Lazima ing’olewe na ndiyo maana shetani anajaribu kung’ang’ana kwa jinsi ya kiroho kuizuia hiyo pete ya kiroho isitoke. Ukishaing’oa shetani hatakuwa na mahali pa kukaa wala kuwana uhalali wowote.

Kumbuka pete inawakilisha nafasi ya kukaliwa hapo na kitu fulani na ndiyo maana haitoshi tu kusema unanyunyiza DAMU YA YESU ni lazima utamke na kuing’oa haijalishi unaiona au huioni.

Jifunze kuing’oa hiyo pete maana wakati mwingine ukinyunyiza DAMU YA YESU mapepo ulipuka na kuanza kusumbua maana yanajua hatua inayofuata ni kung’oa hivyo waweza ishia kukemea pepo na pete hukung’oa.

HATUA YA NNE
*KEMEA SASA PEPO KWA JINA LA YESU*

HATUA YA TANO
*OMBA UPONYAJI KWENYE MAENEO YALIYOPATA SHIDA KATIKA KIPINDI ULICHOKUWA NA HIYO PETE*

Unaweza kujiuliza maeneo gani? Kuna wengine ambao wakiwa na pete za namna hiyo wanakuwa wamefungishwa ndoa za kipepo kwa hiyo wanajikuta wanazini tu na watu wasiowajua au wanaowajua kwenye ndoto, na ukishaona namna hiyo ujue kuna madhara fulani kwenye kizazi chako ambayo huwezi kujua ibilisi amepandikiza kitu gani kwa hiyo ni lazima kuomba uponyaji.

HATUA YA SITA
*OMBA ULINZI WA DAMU YA YESU KWENYE MAENEO MBALIMBALI HASA HILO ENEO ULILOONA LILIKUWA NA PETE*

Maana eneo hilo inamaanisha ya kwamba kuna kitu adui aliweka hapo k**a ishara ya agano na uwe na uhakika anaweka na mapepo yake ya ulinzi ili kukuvuruga hasa unapoota ndoto za namna hiyo uende kutafuta msaada mahali ambapo watazidi kukuongezea mapepo mengi zaidi

Achilia DAMU YA YESU juu ya kutumia mistari ya Biblia ili kukupa ufahamu ambao MUNGU anataka uwe nao ndani yako.

DAMU YA YESU kazi yake ni kumulika NENO na kukuonyesha kilichopo ndani ili usihangaike kubahatisha kwenda ama kuchimba mstari huu ukakosa na kwenda mwingine ukakukosa ama kutokuona kitu. Jifunze kunyunyiza DAMU YA YESU kwenye huo mstari na ukishanyunyiza kazi ya DAMU hiyo ni kufungua hayo makofuli na yaliyopo ndani ili kukuonyesha moja kwa moja unachotakiwa kukipata.

Mungu awabariki Sana Sana

SHALOM 🙏

ONLY CHRIST CAN ACCOMPLISH IT WITHIN US!
AMEN.

02/09/2026

*MAOMBI KATIKA SIKU YA PILI.*

BWANA YESU KRISTO APEWE SIFA 🙏

●FUFUA MAMBO YALIYOKUFA MAISHANI MWAKO NA KWENYE FAMILIA YAKO.

>>Shetani anaweza kuua mambo ya mtu.

"Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele." Yohana 10:10.

"The thief cometh not, but for to steal, and to kill, and to destroy: I am come that they might have life, and that they might have it more abundantly." John 10:10 ( KjV)

>>MUNGU pia anaweza kufufua mambo ya mtu ndiyo sababu ameweka Roho ya Ufufuo ndani ya mtu.

"Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu." Warumi 8:11.

ya maeneo mtu anaweza kufufua k**a yamekufa.

1.KUFUFULIWA KIROHO .

"Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika;Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa." Ufunuo 3:1

Mwilini unaonekana una uhai kumbe rohoni umekufa kabisa.

"Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake." Ezekieli 18:20.

Dhambi na uovu na kutokujifunza Neno la Mungu huua hali ya kiroho ya mtu.

》》》》Ili ufufuke hapo Omba maombi haya:-

i).Omba toba na msamaha kwa Mungu popote ulipoishi maisha yasiyompendeza MUNGU. ( Ufunuo 3:3).

ii).Omba Mungu akupe Neema ya kukesha ili kuimarisha hali yako ya kiroho iliyo katika kufa ( Ufunuo 3:2).

iii).Omba Mungu aliandike jina lako kwenye kitabu cha uzima na kukufufua.( Ufunuo 3:5).

iv) Omba Mungu akulishe Neno lake kwa kukufundisha ili uishi hai kiroho( Mathayo 4:4).

B. KUFUFULIWA KIUCHUMI.

Ibrahimu alikuwa na visima vyake 4 vilivyomsaidia kiuchumi , aivyovitumia kwenye kilimo chake cha Umwagiliaji na kwenye kunyweshea mifugo YAKE. Lakini Maadui zake walikifukia.Ibarahimu alipokufa maadui wakavifukia.

" Isaka akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Ibrahimu babaye; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Ibrahimu; naye akaviita majina kufuata majina alivyoviita babaye." Mwanzo 26:28

"Adui kazi yake ni kuua tu"

Alipofukia visima unafikiri mifugo haikufa?,maana alikuwa na mifugo maelfu, Kilimo cha umwagiliaji hakikufa? ,Mazingira ya watu waliotegeme hayo maji je?

Isaka alipokuja aifuatilia miradi ya baba yake akaanza kuvifukua visima,akayafanya Maono ya baba yake yaishi tena.

LEO KWENYE AGANO TULILO NALO HALITOI TENA MAJI YA KAWAIDA BALI YANATOKA YALE MAJI YA UZIMA. ( YESU ANAMWAMBIA MWANAMKE MSAMARIA PALE KISIMANI. Yohana 4)

MAOMBI:
1.Fukua kila kisima chako kilichofukiwa ( Iwe ni biashara/kazi/miradi n.k Fukua .

2.Mwondoe kila adui aliyefukia .

3.Omba Mungu aachilie uzima wake kwenye Kila jambo lako lililo katika kufa.( Ufunuo 3:1-6)

4.Omba Mungu Mambo mengine yaliyo katika kufa lakini bado hayajafa Mungu ayanusuru yasife. ( ufunuo 3:1-6)

C.FUFUA AFYA YAKO ILIYO KATIKA MAGONJWA NA HALI YA KUFA.

"Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema BWANA, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye." Yeremia 30:17

EZEKIELI 37:1-9

Mlango 37

1 Mkono wa BWANA ulikuwa juu yangu, naye akanichukua nje katika roho ya BWANA, akaniweka chini, katikati ya bonde; nalo limejaa mifupa;
2 akanipitisha karibu nayo pande zote; na tazama, palikuwa na mifupa mingi katika ule uwanda! Nayo, tazama, ilikuwa mikavu sana.
3 Akaniambia, Mwanadamu, je! Mifupa hii yaweza kuishi? Nami nikajibu, Ee Bwana MUNGU, wajua wewe.
4 Akaniambia tena, Toa unabii juu ya mifupa hii, uiambie, Enyi mifupa mikavu, lisikieni neno la BWANA.
5 Bwana MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama, nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi.
6 Nami nitatia mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, na kutia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
7 Basi nikatoa unabii k**a nilivyoamriwa; hata nilipokuwa nikitoa unabii, palikuwa na mshindo mkuu; na tazama, tetemeko la nchi, na ile mifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa mwenziwe.
8 Nikatazama, kumbe! Kulikuwa na mishipa juu yake, nyama ikatokea juu yake, ngozi ikaifunika juu yake; lakini haikuwamo pumzi ndani yake.
9 Ndipo akaniambia, Tabiri, utabirie upepo, mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana MUNGU asema hivi; Njoo, kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi, ukawapuzie hawa waliouawa, wapate kuishi.

■Tabiri juu ya Afya yako ( Amini Mungu anaweza kufanya).

1.Iambie ( Isemeshe) Afya yako kuwa inaweza kuishi tena. ( 37:4-5)

2.Omba pumzi ya Mungu uje juu ya mifupa na afya yako ( 37:5)

3.Ombea viungo vya mwili wako ( Ezekieli aliomba juu ya mifupa/mishipa&ngozi),K**a kuna kiungo hakipo Vizuri omba kipya tabiri juu ya kiungo kipya. ( 37:6-7)

4.Omba viungo vyako vifanye kazi kwa ushirikiano ( Ezekieli aliomba mifupa isogeleane maana ilikuwa mbali mbali) 37:7

5.Itoe Afya yako kaburini ( 37:12)

6.Rejesha afya yako yote ( Yeremia 30:17)

"Afya yako ndiyo mafanikio yako" 3Yohana 1:1-3)

Hakikisha unasoma na unaomba ukiwa na Imani thabiti kwa Bwana Yesu Kristo .

SHALOM 🙏🙏🙏

ONLY CHRIST CAN ACCOMPLISH IT WITHIN US!
AMEN.

02/09/2026

SIKU YA PILI

MAOMBI MAALUM KWA SIKU 21

▪️PAMOJA NA MFUNGO WA MASAA 12HRS.

Tarehe 1 - 21 September.

✅Kuanzia saa 12:00Asubuhi Hadi saa 12;00 jioni

AGENDA;
✅Kufungua Maeneo yaliyofungwa kwenye maisha Yako;

Inawezakana ;

✓Uchumi wako,umefungwa ,au

✓Ndoa Yako imefungwa ,au

✓Watoto wako wamefungwa na Tabia mbaya,au

✓Umefungwa wewe mwenyewe usipate Kazi,au

✓Umefungwa usiolewe)Usioe,au

✓Tumbo lako la Uzazi limefungwa! Au

✓Kibali chako kwenye maisha Yako Kimefungwa,Au

✓Madeni yamekufunga!

Tushughulike na hivyo vifungo!

*Enendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mara mtaona punda amefungwa, na mwana-punda pamoja naye; wafungueni mniletee*
(Mathayo 21:2)

✔️K**a vile huyu punda Yesu alivyoagiza afunguliwe pamoja na Mwana punda, Yesu akufungue na wewe pamoja na familia yako na vyote vilivyo vyako ambavyo vimefungwa na adui,au na miungu mingine ya familia yenu!

*Mfalme alituma watu akamfungua,
Mkuu wa watu akamwachia*
(Zaburi 105:20)

Na Yesu ni Mfalme,Amelituma hili Neno kwako ili Apate Kufungua ulikofungwa!

KABLA YA KUANZA KUOMBEA HIYO AGENDA FAHAMU MAMBO YAFUATAYO;

✅Huwezi kujifungua kutoka kwenye kifungo chochote ambacho hukijui.

✔️Na huwezi kujua kilichokufunga k**a huijui sheria iliyokufunga katika ulimwengu wa roho.

✅ Na huwezi kujifungua k**a hujui sheria inayoweza kuitangua ile sheria iliyokufunga katika ulimwengu wa roho.

✅Na huwezi kujifungua k**a hujui kipengele au vipengele vilivyoko katika ile sheria ambayo shetani ametumia kufunga Maisha/mafanikio yako.

✅Lazima ujue pia kuwa Kuna kufungwa kihalali kabsa na shetani/Ibilisi

*Je! Aliye hodari aweza kunyang'anywa mateka yake, au jeshi lao waliofungwa halali wataokoka?*
(Isaya 49 :24)

✅Na kuna Kufungwa kwa Kuonewa tu na shetani/Ibilisi

"" habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote *walioonewa na Ibilisi;* kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.
(Matendo ya Mitume 10 :38)

Kwahiyo kabla hujaomba Mungu akufungue Vifungo vyako

*1️⃣FAHAMU KWANZA WAPI UMEFUNGWA?*

*2️⃣UMEFUNGWA KIHALALI AU KWA KUONEWA??*

Ndipo Uanze Kuomba sasa!

✔️Uwe mwaminifu kuomba popote pale ulipo,
Omba Kadri ya Neema uipatayo na Roho Mtakatifu atakuongoza.

✅Tafuta mahali Jifungie,Uombe!

✅Asubuhi Omba,
▪️Mchana Omba,
▪️Jioni Omba!

Mungu akufungue mahali Ulikofungwa!

SHALOM 🙏🙏

ONLY CHRIST CAN ACCOMPLISH IT WITHIN US!
AMEN.

Address

Usa River

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when George ABEL Mwache posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to George ABEL Mwache:

Shortcuts

Share