St.Thomas Angelican Church Mpiji Magoe DSM TZ

St.Thomas Angelican Church Mpiji Magoe DSM TZ Spritual and worship services

Picha mbalimbali ktk Misa ya Pasaka 2026
12/04/2026

Picha mbalimbali ktk Misa ya Pasaka 2026

We wish you Mary Christmas all
25/12/2025

We wish you Mary Christmas all

Kumbukizi ya matukio mbalimbali katika sikukuu ya Mikael na watoto 2025. Mt Thomas St.Thomas Angelican Church Mpiji Mago...
05/10/2025

Kumbukizi ya matukio mbalimbali katika sikukuu ya Mikael na watoto 2025. Mt
Thomas St.Thomas Angelican Church Mpiji Magoe DSM TZ ,utukufu ni Kwa Mungu Alie hai

05/10/2025
13/10/2024

Luka 14:16-24
16 Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa akaalika watu wengi,

17 akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale walioalikwa, Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari.

18 Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe.

19 Mwingine akasema, Nimenunua ng'ombe jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe.

20 Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja.

21 Yule mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete.

22 Mtumwa akasema, Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa ingaliko nafasi.

23 Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa.

24 Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu.
*Wazo kuu utayari wa kuitika*
Jumapili njema

Njia ya Msalaba
29/03/2024

Njia ya Msalaba

Je, vituo vya Msalaba ni nini, na tunaweza kujifunza nini kutoka kwao? Ni Njia gani ya Maandiko ya Msalaba?

Mungu ni mwema sana, tunawashukuru waumini Mt. Thomas na wadau wengine wa maendeleo. Tumefika hapa kwa nje. Mungu ni mwe...
09/12/2022

Mungu ni mwema sana, tunawashukuru waumini Mt. Thomas na wadau wengine wa maendeleo. Tumefika hapa kwa nje. Mungu ni mwema mwisho wa mwezi inaweza wekwa Wakfu. Ingawa bado fedha zinahitajika kwaajili ya fensi nk.

30/10/2022

Luka 9:57-62
[57]Nao walipokuwa wakienda njiani, mtu mmoja alimwambia, Nitakufuata ko kote utakakokwenda.
And it came to pass, that, as they went in the way, a certain man said unto him, Lord, I will follow thee whithersoever thou goest.
[58]Yesu akamwambia, Mbweha wana pango, na ndege wa angani wana viota, lakini Mwana wa Adamu hana pa kujilaza kichwa chake.
And Jesus said unto him, Foxes have holes, and birds of the air have nests; but the Son of man hath not where to lay his head.
[59]Akamwambia mwingine, Nifuate. Akasema, Bwana, nipe ruhusa kwanza niende nikamzike baba yangu.
And he said unto another, Follow me. But he said, Lord, suffer me first to go and bury my father.
[60]Akamwambia Waache wafu wawazike wafu wao; bali wewe enenda ukautangaze ufalme wa Mungu.
Jesus said unto him, Let the dead bury their dead: but go thou and preach the kingdom of God.
[61]Mtu mwingine pia akamwambia, Bwana, nitakufuata; lakini, nipe ruhusa kwanza nikawaage watu wa nyumbani mwangu.
And another also said, Lord, I will follow thee; but let me first go bid them farewell, which are at home at my house.
[62]Yesu akamwambia, Mtu aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa Mungu.
And Jesus said unto him, No man, having put his hand to the plough, and looking back, is fit for the kingdom of God.

Jumapili ya Mitende imekuwa ya Baraka sana, Misa ikiongozwa na Baba Canon Mwamazi, Mungu aendelee kukupa Afya njema na M...
05/04/2020

Jumapili ya Mitende imekuwa ya Baraka sana, Misa ikiongozwa na Baba Canon Mwamazi, Mungu aendelee kukupa Afya njema na Maisha Marefu, Amin

Ndipo neno la Bwana lilikuja kwa kinywa cha nabii Hagai, kusema, 4 Je! Huu ndio wakati wa ninyi kukaa katika nyumba zeny...
05/09/2019

Ndipo neno la Bwana lilikuja kwa kinywa cha nabii Hagai, kusema,
4 Je! Huu ndio wakati wa ninyi kukaa katika nyumba zenye mapambo ya mbao, iwapo nyumba hii inakaa hali ya kuharibika?
5 Basi sasa, Bwana wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu.
6 Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji; mnajivika nguo lakini hapana aonaye moto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka-toboka.
Bwana wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu.
8 Pandeni milimani, mkalete miti, mkaijenge nyumba; nami nitaifurahia, nami nitatukuzwa, asema Bwana.
9 Mlitazamia vingi, kumbe vikatokea vichache; tena mlipovileta nyumbani nikavipeperusha. Ni kwa sababu gani? Asema Bwana wa majeshi. Ni kwa sababu ya nyumba yangu inayokaa hali ya kuharibika, wakati ambapo ninyi mnakimbilia kila mtu nyumbani kwake.
Tunamshukuru Mungu kwa hatua nzuri tulio fikia, ndoto na kiu ya Wakristo kuwa na kanisa nzuri kwaajili ya Utukufu wa Mungu inakaribia.
Tunawashukuru wanaojitoa kwaajili ya baraka hizi za Mungu. Bado Tiles chini box moja ni 25,000/=, sement mfuko 14,000, tunahitaji feni k**a sio AC, tunahitaji madirisha ya Aluminium, na vifaa vya madhabahuni, ukitaka kushiriki baraka hizi usikose kuwasiliana nasi, Mungu hata kuacha hivi hivi, Mungu wetu ni mwaminifu sana.
Mawasiliano 0753283004 Katibu wa kanisa.
Ahsante

Address

Ubungo

Telephone

+255658283004

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when St.Thomas Angelican Church Mpiji Magoe DSM TZ posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share