24/09/2021
>Kuzimu na uharibifu havishibi, wala macho ya wanadamu hayashibi. MITHALI 27:20.< Hivi kwa nini Neno la Mungu linasema kuwa 'kuzimu haishibi'. Hivi ni kweli haishibi? Ndiyo haishibi! Sasa k**a hiyo kuzimu haishibi inakula nini ambacho hakiwezi kuishibisha? Ni roho za wanadamu wanaokufa na dhambi, au kwa maneno mengine ni roho za wanadamu wanaofariki dunia bila Mungu wa kweli, au kwa maneno mengine ni roho za watu wanaokufa bila wokovu na utakatifu wa kweli, au kwa maneno mengine Ni roho za wanaomaliza mwendo ambao hawakupitia njia nyembamba na mlango mwembamba. Kwa lugha ya maneno machache ni kwamba, ni roho za waliokufa bila Yesu. Lakini sio kwamba hiyo kuzimu inakula hizo roho, hapana! Bali kuzimu inazipokea tu na kuzihifadhi hizo roho katika vyumba au mashimo yao kuisubiria siku ya mwisho ambapo roho hizo zitatupiwa katika ile jehanam. Nani anazipokea hizo roho huko kuzimu, na zinapohifadhiwa zinakuwa katika Hali gani? Ni shetani na malaika zake ndio wanaozipokea hizo roho huko kuzimu, na roho hizo zinakuwa katika Hali ya kuumizwa na kuteswa daima ndani ya selo au vyumba au mashimo yao. Kwani kuzimu kuna vyumba au mashimo? Ndiyo kuna vyumba ambavyo pia vinatajwa kwamba ni mashimo, hebu kumbuka kwamba neno linaposema kwamba 'mtu anayechimba shimo atatumbukia mwenyewe'. Mashimo yanayomaanishwa na neno la Mungu sio haya tunayoyajua, tunayoweza kuyachimba kwa jembe au sululu, laa, Ni hayo ya huko kuzimu. Sasa mtu anawezaje kuchimba shimo lake huko kuzimu wakati mtu yupo duniani bado hajafa? inawezekana kweli! Ndiyo inawezekana mtu akachimba shimo lake huko kuzimu ili hali bado yuko duniani anaishi. Mmm! kwa namna gani? Kwa kuishi maisha ya dhambi. Kila mwanadamu anayeishi maisha ya dhambi na kutokumjali Mungu anajichimbia shimo lake huko kuzimu. Tunapotenda dhambi moja tu bila kuitubia, tayari tumepeleka kifaa muhimu huko kuzimu ili kufanikisha shimo letu. Kinyume chake Ni kwamba, kwa wale watakatifu walioko duniani, wanapotenda tendo moja jema, tayari wamepeleka kifaa muhimu huko mbinguni ili kufanikisha nyumba zao kujengwa. Mbinguni kuna nyumba za watu zinazojengwa? Ndio zipo zinajengwa, ila mtu wa Mungu anapomaliza mwendo, anapoondoka duniani, naam anapokata roho tu, ile nyumba yake inaishia palepale haiendelei kujengwa, na akifika mbinguni ataikuta imeishia palepale sawa sawa na matendo yake mema aliyoyafanya duniani. Hapo kuna mengi ya kufahamu, lakini hebu turudi kule kuzimu. Sasa yale mashimo huko kuzimu yako mangapi na yana ukubwa kiasi gani tofauti yake ni nini kati ya shimo na shimo? Jibu ni kwamba, hayo mashimo makubwa ya jumla jumla yako 351, ambayo hayo ndani yake kuna vyumba ama vishomo vidogo vidogo visivyo na idadi vinavyoingia roho moja moja. Ukubwa wa shimo moja la jumla Ni k**a bara la Afrika ukichanganya na bara Asia ndiyo ukubwa wake. Sasa hebu fikiri ukubwa wa kuzimu na mashimo yake, na katika kitabu cha Isaya Kuna mahali neno linasema kuzimu inazidi kutanuka / kuongezeka. Sasa roho zote zinazotumbukia kuzimu zinapotea milele, ambalo Ni Jambo la kutisha sana kwa kweli. Hebu kumbuka ilivyoandikwa katika YOHANA 3:16. Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanae wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee Bali awe na uzima wa milele. Sasa neno linaposema,' asipotee' yaani asiende kuzimu, awe na uzima wa milele, yaani aende mbinguni. Nini tofauti kati ya shimo na shimo huko kuzimu? Tofauti ni tofauti iliyopo kati ya dhambi na dhambi, kwa hiyo basi, kuna shimo la dhambi ya uongo, Kuna shimo la dhambi ya uchawi, kuna shimo la dhambi ya ulevi, Kuna shimo la dhambi ya uzinzi na uasherati, kuna shimo la dhambi ya kutolipa zaka na sadaka, kuna shimo la dhambi ya kutolipa madeni na kutotimiza ahadi, nk mpaka yanafika mashimo 351. Asante, barikiwa Sana. . .