Kanisa La Sauti Ya Kalvari Tanzania

Kanisa La Sauti Ya  Kalvari Tanzania Huduma ya SAUTI YA KALVARI. Ni huduma iliyo anzishwa na mchungaji na mwalimu Daudi Missoji Malulu.

20/01/2026

*Hiyo mistari ni lugha ya picha Kwa kizazi chetu na kanisa.*

Ukitafakari maisha yetu vijana tulio *okoka* utagundua kuwa Huwa tunavutiwa sana na namna ya ulimwengu huu.
Mtindo wa maisha.
Mavazi na muonekano.
Miziki pamoja na nyimbo lakini pia hata wapo vijana ndani ya kanisa wanaowatamani mabinti nje ya kanisa.
Na mabinti vivyo hivyo wapo wanao watamani vijana wakiume nje ya kanisa.

Kituambacho ni hatari
Ukisoma hapo utaona Mungu anakasirika alafu nik**a anaamua kumuacha mwanadamu Sasa afanye anavyotaka.

Usikubali Mungu akuache ufanye unavyotaka. Tamani kuongozwa na Mungu.

19/01/2026

*Utangulizi wa kitabu Cha mwanzo sura ya kwanza Hadi ya tatu.*

Tunajifunza mambo mengi hapo kwenye sura hizo. Lakini yapo mambo kadhaa tutakayoyafafanua.

1. Mungu ni wa utaratibu. Kila jambo limefanyika Kwa mpangilio.
2. Mungu hufanya kazi timilifu Kwa wakati. Ukisoma utaona Mungu nafanya jambo Fulani Kwa wakati Fulani na linakamilika bila mapungufu. Kesho anaanza jambo JIPYA na linakamilika pia
3. Mungu huandaa mazingira kwanza kabla ya kumuweka yeyote Mahali popote. _Ukisoma utaona Mungu alituandalia mazingira kabla ya kutuweka_
4. Mungu alimuumba mtu Ili akatawale.
5. Mungu alimuumba mtu alimuumba mwanamume na mwanamke
6. Uumbaji ulifanyika kwanza katika ulimwengu wa Roho ndio ukaja katika ulimwengu wa mwili Sura ya 2
7. Tunaona Mungu anampa AGANO adamu na namna ya kuishi.
8. Tunasoma katika sura ya 3 na kuona anguko na dhambi inaanza baada ya adamu kuasi AGANO LA MUNGU.
9. Ahadi ya kuja Kwa Yesu inaanza kupatikana hapa sura ya tatu anaposema uzao wa mwanamke utamponda nyoka kichwa. Na tunajua uo uzao wa mwanamke ni YESU KRISTO.
Jamani ni watie moyo TUSOME na badae tushirikiane pamoja kuchangia.

16/01/2026

https://chat.whatsapp.com/JKi1XvFPzrv5BAoQc0KR3t

Karibu HUB OF HOPE TUSOME BIBLIA PAMOJA

Tukiwa mwanzoni kabisa mwa mwaka 2026. Nikukaribishe tushirikiane kuisoma BIBLIA nzima Kwa pamoja.
Jiunge nasi k**a moyo wako uko tayari kutoa sadaka ya muda kwaajili ya kumfahamu Mungu

Address

P. O BOX TANGA
Tanga

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kanisa La Sauti Ya Kalvari Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Kanisa La Sauti Ya Kalvari Tanzania:

Shortcuts

Share