20/11/2017
MWANADAMU K**A JENEZA
Fungu kuu:- Akakaribia, akaligusa jeneza; wale waliokuwa wakilichukua wakasimama. Akasema, kijana, nakuambia Inuka. Luka 7:14
Sifa za jeneza
Jeneza hutengenezwa kwa mbao, na misumari huku likipakwa vanishi au rangi mbali mbali nzuri za kuvutia.
Kuna mengine yenye thamani kubwa hunakishiwa kwa madini yenye thamani kubwa k**a dhahabu na hutumiwa na watu matajiri wakubwa Duniani.
Mengine kwa ndani huwekewa sponge na vitambaa raini vyeupe kulifanya lipendeze zaidi.
Kwasasa mtu kuzikwa bila jeneza huonekana k**a kumdhalilisha marehemu.
Lakini pamoja na kupambwa kote huko Jeneza hubeba Maiti.
Kwa wakristo majeneza hufukiwa ndani ya makaburi lakini kwa waislamu marehemu hutolewa ndani ya jeneza baada ya kufika eneo la kuzikia.
Neno jeneza ndani ya Biblia limeoneka mara mbili pekee ambapo sehemu ya kwanza ni katika 2Samweli 3:31 “Kisha Daudi alimwambia Yoabu, na watu wote waliokua pamoja naye, Rarueni nguo zenu, mkajivike nguo za magunia, mkamlilie Abneri. Naye mfalme Daudi akaifuata jeneza.”
Na sehemu ya pili ni katika Luka 7:14 “Akakaribia, akaligusa jeneza; wale waliokuwa wakilichukua wakasimama. Akasema, kijana, nakuambia Inuka.”
Kwanini mwanadamu k**a jeneza?
Yakobo 2:17 “Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo imekufa nafsi mwake” imani inapaswa kuwa hai ndani ya mwanadamu ili itende kazi lakini imani isipo kua hai imekufa kabisa (Maiti).
Imani ambayo iko hai ikoje?
Yakobo 2:14 “Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani lakini hana matendo? Je! Ile imani yaweza kumwokoa? Ukweli ni kwamba huwezi kusema mtu yuko hai ikiwa hana matendo ndani yake, wanasayansi wanazo sifa kuu nane za viumbe hai ambazo ni:-
Movement/locomotion (kutembea/kujongea). Imani haipaswi kukaa sehemu moja ni lazima itoke kufanya kazi. Yakobo 1:27 “Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.” Fungu hili linatuambia dini yenye imani hai sio kukaa sehemu moja na kumuabudu Mungu bali pia kwenda kuwatazama wasio jiweza.
Irritability/sensitivity (kuhisi). Imani iliyo hai ni lazima ihisi uwepo wa Mungu katika maisha ya mwanadamu. Yohana 20:29 “Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki.
Feeding/Nutrition (kula). Imani ili iwe hai nilazima ile chakula ambacho ni mkate wa uzima yaani maandiko matakatifu. Amosi 8:11 “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa ya kukosa chakula, wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya Bwana”.”
Respiration (upumuaji). Ili mtu awe hai ni lazima awe anapumua, Mungu alipo muumba mwanadamu alimpulizia pumzi ya uhai, Mwanzo 2:7 “BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.” Wakati fulani Yesu alitoa mfano wa wanawali kumi ambapo watano walikua welevu wenye mafuta ya kutosha lakini wengine wapumbavu hawakua na mafuta ya kutosha.Katika Mathayo 25:1-13. Mafuta pamoja na pumzi ni uwepo wa roho mtakatifu katika imani. Imani bila roho mtakatifun ni sawa na nyumba bila msingi.
Excretion (utoaji wa taka mwili). Imani iliyo hai ni ile inayo muongoza mtu kutambua makosa yake na kutubu yaani kuondoa taka katika hekalu la roho mtakatifu. Mathayo 3:2 “Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.” Mathayo 4:17 “Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubili akisema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.” 1yohana 1:9 “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondelee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
Reproduction (kuzaa). Yakobo 2:20 “Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai? Luka 3:9 “na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.” Luka 13:7 “Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu?.”
Growth (kukua). Imani inapaswa kukua k**a iko hai, itakua kwa kulishwa neno la Mungu na kufanya mazoezi ya kutoka kufanya kazi ili ikomae iweze kupitia nyakati nzuri na mbaya ikiwa imara.
Death (kifo). Imani inakufa lakini inakufa kwa wakati maalumu ambapo mwanadamu anakufa na vitu vyote alivyo kua anavifanya vinakufa.
Imani inapokosa sifa hizo hapo juu hiyo itakua imekufa ndani ya mwanadamu na mwanadamu atakua amebeba maiti ya imani ndani yake huku akiwa anaendelea kwenda kanisani kusali na kujipamba kwa nje kuuonyesha ulimwengu jinsi ambavyo ni mzuri wa umbo na sura na kusahau kuonyesha uzuri wa ndani ambao ni matendo ya imani iliyo hai.
Lakini endapo mwanadamu ataacha kutenda matendo ya imani, maiti ya imani itaanza kuharibika kwa maana ya kwamba uchafu utaanza kutoka ndani yake k**a uchafu uwezavyo kutoka ndani ya jeneza lililo beba maiti kwa muda mrefu k**a vile funza na harufu mbaya itakayo pelekea jeneza kufukiwa haraka iwezekanavyo.
vivyo hivyo wizi, ujambazi, ubakaji, ukahaba, ulevi, matusi na mengine mengi yafananayo na hayo yaweza onekana kwa mtu aliye mbeba marehemu imani. Hatima yake huwa kifo kisicho cha matumaini au kuambulia maradhi yasiyo na tiba k**a UKIMWI na magonjwa yaendanayo na huo. Hatima ya mtu huyu huwa ni kifo pekee chenye majuto makubwa ndani yake.
Nini cha kufanya?
Kaa chini ujitathimini k**a wewe ni jeneza au la! Na k**a ni jeneza umebeba maiti ya namna gani? Ukisha kugundua yote hayo piga magoti mwite yesu akuguse k**a alivyo gusa jeneza la kijana na kumwambia ainuke, umwambie akuguse na aipatie pumzi maiti ya imani iliyoko ndani yako nayo itanena tena!!!!!! Wakati ndugu wa Lazaro wakiwa wameanza kumsahau na kutambua ya kwamba ndugu yao atafufuka katika ufufuo wa kwanza lakini Yesu alimfufua pasipo wao kutarajia… alimwita Lazaro kutoka kaburini na Lazaro akatoka akawa hai tena. Imani yako ilyo kufa inaweza kuwa hai tena ukimfanya Yesu kuwa rafiki yako wa karibu k**a Lazaro.
Imeandaliwa na Musa J. Mabula Call:- +255 685 450 410 +255 714 750 576 Whatsapp:- +255 623 863 093 Email:- [email protected]
MUNGU AWABARIKI SANA