mt.zephania_kapinga

mt.zephania_kapinga Mjue sana Mungu ili uwe na Amani ndivyo mema yatakavyo kujia Ayubu 22:21

16/12/2025
ukipenda kubarikiwa jifunze kubariki watu wengine na kuwa msaada bila kujali rangi au dini.if you like to be blessed, le...
21/10/2022

ukipenda kubarikiwa jifunze kubariki watu wengine na kuwa msaada bila kujali rangi au dini.

if you like to be blessed, learn to bless other people and be helpful regardless of race or religion.

17/09/2022

USISHINDANE NA MTU MWOVU WALA KUSHIRIKIANA NAE.

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu zangu wote.
Karibuni Sana tujifunze Neno la MUNGU.

Mathayo 5:39 "Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili."

Neno "Mtu mwovu" lina maana mbili.

✓✓Maana ya kwanza ya mtu mwovu ni mtu katili, asiyekuwa na huruma, mwenye dhuluma na asiyetenda haki.

✓✓Maana ya pili ya mtu mwovu ni mtu mtenda maovu.
Maovu au uovu ni hali ya mtu kutenda kinyume na wema.

Kwa hiyo ukiona mtu kila Mara anatenda kinyume Cha wema, tambua kwamba mtu huyo ni mwovu.
Huruma ya mtu mwovu Siku zote inaitwa ukatili.
Mithali 12:10 "Mwenye haki huufikiri uhai wa mnyama wake; BALI HURUMA ZA MTU MWOVU NI UKATILI."

Kwanini Biblia inatukataza kushindana na mtu mwovu wala kushirikiana nae?

1. Mtu mwovu hana hofu ya MUNGU ndani yake hivyo kinywa chake ni rahisi kunena mabaya hivyo kukufanya utende dhambi kwa kujibishana naye au kukufanya unajisike kiroho.

Mathayo 12:34 "Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake."

2. Mtu mwovu anaweza akakukosesha mbele za MUNGU k**a ukimpa nafasi mtu huyo katika maisha yako.

Mtu mwovu ni rahisi sana kumkosesha hata mtu mwema.
Isaya 9:16 "Kwa maana wawaongozao watu hawa ndio wawakoseshao, na hao walioongozwa na watu hao wameangamia."

Mfano hao ni Yeroboamu aliyekuwa mwovu akawakosesha Israeli wote katika wakati wake.

1 Wafalme 14:15 Kwa kuwa BWANA atawapiga Israeli k**a manyasi yatikiswavyo majini; naye atawang'oa Israeli katika nchi hii njema, aliyowapa baba zao, naye atawatawanya ng'ambo ya Mto; kwa sababu wamejifanyia maashera yao, wakimkasirisha BWANA. Naye atawatoa Israeli KWA AJILI YA MAKOSA YA YEROBOAMU, aliyoyakosa, ambayo KWA HAYO AMEWAKOSESHA ISRAELI.

3. Mtu mwovu katika moyo wake hutoa maovu tu.

Luka 6:45b " .......... na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake."

4. Mtu mwovu Siku zote huzaa matunda mabaya, yaani husababisha matokeo mabaya.

Mathayo 7:17-18 " Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na MTI MWOVU HUZAA MATUNDA MABAYA. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, WALA MTI MWOVU KUZAA MATUNDA MAZURI."

5. Mtu mwovu hutokana na shetani maana shetani ndiye mkuu wa waovu wote.

Mathayo 13:38 "lile konde ni ulimwengu; zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na YALE MAGUGU NI WANA WA YULE MWOVU;"

Kaini ni mfano hai wa mtu mwovu.
1 Yohana 3:12 "si k**a Kaini alivyokuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake. Naye alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki."

6. Mtu mwovu hutumiwa na shetani ili kukuondolea mambo ya ki MUNGU ndani yako.

Mathayo 13:19 "Kila mtu alisikiapo neno la ufalme asielewe nalo, HUJA YULE MWOVU, AKALINYAKUA LILILOPANDWA MOYONI MWAKE. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia."

7. Neno la MUNGU linatukataza kushirikiana na waovu.

Kutoka 23:1-2 " Usivumishe habari za uongo; usitie mkono wako pamoja na mwovu, kuwa shahidi wa udhalimu. Usiandamane na mkutano kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lo lote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotoa hukumu;"

Mtu mwovu anaweza kukuambia mengi na karibia yote ni ya uongo, na kwa uongo huo anaweza hata ukawachukia hata watu wengine aliowahusisha alipokuambia, na kumbe yeye ndio tatizo maana ni mwovu.

Mithali 12:5 "Mawazo ya mwenye haki ni adili; BALI MASHAURI YA MTU MWOVU NI HADAA."

8. Mtu mwovu hujaa uchungu tu, anaweza hata kukuambukiza uchungu.

Ayubu 15:20 "Mtu mwovu huwa na uchungu siku zake zote, Hata hesabu ya miaka aliyowekewa mwenye kuonea."

Ndugu usishindane na mtu mwovu.
Ndugu usishirikiane na mtu mwovu.
Jitenge mbali na waovu maana ukiwapa nafasi wanaweza kukupoteza.

Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Asante k**a umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU K**a Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.

Address

Tanga

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when mt.zephania_kapinga posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to mt.zephania_kapinga:

Share