Nabii Ernest & Veronica Kangajaka Ministries

Nabii Ernest & Veronica Kangajaka Ministries Official page of Nabii Ernest & Veronica Kangajaka Ministries | BEWARE OF FRAUDRISTERS!!

Je, Uko Tanga Mjini? Hauna mchungaji wa kukusimamia kiroho? Wala huna kanisa la kudumu la kuabudu? Usiendelee kuwa mpwek...
05/09/2026

Je, Uko Tanga Mjini? Hauna mchungaji wa kukusimamia kiroho? Wala huna kanisa la kudumu la kuabudu? Usiendelee kuwa mpweke na peke yako, Tunakukaribisha kwa upendo mkubwa wa Yesu Kristo, The City Of God Ministries mahali ambapo utalelewa kiroho, utajifunza, utapata jamii ya waamini wenye upendo, na kusimamiwa na mchungaji anayeji hatima ya maisha yako ya kiroho, karibu sana katika nyumba ya Mungu. ....mahaliambapo ukuaji wako utakuwa dhahili, kiroho na kiufahamu. Chukua hatua kujiunga na jamii ya watakatifu waaminio. Piga namba hii 0746911291, 0785 911 212
Nabii Ernest & Veronica Kangajaka Ministries

Nabii Ernest Kangajaka

Kesho ibada zetu ni saa tatu 9:30 Asubuhi hadi saa saba 13:30 mchana.

Umebarikiwa.

AINA MBILI ZA WOKOVU1. Aina ya Kwanza: Wokovu wa Kujitungia• Andiko Kuu: Waefeso 2:9 – "Wala si kwa matendo, mtu awaye y...
02/09/2026

AINA MBILI ZA WOKOVU
1. Aina ya Kwanza: Wokovu wa Kujitungia
• Andiko Kuu: Waefeso 2:9 – "Wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu."
• Matendo Mema: Unategemea matendo ya kibinadamu ili kukubalika.
o Uthibitisho: Isaya 64:6 – "Tendo letu la haki limekuwa k**a nguo iliyochafuka mbele za Mungu."
• Toba na Vitubio Kila Siku: Unamlazimu mtu kuomba toba kila siku ili kulinda wokovu.
o Uthibitisho: Waebrania 10:11 – Inaonyesha udhaifu wa makuhani wa kale waliotoa dhabihu kila siku ambazo hazikuweza kuondoa dhambi kabisa.
• Jitihada Zako Binafsi: Unasimama juu ya juhudi za mwanadamu badala ya neema.
o Uthibitisho: Wagalatia 2:16 – "Mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria."
• Hofu ya Kupoteza Wokovu: Mwamini anaishi kwa uoga wa kuhukumiwa wakati wowote.
o Uthibitisho: 1 Yohana 4:18 – "Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililokamilika hulifukuza hofu, kwa sababu hofu ina adhabu."
• Duniani Hakuna Kuokoka: Mtazamo kwamba mwanadamu hawezi kuwa na uhakika wa wokovu akiwa hai.
o Uthibitisho: 1 Yohana 5:13 – Uhakika upo: "Nimewaandikia ninyi mambo hayo... ili mjue kwamba mna uzima wa milele."
• Swali: Yesu Amekuja Kufanya Nini? K**a mwanadamu anaweza kujiokoa kwa sheria, kifo cha Kristo hakina maana.
o Uthibitisho: Wagalatia 2:21 – "K**a haki hupatikana kwa njia ya sheria, basi Kristo alikufa bure."
• Maombi ya Msamaha Ndiyo Msingi: Kutegemea sala za kuomba msamaha badala ya kumwamini mtoa wokovu.
o Uthibitisho: Warumi 10:3 – "Kwa kuwa, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitiisha chini ya haki ya Mungu."
• Maombi ya Kiongozi wa Dini: Kuamini kuwa kiongozi wa kibinadamu ndiye mwenye mamlaka ya kuondoa dhambi zako.
o Uthibitisho: 1 Timotheo 2:5 – "Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, mwanadamu Kristo Yesu."
________________________________________
2. Aina ya Pili: Wokovu wa Kristo Mwenyewe
• Andiko Kuu: Mathayo 1:21 – "Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake YESU, kwa kuwa yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao."
• Kristo Ndiyo Msingi: Kristo pekee ndiye msingi imara na thabiti wa wokovu.
o Uthibitisho: 1 Wakorintho 3:11 – "Kwa maana hakuna mtu awezaye kuweka msingi mwingine, isipokuwa ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo."
• Njia ya Imani: Wokovu unapatikana kwa kuamini tu, si kwa nguvu zako.
o Uthibitisho: Warumi 5:1 – "Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo."
• Siyo Matendo Mema na ya Sheria: Hautegemei matendo ya sheria wala haki binafsi.
o Uthibitisho: Tito 3:5 – "Siyo kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi, bali kwa rehema yake alituokoa."
• Siyo Jitihada Zako: Ni zawadi ya bure (neema) kutoka kwa Mungu.
o Uthibitisho: Waefeso 2:8 – "Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni zawadi ya Mungu."
• Msamaha ni wa Milele: Kazi ya Kristo ilimaliza kabisa deni la dhambi zilizopita, zilizopo, na zijazo.
o Uthibitisho: Waebrania 10:14 – "Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa."
• Siyo Maombi ya Toba na Kufunga: Msamaha hautegemei matambiko ya kidini au kujitesa kwa kufunga ili kusamehewa.
o Uthibitisho: Wakolosai 2:14 – Alikwisha kuifuta ile hati ya mashtaka iliyokuwa inatukabili, akaiondoa isiwepo, akiigongomea msalabani.
• Imani katika Dhabihu Iliyotolewa Mara Moja: Kristo alikufa mara moja tu na hahitaji kurudia dhabihu yake.
o Uthibitisho: Waebrania 9:28 – "Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja tu azichukue dhambi za watu wengi."
________________________________________
Nabii Ernest & Veronica Kangajaka Ministries

Nabii Ernest Kangajaka

The City Of God Ministries
0746 911291
0785 911 212

Mwezi wa tisa ni mwezi wa Kisleu mwezi wa mageuzi ya kiroho.Zakaria 7:1-9Mungu awabariki nyote.Nabii Ernest & Veronica K...
02/09/2026

Mwezi wa tisa ni mwezi wa Kisleu mwezi wa mageuzi ya kiroho.

Zakaria 7:1-9

Mungu awabariki nyote.

Nabii Ernest & Veronica Kangajaka Ministries

Nabii Ernest Kangajaka

The City Of God Ministries

0785 911 212
0746 911291

01/09/2026

I got over 1,000 reactions on my posts last week! Thanks everyone for your support! 🎉

Asante sana Peter Mponjoli pamoja viongozi wote kwa upendo mkuu ambao mmenionyesha katika huduma kwa siku mbili zimekuwa...
30/08/2026

Asante sana Peter Mponjoli pamoja viongozi wote kwa upendo mkuu ambao mmenionyesha katika huduma kwa siku mbili zimekuwa za Baraka. Mbarikiwe. Nabii Ernest & Veronica Kangajaka Ministries

Nabii Ernest Kangajaka
0746 911291
0785 911 212

God is Great, tumekuwa na muda mzuri sana hapa pwani vikindu, chanungu kwa pastor Peter Mponjoli, imekuwa Baraka sana, k...
29/08/2026

God is Great, tumekuwa na muda mzuri sana hapa pwani vikindu, chanungu kwa pastor Peter Mponjoli, imekuwa Baraka sana, karibu sana kesho jumapili kanisa la Pentecost Apostolic Church. Muda saa 3 Asubuhi hadi saa 7 mchana, usipange kukosa.

Nabii Ernest & Veronica Kangajaka Ministries , Nabii Ernest Kangajaka atahudumu lete wagonjwa na changamoto ambazo zimeshindika.

24/08/2026

Usikose semina hii maisha yako hayatabaki k**a yalivyo kuwa.

15/08/2026

Hekima inaambukizwa......

Kuna watu wengi hivi leo wanateseka kwa sababu ya maneno ambayo waliwahi kusema kinyume na maisha yao, na hawakujua madh...
14/08/2026

Kuna watu wengi hivi leo wanateseka kwa sababu ya maneno ambayo waliwahi kusema kinyume na maisha yao, na hawakujua madhara yake wamejikuta wamejiweka vifungoni. Huku kila siku wanatafuta maombi ya kufunguliwa.

Mithali 6:2 Basi Umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, umek**atwa kwa maneno ya kinywa chako.

K**a hufahamu nguvu ya kinywa chako na maneno unasema kila siku utadhani kuna mchawi anakuroga, utashinda kwenye maombi kumbe wewe ni mjinga. Unahitaji mafundosho sahihi kukujenga kiroho na kiufahamu.

K**a ungependa kujifunza Neno la Mungu kwa kina karibu kwenye ibada leo hii Ijumaa hapa The City Of God Ministries chumbageni mtaawaTumaini Karibu na stand ya mwembe mawazo Jijini Tanga. Muda ni saa kumi na nusu jioni.

0746 911291
Kwa mawasiliano.
Nabii Ernest & Veronica Kangajaka Ministries

Nabii Ernest Kangajaka
0785 911 212

Karibu kwenye ibada kesho Ijumaa hapa The City Of God Ministries Chumbageni Tanga Mjini, ni ibada ya maombi, uponyaji na...
13/08/2026

Karibu kwenye ibada kesho Ijumaa hapa The City Of God Ministries Chumbageni Tanga Mjini, ni ibada ya maombi, uponyaji na kufunguliwa, muda ni saa kumi na nusu16:30 Jioni hadi saa kumi na mbili kamili 18:00 jioni, Njoo na imani, njoo na matarajio, yote yanawezekana kwa Mungu.

Nabii Ernest Kangajaka
Nabii Ernest & Veronica Kangajaka Ministries
Atahudumu mkaribishe mwingine.

0785 911 212
+255 746911291
Kwa maelekezo na jinsi ya kufika kanisani.

Address

Tanga
16

Opening Hours

Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00
Sunday 09:00 - 17:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Nabii Ernest & Veronica Kangajaka Ministries posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Nabii Ernest & Veronica Kangajaka Ministries:

Shortcuts

Share