13/08/2026
LEO KATIKA HISTORIA
MORAVIAN PENTEKOSTE 13 AUGUST 1727
Historia ya Pili ya kanisa inaanza mwaka 1722 na mtu anaitwa Christian David, fundi seremala ambaye alizaliwa huko Moravia 31st Desemba 1690 na kukulia katika Ukatoliki. Lakini bado hakupata amani na ukatoliki, akajaribu dini ya Uyahudi hakupata amani akajaribu kupata amani kwa kujizfunza Ulutheri pia hakupata amani. Baadaye akahamia Ujerumani na kuanza kusali kanisa la Lutheran Berlin. Lakini pia hakuridhika maana anasema aliona ibada zao ziko baridi (stiff and cold). Baadaye akajiunga na Jeshi huko pia hakuweza kupata amani.
Baadaye mwaka 1717 akahamia Gorlitz, in Silesia; akakutana na Wachungaji wa ‘’Pietism movement’’ Schäfer and Schwedler. Akiwa Gorlitz aliugua kwa wiki 20 alikuwa hawezi kunyanyua mguu wala mkono, akawa anaombewa na mchungaji Schwedler akapona. Ndipo na yeye sasa akaanza kusafiri kwenda kwao Moravian na kuwashuhudia wale Ndugu juu ya kuponywa kwake na Imani mpya aliyopokea walimuita BUSH PREACHER kwajili ya kukatiza vijiji hadi vijiji.
25th May 17222 alikutana na Nicholas Ludwig Von Zinzendorf. David akamwambia Zinzendorf kuwa anataka eneo ambako yeye na ndugu zake walioko Moravian wanaweza kufanya makimbilio na kuendesha ibada za dini ya kikristo ambayo inazingatia mafundisho ya awali ya kikristo
Alipokubaliwa tu, David alirudi kwao Moravia na mnamo 27th May 1722, Christian David aliwaongoza watu kumi ( familia tatu) kutoka Moravia, wakapanda na kushuka milima hadi Berthelsdorf na wakafika 8th June 1722. Mnamo Jumatano 17th June 1722, David alikata mti wa kwanza kwa ajili ya kuanza makazi yao. Zinzendorf aliporudi safari alishangaa kuwakuta wageni katika maeneo yake
KUKUA KWA HERRNHUT
Mpaka kufika March 1727, wakimbizi hawa walikuwa wameongezeka mpaka kufikia watu wazima 220, pamoja na watoto 87 wakiishi kwenye nyumba 30 tofauti.
KUPISHANA KWA IMANI NA MAPOKEO
Ndani yake humu kulikuwa pia na mchanganyiko wa watu wenye asili ya madhehebu mengine waliojiunga lakini hawakuacha mapokeo ya makanisa yao walikotoka. Kulikuwa na Baptists, Presbyterians (Reformed), Lutherans, Schwenkfelder’s, na Umoja wa Ndugu (Moravians), kukawa na migawanyiko na magomvi kila siku na kuhukumiana kuhusu mapokeo na dini zao kiasi cha kuhatarisha umoja wao
Ili kuondoa huo ugomvi Zinzendorf, alianza kuzungukia kila nyumba na kufanya Maombi……kisha akaanza kuwaita pamoja watu na kujifunza Maandiko hasa namna ya kudumisha umoja. Alisisitiza kuwa ni vyema kuangalia zaidi mambo ambayo wanakubaliana kuliko kuangalia zaidi mambo ambayo wanapishana.
PATANO LA NDUGU
Katika kupekua pekua nyaraka akutana na mwongozo wa nidhamu kwa wana Umoja wa Ndugu uliokuwa umeandikwa na Askofu Amos Comenius. Zinzendorf alifurahi sana kuona kumbe Umoja wa Ndugu walikuwa tayari na utaratibu mzuri wa nidhamu tangu miaka mingi. Ndipo alipowaambia wana Herrnhut na walifurahi sana kuona muongozo wa kiongozi wao umeheshimiwa.
Ndipo hapo Zinzendorf alitumia kutengeneza Patano la Wana wa Umoja wa Ndugu (Brotherly Agreement.) Kila mwana umoja wa ndugu alisaini na kuridhia hii ilikuwa 12th May 1727 ambalo ndio lilikuja kuboreshwa mwaka 1957 na tena mwaka 1995 kwenye Unity Synod iliyofanyika hapa Dar es Salaam.
MAOMBI HUTANGULIA UAMSHO
MAOMBI
22 May 1727 Maombi ya mkesha
16th July 1727 Jumuia ikaanza Maombi mazito ya pamoja kwa namna ambayo haijawahi kutokea kabla
22July 1727
Maombi ya mkesha
5th August 1727
Zinzendorf na watu wengine 14 walikesha kwenye Maombi Hutberg kuomba Mungu ashushe nguvu za Roho Mtakatifu na usiku ule walikuwa uweponi sana”
06th August 1727
Binti wa miaka 11 Susanne Kuhnel, alikutana na nguvu za Maombi baada ya kukesha siku tatu akiomba ilikuwa baada ya kufiwa na mama yake Kufuatia Ushuhuda huu watoto wengi nao wakapokea Uamsho pia sawasawa na neno katika YOEL…………
10TH August 1727
Mchungaji wa kanisa la Berthelsdorf John Andrew Rothe alikuwa anaendesha Maombi mchana na waumini kadhaa walishangaa kushikwa na nguvu za Mungu akashangaa anazama kwenye mavumbi na kundi lote wakaanguka mavumbini na kuanza kuomba kwa muda mrefu, huku wakilia na kufunikwa na nguvu za Mungu..
THE MORAVIAN PENTECOST
13 August 1727
Wakati wanaenda kanisa kutoka Hernnhut kwenda Bethersdolf (kilometer 3) kila mmoja Alikuwa akiongea na mwenzie kwa pamoja kuonyesha hali fulani ya umoja. Ibada ilianza kwa wimbo ‘’ Uniokoe Mimi Mungu Wangu (Wimbo namba 721) kwenye Moravian Hymn Book). Kisha wakaimba wimbo mwingine ghafla waumini wakaanza haijulikana k**a wanaimba au wanalia wakaanza kuomba namna ambayo hawajawahi kuomba
Hawakukumbuka kula waliendelea kubakia maeneo ya kanisa mpaka Zinzendorf alipokumbuka na kuagiza chakula kutoka nyumbani kwake wakala wote kwa pamoja kwa upendo na ndio ikawa Mwanzo wa KARAMU YA UPENDO katika kanisa la Moravian
Baada ya 13th August 13th, kulikuwa na mwako mkubwa wam kiroho , yaani kila kichaka ukipata ulikuwa unawakuta waumini wanaomba kila mtu kivyake”
Watoto siku moja baada ya Maombi walizunguka mitaani wakiimba na kusali kwa sauti za juu huku wakizunguka kijjiji chote
LEO WATOTO WETU WA WANASHINDANA KUIMBA KWA KUTUMIA FLASH NA KUCHEZA STEPS K**A VIJANA. HAWANA NAFASI YA KUSHINDANA KUSOMA NA KUSHIKA BIBLIA.’
MAMBO GANI YALITOKEA?
Kiu ya neno iliongezeka wakaanzisha ibada tatu kila siku 5am; 7:30am; and 9pm).
IDADI YA IBADA ZAO SIKU YA JUMAPILI
SAA 11 ALFAJIRI MORNING BLESSING
12.00- 3.00 ASBH Madarasa ya Biblia ya Kwaya ( Kila group Kivyao"."
Saa 4:00: Ibada ya Watoto
Saa 5:00 Ibada ya Asubuhi Ushirikani
Saa 7: 00 Kiongozi Mkuu aliendesha Ibada
Saa9: Ibada ya wageni ( waliokosa ibada za Asubuhi)
Saa 10: 00 Kulikuwa na ibada kule Lutheran Berthelsdorf
Saa 2:00 Usiku kulikuwa na ibada Herrnhut
MAOMBI YA MNYORORO (HOURLY INTERCESSION PLAYERS)
26.08.1724 Wanawake 24 na wanaume 24 wakaanza maombi ya zamu ya mnyororo. Wastani wao walikuwa miaka 30
27.08 1727 Ikawekwa utaratibu maombi ya mnyororo na watu 77 na watoto pia wakawa wanashika zamu ya maombi kwa muda wa miaka 100
UMISIONARI WA KIMORAVIAN
K**a ilivyokuwa kwa wanafunzi wa YESU katika Kitabu cha Matendo ya Mitume, pia Morvaina baada ya kupata Kipawa cha Roho Mtakatifu, wakapata msukumo wa kuanza kufanya umisionari katika sehemu mbalimbali za ulimwengu wakianzia visiwa vya St Thomas 21.08.1732