Antioch CLC

Antioch CLC Tanzania Asseblies of God - Antioch Christian Life Center.

02/06/2024

KARIBU UABUDU PAMOJA NASI
RATIBA ZA IBADA T.A.G ANTIOCH CHRISTIAN LIFE CENTRE

Jumatano / Ijumaa [ Saa10:30 - 12:00 jioni ]
Jumapili (IBADA YA KWANZA) [ Saa1:00 - saa3:30 Asubuhi ]
MAANDIKO NA UANAFUNZI [ Saa3:30-4:30 Asubuhi ]
Jumapili (IBADA YA PILI) [ 4:30-6:30 Mchana ]

28/04/2024
19/04/2024

ANZA SIKU NA BWANA
KWA NENO NA MAOMBI

_*NENO LA MUNGU LI HAI*_
_*TENA LINA NGUVU*_
_*(WAEBRANIA 4:12).*_

*MATHAYO 28:19&20.*
19.Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
20. na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Mpendwa jifunze;
■ *Kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa Yesu.*
■ *Kuwafundisha watu neno la Mungu.*
Mpendwa,
1.Je, wewe unachukua
hatua gani ya kuwafikia
wengine?
2.Je, wewe huwa
unawashirikisha
wengine habari njema
za Yesu Kristo?
*TAFAKARI*
Mpendwa, kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa Yesu, ni agizo la Yesu Kristo. Ni agizo ambalo kila mtu aliyemwamini Yesu anapaswa kulifanya kwa sehemu yake na katika uwezo wake bila kutoa kisingizio.
👉🏽Mpendwa, kuenenda ni kwenda, lakini 'enendeni' kunaweza kufanywa kwa namna tofauti k**a ifuatavyo;
●Kutoka na kwenda kuwashuhudia watu habari za Yesu Kristo.
●Kuonesha tabia na mwenendo safi unaotoa uhalisia wa maisha ya Yesu Kristo na kufanyika baraka kwa watu wengine.
●Kuenenda ni pamoja na kuwaombea wengine ili wamjue Yesu Kristo kuwa Mwokozi wao.
●Ni kuwawezesha watumishi wa Mungu kwa maombi, hali na mali ili waweze kuwafikia watu kwa habari njema za Yesu Kristo.
●Kuwafundisha neno la Mungu ili waijue kweli yote ya Mungu.
👉🏽Mpendwa, kuijua kweli ya Mungu ni pamoja na kulishika neno la Mungu, kujua wokovu na kuukulia wokovu, ubatizo, Roho Mtakatifu na namna ya kuishi maisha matakatifu ya kumpendeza Mungu. Lakini katika hayo yote, jambo la kwanza kabisa ni kumwamini *YESU KRISTO na kumpokea kuwa BWANA NA MWOKOZI* wa maisha yako. Yesu atakusamehe dhambi zako zote na kukupa uzima wa milele.

*Omba sala hii;*
👉🏽 _Eee Bwana Yesu, naomba unisamehe dhambi zangu zote, ninatubu kwako. Nimefungua moyo wangu ingia ndani yangu sasa. Nami ninakukiri *YESU kuwa BWANA NA MWOKOZI* wa maisha yangu. *AMINA*._
👆🏽 *IKIWA UMEOMBA SALA HII KWA IMANI, SASA UMEOKOKA.*
*(WARUMI 10:9&10)*

Barikiwa sana mtu wa Mungu. _*Uwe na Ijumaa njema.*_

_*19 Aprili, 2024.*_~:; Elimringi Ernest Mariki ::~

18/04/2024

Mchungaji kiongozi ( Professor: Pastory Majembe ) pamoja na wazee wa kanisa wakifanya uzinduzi wa kitabu cha HISTORIA YA KANISA LA ANTIOKIA CHRISTIAN LIFE CENTRE. Katika ibada ya tarehe 14/04/2024

18/04/2024

HISTORIA YA KANISA IKISOMWA Katika kuadhimisha miaka 30 ya kanisa la T.A.G ANTIOKIA (lililopo tabata kisukuru).
14 / 04 / 2024

14/04/2024

official_antioch_online ZONE YA KANAANI ΚΑΤΙΚΑ ΜMAADHIMISHO YA MIAKA 85 YA KANISA LA T.A.G IKIWA NI KUTIMIZA MIAKA 30 YA KANISA LA T.A.G ANTIOKIA

KARIBUNI SANA
14/04/2024

KARIBUNI SANA

14/04/2024

official_antioch_online ZONE YA KISUKURU ΚΑΤΙΚΑ ΜMAADHIMISHO YA MIAKA 85 YA KANISA LA T.A.G IKIWA NI KUTIMIZA MIAKA 30 YA KANISA LA T.A.G ANTIOKIA

Shalom.Kwa Neema ya Mungu, Mch Kiongozi wa kanisa la TAG Antioch Christian Life Center Prof. Pastory Majembe, anakualika...
28/03/2024

Shalom.

Kwa Neema ya Mungu, Mch Kiongozi wa kanisa la TAG Antioch Christian Life Center Prof. Pastory Majembe, anakualika Katika Semina ya siku 5 ya Pasaka,

Karibu Tujifunze Kuhusu Umuhimu wa Pasaka Kwenye maisha ya Mkristo

Njoo pamoja Na rafiki yako.,
Hakuna Kiingilio.
Watu wote Mnakaribishwa.

KWAYA YA UMOJA Madhabahuni wakimtukuza MUNGU Kwanjia ya uimbaji, siku ya Jana (24/03/2024).
25/03/2024

KWAYA YA UMOJA Madhabahuni wakimtukuza MUNGU
Kwanjia ya uimbaji, siku ya Jana (24/03/2024).

SHUKRAN KWA IDARA YA SIFA NA MUZIKI KWAKUTUANDALIAIBADA NZURI SIKU YA JANA (24/03/2024).
25/03/2024

SHUKRAN KWA IDARA YA SIFA NA MUZIKI KWAKUTUANDALIA
IBADA NZURI SIKU YA JANA (24/03/2024).

Address

Tabata

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Antioch CLC posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share