15/12/2025
BABA VS MTOTO
Baba Yetu wa Imani kwa Wakristo ni Ibrahimu ambaye alimzaa Isaka k**a mtoto wa ahadi (Mwanzo 17:17-19),( Mwanzo 21: 1-7). Katika Hali ya uzee sana alimzaa mtoto huyu. Sasa tukiachana na Habari ya kuzaliwa kwa isaka ,tuangalie kidogo uhusiano wa Baba na mtoto wake.
BABA ni Nani hasa
1. Mtu ambaye ameaminiwa na Mungu kwa ajili ya kukamilisha Ratiba na utaratibu wa kumleta mwanadamu husika kwa kipindi husika hapa duniani. Mwanzo 17: Ukisoma utangundua Mungu anamtaka Isaka lakini atakujaje jukumu kapewa Ibrahimu, naye ibrahimu atampata mtoto uzeeni si k**a atakavyo Bali Bwana yeye atakaye.
2. Mtu ambaye amepewa jukumu la kuhakikisha anasikiliza maelekezo ya Mungu kwa ajili ya huyo mtoto.(Mwanzo 22:1-2, Mungu anamtaka Isaka),( mathayo 2:13-15, Yusufu babaye Yesu anapokea maelekezo ya Mungu juu ya kuokoa uhai wa Mtoto). Hivyo kumbe ili litimie kusudi la Mungu kwa ajili ya Mtoto inambidi Baba atimize jukumu hili kubwa la KUSIKILIZA NA KUTEKELEZA MAELEKEZO YA MUNGU.
3.NI Mtu ambaye amepewa neema na Kibali cha kupitisha Baraka za Mungu kwa Mtoto. (Mwanzo 24:1-4, kwa neno la Ibrahimu Isaka akampata Rebeka( Msichana mzuri wa uso, mwenye nuru, mwenye kuzaa mapacha yaani Esau na Yakobo) ,, (Mwanzo 27:1-4, Isaka akiwa na ratiba ya kuachilia Baraka kwa wanae maana muda wa kufa kwake umekaribia),, ( Mwanzo 49:1-2, yakobo akawaita wanae na kuwabariki kila mmoja kwa Kadri Mungu alivyosema naye) ,, (Mathayo 28:18-20 Yesu anawabariki Thenashara kwa utume mkuu),,( Matendo 1:6-9, Muda wa Yesu kupaa mawinguni aliwabariki wanafunzi wake huku akiwaeleza yatakayo tukia hapo baadae na nini watapaswa kufanya),. Baba kitamkie kizazi chako Baraka hata k**a uko mbali na wanao , tafadhali usiondoke na Baraka zao. Na hasa kwa HOJA hii ndiyo maana shetani hataki Baba awe na mahusiano mazuri na wanae,. Mahusiano yakiwa vibaya basi moyo wa Baba hauwezi kukunjuka na kutamka kitu chema,. Mzee akitamka Baraka kwako hata vita vikiinuka sana Havitakunyamazisha.
4: Ni mtu ambaye ni Kianzio cha mwanae katika hatua mbali mbali za Kimaisha (Mwanzo 26: 12-24, Isaka anatembelea neema ya Baba yake,yaani haanzii zero kimaisha anaanzia sehemu furani , visima vipo japo vimefukiwa ,, Mfano mzazi akiwa na mashamba,viwanja,Mikorosho, majumba, vitega uchumi mbalimbali asiviuze ama kuvitapanya kisa anaona anazeeka ),,( 1Wafalme 6:11-12, liko neno lililotamkwa kipindi cha Daudi babaye Sulemani ambalo litakuwa kipindi cha Sulemani mtoto:- pamoja na watoto kupambana kuishi maisha Yao lakini ukweli ni kwamba Kuna sehemu ya maisha Yao ni matokeo ya maisha ya wazazi wao,. Basi k**a ni hivyo mzazi mwema hutoa mchango Chanya katika maisha ya wanae , na mwovu vile vile hutoa ( impat negative values) matokeo hasi. Na hapa ndiyo utasikia Yale maneno ya Jino kwa Jino ama sitamtupa kabisa kwa ajili ya wema wa Baba yake ama mzazi wake.
5. Baba ni Mwalimu( like Father like Son),, Mtoto wa Nyoka naye ni Nyoka., kwa sehemu kubwa mtoto wa Kiume anarithi tabia za Baba k**a yuko karibu na Baba and vise verser is true, japo hormones pia zina nafasi yake. Muhimu hapa kutambua kuwa Mtoto umleavyo ndivyo akauavyo ( mtoto umfundishavyo ndivyo anavyokuwa), unaweza jiuliza kwanini wamasai ni wafugaji? Jibu ni Baba zao ni wafugaji ,Hali kadhalika wasukuma kwa tamaduni zao na wachaga kwa malezi yao
( mathayo 4: 21, Baba mvuvi na watoto wavuvi pia)
Kwa uchache tu Baba hakikisha kizazi chako unakifanyia matamko mema. Ishi maisha ambayo wanao na walimwengu Mabaya,.. Mungu atusaidie wa Baba wote tutimize jukumu kubwa alilotupa Mungu.
9:1-7
Kisha Daudi akasema, Je! Amesalia mtu mmoja katika nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema kwa ajili ya Yonathani?
Basi Mefiboshethi, mwana wa Yonathani, mwana wa Sauli akaenda kwa Daudi, akaanguka kifudifudi, akasujudu. Daudi akasema, Mefiboshethi! Naye akaitika, Mimi hapa, mtumishi wako! Daudi akamwambia, Usiogope, maana bila shaka nitakutendea mema; kwa ajili ya Yonathani, baba yako, nami nitakurudishia mashamba yote ya Sauli, babu yako; nawe utakula chakula mezani pangu daima.
Mwl.Chagata✍️