muslim_ikhwaan

muslim_ikhwaan Allah anasema "na iogope siku utakayo rejeshwa kwa mola wako"

Ndugu waislamu tutumie mda huu kutaka maghfira na Toba kwa Allah
07/09/2025

Ndugu waislamu tutumie mda huu kutaka maghfira na Toba kwa Allah

04/09/2025

Hakika Quran ni kitabu kisicho na shaka ndani yake

An-Nur 24:2ٱلزَّانِيَةُ وَٱلزَّانِى فَٱجْلِدُوا۟ كُلَّ وَٰحِدٍ مِّنْهُمَا مِا۟ئَةَ جَلْدَةٍۖ وَلَا تَأْخُذْكُم بِهِمَا ر...
03/09/2025

An-Nur 24:2

ٱلزَّانِيَةُ وَٱلزَّانِى فَٱجْلِدُوا۟ كُلَّ وَٰحِدٍ مِّنْهُمَا مِا۟ئَةَ جَلْدَةٍۖ وَلَا تَأْخُذْكُم بِهِمَا رَأْفَةٌ فِى دِينِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْءَاخِرِۖ وَلْيَشْهَدْ عَذَابَهُمَا طَآئِفَةٌ مِّنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ

Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani

Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume, mtandikeni kila mmoja katika wao bakora mia. Wala isikushikeni huruma kwa ajili yao katika hukumu ya Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na lishuhudie adhabu yao kundi la Waumini.

English - Tafsir Ibn Kathir (Abridged)

Which was Revealed in Al-Madinah
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَـنِ الرَّحِيمِ

In the Name of Allah, the Most Gracious, the Most Merciful.
The Importance of Surat An-Nur
سُورَةٌ أَنزَلْنَـهَا

(A Surah which We have sent down) Here Allah is pointing out the high esteem in which He holds this Surah, which is not to say that other Surahs are not important.

وَفَرَضْنَـهَا

(and which We have enjoined,) Mujahid and Qatadah said, "This means: We have explained what is lawful and unlawful, commands and prohibitions, and the prescribed punishments." Al-Bukhari said, "Those who read it: Faradnaha, say that it means: "We have enjoined them upon you and those who come after you."

وَأَنزَلْنَا فِيهَآ ءَايَـتٍ بَيِّنَـتٍ

(and in it We have revealed manifest Ayat,) means, clearly explained,

لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ

(that you may remember.)
The Explanation of the Prescribed Punishment for Zina (Illicit Sex)
Then Allah says:

الزَّانِيَةُ وَالزَّانِى فَاجْلِدُواْ كُلَّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا مِاْئَةَ جَلْدَةٍ

(The Zaniyah and the Zani, flog each of them with a hundred stripes.) This honorable Ayah contains the ruling on the law of retaliation for the person who commits illegal s*x, and details of the punishment. Such a person will either be unmarried, meaning that he has never been married, or he will be married, meaning that he has had in*******se within the bounds of a lawful marriage, and he is free, adult and of sound mind. As for the virgin who is unwedded, the prescribed punishment is one hundred stripes, as stated in this Ayah. In addition to this he is to be banished from his homeland for one year, as was recorded in the Two Sahihs from Abu Hurayrah and Zayd bin Khalid Al-Juhani in the Hadith about the two bedouins who came to the Messenger of Allah ﷺ. One of them said, "O Messenger of Allah, this son of mine was employed by this man, and committed Zina with his wife. I paid a ransom with him on behalf of my son one hundred sheep and a slave-girl, but when I asked the people of knowledge, they said that my son should be given one hundred stripes and banished for a year, and that this man's wife should be stoned to death." The Messenger of Allah ﷺ said:

«وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَأَقْضِيَنَّ بَيْنَكُمَا بِكِتَابِ اللهِ تَعَالى، الْوَلِيدَةُ وَالْغَنَمُ رَدٌّ عَلَيْكَ، وَعَلى ابْنِكَ جَلْدُ مِائَةٍ وَتَغْرِيبُ عَامٍ، وَاغْدُ يَا أُنَيْسُ لِرَجُلٍ مِنْ أَسْلَمَ إِلَى امْرَأَةِ هذَا،فَإِنِ اعْتَرَفَتْ فَارْجُمْهَا»

(By the One in Whose Hand is my soul, I will judge between you both according to the Book of Allah. Take back the slave-girl and sheep, and your son is to be given one hundred stripes and banished for one year. O Unays -- he said to a man from the tribe of Aslam -- go to this man's wife, and if she confesses, then stone her to death.) Unays went to her and she confessed, so he stoned her to death. This indicates that if the person who is guilty of illegal s*x is a virgin and unmarried, he should be banished in addition to being given one hundred stripes. But if married, meaning he has had in*******se within the bounds of lawful marriage, and he is free, adult and of sound mind, then he should be stoned to death. Imam Malik recorded that `Umar, may Allah be pleased with him, stood up and praised and glorified Allah, then he said; "O people! Allah sent Muhammad with the truth, and revealed to him the Book. One of the things that was revealed to him was the Ayah of stoning to death, which we have recited and understood. The Messenger of Allah ﷺ carried out the punishment of stoning and after him we did so, but I am afraid that as time goes by, some will say that they did not find the Ayah of stoning in the Book of Allah, and they will go astray because they abandoned one of the obligations revealed by Allah. Stoning is something that is prescribed in the Book of Allah for the person -- man or woman -- who commits illegal s*x, if he or she is married, if decisive evidence is produced, or if pregnancy results from that, or if they confess to it." It was also recorded in the Two Sahihs in the lengthy Hadith of Malik, from which we have quoted briefly only the portion that is relevant to the current discussion.
Do not feel pity for Them when carrying out the Prescribed Punishment
وَلاَ تَأْخُذْكُمْ بِهِمَا رَأْفَةٌ فِى دِينِ اللَّهِ

(Let not pity withhold you in their case, in a punishment prescribed by Allah,) Meaning, with a ruling prescribed by Allah. So the meaning of the Ayah is: "Do not feel too sorry for them where the laws of Allah are established." This does not mean that we should not naturally feel pity when carrying out the punishment. What is prohibited here is the kind of pity that may make the judge ignore the punishment altogether. This is what is not permitted for the judge. Mujahid said,

وَلاَ تَأْخُذْكُمْ بِهِمَا رَأْفَةٌ فِى دِينِ اللَّهِ

(Let not pity withhold you in their case, in a punishment prescribed by Allah,) "If the matter is taken to the ruling authority, the punishment has to be carried out and cannot be stopped." This was also narrated from Sa`id bin Jubayr and `Ata' bin Abi Rabah. It was recorded in a Hadith:

«تَعَافَوُا الْحُدُودَ فِيمَا بَيْنَكُمْ، فَمَا بَلَغَنِي مِنْ حَدَ فَقَدْ وَجَبَ»

(Compromise with the matter of prescribed punishment mutually sorting it out among yourselves, for once a matter where the prescribed punishment is required reaches me, I am obliged to carry it out.) Allah's saying:

إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الاٌّخِرِ

(if you believe in Allah and the Last Day. ) means, then do that, carry out the punishments on those who commit illegal s*x, and strike them hard without causing any wound, so that he and others like him will be deterred by the terror of that. In Al-Musnad, it was recorded that one of the Companions said, "O Messenger of Allah, when I slaughter a sheep I feel pity for it." He said,

«وَلَكَ فِي ذلِكَ أَجْرٌ»

وَلْيَشْهَدْ عَذَابَهُمَا طَآئِفَةٌ مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ

(And let a party of the believers witness their punishment.) This is more humiliating for the people who are guilty of illegal s*x, if they are flogged in front of the people. This is because it is more effective as a deterrent and it conveys the sense of scandal and rebuke. Al-Hasan Al-Basri said,

وَلْيَشْهَدْ عَذَابَهُمَا طَآئِفَةٌ مِّنَ الْمُؤْمِنِين

An-Nahl 16:68Na Mola wako Mlezi amemfunulia nyuki: Jitengenezee majumba yako katika milima, na katika miti, na katika wa...
03/09/2025

An-Nahl 16:68

Na Mola wako Mlezi amemfunulia nyuki: Jitengenezee majumba yako katika milima, na katika miti, na katika wanayo jenga watu

17/09/2022

UJUMBE WA QUR'AN

*يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِن تَتَّقُوا۟ ٱللَّهَ يَجْعَل لَّكُمْ فُرْقَانًۭا وَيُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّـَٔاتِكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ۗ وَٱللَّهُ ذُو ٱلْفَضْلِ ٱلْعَظِيمِ*

TAFSIRI....

*Enyi mlio amini! Mkimcha Mwenyezi Mungu* ( kwa siri na dhahiri) *atakupeni kipambanuo*, ( uwezo wa kupambanua baina ya Haki na upotovu, na atakutunukieni ushindi wa kutenga baina yenu na maadui zenu) *na atakufutieni makosa* ( atakusitirieni maovu yenu yaondoke), *na atakusameheni, na Mwenyezi Mungu* ( daima) *ni Mwenye fadhila kubwa*.

Qur'an Al Anfal ( 8: 29)

*﷽**AHKAAM ZA KUTOA MIMBA*   🌹 🌹  •••☆☆☆☆☆☆•••🌹🌹           🍃🍃🍃🍃🍃🍃    📚Anasema Allahu katika Kitabu chake-( *وَلَا تَقْتُ...
17/02/2022

*﷽*
*AHKAAM ZA KUTOA MIMBA*

🌹 🌹 •••☆☆☆☆☆☆•••🌹🌹

🍃🍃🍃🍃🍃🍃


📚Anasema Allahu katika Kitabu chake-

( *وَلَا تَقْتُلُوا أَوْلَادَكُمْ خَشْيَةَ إِمْلَاقٍ ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُهُمْ وَإِيَّاكُمْ ۚ إِنَّ قَتْلَهُمْ كَانَ خِطْئًا كَبِيرًا* )
الإسراء (31) Al-Israa

🍃 *MAANA YAKE* 🍃
Wala msiwauwe wana wenu kwa kuogopa umasikini. Sisi tunawaruzuku wao na nyinyi. Hakika kuwaua hao ni khatia kubwa.
⚡⚡⚡⚡⚡

🍃 *MAFUNZO YAKE* 🍃

⚡Kutoa mimba ikiwa ni kabla ya *kupuliziwa roho au baada ya kupuliziwa roho kisheria ni haraam*
Wakati unaokubalika kutoa mimba ni pale tu itakapokuwa kuna dharura za kisheria ndipo panaweza kukubalika tena kwa masharti yake.
*Dharura hizo,* _ni k**a kumehakikishika kuwa kuna uwezekana wa mama kufariki kwa kuwa na kiumbe hicho, au kuendelea kwake kuwa na mimba hiyo kutamletea mauti._
Na isitoshe kukubalika huko, bali kumetakiwa uthibitisho huo utolewe na daktari mwenye kuaminika kabisa. Na muhimu kwanza atafutwe daktari Muislamu mwenye kuaminika, ikishindikana, basi daktari yeyote ambaye ni muaminifu sana.

*Sababu isiyo ya kisheria*
Ama kuitoa mimba tu kwa sababu ya kutotaka mtoto, au kukhofia riziki yake, au malezi yake, au kuchelea gharama za maisha k**a kumsomesha, kumvisha, au kumlisha n.k. hayo yote hayaruhusiwi kisheria kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:
( *وَلَا تَقْتُلُوا أَوْلَادَكُمْ خَشْيَةَ إِمْلَاقٍ ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُهُمْ وَإِيَّاكُمْ ۚ إِنَّ قَتْلَهُمْ كَانَ خِطْئًا كَبِيرًا* )

الإسراء (31) Al-Israa

Wala msiwauwe wana wenu kwa kuogopa umasikini. Sisi tunawaruzuku wao na nyinyi. Hakika kuwaua hao ni khatia kubwa.

*Khilaafu za Maulamaa*
📃Ingawa kuna baadhi ya Maulamaa wanaonelea kuwa inafaa kutoa mimba katika siku za arobaini za mwanzo, lakini iliyo sahihi zaidi ni kutokufaa kutoa katika hali zote ila kwa dharura kubwa kabisa inayokubalika katika sheria.
Ama katika hatua ya pili ya siku arobaini nyingine ambayo ni 'alaqah (kipande cha damu), au hatua ya tatu ya siku arobaini nyingine ambayo inajulikana k**a ni 'mudhwgah' (kipande cha nyama), haitoruhusiwa kutolewa hiyo mimba *hadi jopo la madaktari wenye kuaminika wathibitishe kuwa kweli kuendelea kuwepo mimba hiyo kutasababisha mama kufariki au ikiwa kumeonekana na kujulikana kuwa kiumbe (kijusi) hicho kimeshakufa tumboni ndipo katika hali hiyo kutaruhusika kutolewa baada ya kila njia kutumika kuondosha hatari hiyo kufeli. *

*Madhanbi Makubwa*!!!!
Baada ya hatua hiyo ya tatu, na kufika miezi minne (siku mia na ishirini, yaani arobaini tatu) ambapo ndio roho itakuwa ishapuliziwa hicho kiumbe, hapo patakuwa haparuhusiki kabisa na ni madhambi makubwa kabisa ila kwa dharura kuu kabisa k**a ilivyotajwa hapo nyuma, na tena kuwe kumefanyika juhudi kubwa za kuokoa hali sababishi (chenye kusababisha) na kwa hali hiyo kutakuwa kumetumika maslahi ya 'unafuu kati ya madhara mawili'. Na unafuu hapo ni uhai wa mama ambao ndio bora zaidi na wa msingi zaidi kuliko wa huyo kiumbe. Kwa sababu mama tayari kamili na anaishi na kuwepo kwake bado kuna matumaini ya kupatikana vizazi vingine, pia ni mwenye majukumu na wajibu katika maisha, na msimamizi wa nyumba, mlezi, n.k., hali hicho kiumbe kilichopo tumboni, hakina uhakika wa kuishi hadi kitakapozaliwa na haijulikani k**a kitakapozaliwa kitakuwa hai au la, na pia kisicho na majukumu yoyote kwa wakati huo. Kwa hali hiyo, kati ya kulinda na kuokoa hali moja kati ya mbili, basi kumuokoa na kumlinda mama ni bora zaidi kuliko kile kilichoko tumboni.
Hali hiyo uliyoieleza, inaonyesha hakukuwa na dharura hiyo, na hivyo huyo mwanamke katenda kitendo kiovu ambacho sheria haikikubali kabisa.

*Toba na Kafara*
Tendo hilo la dhambi, linahitaji toba kwa mtendaji; toba ya dhati kabisa.
Ama kafara ya kitendo hicho, wametofautiana Maulamaa wakati wake na hata aina ya kafara yenyewe. Baada ya kutazama pande zote, lililo lenye nguvu ni kuwa, kabla ya kupuliziwa roho kiumbe (kijusi), hakulazimiki kutoa kafara (fidia), pamoja na kuwa kuna wanaoona kuwa inapaswa kutolewa. Lakini aliyefanya kitendo hicho anatakiwa atubu toba ya kweli na azidishe kufanya 'amali nyingi za kheri na kutoa sadaka sana kulipa maovu yake, kwani mema hufuta maovu.

1⃣Ama baada ya _*kupuliziwa roho, hakuna tofauti kukubaliwa kwake kuwepo na kafara au kutolewa fidia 'Diyah' (blood money)*_ Baadhi ya Maulamaa wamesema kuwa kunatolewa fidia ya pesa kwa wale wenye kuhusiana na kiumbe hicho kwa kiasi cha gramu 213 za dhahabu, na wanalipwa wale wanaomrithi kile kiumbe (yaani kaka, dada au babu, bibi n.k. kulingana na sheria ya Mirathi), hatopewa yule aliyeshiriki kukitoa (kukiua) japo anaweza kumrithi. Na ikiwa wanaomrithi wakasamehe basi hakuna malipo. Kisha anatakiwa aache huru mtumwa (ikiwa inawezekana hilo), ikiwa haiwezekani au hakuna hali hiyo, basi anatakiwa afunge miezi miwili mfululizo ambayo ni kafara kwa ajili kuua.
K**a Asemavyo Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

*“Na haiwi Muumini kumuua Muumini ila kwa kukosea. Na mwenye kumuua Muumini kwa kukosea basi amkomboe mtumwa aliye Muumini, na atoe diya kuwapa jamaa za maiti, isipokuwa waache wenyewe kuwa ni sadaka. Na akiwa ni jamaa wa maadui zenu, hali yeye ni Muumini, basi ni kumkomboa mtumwa aliye Muumini. Na akiwa ni miongoni wa watu ambao pana ahadi baina yenu na wao basi wapewe diya watu wake na akombolewe mtumwa Muumini. Na asiye pata, basi afunge miezi miwili mfululizo, kuwa ni toba kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hekima*
” [An-Nisaa: 92]
Hivyo, utaratibu wa kufanya kwa yule aliyetoa mimba baada ya siku mia na ishirini (miezi minne) yaani baada ya kupuliziwa roho, ni huu:

Kufanya toba ya kweli, na milango ya toba iko wazi hadi wakati karibu jua litakapochomoza upande wa magharibi (kabla halijachomoza), au wakati wa gharghar (roho itakapokuwa imefika kooni wakati wa kutolewa ‘mkoromo wa mauti’). Na masharti ya toba ni haya yafuatayo:

⚡ *Masharti ya Toba*⚡
Kulipa fidia 'Diyah' (blood money);

Kafara kwa kukiua kiumbe, nayo ni kuacha huru mtumwa, au kufunga miezi miwili mfululizo.

*Mimba ya Zinaa*
⚡🍃Pia kutoa mimba kwa sababu imetokana na kitendo cha zinaa, ni jambo lisilokubalika kabisa. Kiumbe hakina makosa na tunajua kuwa habebi kiumbe madhambi ya mwengine. Allaah Anasema:
"Wala habebi mbebaji mzigo wa mwengine" [Al-An’aam: 164]
Na Amesema tena:
Na mbebaji habebi mzigo wa mwingine.)) [Faatwir 35:18]
Pia tukitazama kisa cha mwanamke wa ki-Ghaamidy aliyezini na akaenda kwa Mtue kutaka apewe adhabu ya mzinifu, na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamtaka aende hadi atakapozaa, na kasha akamrudisha tena hadi amnyonyeshe huyo mtoto na kisha mtoto alipokuwa mkubwa ndipo akatekeleza adhabu kwake. (Swahiyh Muslim).

Tukio hilo linatuonyesha kuwa mtoto japo wa kitendo cha zinaa hairuhusiwi kabisa kuuliwa anapokuwa tumboni.
Na tufahamu kuwa kila kiumbe kinachozaliwa kinakuwa ni Muislam, na huenda huyo mtoto wa tendo la zinaa akawa Muislam bora sana kuliko wengi. Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aallihi wa sallam) anasema: "Kila mtoto anazaliwa katika hali ya fitwrah (maumbile ya asli; Uislam)..." imepokewa na al-Bukhaariy

*Mwanamke aliyebakwa*
⚡🍃Vilevile mwanamke ambaye amebakwa, haruhusiwi kutoa mimba yake kwa kauli yenye nguvu, ingawa baadhi ya Maulamaa wanasema anaweza kutoa katika siku zile arobaini za mwanzo ikiwa kuwa kwake na hiyo mimba kutamsababishia madhara katika jamii yake au kwa watu wake ima kwa kumtenga, kumsusa au hata kumuua kwa kigezo cha ‘kulinda hadhi’ ya familia au ukoo. Lakini, pamoja na sababu hizo, utakuta hazitoshi kuhalalisha kutoa mimba kwani kufanya hivyo, ni kutenda dhambi nyingine na inajulikana kuwa hicho kilichopo tumboni hakihusiki kwa njia moja au nyingine na jarima ile ya kubakwa mwanamke huyo, na maadam haikuwa ridhaa ya mwanamke kufanywa hivyo na alijitahidi kupambana na mbakaji/wabakaji akazidiwa, ni wajibu wake kukihifadhi hicho kiumbe na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Atakilinda na kukijaalia kuwa ni chema na poza kwa mama yake.

⚡Na ikiwa mwanamke huyo hajaolewa, basi ni jambo jema kwa wanaume wa Kiislam kumsitiri na kumsaidia kumtoa katika mitihani hiyo iliyomkumba. Ama k**a ana mume, basi mume wake ajitahidi japo ni vigumu sana, kusubiri na kukikubali kiumbe hicho ambacho hakina hatia yoyote ile. Na malipo makubwa yanawasubiri watu aina hiyo.

*واللهُ أعلمُ*

*Wabillah Tawfiq*

۩• •۩┈┈┈•⊰ ۩ 🍃🍒🍃 ۩ ⊱•┈┈┈۩• •۩

Mauti ni Safari Ya Furaha Kwa Wenye Kufanya MEMA na ni Safari  Ya Majonzi  na Majuto Kwa Watendao MAOVU.Je,Mimi na Wewe ...
19/12/2021

Mauti ni Safari Ya Furaha Kwa Wenye Kufanya MEMA na ni Safari Ya Majonzi na Majuto Kwa Watendao MAOVU.Je,Mimi na Wewe Safari Hii ikitufikia tutakuwa Katika Kundi Gani?..Nakuomba jitaidi kufanya ibada hujui kwamb mwaka huu ndo utakua mwaka wako wa mwish au ukavuka wakumbushe
Watu 10 kwa kushare Au Zaidi.Na Ukipuuzia Uwe Na La Kujibu Mbele Ya Mwenyezi Mungu, Mimi Nimekukumbusha Nawe Wakumbushe na Wengine.
EWE MWENYEZI MUNGU SHUHUDIA
UJUMBE NIMEUFIKISHA

KISA CHA DHALIMU NA MVUVI~~~~~~~~~~~~~~~Inahadithiwa kuwa kulikuwa na mtu katili mdhulumaji kazi yake yeye nikudhulumu n...
03/12/2021

KISA CHA DHALIMU NA MVUVI
~~~~~~~~~~~~~~~
Inahadithiwa kuwa kulikuwa na mtu katili mdhulumaji kazi yake yeye nikudhulumu na kuwa saidia majambazi juu ya kuwaibia watu na kuwadhulumu na yeye alikuwa ndiye dhalimu mkubwa kuliko wote, siku moja akiwa anapita ktk fukwe ya bahari alimuona mvuvi ambaye alikuwa amevua samaki mkubwa sana yule dhalimu alimuona yule samaki , akamfuata yule mvuvi akamwambia maneno yakumtisha: nipe huyu samaki kwani wewe nani aliyekuruhusu kuvua ktk hii bahari yule mvuvi akamjibu kwa unyonge: lakini hiki ni chakula cha watoto wangu wadogo sina chakula chengine cha kuwapelekea ispokuwa huyu samaki tu, yule dhalimu alimpiga Kofi moja tu na akamchukua yule samaki kwa nguvu na akamuangusha yule mvuvi baharini yeye akaondoka na samaki.

Wakati yule dhalimu akiwa anarudi nyumbani kwake alifungua yule samaki mdomo wake kwa uwezo wa Allah na akaung'ata mkono wake kwa nguvu,alipofika yule dhalimu nyumbani kwake alimvuta yule samaki ili auchie mkono wake alimsababishia jeraha kibwa na maumivu makali, hadi usiku kucha hakupata usingizi kwa ajili ya maumivu ilipofika Asubuhi haraka alienda hospital akamuelezea dokta yaliyotokea, doctor akamwambia hii ni hatari sana italazimu tuukate mkono wako kabla sumu yake haijaenea mwilini ikakusababishia kifo.

Dhalimu alirudi nyumbani kwake akiwa mwenye huzuni akiwa hajui lakufanya , lakini mwisho aliamua azisikilize nasaha za doctor ukatwe mkono wake.

Hakika ulikatwa mkono wake, watu walimuuliza kilichotokea alikuwa yule dhalimu anawajibu huku akilia: hakika yamenitokea haya kwa sababu ya mvuvi wa samaki, siku moja huyu dhalimu alimuhadithia mzee mmoja naye mzee akamnasihi kuwa amtafute huyo mvuvi na amuombe msamaha akaendelea kumwambia: lau k**a ungelimtafuta kabla ya kukatwa mkono wako ukamuomba msamaha usingelikatwa mkono wako, kweli alitoka yule dhalimu kwenda kumtafuta mvuvi wa samaki kila sehemu hadi alimpata alipomuona tu aliinama kwenye miguu yake akaibusu huku akilia kwa uchungu na akimuomba msamaha yule mvuvi alishangaa sana na akamuuliza kwani wewe ni nani!!?
Yule dhalimu akamuelezea kuwa yeye ni yule aliyemchukuwa yule samaki wake kwa nguvu siku nyingi zilizopita na akamuhadithia yote yaliyotokea, yule mvuvi alilia sana kwa Yale yaliyomtokea yule dhalimu akamwambia nimekusamehe, yule dhalimu akamwambia: naomba uniambie ulifanya nini nilipomchukua yule samaki wako kwa nguvu?
Akasema yule mvuvi: nilisema ivi kumuomba Allah: Ewe mola wangu hakika huyu dhalimu amenidhulumu na ameichukua rizki yangu na rizki ya watoto wangu na amenishinda kwa nguvu zake ewe mola wangu nionyeshe nguvu zako kwake...
Hiyo ni dua ya aliyedhumiwa.
______________
Tahadhar sana kutumia nguvu zako cheo chako mamlaka yako ukawadhulumu watu silolote sichochote uwezo wake Allah nimkubwa zaidi yako akitaka kitu husema KUN FAYAKUUN

Kisa hiki kimetafsiriwa:

🌿DARSA YA FIQHI🌿

UJUMBE WA USIKU~~~~~~~~~~~~LEO KTK UJUMBE WA USIKU:Usihuzunike pindi ALLAH atakapo kunyima kitu unacho kipenda, na wala ...
23/10/2021

UJUMBE WA USIKU
~~~~~~~~~~~~
LEO KTK UJUMBE WA USIKU:

Usihuzunike pindi ALLAH atakapo kunyima kitu unacho kipenda, na wala usikate tamaa pindi utakapo lazimika kuishi na hali yenye kukuumiza, kwa sababu ALLAH mtukufu amesema kwa rahma zote:

وَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تُحِبُّوا شَيْئًا وَهُوَ شَرٌّ لَّكُمْ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

*Na asaa mkachukia jambo na hali lenyewe ni khayr kwenu. Na asaa mkapenda jambo na hali lenyewe ni la shari kwenu. Na Allaah Anajua na nyinyi hamjui.*

[ Albaqarah 216 ].

🌿NAWATAKIA UCKU MWEMA🌿

UMETANGULIZA NINI AAKHERAH?Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’alaa) ;18. Enyi mlioamini! Mcheni Allaah, na nafsi itazame i...
13/09/2021

UMETANGULIZA NINI AAKHERAH?

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’alaa) ;

18. Enyi mlioamini! Mcheni Allaah, na nafsi itazame imetanguliza nini kwa ajili ya kesho (Siku ya Qiyaamah), na mcheni Allaah. Hakika Allaah ni Khabiyr ( Mjuzi wa yaliyodhahiri na yaliyo fichikana) kuhusu myatendayo.
[Al-Hashr: 18]

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَلْتَنظُرْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ لِغَدٍ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ﴿١٨﴾

Siku ya Qiyaamah katika Qur-aan imetajwa kwa majina kadhaa.

Baadhi ya ‘Ulamaa wamenukuu idadi yake kuwa ni majina thelathini na moja takriban. Miongoni mwayo;

Al-Ghad (kesho),

As-Saa'ah (saa),

At-Taghaabun (siku ya hasara au sikuya kulipizana),

Yawmul-Ba'th (siku yakufufuliwa),

Yawmul-Aakhirah (siku ya Mwisho),

Yawmud-Diyn (siku ya malipo),

Yawmul-Faswl (siku ya hukumu),

Al-Waaqi'ah (tukio),

Yawmul-Wa'iyd (siku ya makamio)
na majina mengineo.

Kwa hayo, jiulize Muislamu, je, umetanguliza nini Aakhirah?

Umetimiza Swalah zako ipasavyo?

Umetanguliza Swalaah za Sunnah?

Umetekeleza Zakaah na umetoa swadaqah?

Umefunga Swiyaam Ramadhaan na Swiyaam za Sunnah?

Umetekeleza Hajj na 'Umrah?

Umesoma Qur-aan kwa wingi na kufuata maamrisho yake na kujiepusha na makatazo yake?

Umeamrisha mema na kukataza maovu?

Umetanguliza wema wa ainayoyote?

Kumbuka kwamba jema lolote utakalolitenda litakuwa ni akiba yako Aakhirah na bila shaka utakuja kulikuta na utapata malipo yake siku ya Qiyaamah k**a Anavyosema Allaah Subhaanau wa Ta’alaa:))

Na simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah, na lolote mnalolitanguliza kwa ajili ya nafsi zenu katika kheri mtalikuta kwa Allaah, hakika Allaah kwa myafanyao ni Baswiyr (Mwenye kuona)))
[Al-Baqarah: 110].

وَأَقِيمُواْ الصَّلاَة

َ وَآتُواْ الزَّكَاةَ وَمَا تُقَدِّمُواْ لأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ اللّهِ إِنَّ اللّهَ بِمَاتَعْمَلُونَ بَصِيرٌ((

Mlete mwanao apate malezi BoraFor more information contact me @0654729993Nipigie namba apo juu
05/09/2021

Mlete mwanao apate malezi Bora
For more information contact me @0654729993
Nipigie namba apo juu

Address

Mkuzo
Songea

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when muslim_ikhwaan posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to muslim_ikhwaan:

Share