01/06/2025
2 wakoritho 6:17-18” Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike”hapa ndipo tatizo lilipo na ndipo kasema usiguse kichafu
1 wakoritho 2:9 “lakini, k**a ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. maana yake mungu amendaa kitu kwa hao wampendao nilijaribu nilitaka kujua mstari huu ni halisi kwahiyo nilifanya vipomo nilijitenga na nikasema sitagusa kilicho najisi na nilipokuwa chuo cha biblia nilianza kuona watu wanaanza kunililetea fedha wanani kabidhi ikiwa siwafahamu, nikagundua kumbe Mungu ametuandalia kitu.
Katika Mungu hakuna uchache nilizunguka nikiwa na watu katika injili nilitaka kujua atanipokea, nilitaka kujua wapi tutakula maana yeye nimwenyeji wangu, kwahiyo nilijaribu nijue je nikweli na lifanya kazi? na ikawa. Ili tupate hicho alicho sema kuna mambo mawili tunapasa kufanya, yapasa tujitenge nao na tusiguse kilicho kichafu, inawezekana tusitende dhambi lakini ukagusa na kushirikiana nao ukanajisika. kwasababu yeye ni mtakatifu, utakatifu hauendani na uchafu(unajisi). Na nilipoamua kufanya hivyo niliona Mungu akiniletea watu tofauti, kwaajili ya kusababisha kazi yake iende sikupungukiwa Fedha, chakula wala sehemu ya kulala.
K**a Elia alikuwa narishwa na kunguru walikuwa wanapata wapi,? nikasema kwangu mimi jambo hili ndilo nitakalo lizingatia. Nataka jitenge nao, wakati mwingine ni vigumu maana sikio letu linapenda upuuzi macho yetu yanapenda upuuzi na tunapenda kutenda katika vitu vya kipuuzi, lakini kwangu mimi nilijitengana watu wakaona k**a nichanganyikiwa. Nilikuwa naimba kila wakati kwasababu nilikuwa sitaki kusika maneno yoa, nilifanya maamuzi ya kujitenga nao na nilikuwa peke yangu. Na mimi peke yangu ndio niliyefanikiwa na kufanya vizuri na vya tofauti.