Efatha Church Kiomboi

Efatha Church Kiomboi Huduma ya Efatha ni huduma ya ukombozi na uponyaji kwa Damu ya YESU.

Zaburi 136:1 Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
25/03/2025

Zaburi 136:1
Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

IBADA YA JUMAPILI TAR. 16.03.2025MCHUNGAJI:LUCY E.MOSHISOMO: MWENENDOTUPO KATIKA MWAKA WA KUKAA KATIKA NAFASI ILI TUMILI...
16/03/2025

IBADA YA JUMAPILI TAR. 16.03.2025
MCHUNGAJI:LUCY E.MOSHI
SOMO: MWENENDO
TUPO KATIKA MWAKA WA KUKAA KATIKA NAFASI ILI TUMILIKI, KWAHIYO LAZIMA TUANGALIE MWENENDO WETU.
Zaburi 50:23
Unapotoa sadaka ya kushukuru unamwambia Bwana fanya tena.
Anaposema nitakuonyesha wokovu anasema nitakupa neema, maana neema unapokea mambo ambayo hukustahili kupokea.
Haya yote yanatokea baada ya kutengeneza mwenendo.
Mwenendo ni tabia ya siri ya mtu, namna anavoishi.
Mwewendo pia ni tabia ya mtu. Tabia inaweza kumfanya mtu asipokee kile anachostahili kuupokea.
Wafilipi 1:27
Waefeso 4:22
Biblia inasema uache mwenendo wa kwanza uliozaliwa kwa baba na mama kwa sababu wewe umezaliwa mara ya pili.
- unapoanza kubadilisha mwenendo jua namna ya kuongea.

IBADA YA JUMAPILI TAR 9.2.2024MCHUNGAJI: LUCY EMANUEL MOSHISOMO: KUKAA KATIKA NAFASI ILI UWEZE KUMILIKI.   Zaburi 118:5 ...
09/02/2025

IBADA YA JUMAPILI TAR 9.2.2024
MCHUNGAJI: LUCY EMANUEL MOSHI
SOMO: KUKAA KATIKA NAFASI ILI UWEZE KUMILIKI.
Zaburi 118:5
Katika shida yangu nalimwita BWANA;BWANA akanijibu akaniweka panapo nafasi.
Anayemwema mtu kwenye nafasi ni Mungu mwenyewe.
Unatakiwa imara katika nafasi uliowekwa usitikisikie.
Tambua nafasi yako pia tambua nafasi ya mwingine.
1.Tunawezaje kukaa kwenye nafasi zetu?
Tunaweza kukaq kwenye nafasi zetu kwa kumgeukia Bwana. Maana nafasi tumepewa na Bwana.
2 Nyakati 20:3

FAIDA ZA KUKAA KWENYE NAFASI
Matendo ya mitume 2:1-4
1.Walikaa pamoja wakiomba kwa pamoja na wakapokea kwa pamoja.
Mwanzo 21:14-17.
2.Unakuwa salama wewe na uzao wako.
Hatakuacha pekeako usaidizi utakujilia ulipo.
Tamani kuwa na Yeye nyakati zote.

-Ili uweze kukaa kwenye nafasi fuata maelekezo ya Yesu kuhusu maombi.
Mathayo 6:9
Namna ya kuomba.
1.Kunatofauti ya kusema na kuzungumza
Kuomba maana yake tunaomba yale ambayo hayapo kwenye ahadi yake, tunaomba ili atupatie.
Ahadi ni yale mambo hatuombi ila tunadai atupe maana alituahidi

HERI YA SIKU YA KUZALIWA BABA YETU JOSEPHAT ELIAS MWINGIRAMtu anayeupendeza moyo wa Mungu mwenyewe, kielelezo cha kweli ...
31/12/2024

HERI YA SIKU YA KUZALIWA BABA YETU JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA

Mtu anayeupendeza moyo wa Mungu mwenyewe, kielelezo cha kweli cha ubaba, mshauri, na kiongozi mwema katika Kristo. Imani yako isiyoyumba, usimamizi wa kipekee, na mafundisho yenye matokeo yameathiri sana na kubadilisha maisha ya watu wengi duniani kote. Kujitolea kwako kuendeleza ufalme wa Mungu kunatumika k**a msukumo kwetu sote.

Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa mchango wako wa thamani kwa Mwili wa Kristo na huduma yako ya kujitolea kwa Bwana. Uongozi wako umekuwa mwanga elekezi nchini Tanzania na duniani kote. Tuna imani kamili kwamba Mungu ataendelea kukutia nguvu katika kila eneo, akikujalia nguvu, utukufu, neema na hekima unapotimiza kusudi lake maishani mwako.

Kwa heshima kubwa na shukrani, tunakuheshimu na tunakupenda Baba yetu wa Kiroho, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.

HERI YA MWAKA MPYA 2025
31/12/2024

HERI YA MWAKA MPYA 2025


IBADA YA JUMAPILI TAR 13.10.2024MCHUNGAJI: LUCY E. MOSHI  SOMO: KUIENDEA SIKU YAKO NA KUIFIKIA SIKU YAKO.   Mwanzo 2:1-3...
13/10/2024

IBADA YA JUMAPILI TAR 13.10.2024
MCHUNGAJI: LUCY E. MOSHI
SOMO: KUIENDEA SIKU YAKO NA KUIFIKIA SIKU YAKO.
Mwanzo 2:1-3
Mungu aliitakasa na kuitenga siku ya saba, ndivyo ilivo kuna watu wametengwa kwa aajili ya kazi au mambo flani ya Mungu.
Mambo ya walawi 20:26
Nanyi mtakuwa watakatifu kwangu mimi; kwa kuwa mimi BWANA ni mtakatifu nami nimewatenga ninyi na mataifa, ili kwamba mwe wangu.
Kabla ya mambo yote lazima ujue kwamba mimi nimechaguliwa na kutengwa na watu wengine, ili kuruhusu siku iliyoandaliwa kukujilia.
Warumi 12:2
Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
-Katika kuelekewa katika umiliki wetu kuna tabia ambazo hazitakiwi kuonekana kwetu maana hayatatuwezesha kufikia umili wetu, vitatuzuilia kupokea yale tunatamani kuyapokea.
Waefeso 4:23 -24
na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu;mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.
-lazima kuwe na mabadiliko ili kufikia umiliki watu. Kunasababu ya kufanya mabadiliko na kuna mabadiliko mengine huja kwa maumivu.

IBADA YA JUMAPILI TAR. 08.09.2024MCHUNGAJI:LUCY E. MOSHI SOMO:HOFU YA MUNGU   K**a ndani yako hakuna hofu ya Mungu utafa...
08/09/2024

IBADA YA JUMAPILI TAR. 08.09.2024
MCHUNGAJI:LUCY E. MOSHI
SOMO:HOFU YA MUNGU
K**a ndani yako hakuna hofu ya Mungu utafanya vitu ambavyo havimpendezi Mungu.
1. Ni maisha ambayo mtu anaishi kwa kuzingatia. Unazingatia umejifunza nini umesikia nini.
2. Ni mtu anayemweshimu Mungu
K**a mtu hana hofu ya Mungu utamjua kwa kutenda kwake na kunena kwake.
Luka 12:5
Lakini nitawaonya mtakayemwogopa; mwogopeni yule ambaye akiisha kumwua mtu ana uweza wa kumtupa katika Jehanum; naam, nawaambia, Mwogopeni huyo.
1Wakoritho14:33
Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile k**a ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu.
Mwanzo 20:1-11
Ibrahimu alipoingia katika mji ule akagundua hawa watu hawana hofu ya Mungu, wanaweza kufanya chochote katika maisha yangu.
Akamwambia mke wake ukiulizwa wewe nani usiseme k**a wewe ni mke wangu wakijua wataniua kwa sababu watu hawa hawana hofu ya Mungu.

Usipange kukosa mwana wa Mungu.
19/08/2024

Usipange kukosa mwana wa Mungu.

Maombezi na ukombozi
18/08/2024

Maombezi na ukombozi

IBADA YA LEO TAR 18.08.2024     MCHUNGAJI: LUCY E.MOSHISOMO: KAZI YA KUKAA NDANI YA YESU.  Baada ya kuokoka kazi ya kudu...
18/08/2024

IBADA YA LEO TAR 18.08.2024
MCHUNGAJI: LUCY E.MOSHI
SOMO: KAZI YA KUKAA NDANI YA YESU.
Baada ya kuokoka kazi ya kudumu ndani ya wokovu ni ya kwako.
Yohana 15:1-5
Kaeni ndani Yangu nami ndani yenu.
Mimi ni mzabibu nanyi ni matawi akaaye ndani yangu nami ndani yake huzuaa sana mana pasipo Mimi ninyi hamuwezi kufanya jambo lolote.
Anaposema habari ya kuzaa maana yake kuna maongezeko. Na ili kuwe na maongezekeo lazima mtu akae kwenye mzabibu.
Namna gani tunaweza kukaa ndani yake:
1. Uwe ni mtu wa kushika maagizo yatokayo kwenye mzabibu.
2. Heshimu matakatifu ya Mungu- heshimu viongozi waliopo mbele yako.
Wafilipi 4:8
Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.

Ziara ya Mchungaji wa kanda ya kiomboi, alipotembelea kituo cha Efatha kinampanda.
18/08/2024

Ziara ya Mchungaji wa kanda ya kiomboi, alipotembelea kituo cha Efatha kinampanda.

Address

New Kiomboi
Singida

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Efatha Church Kiomboi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share