28/04/2023
UFALME WA MUNGU - [ADVANCED LEVEL -01]
kuwaza kuingia katika UFALME WA MUNGU basi haya ambayo yameandikwa hapa yanakufaa sana.
📌Shalom!!!, Bwana Yesu Kristo apewe sifa!!! Nakusalimu wewe uliyepata neema ya kuyasikia haya mahali popote pale ulipo, karibu!!!
✍🏽Ni jambo jema kuwa sisi sote tumekuwa na shauku ya kumjua zaidi Bwana Mungu na Ufalme wake na mapenzi yake ndani ya huo Ufalme.
✝️Pamoja na shauku hiyo, si watu wote wanafanikiwa kumjua Mungu na Ufalme wake na mapenzi yake ndani ya UFALME wake , na kuingia ndani ya UFALME WA MUNGU.
📚Tuanze hapa kwa maneno haya ya Bwana Yesu Kristo juu ya UFALME na tutajua hasa nini huwa kinazungumzwa ndani ya UFALME WA MUNGU na hicho ni lengo kuu la fundisho hili. 👇🏽
📖Mathayo 7:21-23
[21] Si kila mtu aniambiaye, Bwana , Bwana , ATAKAYEINGIA katika UFALME WA MBINGUNI ;bali ni yeye AFANYAYE MAPENZI YA BABA YANGU aliye mbinguni.
[22] Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, HATUKUFANYA UNABII kwa jina lako, na kwa jina lako KUTOA PEPO , na kwa jina lako KUFANYA MIUJIZA MINGI ?
[23] Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, NINYI MTENDAO MAOVU .
📚 Nimeanza kwa maneno hayo ambayo Bwana Yesu Kristo anasema kwa namna ya ajabu kidogo , juu ya UFALME WA MUNGU na kwa kweli si maneno ya kuyafurahia kwa anayeambiwa /anayelengwa,,,,,, lakini mambo ambayo nilitaka tuyaone kwenye maandiko hayo ni k**a ifuatavyo;~
[1] UHUSIANO ULIOPO KATI YA UFALME WA MUNGU NA KUYAFANYA MAPENZI YAKE
✍🏽Kulikuwa na haja gani ya hao ndugu kujitetea kwao na kutaka kupata kibali mbele ya Bwana Yesu Kristo kuingia katika UFALME WA MBINGUNI kwa kutumia MAMBO WALIYOYAFANYA K**A UTUMISHI WAO /UTENDAJI WAO ikiwa hakuna Uhusiano wowote wa KUTENDA HUKO NA HABARI ZA UFALME ?!
hivi kuna uhusiano wa namna ya KUTENDA MAPENZI YA MUNGU na kuingia katika UFALME WA MUNGU .
🎓Swali litakuja, je ni yapi hayo mapenzi ya Mungu, ambayo YESU KRISTO alisema hakuna namna ya kuingia katika UFALME WA MBINGUNI /Mungu isipokuwa umeyafanya.
📖Mathayo 7:21
Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni YEYE AFANYAYE MAPENZI YA BABA YANGU ALIYE MBINGUNI.
👆🏽Baada ya kauli hiyo unaona kundi kubwa la watu watakaokuja kuonesha namna yao ya UTENDAJI wakidhani yalikuwa ni mapenzi ya Mungu, na mambo hayo ni ;-
(a) KUFANYA UNABII KWA JINA LA YESU,
(b) KUTOA PEPO KWA JINA LA YESU,
(c) KUFANYA MIUJIZA MINGI KWA JINA LA YESU.
👆🏽Na Yote hayo YESU KRISTO akatoa kauli kuwa KUFANYA HAYO YOTE SI KUFANYA MAPENZI YA MUNGU nao ni UOVU .
=} Inawezekana ikakushangaza kidogo kuona kauli k**a hiyo ya BWANA YESU, kuwa KUTOA PEPO KWA JINA LAKE, KUFANYA UNABII KWA JINA LAKE, NA KUFANYA MIUJIZA MINGI KWA JINA LAKE, SI MAPENZI YAKE, jambo ambalo machoni pa wapendwa wengi huyaona mambo hayo ndio UTUMISHI / NDIO HASA KUMTUMIKIA MUNGU na ndio MAPENZI YAKE kitu ambacho BWANA WAO YESU KRISTO anasema huo ni UOVU.
👆🏽Yesu Kristo hakatai kuwa HAVIKUFANYIKA (ni kweli walitoa pepo tena kwa jina lake, walifanya unabii na kufanya miujiza mingi k**a kuponya wagonjwa, viwete kuona, n.k)..... Kwa hiyo ni KWELI VYOTE HIVYO VILIFANYIKA tena kwa jina la Yesu Kristo na hao walioyafanya hayo WANAMWITA YESU KRISTO kuwa ni BWANA, BWANA WAO.
📖"SI KILA MTU ANIAMBIAYE BWANA, BWANA...... "
kwa maneno mengine ni watu ambao walimwamini KRISTO k**a BWANA wao. Lakini walifanya uovu katika kuyafanya hayo.
✍🏽NGOJA NILIWEKE HILI WAZI.
MAPENZI YA MUNGU HASA ambayo ndio lengo /target (shabaha) ya Mungu, katika UFALME WAKE NI WATU KUBATIZWA yaani KUINGIA UHUSIANO NA MUNGU na huko ndiko KUZALIWA MARA YA PILI NA KUWA WANA WA MUNGU .
✍🏽Labda utakuwa hujanielewa vizuri,,, niseme hivi MAPENZI YA MUNGU ni wewe KUZALIWA MARA YA PILI na KUWA MWANA WA MUNGU NDANI YA UHUSIANO NA YEYE kwa njia ya KRISTO YESU pekee !!!
👆🏽Na hicho ndicho kinachokupa kuingia NDANI YA UFALME WA MUNGU /MBINGUNI.
✝️Hebu tusome wote maandiko haya
📖Mathayo 28:19-20
[19] Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote KUWA wanafunzi, MKIWABATIZA kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu ;
[20] na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
✝️👆🏽Mistari hiyo inatupa kuona kuna kufanywa kuwa MWANAFUNZI wa Yesu Kristo lakini hiyo inatosha?! Jibu ni Hapana kuna zaidi unapaswa kufika na mahali hapo ni kwenda KUBATIZWA!!!
✝️👆🏽 KUBATIZWA huko ni kupi? Jibu ni rahisi ni juu ya kuingia kwenye UHUSIANO NA MUNGU kwa njia ya KRISTO YESU.....UHUSIANO au MUUNGANIKO huo huitwa NDOA YA AGANO JIPYA kati ya KRISTO NA WANADAMU.
✝️👆Aina hiyo ya UHUSIANO ndio inayokufanya kuzaliwa katika familia ya MUNGU na Familia hiyo iko kwa namna ya Utawala wa KIFALME ndio huo uitwao UFALME WA MUNGU.
✝️📚Kwa hiyo kwa lugha rahisi kabisa k**a ambavyo ilivyo kwa ndoa ya mfano ya MME na Mme kuwa mwili mmoja ndivyo ilivyo MUUNGANIKO wa mtu na KRISTO YESU na kuwa Roho mmoja na huo ndio UBATIZO unaozungumzwa na biblia ambao pasipo huo huwezi kuzaliwa mara ya pili na kuingia katika UFALME WA MUNGU.
✝️👆🏽Katika maandiko utakutana na maneno k**a haya kueleza UBATIZO huo 👇🏽
📖Warumi 6:3-5
[3] Hamfahamu ya kuwa sisi sote TULIOBATIZWA katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?
[4] Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya UBATIZO katika mauti yake, kusudi k**a Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.
[5] Kwa maana k**a MLIVYOUNGANIKA naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake;
🎓✍🏽 Hakuna UFUFUO kwa UZIMA WA MILELE isipokuwa umebatizwa,
➡️Hakuna UZIMA WA MILELE isipokuwa UMEBATIZWA,
➡️HAKUNA kuingia katika UFALME WA MUNGU isipokuwa UMEBATIZWA.
[2] Jambo la pili ambalo nilitamani tuone kwa pamoja ni hili :-
➡️ KUNA UWEKANO WA MTU KUMWAMINI YESU KRISTO NA ISIFIKE /ASIKUBALI KUFIKA MAHALI PA YEYE KUBATIZWA NDANI YA KRISTO YESU .
✍🏽K**a nilivyokwisha kueleza maana halisi ya KUBATIZWA k**a inavyozungumzwa ndani ya Biblia, kuwa ni mtu KUKUBALI kuingia katika UHUSIANO na KRISTO YESU kiasi cha yeye na maisha yake yote kumezwa ndani ya KRISTO YESU na UHUSIANO HUO WA KIMAISHA , uletao tokeo la maisha mapya ya KRISTO YESU kwa mtu huyo.
📚 Lakini unaweza ukawa na swali kuwa inawezekanaje mtu akafika mahali pa KUMWAMINI YESU KRISTO na ASIKUBALI / ASIFANIKIWE KUBATIZWA ? ....ok Swali zuri!!
📖 Jambo moja la ajabu ni kuwa mtu yeyote anayefika mahali pa KUBATIZWA kwanza alianza na KUMWAMINI YESU KRISTO k**a BWANA na hitimisho la imani yake ikawa ni maamuzi yake ya KUUNGANA NA KRISTO katika UHUSIANO (USHIRIKA) wa MAISHA kwa yeye kuyaacha maisha yake na aanze kuishi ndani ya maisha ya KRISTO YESU, nikiwa na maana hii AISHI kwa MWELEKEO WA MAISHA YA BWANA wake au k**a ATAKAVYO BWANA YESU KRISTO.
👆🏽➡️ Nimesema kuwa kuna uwezekano wa mtu kumwamini YESU KRISTO lakini aisisalimishe maisha yake kwa Kristo Yesu ndani ya UHUSIANO wa KIAMAISHA na YESU KRISTO UHUSIANO utakaomfanya azaliwe katika uzao mpya wa familia ya UFALME WA MUNGU yaani kuzaliwa mara ya pili ,,,
👆🏽✍🏽Ndio maana agizo la BWANA Yesu Kristo katika [ Mathayo Mt 28 :18-20) kwa wanafunzi wake lilikuwa si tu kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi pakee yake, bali na KUWABATIZA k**a wangefundisha mataifa na wakawa wanafunzi wa YESU KRISTO halafu wasifanye ushirika na KRISTO YESU hapo tutasema mapenzi ya Mungu HAYAFANYIKA (rudia tena kusoma hapa).
✝️👆🏽Maelezo hayo, tunayaona hapa kwa maneno mengine katika kitabu cha MARKO 16, BADO MSISITIZO UKIWA NI WATU KUBATIZWA!!! maana ndio hasa mapenzi ya Mungu.
📖Marko 16:15-16
[15] Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
[16] AAMINIYE na KUBATIZWA ATAOKOKA ; asiyeamini, atahukumiwa.
⬆️Angalia vizuri huo mstari wa 16 Injili ya Marko 16, kuna vitu viwili vikubwa hapo, KUAMINI na KUBATIZWA.......
✍🏽Kwa hiyo, katika hatua za mtu kwenda KUOKOKA haubatizwi ndipo UAMINI , isipokuwa UNAAMINI ndipo UNABATIZWA na hicho kitendo cha KUBATIZWA ndio huzaa WOKOVU unaokupa KUINGIA KATIKA UFALME WA MUNGU.
🎓Narudia tena TUNAAMINI KWANZA ndipo TUNAPOENDA KUUNGANA na KRISTO YESU, kwa MUUNGANIKO wa ki-ndoa yaani kuishi maisha MAMOJA yaani maisha yake KRISTO YESU BWANA, KUSUDI MOJA , FAMILIA MOJA YA KIFALME, na WARITHI WA BARAKA ZILE ZA MUNGU KATIKA HUO UHUSIANO - k**a matokeo ya UBATIZO HUO.
📖 "WOKOVU hauji tu kwa KUMWAMINI pekee lakini huja kwa KUBATIZWA baada ya KUMWAMINI"..... Hii ndio inaleta maana ya maneno haya...
" AAMINIYE na KUBATIZWA ATAOKOKA ".......... katikati ya maneno AAMINIYE na KUBATIZWA kuna kiunganishi neno "na" lenye maana sana katika sentensi hiyo kukamilisha au kuleta umaana wa tokeo la mwisho ambalo ni MTU KUOKOKA na tokeo hilo halifikiwi isipokuwa MTU huyo aliyeamini AMEBATIZWA!!! Amen 🙌🏾
➡️ Ndio maana nikasema kuna uwezekano wa mtu kumwamini YESU, na asifanye maamuzi ya kuingia kwenye uhusiano na KRISTO YESU na hili lilitokea kwa unabii katika kitabu cha Injili ya YOHANA MT 8 hebu tusome kwa pamoja habari hii ambayo ni unabii wa mambo yqnayotimia katika nyakati hizi tulizonazo....
📖Yohana 8:31
Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi WALIOMWAMINI , Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli;
⬆️ Ohh !!! , mstari huo unaonesha wazi Bwana Yesu akianza kuzungumza na wayahudi, na tunaona hawa watu tayari mioyoni mwao walikuwa tayari WANA-IMANI na YESU KRISTO lakini IMANI yao haikuwapa KUOKOKA na kuzaliwa mara ya pili ili wawe WANA WA MUNGU yaani kuwa ndani ya FAMILIA YA MUNGU kwa njia ya UBATIZO nazungumza UBATIZO k**a MFUMO WA MAISHA sizungumzii ubatizo wa kuzamishwa ndani ya maji mengi tukio la siku moja,.....
⬆️Ukiendelea kusoma habari hiyo, utaona maneno haya
📖Yohana 8:32-33
32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka HURU .
[33] Wakamjibu, SISI TU UZAO WAKE IBRAHIMU , wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wasemaje, Mtawekwa huru?
⬆ Kumbuka Uzao wa IBRAHIMU unatambulika kwa njia ya IMANI (IBRAHIMU anazaa kwa njia ya IMANI) sawa na ⬇️
📖Wagalatia 3:7 Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa IMANI , hao ndio wana wa IBRAHIMU .
✍🏽Ok sasa turudi hapo juu unaona wayahudi wakijitetea kuwa wao HAWAJAWAHI KUWA UTUMWANI wakati wowote kwa sababu wao ni uzao wa IMANI- IBRAHIMU..... (wamezaliwa katika imani).... lakini YESU KRISTO akawaeleza hiyo hiyo kuwa mtu wa IMANI haitoshi mpaka utakapozaliwa kuwa uzao wa MUNGU na kuwekwa huru mbali na ASILI YA UTUMWA WA DHAMBI kwa njia ya UBATIZO (Ingawa hapo katika Injili ya YOHANA MT 8 hajatumia neno UBATIZO ametumia neno - KUZALIWA KATIKA UZAO MPYA WA MUNGU).
⬇️Chukua mistari hii na uitafakari
📖Yohana 8:34, 36, 41-42, 47, 51
[34] Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.
[36] Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.
41 Ninyi mnazitenda kazi za baba yenu. Ndipo walipomwambia, Sisi hatukuzaliwa kwa zinaa; sisi tunaye Baba mmoja, yaani, Mungu.
[42] Yesu akawaambia, K**a Mungu angekuwa baba yenu, mngenipenda mimi; kwa maana nalitoka kwa Mungu, nami nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma.
[47] Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; hivyo ninyi HAMSIKII KWA SABABU NINYI SI WA MUNGU .
[51] Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele .
[3] Jambo la tatu ni hili :-
" Mambo yafanyikayo kwa IMANI hayamfanyi kuwa AMEOKOKA ".
📖 Marko 16:17-18
[17] Na ishara hizi zitafuatana na hao WAAMINIO ; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya ;
[18] watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya .
⬆️ Jambo la ajabu kidogo ambalo si kila mtu anaweza kuliona hapo kwenye mistari hiyo ni kuwa BWANA YESU KRISTO alitoa ruhusa ya mambo kadha wa kadha KUFANYIKA tena KWA JINA LAKE kigezo kikiwa ni IMANI tu katika KWA JINA LAKE juu ya utendaji wa hayo KWA UWEZO /MAMLAKA YA mwenye JINA HILO na si kwa WALIOBATIZWA akasema ISHARA HIZI zitafuatana nao WAAMINIO .
⬇️⬆️ Usifurahie KUTOA PEPO kwa Jina lake , KUFANYA UNABII kwa jina lake, Kuweka mikono juu ya wagonjwa wakapata afya, ukaishia hapo YESU KRISTO anaziita hizo ni ISHARA. Rudia tena kusema ISHARA,,,, ok kwa kifupi kabisa ISHARA huwa ni lugha ya mafumbo, inayozungumza kitu HALISI KWA MFANO .
✝️ Kwa hiyo ISHARA si mambo halisi ila ni kivuli cha MAMBO HALISI.
Unaweza kuweka mkono juu ya mgonjwa akapata AFYA na si UZIMA kuna tofauti kati AFYA NA UZIMA, si kila mwenye AFYA ana UZIMA, kwa hiyo AFYA ni ISHARA inayozungumza juu ya UZIMA WA MILELE ule wenye asili ya MBINGUNI.
⬆️ ISHARA zote zinazosemwa kuwa zitafanywa na wale WAAMINIO kwa lugha rahisi zinazungumza juu ya tendo moja UBATIZO / KUOKOKA/ KUZALIWA KATIKA MAISHA MAPYA NDANI YA FAMILIA YA KIFALME YA MUNGU.
✝️✍🏽Tena kuna uwezekano wa kuyafanya hizo ISHARA hata k**a HUJABATIZWA maadamu tu wewe ni miongoni mwa waitwao " WAAMINIO " ndio maana unaona hao YESU KRISTO anakuja kuwakataa kwenye MATH 7 kwa kuwaambia ⬇️
📖 Mathayo 7:22-23
[22] Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, HATUKUFANYA UNABII kwa jina lako, na kwa jina lako KUTOA PEPO , na kwa jina lako KUFANYA MIUJIZA MINGI?
[23] Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi MTENDAO MAOVU .
⬆️Kuishia tu kufanya ISHARA KWA JINA LAKE kwa sababu ya IMANI na USIINGIE ndani ya UHUSIANO na BWANA YESU KRISTO (KUBATIZWA) huko ndiko KUFANYA MAOVU.
🎓📚 Wanafunzi wa YESU KRISTO nao kidogo waingie kwenye mtego huo ambao wengi wa watumishi hufurahia sana kuona " ISHARA " hizo zikifanyika na wasikumbuke kuwa MAPENZI YA MUNGU ni watu KUBATIZWA na sio kufanywa kwa ISHARA.
📖Luka 10:17-20
[17] Ndipo wale sabini WALIPORUDI KWA FURAHA , wakisema, Bwana, hata pepo WANATUTII KWA JINA LAKO.
[18] Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni k**a umeme.
[19] Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.
[20] Lakini, MSIFURAHI KWA VILE PEPO WANAVYOWATII ; bali furahini kwa sababu MAJINA YENU YAMEANDIKWA MBINGUNI .
⬆️ Unaweza kufikiria kuwa FURAHA ya wale watumishi wa YESU KRISTO walipoleta mrejesho wa UTUMISHI WAO juu ya KUTOA PEPO KWA JINSI LAKE hiyo Furaha yao HAIKUWA FURAHA ya YESU KRISTO,...kwa sababu msingi wa FURAHA yao ilikuwa ni PEPO KUWATII waliamuru kwa jina la BWANA YESU KRISTO, huku FURAHA YA KRISTO YESU ikawa juu ya kitu kingine " MAJINA YAO KUANDIKWA MBINGUNI "
⬆️ Furaha ya UTUMISHI wako ni ipi? Furaha ya IMANI yao ni ipi? Je lengo la UTUMISHI wako ndio lengo la MUNGU? Kusudi na mikakati ya UTUMISHI wako kwa Mungu ni sawasawa na BWANA wa huo UTUMISHI?! maana inawezekana kabisa akawa ni Bwana, Bwana katika UTUMISHI wako na akaishia kusema " SI KILA MTU ANIAMBIAYE BWANA, BWANA ATAKAYEINGIA KATIKA UFALME WA MBINGUNI....... " kwa Imani yako akawa ni BWANA lakini ukagoma KUBATIZWA.
🎓✍🏽Mwisho nihitimishe kwa kusema kuwa yote ulivyojifunua mahali hapa, yalikuwa na lengo la kukuleta mahali pa KUBATIZWA uingie katika NDOA ya Wewe na KRISTO YESU ndoa ya MAISHA YAKO YOTE yasiwe tena yako uishi katika MAISHA YAKE, na UBATIZO HUO ndio UNYAKUO unaozungumzwa ndani ya Biblia yaani KUHAMISHWA TOKA MAUTINI na kuingia UZIMANI......
⬆️Huko ndiko hasa KUINGIA KATIKA UFALME WA MUNGU, na jina lako KUANDIKWA katika FAMILIA YA MUNGU maana kila FAMILIA inajulikana kwa majina ya wanafamilia nayo yanawekwa kwenye kumbukumbu.
✝️ Karibu katika familia ya Mungu duniani na uanze kuishi maisha mapya ndani ya mahusiano ya Wewe na KRISTO YESU hapo hapa DUNIANI na KUPOKEA UZIMA WA MILELE......ingekuwa ni mkutano wa nje ningesema 🗣️🔊 "WANAOTAKA KUBATIZWA katika MAISHA haya ningesema wasongee hapa mbele"
❤️Ikiwa uko tayari kwa MAAMUZI HAYA tafadhali wasiliana nasi kwa namba hii
📞 # 0752023082 au 0627975451
✝️Karibu katika karamu ya Mwana-kondoo, vinono vimekwisha kuchinjwa!!!
🙏🏽Namshukuru Mungu aliyetupa kunena habari hizi kwa neema ya ajabu, lakini pia kwa namna ya pekee nikushukuru kwa wewe uliyepata nafasi ya kusoma siri hizi za mbinguni ambazo si kila wakati utakutana nazo. Ni maombi yangu Mungu akupe kuyapokea k**a yalivyokusudiwa!!!
🎓Shalom!!!
Imeandaliwa na sisi FAMILIA YA KIFALME ILE YA MUNGU DUNIANI - B.O.J MINISTRY na kuandikwa na mimi ndugu yenu katika Kristo Yesu
# Benjamin Jacob Hema
All Credits : Norbert Nicolaus Rulanyaga [ Our beloved teacher] .
HEAVEN ON EARTH