PAGT Kambarage Shinyanga

PAGT Kambarage Shinyanga We are people of purpose and destiny of faith in the one and true living God. We exist to share the gospel message of Jesus Christ.

The Pentecostal Assemblies of God (Tanzania) abbreviated PAG (T), was started by the Canadian Missionaries under the auspices of the Pentecostal Assemblies of Canada (PAOC), German branch back in the early 1950’s. These early Missionaries arrived in Tanganyika (former name of Tanzania) from Kenya along the borders of Mara region and established the mission station at Nyasirori area, in the current

Butiama district. Before Nyasirori mission station was started, the PAG (T) evangelists and pastors received their ministerial training from Nyang’ori Bible School in Kenya, which was established in 1950’s, and when they came back, they planted local churches predominantly in Mara region. As the mission work grew up in Tanganyika, PAOC missionaries established a Bible School in Nyasirori area and immediately started training and preparing national leaders for the work of the ministry. We are God’s people empowered by and dependent on the Holy Spirit to tell the life-transforming story of Jesus Christ. He is the Way, the Truth and the Life. If you are seeking for answers, try Jesus, He never fails. The Bible says, "Jesus Christ came that you might have life and life more abundantly." John 10:10
VISION
To be a church that transforms the spirit, soul, and body of every person through the Gospel of Jesus Christ. MISSION
To worship God in spirit and truth, preaching the Gospel through the power of the Holy Spirit to every person at every place and strengthening local churches which shall be a catalyst for change that brings the Kingdom of God upon every creature.

Tumehitimisha vyema Jumapili ya Pentekoste. Ili kuwa mashahidi wa kweli, Roho Mtakatifu ni hitaji la kila aaminiye na hu...
24/05/2026

Tumehitimisha vyema Jumapili ya Pentekoste. Ili kuwa mashahidi wa kweli, Roho Mtakatifu ni hitaji la kila aaminiye na huo ndio Upentekoste wetu.

29/03/2026
Tunamshukuru Mungu kwa ibada ya leo. Mtumishi wa Mungu Askofu na Mwangalizi mstaafu wa wilaya ya Busega  Rev. Yohana Mas...
08/03/2026

Tunamshukuru Mungu kwa ibada ya leo. Mtumishi wa Mungu Askofu na Mwangalizi mstaafu wa wilaya ya Busega Rev. Yohana Masunga alihubiri.

Leo Jumamosi kituo cha Maendeleo ya Mtoto na kijana TZ0608 kanisa la PAG Kambarage; kimepokea wageni kutoka mkoani Simiy...
07/03/2026

Leo Jumamosi kituo cha Maendeleo ya Mtoto na kijana TZ0608 kanisa la PAG Kambarage; kimepokea wageni kutoka mkoani Simiyu wilaya Busega.
Ujumbe huo uliongozwa na Mchungaji Kiongozi wa kanisa la PAGT Mkula Busega Rev.Yohana Masunga akiongozana Watendakazi na Katibu wa Kamati Kituo cha TZ0615 ikiwa ni ziara ya mafunzo.

Wageni hao pamoja na mambo mengine waliweza kujionea shughuli mbalimbali za kiprogram wakiongozwa wenyeji wao Mchungaji Kiongozi Rev.Thomas Faida pamoja na Mratibu wa Kituo Dr. George K Francis.

Ni kesho tutakuwa mbashara hapa kuanzia saa saa 5 asubuhi.
07/03/2026

Ni kesho tutakuwa mbashara hapa kuanzia saa saa 5 asubuhi.

Ibada ya 25/01/2026 ikiwa ni hitimisho la maombi ya siku 21 Kufunga na Kuomba. Kwa hakika Mungu ameonekana kwa namna ya ...
26/01/2026

Ibada ya 25/01/2026 ikiwa ni hitimisho la maombi ya siku 21 Kufunga na Kuomba. Kwa hakika Mungu ameonekana kwa namna ya ajabu sana.

SIKU 21 ZA MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBAAlhamisi, Tarehe 22 Januari 2026OMBI KUU: MAHITAJI BINAFSI1️⃣ Mahusiano yako na Mu...
22/01/2026

SIKU 21 ZA MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA
Alhamisi, Tarehe 22 Januari 2026

OMBI KUU: MAHITAJI BINAFSI

1️⃣ Mahusiano yako na Mungu
Jiombee neema ya kumjua na kumpenda Mungu kibinafsi, na kumtumikia kwa moyo wako wote kwa upya katika mwaka 2026. Ombea huduma yako iwe ya kiwango cha juu zaidi, ikiambatana na uthibitisho wa nguvu za Roho Mtakatifu. 📖 Mathayo 22:37

2️⃣ Familia yako
Ombea familia yako—wazazi, watoto, au wakwe—ili Mungu awabariki katika kila eneo: kiroho, kimwili, kijamii na kiuchumi. Omba mafanikio, baraka za kiungu, upendo wa kweli, na mshikamano wa kudumu katika familia yako yote. 📖 Zaburi 128:1–4

3️⃣ Ulinzi dhidi ya mipango ya adui
Kemea nguvu za giza na mipango ya Ibilisi na mawakala wake inayoweza kuharibu mikakati uliyojiwekea kufanikisha malengo yako ya mwaka 2026. Omba ulinzi wa kiroho na kimwili, pamoja na uthabiti na ufanisi katika utendaji wako wa kila siku. 📖 Zaburi 91:11–12

4️⃣ Ulinzi na nguvu kwa mwaka 2026
Omba ulinzi wa kiungu katika mwaka wote wa 2026. Kemea roho za ajali, magonjwa, na udhaifu. Omba Mungu akupe nguvu, afya njema, imani, na ujasiri kila siku ili utimize wajibu wako binafsi na wa familia kwa mafanikio makubwa zaidi. 📖 Wafilipi 4:13

SIKU 21 ZA MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBAJumanne, 20 Januari 2026OMBI KUU: KANISA NA UAMSHO1️⃣ Omba Roho Mtakatifu achochee...
20/01/2026

SIKU 21 ZA MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA
Jumanne, 20 Januari 2026

OMBI KUU: KANISA NA UAMSHO

1️⃣ Omba Roho Mtakatifu achochee uamsho ndani ya kanisa lako la mahali.
Omba moto wa kiroho uwashwe upya — toba ya kweli, utakatifu, bidii ya maombi, ujazo wa Roho Mtakatifu, miujiza, na shauku ya kumtumikia Mungu. 📖 Matendo 4:31

2️⃣ Ombea Kanisa lisimame katika kweli ya Neno la Mungu.
Ombea wachungaji, walimu, na watumishi wote wajazwe ujasiri wa kuhubiri bila woga.
Omba Kanisa liishi katika utakatifu, liwe nuru na chumvi duniani.
📖 2 Wakorintho 10:4 • Luka 18:1

3️⃣ Omba Mungu amimine roho ya maombi kwa watu Wake,
ili udhihirisho wa nguvu za Roho Mtakatifu uwe halisi.
Kemea nguvu zote za giza na roho zinazopinga kazi ya Mungu.
Ombea Kanisa la ulimwengu mzima. 📖 Mathayo 9:37–38

4️⃣ Ombea mavuno ya roho, watu wengi wamjue Kristo.
Omba uamsho upelekee watu wengi kuokoka, kubatizwa, na kuunganishwa katika familia ya wana wa Mungu.

🙏 Tuombe kwa bidii, tukiamini Mungu wa uamsho!

SIKU 21 ZA MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBAKAULI MBIU: MAENDELEO YA PAG TANZANIAJumatatu, 19 Januari 20261️⃣ Maombi kwa Viong...
19/01/2026

SIKU 21 ZA MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA

KAULI MBIU: MAENDELEO YA PAG TANZANIA

Jumatatu, 19 Januari 2026

1️⃣ Maombi kwa Viongozi wa Taifa
Ombea Halmashauri Kuu na Kamati Tendaji ya Taifa ya PAG Tanzania, ili Mungu awajalie umoja na hekima ya kufanya maamuzi yenye busara katika kupanga, kusimamia, na kutekeleza maendeleo ya Kanisa kwa utukufu wake.
📖 Zaburi 133; Waefeso 4:1–4

2️⃣ Maombi kwa Viongozi Wote wa PAG Tanzania
Ombea viongozi wote kuanzia ngazi ya kanisa la mahali hadi taifa, ili Mungu awape umoja wa Roho na nia moja katika kutekeleza Mpango Mkakati. Ombea mshikamano na ukemee roho ya mgawanyiko.
📖 Wafilipi 2:1–2; 2 Wathesalonike 3:10–12

3️⃣ Maombi kwa Uchumi wa Washirika
Ombea uchumi wa washirika wa makanisa ya PAG Tanzania. Muombe Mungu abariki kazi za mikono yao na kuwafungulia milango ya fursa mbalimbali, wakimtumikia kwa kutoa zaka na matoleo kwa moyo wa hiari, shukrani, na uaminifu.

4️⃣ Maombi kwa Maendeleo ya Kanisa
Ombea maendeleo ya Kanisa la PAG Tanzania kuanzia kanisa la mahali hadi taifa. Mshukuru Mungu kwa neema ya kununua ekari hamsini (50) Itigi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha umisheni na maendeleo ya jamii.

5️⃣ Shukrani na Imani kwa Mwaka 2026
Mshukuru Mungu kwa maendeleo ambayo kanisa lako la mahali, wilaya, au jimbo limefanya mwaka 2025, na mwamini kwa maendeleo makubwa zaidi katika mwaka 2026.

🙏 Tuungane katika maombi kwa ajili ya maendeleo ya Kanisa na Taifa!

🔥 SIKU 21 ZA MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA 📅 Tarehe: Ijumaa, 16 Januari 2026MADA: HUDUMA ZA JAMII NA MAENDELEO ENDELEVU 🌍W...
16/01/2026

🔥 SIKU 21 ZA MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA 📅 Tarehe: Ijumaa, 16 Januari 2026

MADA: HUDUMA ZA JAMII NA MAENDELEO ENDELEVU 🌍

Wapendwa, leo tunaelekeza maombi yetu katika Huduma za Jamii na Maendeleo kupitia kanisa letu la PAG Tanzania. Ungana nasi katika vipengele hivi:

1️⃣ SHUKRANI KWA "LIGHT OF HOPE" Tunampa Mungu utukufu kwa kuliongoza shirika letu la Light of Hope (PAG Tanzania) kuandaa Mpango Mkakati wa Miaka Mitano. Tunashukuru kwa neema na maono ambayo Bwana amewapa viongozi wetu. 📖 Mhubiri 11:1–2

2️⃣ RASILIMALI NA WAFADHILI Tuliombee shirika ili Bwana afungue milango ya rasilimali (fedha, wataalamu, na vitendea kazi). Tunaomba Mungu awainue wafadhili wa ndani na nje wenye mzigo wa kuona maono haya yanatimia kwa viwango vya juu. 📖 Yakobo 1:27 • Matendo 20:35

3️⃣ HUDUMA KWA WAHITAJI Tunamshukuru Mungu kwa makanisa yote ya PAG Tanzania yanayojitoa kuwahudumia wahitaji, wajane, na yatima. Tunaomba washirika wazidi kuwa na moyo wa ukarimu na upendo usiobagua. 📖 Isaya 58:10–11

4️⃣ UONGOZI WA IDARA Tunaombea Idara ya Huduma za Jamii kuanzia ngazi ya kanisa la mahali hadi Taifa. Viongozi wapewe hekima, uadilifu, na moyo wa kujitoa kutimiza majukumu yao kwa ufanisi.

🙏 Tuko pamoja katika kuliitia jina la Bwana.

SIKU 21 ZA MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBAAlhamisi, Tarehe 15 Januari 2026WATOTO, VIJANA, HUDUMA ZA SHULENI NA VYUONI1️⃣ Uli...
15/01/2026

SIKU 21 ZA MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA
Alhamisi, Tarehe 15 Januari 2026

WATOTO, VIJANA, HUDUMA ZA SHULENI NA VYUONI

1️⃣ Ulinzi kwa watoto na vijana
Ombea ulinzi wa kimwili, kiroho, na kiakili juu ya watoto na vijana.
Kemea roho za uharibifu, uasi, na tabia hatarishi zinazoathiri kizazi cha sasa.
Waombee wazazi, walezi, na kanisa watimize kikamilifu wajibu wa malezi. 📖 Zaburi 121:7–8

2️⃣ Ajira na kujiajiri kwa wahitimu
Ombea vijana waliomaliza vyuo wapate fursa za ajira katika taasisi na kampuni mbalimbali.
Waombee watumie vipaji na elimu zao kwa ubunifu ili kujiajiri.
Pinga roho ya kukata tamaa na msongo wa mawazo.
📖 Mithali 22:6 • Yeremia 29:11 • Yoeli 2:28

3️⃣ Uamsho wa kiroho
Ombea uamsho wa kiroho miongoni mwa watoto na vijana.
Waombee wazazi na walezi washirikiane na kanisa, shule, vyuo, na jamii katika malezi bora.

4️⃣ Waalimu na viongozi wa idara
Ombea waalimu wa watoto na vijana pamoja na wakurugenzi wa idara wapewe neema, ujasiri, na mzigo wa kuwafundisha watoto katika kweli ya Biblia.
Waombee ubunifu katika kupanga na kuendesha programu za watoto na vijana.

🙏 Tuungane katika maombi kwa ajili ya kizazi chetu!

Address

Kambarage
Shinyanga

Telephone

+255754404522

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when PAGT Kambarage Shinyanga posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to PAGT Kambarage Shinyanga:

Share