26/02/2025
Je Unahitaji Muongozo wa Kiroho juu ya kesho yako??
Wale waongozwao na Roho ndio wana wa Mungu, usikubali kuishi maisha ya kubahatisha bila kujua Mapenzi ya Mungu ni yapi juu yako Mwaka huu 2025.
Mtumishi wa Mungu Mtume Mtalemwa amekuandalia Mkesha mkubwa wa KADI ZA KINABII, kwenye Mkesha huo atagawa Kadi zenye UNABII na muongozo wa mwaka mzima, juu ya kile Mungu anasema katika maisha yako.
KADI hizi zimeandikwa na Mtumishi wa Mungu kwa muongozo wa roho Mtakatifu juu ya Kila Mgeni atakayefika siku hiyo, Kadi zinatolewa Bure bila malipo.
Mahali: ECG Dar-Es-Salaam The Jesus Nation Church,Makongo Juu, siku ya Ijumaa, tarehe 7 March 2025 kuanzia saa 12 jioni.