01/10/2025
*UNYENYEKEVU NA UJASIRI NDANI YA NDOA*
Mtu ambaye ni mnyonge kihisia au kimaisha (mtu ambaye hajikubali), hutafuta kuwapendeza watu, hawezi kuvumilia pale mwenzi wake au watu wengine wakikasirika kwa sababu yake, kwa hiyo ni mtu ambaye anapenda kumpendeza mwingine ili apate kukubaliwa, hivyo hawezi kumkosoa mwenzi wake kukosoa wengine na kuelezea jinsi gani ameumizwa, lakini mtu k**a huyu kwa sababu hawezi kumkosa mwenzi wake, hivyo hawezi hata kusamehe, ataumizwa lakini ataficha maumivu hayo, na hata hawezi kuwa muwazi kuhusu maumivu ambayo anapitia, hataki kukosoa kwa sababu anaamini upendo kwa mwenzi wake utapotea, kwa hiyo ataona bora amani na upendo vitawale kuliko ukweli, kwa hiyo bora adanganywe au adanganye kuliko kusema Ukweli ambao unaweza kumfanya apoteze penzi linalomuinua kimaisha,
Tunahitaji unyenyekevu lakini pia ujasiri mkubwa ambao hautokani na ulimwengu huu, kwa sababu, k**a unyenyekevu unaotokana na maisha, ujasiri wa ulimwengu huu unaweza kuletwa kwa sababu ya elimu, mafanikio, cheo, n.k. lakini ujasiri huu usiwe na unyenyekevu kwa wakosaji ambao hawajafanikiwa k**a wewe. Hivyo unaweza kusema ukweli hata pasipo kuwathamini na kuonyesha upendo kwa wengine kwa sababu ujasiri wako ni kwa sababu ya maisha yako uliyonayo,
Injili ya Yesu Kristo inatugeuza na kutufanya kuwa wanyenyekevu lakini pia ni wajasiri, kwa sababu injili inasema, "sisi ni waovu na wenye dhambi sana hata Yesu Mwana wa Mungu afe kwa ajili yetu, ni waovu sana kiasi kwamba ni kifo tu cha Mwana wa Mungu ndio kingetosha kutuokoa" lakini pia "tunapendwa sana na kuthaminiwa kiasi kwamba Mwana wa Mungu(Bwana wa dunia hii alitupenda kiasi hiki) alikuwa tayari kufa kwa ajili yetu", hivyo injili inatunyeyekesha hadi mavumbini na wakati huohuo inatuinua hadi mbinguni. Dr Timothy Keller" anasema we are sinners but completely loved and accepted in Christ at the same time"
Hivyo tunaweza kusema Ukweli katika Upendo kwa sababu kuna neema ya Mungu itokanayo na injili, inayotufanya wajasiri katika kusema Ukweli na wanyenyekevu katika kuonyesha upendo na kuthamini wengine.
Hongera sana kwa kujifunza mpaka hapa, TUTAENDELEA, DOTTO JOHN SWEYA,, 0787732433, 25/09/2025, kumbuka UNAWEZA KUFURAHIA NDOA YAKO,