Efatha Ministry- Rujewa Mbarali

Efatha Ministry- Rujewa Mbarali Healing & Deliverance by the blood of Jesus(Mark 7:34)
Welcome to Efatha Church where Jesus is at work.

Karibu katika Ibada ya Mkesha wa Mwaka Mpya utakayofanyika katika KANISA LA EFATHA MWENGE, DAR ES SALAAM TANZANIA, Kanis...
19/12/2023

Karibu katika Ibada ya Mkesha wa Mwaka Mpya utakayofanyika katika KANISA LA EFATHA MWENGE, DAR ES SALAAM TANZANIA, Kanisa linatazamana na Lugalo Suma JKT.

Ibada hii ya Mkesha itafanyika tarehe 31/12/2023 siku ya Jumapili saa 03:00 usiku na itaongozwa na Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.

Mwana wa Mungu usipange kukosa njoo tufunge Mwaka 2023 na tuanze Mwaka Mpya 2024 na Bwana.

Kwa wewe uliyembali utaweza kufuatilia Ibada hii Mubashara kupitia mitandao yetu ya kijamii k**a YouTube, Facebook na Instagram kwa Jina la Efatha Church

Tafadhali wajulishe na Wengine na Mungu Akubariki.

ASKOFU THABO MASENYA KUTOKA AFRIKA YA KUSINI: Zaburi 30:11 “Uligeuza matanga yangu kuwa machezo; Ulinivua gunia, ukanivi...
26/11/2023

ASKOFU THABO MASENYA KUTOKA AFRIKA YA KUSINI:

Zaburi 30:11 “Uligeuza matanga yangu kuwa machezo; Ulinivua gunia, ukanivika furaha.” Watu wengi wanapitia katika magumu au mabaya lakini huo sio mpango wa Mungu; kila aina ya ubaya, huzuni au maumivu uliyokutana nayo acha Bwana akayaondoe na akuletee furaha na mashangilio katika maisha yako.

Neno la Mungu linasema “Uligeuza matanga yangu kuwa machezo;” Katika matanga yoyote uliyokutana nayo katika maisha yako Mungu akalete mazuri kwako.

Biblia inasema kuwa “Bwana hufurahia katika ustawi wa watumishi wake” Mungu anafurahia ustawi wa watumishi wake, ustawi wowote utakaokutana nao fahamu kuwa utamfurahisha Mungu, Mungu kamwe hafurahii unapoteseka, Bali anafurahi pale ambapo wewe unastawi.

Ibilisi amewaaminisha wengi ya kuwa kumtumikia Mungu ni mateso, lakini Biblia inasema kuwa “Yesu alipitia mateso ili sisi tuweze kuwa na furaha” Ni mapenzi ya Mungu juu yako ya kuwa upitie katika mazuri na ustawi na siyo magumu. Mungu anataka upitie katika ustawi na siyo umaskini, nia ya Mungu katika maisha yako ni kwamba uweze kuona mazuri yake mahali unapoishi na sio kupitia katika maumivu na huzuni.

Hakuna sababu ya wewe kusherekea ustawi wa Mungu utakapofika mbinguni, la! Bali utafurahia hapa hapa duniani kwa maana Yesu amekwisha kulipa gharama yake ili wewe uishi maisha mazuri huku duniani.

K**a ustawi wako umeshikiliwa kuzimu, leo Baba yangu wa mbinguni akakufanye ukawe huru kutoka katika kila mtego wa ibilisi; kwa maana sio mpango wa Mungu wewe ung’ang’ane; acha baraka za Mungu alizokuwekea zikafunuliwe kwako kwa Jina la Yesu na ukazifurahie.

MAMA ELIAKUNDA MWINGIRAZaburi 27:1-4 “ Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wang...
26/11/2023

MAMA ELIAKUNDA MWINGIRA

Zaburi 27:1-4 “ Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani? Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka. Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo nitatumaini. Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake.”

Bwana ni nuru ya wokovu wetu hivyo hatuogopi hofu wala mashaka, hatutishiki na adui atakapojipanga dhidi yetu kwa maana Bwana atatupigania na tutakuwa salama.

Hakuna adui atakayefanikiwa katika maisha yako, wewe uliyemjua Bwana ng’ang’ana na Bwana, mtumaini Yeye na weka macho yako kwake kamwe hata kuacha; Yeye ni Bwana wa majeshi anapigana na wanaopigana na wewe ukiwa na Yeye uko salama kwa maana Bwana ni nuru yako vita vijapokutokea hautaogopa kwa maana upo na Bwana wa mabwana.

USHUHUDA:MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRAMimi pamoja na mke wangu tunapenda kumshukuru sana Mungu kwa kutujalia ku...
26/11/2023

USHUHUDA:

MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA
Mimi pamoja na mke wangu tunapenda kumshukuru sana Mungu kwa kutujalia kutimiza miaka 30 ya ndoa. Mungu amekuwa mwema sana kwetu kila iitwapo leo na ameyafanya maisha yetu kuwa baraka kwa wengi.

Kuachana ni jambo baya sana lakini kupendana ni kuzuri. Ili muweze kusameheana na kuchukuliana; upendo unahitajika, bila upendo kamwe hamtaweza. Ukiona mtu hawezi kusamehe fahamu kuwa hana upendo.

Mungu ni pendo na ukiona mtu anasamehe fahamu kuwa anaupendo na k**a anasamehe jua kuwa ana Mungu. Ukiona mtu ameshindwa kusamehe jua kuwa hana Mungu na k**a hana Mungu basi hana pendo.

MAMA ELIAKUNDA MWINGIRA:
Mungu ni mwema sana, namshukuru Mungu kwa pendo lake na fadhili zake kwetu mpaka kufikia siku hii ya leo tumefikisha miaka 30 ya ndoa.

Namshukuru sana Mungu kwa kunipa mume mzuri anayenipenda na kuniheshimu. Kitu kinachofanya watu wawe pamoja ni upendo.
Wengine wanapokaa miaka mingi wanachokana, mwanangu Mungu asikupe kumchoka mwenzi wako, k**a mlianza katika pendo maana pendo halihesabu mabaya halijivuni na halikosi kuwa na adabu. Mungu akupe neema ya hilo pendo.

Nawatakia wote mlioolewa mkawe na maisha mazuri ya ndoa na wale ambao hamjaolewa Mungu akawape wenza sahihi na mkafurahie maisha yenu ya ndoa.

USHUHUDA.Naitwa Lucy Nicetus, namshukuru sana Mungu kwa matendo yake makuu kwangu, kwanza napenda kumshukuru sana kwa ku...
26/11/2023

USHUHUDA.

Naitwa Lucy Nicetus, namshukuru sana Mungu kwa matendo yake makuu kwangu, kwanza napenda kumshukuru sana kwa kutimiza miaka 13 ya wokovu na miaka 23 ya ndoa yangu.

Pia napenda kumshukuru sana Mungu kwa kuniponya, siku moja nilianguka na pingili za mgongo zilisagika, hali hiyo ilinipelekea kupata maumivu makali sana ya mgongo na hata kushindwa kutembea, ndani ya miezi miwili nililala kitandani siwezi kutembea, ilipofika kipindi cha kwenda kusanyiko nilimwambia Mungu sijui itakavyokuwa lakini mimi naenda. Namshukuru sana Mungu baada ya kusanyiko la mwaka huu mwezi wa kumi na kurejea nyumbani nikaanza kupata afya nzuri na sasa natembea vizuri kabisa bila maumivu yoyote.

Lakini pia napenda kumshukuru sana Mungu kwa kutimiza miaka 13 ya wokovu na kupitia wokovu wangu nimemuona Mungu akifanya mambo mengi sana katika maisha yangu. Niliokoka nikiwa sina nyumba lakini mpaka sasa nina nyumba mbili na nina usafiri. Hakika kumtumikia Mungu kuna faida.

USHUHUDA:Naitwa Mchungaji Gerwin Lianjara, napenda kumshukuru sana Mungu kwa kuniponya; nakumbuka ilikuwa ni mwanzoni mw...
26/11/2023

USHUHUDA:

Naitwa Mchungaji Gerwin Lianjara, napenda kumshukuru sana Mungu kwa kuniponya; nakumbuka ilikuwa ni mwanzoni mwa mwaka huu baada ya mkesha wa mwaka mpya, siku ya tatu nikaanza kuumwa miguu iliyopelekea kushindwa kutembea sawa sawa nikawa natumia magongo, nilikuwa na maumivu ya kiuno pamoja na mgongo. Tarehe 19 mwezi wa pili nilipata neema ya kukutana na Mtume na Nabii Josephat Mwingira, niliongea naye na kabla sijamwambia kile kilichokuwa kinanitesa yeye akaniambia nini kilikuwa kinanisumbua na nifanye nini ili niweze kuwa sawa, aliniambia natakiwa kupunguza uzito, kufanya mazoezi na kuacha vyakula vyote vinavyosababisha kuongezeka uzito. Lakini pia aliniombea na akaniambia nisiwe na hofu wala mashaka kwani nitakuwa sawa.

Baada ya kufuata kile alichoniambia niliona matokeo chanya kwani nilikuwa na kilo 106 nikapungua mpaka kilo 80. Namshukuru sana Mungu kwa ajili ya ushauri wa Mtumishi wake maana kupitia huo mimi nipepona kabisa.

IBADA MAALUM YA JUMAPILI, TAREHE 26/11/2023 KATIKA KANISA LA EFATHA MWENGE DAR ES SALAAM TANZANIA.KATIBU MKUU WA KANISA ...
26/11/2023

IBADA MAALUM YA JUMAPILI, TAREHE 26/11/2023 KATIKA KANISA LA EFATHA MWENGE DAR ES SALAAM TANZANIA.

KATIBU MKUU WA KANISA LA EFATHA- MTUME EMMANUEL CHAO

Mshukuru Mungu kwa kile ambacho amefanya kwako tangu mwezi wa kwanza mpaka kufika mwezi huu wa kumi na moja kwa maana mwezi wa kumi na mbili anakwenda kufanya makubwa zaidi kwako.

Zaburi 103:2-3 “Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote. Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,”

Nenda mbele za Baba yako wa mbinguni na umuombe akusamehe na aruhusu Damu yake itakase yale yote ambayo umetenda kwa kuwaza au kunena kwako na ukamkosea Yeye.

Muombe Mungu akuhuishe na kufungua macho na masikio yako ili uweze kusikia kutoka kwake yale unayopaswa kusikia.

Yohana 4: 23- 24 "Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa m...
28/05/2023

Yohana 4: 23- 24 "Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu k**a hao wamwabudu. Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli".

27/05/2023

Address

P. O. Box 162 Ihanga
Rujewa

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Efatha Ministry- Rujewa Mbarali posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Efatha Ministry- Rujewa Mbarali:

Share