Parokia ya Mtakatifu Benedikto Peramiho

Parokia ya Mtakatifu Benedikto Peramiho St. Benedict Parish–Peramiho is a Catholic community rooted in the Benedictine tradition.

Located in Peramiho, Southern Tanzania, the parish serves families and youth through liturgy, sacraments, and pastoral ministry.

09/07/2026

I got over 4,000 reactions on my posts last week! Thanks everyone for your support! 🎉

St.Benedict's  Abbey Peramiho
29/05/2026

St.Benedict's Abbey Peramiho

Parokia ya Mtakatifu Benedikto Peramiho Jimbo Kuu La Songea @ Karibuni Peramiho
29/05/2026

Parokia ya Mtakatifu Benedikto Peramiho Jimbo Kuu La Songea @ Karibuni Peramiho

14/04/2026

: Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, TEC linasikitika kutangaza kifo cha Askofu Bernardin Francis Mfumbusa wa Jimbo Katoliki Kondoa, kilichotokea leo Aprili 14, 2026 majira ya Saa 11:45 asubuhi kwenye Hospitali ya Benjamin Mkapa, BMH alikokuwa amepelekwa kwa matibabu ya dharura.

Askofu Mfumbusa anatarajiwa kuzikwa Jumatano Aprili 22, 2026 Jimboni Kondoa.

Itakumbukwa kwamba, Aprili 9, 2026 Baba Mtakatifu Leo XIV alikuwa amemteua Askofu Bernardin Francis Mfumbusa, Rais wa K**ati ya Mawasiliano ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Afrika na Madagascar, “Pan African Episcopal Conference For Social Communication, CEPACS,” kuwa ni Mjumbe wa Baraza la Kipapa la Mawasilianiano ya Jamii.

Kanisa limempoteza Askofu na mtaalam mbobezi wa Mawasiliano ya Jamii.

Itakumbukwa kwamba, Hayati Askofu Bernardin Francis Mfumbusa wa Jimbo Katoliki Kondoa, alizaliwa Aprili 1, 1962 mjini Kondoa na ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 64 tangu alipozaliwa.

Baada ya malezi na majiundo yake ya Kikasisi, Juni 14, 1992 alipewa Daraja Takatifu ya Upadre mikononi mwa Askofu Matthias Joseph Isuja, aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Dodoma.

Baba Mtakatifu Benedikto XVI Machi 12, 2011 akaanzisha Jimbo Katoliki la Kondoa na kumteuwa Askofu Bernardin Francis Mfumbusa kuwa Askofu wake wa kwanza, na hivyo kuwekwa wakfu na Kardinali Polycarp Pengo, aliyekuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mei 15, 2011, akisaidiana na Askofu Mkuu Yuda Thaddeus Ruwa’ichi aliyekuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza pamoja na Askofu Augustine Ndeliakyama Shao, C.S.Sp., wa Jimbo Katoliki la Zanzibar.

Kumbe Askofu Bernardin Francis Mfumbusa amefariki dunia akiwa amelitumia Kanisa k**a Padre kwa Miaka 33 na k**a Askofu mwenye dhamana ya kufundisha, kuongoza na kuwatakatifuza watu wa Mungu kwa miaka 14.

TAFAKARI YA MASOMO YA MISA – JUMAPILI DOMINIKA YA 5 YA KWARESIMA , MACHI 22, 2026N. Br. Michael Daniel Kitabagala OSB UT...
21/03/2026

TAFAKARI YA MASOMO YA MISA – JUMAPILI DOMINIKA YA 5 YA KWARESIMA , MACHI 22, 2026

N. Br. Michael Daniel Kitabagala OSB

UTANGULIZI
Ndugu wapendwa, leo tunasimama mbele ya fumbo kubwa la maisha: kifo na uzima. Katika ulimwengu wa leo, watu wengi hawaogopi kufa tu, bali wanaishi wakiwa tayari wamekufa ndani—moyo umechoka, matumaini yamezimika, imani imepoa. Lakini Neno la Mungu leo linakuja k**a radi katikati ya giza: Mungu bado anafufua!

SOMO LA KWANZA
(Eze 37:12-14)
Nabii Ezekieli anaoneshwa mifupa mikavu—hakuna uhai, hakuna tumaini. Hii ni picha halisi ya maisha ya wengi leo. Kuna mtu alishapoteza matumaini ya ndoa yake, mwingine biashara imeanguka kabisa, mwingine amejeruhiwa moyoni kiasi kwamba haamini tena katika upendo. Lakini Mungu anasema: “Nitayafungua makaburi yenu.”
Hii si hadithi—ni ahadi. Mungu haogopi hali iliyoharibika. Anachohitaji ni nafasi ya kuingiza Roho wake. Pale ambapo wewe unaona mwisho, Mungu anaona mwanzo.

SOMO LA PILI
(Rum 8:8-11)
Paulo anatukumbusha ukweli mgumu lakini wa kuokoa: maisha bila Roho wa Mungu ni kifo hata k**a unaonekana hai. Unaweza kuwa na kazi nzuri, pesa, marafiki—but ndani hakuna amani. Ndiyo maana leo tunaona watu wana kila kitu lakini bado wanahangaika, wanakunywa ili kusahau, wanatafuta furaha isiyodumu.
Lakini Paulo anasema: Roho aliyemfufua Kristo yuko ndani yako. Hii ni nguvu ya ajabu—nguvu ya kuinuka tena baada ya kuanguka, nguvu ya kuanza upya hata pale uliposhindwa mara nyingi.

INJILI
(Yn 11:1-45)
Yesu anafika kwa Lazaro akiwa tayari siku nne kaburini—harufu tayari imeshaanza. Hii ina maana hakuna matumaini kibinadamu. Lakini hapa ndipo Mungu anapofanya kazi yake.
Kabla ya muujiza, Yesu anasema: “Toeni jiwe.” Hii ndiyo changamoto ya leo. Tunataka Mungu abadili maisha yetu, lakini hatutaki kuacha dhambi. Tunalia juu ya matatizo ya familia, lakini hatutaki kusamehe. Tunataka kufanikiwa, lakini hatutaki kubadilika.
Kisha Yesu anaita: “Lazaro, njoo nje!” Hii ni sauti inayovunja kifo. Leo anakuita wewe: toka katika maisha ya dhambi, toka katika kukata tamaa, toka katika uvivu wa kiroho. Lakini kumbuka—Lazaro alitoka, ila bado amefungwa sanda. Hii ina maana hata baada ya kuanza upya, bado unahitaji kujinasua hatua kwa hatua—kwa sala, Sakramenti, na juhudi binafsi.

KATIKA MAISHA YETU
Ndugu zangu, tuwe wakweli: kuna “makaburi” mengi katika maisha yetu leo.
Kuna ndoa zinaishi kwa mazoea, hakuna furaha—hilo ni kaburi.
Kuna vijana wamekata tamaa ya maisha, wanaona hawana thamani—hilo ni kaburi.
Kuna watu wanaenda kanisani kila Jumapili lakini mioyo yao iko mbali na Mungu—hilo ni kaburi la kiroho.

Na ukweli mchungu ni huu: watu wengi wamezoea hali hizo, wamekubali kuishi ndani ya makaburi yao.

Lakini leo Yesu anasimama mbele yako na kusema: “Usikubali kubaki hapo.”
Ondoa jiwe la moyo mgumu. Acha dhambi inayokufunga. Kubali kubadilika.
Maana hakuna hali ambayo Yesu hawezi kuifufua—isipokuwa ile unayokataa kumkabidhi.

HITIMISHO
Ndugu wapendwa, Ukristo si dini ya watu waliokata tamaa—ni maisha ya watu wa ufufuko.
Usiseme “nimechelewa” — Lazaro alikuwa siku nne kaburini.
Usiseme “haiwezekani” — Mungu wa leo bado ni yule yule.

Leo chagua kutoka katika kaburi lako.
Leo chagua kuanza upya.
Leo chagua kuishi.

Sala:
Bwana Yesu, wewe ni ufufuo na uzima, ingia katika maeneo yaliyokufa ndani yangu. Nipe ujasiri wa kuondoa jiwe la moyo wangu na nguvu ya kuitikia sauti yako. Nifanye niishi k**a mtu wa matumaini na uzima kila siku. Amina.

MASOMO YA MISA, MACHI 22, 2026DOMINIKA YA 5 YA KWARESIMAMWANZO:Zab. 43:1 – 2Ee Bwana, unihukumu, unitetee kwa taifa lisi...
21/03/2026

MASOMO YA MISA, MACHI 22, 2026
DOMINIKA YA 5 YA KWARESIMA

MWANZO:
Zab. 43:1 – 2

Ee Bwana, unihukumu, unitetee kwa taifa lisilo haki, uniokoe na mtu wa hila asiye haki. Kwa kuwa wewe ndiwe Mungu uliye nguvu zangu.

SOMO 1
Eze. 37:12 – 14

Bwana Mungu asema hivi; Tazama, nitafunua makaburi yenu, na kuwapandisha kutoka katika makaburi yenu, enyi watu wangu, nami nitawaingizeni katika nchi ya Israeli. Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapoyafunua makaburi yenu, na kuwatoa ninyi katika makaburi yenu, enyi watu wangu. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, nanyi mtaishi, nami nitawawekeni katika nchi yenu, nanyi mtajua ya kuwa mimi, Bwana, nimesema hayo, na kuyatimiza asema Bwana, nimesema hayo, na kuyatimiza asema Bwana.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 130 (K) 7

(K) Kwa Bwana kuna fadhili, na kwake kuna ukombozi mwingi.

Ee Bwana, toka vilindini nimekulilia,
Bwana, uisikie sauti yangu.
Masikio yako na yaisikilize
Sauti ya dua zangu. (K)

Bwana, k**a Wewe ungehesabu maovu,
Ee Bwana, nani angesimama?
Lakini kwako kuna msamaha,
Ili Wewe uogopwe. (K)

Nimemngoja Bwana, roho yangu imengoja,
Na neno lake nimelitumainia.
Nafsi yangu inamngoja Bwana,
Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi,
Naam, walinzi waingojao asubuhi.
Ee Israeli, umtarajie Bwana. (K)

Maana kwa Bwana kuna fadhili,
Na kwake kuna ukombozi mwingi.
Yeye atamkomboa Israeli
Na maovu yake yote. (K)

SOMO 2
Rum. 8:8 – 11

Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho.

Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu I hai, kwa sababu ya haki. Lakini, ikiwa Roho wake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO
Yn. 11:25, 26

Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima, asema Bwana; Yeye aniaminiye mimi, hatakufa kabisa hata milele.

INJILI
Yn. 11:1 – 45

Basi mtu mmoja alikuwa hawezi, Lazaro wa Bethania, mwenyeji wa mji wa Mariamu na Martha, dada yake. Ndiye Mariamu yule aliyempaka Bwana marhamu, akamfuta miguu kwa nywele zake, ambaye Lazaro nduguye alikuwa hawezi.

Basi wale waumbu wakatuma ujumbe kwake wakesema, Bwana, yeye umpendaye hawezi. Naye Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo. Naye Yesu alimpenda Martha na umbu lake na Lazaro. Basi aliposikia ya kwamba hawezi, alikaa bado siku mbili pale pale alipokuwapo. Kisha, baada ya hayo, akawaambia wanafunzi wake, Twendeni Uyahudi tena.

Wale wanafunzi wakamwambia, Rabi, juzijuzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga kwa mawe, nawe unakwenda huko tena? Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu. Basi akienda usiku hujikwaa; kwa sababu nuru haimo ndani yake.

Aliyasema hayo; kisha, baada ya hayo, akawaambia, Rafiki yetu, Lazaro, amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha. Basi wale wanafunzi wakamwambia, Bwana, ikiwa amelala, atapona. Lakini Yesu alikuwa amenena habari ya mauti yake; nao walidhani aya kuwa ananena habari ya kulala usingizi. Basi hapo Yesu akawaambia waziwazi, Lazro amekufa. Nami nafurahi kwa ajili yenu kwamba sikuwapo huko, ili mpate kuamini; lakini na twendeni kwake. Basi Tomaso, aitwaye Pacha, akawaambia wanafunzi wenziwe, Twendeni na sisi ili tufe pamoja naye.

Basi Yesu alipofika, alimkuta amekwisha kuwamo kaburini yapata siku nne. Na Bethania ilikuwa karibu na Yerusalemu, kadiri ya maili mbili hivi; na watu wengi katika Wayahudi walikuwa wamekuja kwa Martha na Mariamu, ili kuwafariji kwa habari ya ndugu yao.

Basi Martha aliposikia kwamba Yesu anakuja, alikwenda kumlaki; na Mariamu alikuwa akikaa nyumbani. Basi Martha akamwambia Yesu, Bwana, k**a ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. Lakini hata sasa najua ya kuwa yoyote utakayomwomba Mungu, Mungu atakupa. Yesu akamwambia, Ndugu yako atafufuka. Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho. Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo? Akamwambia, Naam, Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni.

Naye alipokwisha kusema hayo, alikwenda zake; akamwita umbu lake Mariamu faraghani, akisema, Mwalimu yupo anakuita. Naye aliposikia, aliondoka upesi, akamwendea. Na Yesu alikuwa hajafika ndani ya kijiji; lakini alikuwa akalipo pale pale alipomlaki Martha. Basi wale Wayahudi waliokuwapo na Mariamu nyumbani, wakimfariji, walipomwona jinsi alivyoondoka upesi na kutoka, walimfuata; huku wakidhania ya kuwa anakwenda kaburini ili alie huko.

Basi Mariamu alipofika pale alipokuwapo Yesu, na kumwona, alianguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, k**a ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. Basi Yesu alipomwona Analia, na wale Wayahudi waliofuatana naye wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake, akasema, Mmemweka wapi? Wakamwambia, Bwana, njoo utazame. Yesu akalia machozi. Basi Wayahudi wakasema, Angalieni jinsi alivyompenda. Bali wengine wao wakasema, Je! Huyu aliyemfumbua macho yule kipofu, hawezi kumfanya na huyu asife? Basi Yesu hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne. Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu? Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba nakushukuru kwa kuwa umenisikia. Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma.

Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia Mfungueni, mkamwache aende zake.

Basi wengi katika Wayahudi waliokuja kwa Mariamu, na kuyaona yale aliyoyafanya, wakamwamini.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

18/03/2026

TAFAKARI YA MASOMO YA MISA ALHAMISI, MACHI 19, 2026
Sherehe ya Mt. Yosefu, Mume wa Bikira Maria

Masomo: 2Sam 7:4–5,12–14,16; Zab 89:2–5,27,29; Rum 4:13,16–18,22; Mt 1:16,18–21,24

---

Utangulizi
Leo Kanisa linaadhimisha sherehe ya Mtakatifu Yosefu, mfano wa pekee wa imani, utii na unyenyekevu. Katika kipindi hiki cha Kwaresima, tunaletewa sura ya mtu ambaye hakuhubiri kwa maneno mengi, bali alihubiri kwa maisha yake. Yosefu anatufundisha kwamba utakatifu haupo katika kusema mengi, bali katika kufanya mapenzi ya Mungu kwa uaminifu wa kimya.

---

Injili kutoka Injili ya Mathayo inatupa picha ya moyo wa Yosefu. Alipogundua kuwa Bikira Maria ana mimba kabla ya kuishi pamoja, alichagua kumwacha kwa siri ili kumlinda. Huu ulikuwa uamuzi wa haki na huruma. Lakini Mungu alipomfunulia mpango wake kupitia malaika katika ndoto, Yosefu hakusita. “Alipoamka, alifanya k**a malaika wa Bwana alivyomwambia.” Hapo tunaona moyo wa utii wa kweli—kusikiliza sauti ya Mungu na kuitii bila kuchelewa.

---

Somo la kwanza na la pili vinatuonyesha mpango mkubwa wa Mungu katika historia ya wokovu. Ahadi aliyompa Daudi na imani ya Ibrahimu vinafikia utimilifu wake katika Kristo. Yosefu anakuwa sehemu ya mpango huu si kwa nguvu zake, bali kwa imani na utii wake. Hata k**a hakuelewa kila kitu, alikubali kushiriki katika mpango wa Mungu kwa ujasiri.

---

Maisha ya Yosefu yanatufundisha mambo muhimu kwa maisha ya leo. Kwanza, utii kwa Mungu kuliko sauti za dunia. Katika jamii yenye kelele nyingi na mitazamo mingi, Mkristo anaitwa kusikiliza sauti ya Mungu na kuifuata hata k**a si rahisi. Pili, familia ni wito kabla ya mambo mengine. Yosefu aliweka mbele ulinzi wa familia yake—Yesu na Maria—kuliko maslahi yake binafsi. Hii ni changamoto kubwa kwa wazazi wa leo: kulinda na kulea familia katika imani na maadili mema.

---

Tatu, Yosefu ni mtu wa kazi. K**a seremala, alifanya kazi kwa bidii na uaminifu. Anatufundisha kwamba kazi halali ni sehemu ya utakatifu. Nne, Yosefu ni mlinzi na mlezi. Katika dunia ya leo yenye changamoto nyingi—mitandao, maadili yanayobadilika, na shinikizo la maisha—familia zinahitaji watu wa kusimama k**a Yosefu: walinzi wa upendo, imani na maadili.

---

Kwa hiyo, sherehe hii inatualika tujiulize: Je, mimi ninaishi kwa utii kwa Mungu? Je, nalinda familia yangu na imani yangu? Je, nafanya kazi kwa uaminifu na haki? Tukimuiga Yosefu, tutakuwa watu wanaoishi si kwa kelele za dunia bali kwa mapenzi ya Mungu.

---

Sala
Ee Mungu Baba, tunakushukuru kwa zawadi ya Mtakatifu Yosefu. Tujalie tuige imani yake, utii wake na unyenyekevu wake. Tufanye kuwa watu wa matendo mema na walinzi wa familia zetu katika imani.
Yesu, tunakuamini wewe. Amina. 🙏📖

MASOMO YA MISA TAKATIFU SHEREHE YA MTAKATIFU YOSEFU MUME WA BIKIRA MARIA , ALHAMISI  MACHI 19, 2026ANTIFONA YA KUINGIA: ...
18/03/2026

MASOMO YA MISA TAKATIFU SHEREHE YA MTAKATIFU YOSEFU MUME WA BIKIRA MARIA , ALHAMISI MACHI 19, 2026

ANTIFONA YA KUINGIA: Lk.12:42
Huyu ndiye wakili mwaminifu na mwenye busara ambaye Bwana alimweka juu ya watumishi wake.

KOLEKTA:
Ee Mungu mwenyezi, umemkabidhi mtakatifu Yosefu kazi ya kutunza kiaminifu mwanzo wa mafumbo ya wokovu wa binadamu. Tunakuomba, kwa maombezi yake, ulijalie Kanisa lako litumikie daima kwa makini mafumbo hayo. Kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo Mwanao, anayeishi na kutawala nawe katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu, milele na milele.

SOMO 1:
2Sam.7:4-5,12-14,16
Ikawa usiku uo huo, neno la Bwana likamfikia Nathani kusema, Enenda, ukamwambie mtumishi wangu, Daudi, Bwana asema hivi, Je! Wewe utanijengea nyumba, nikae ndani yake? Nawe siku zako zitakapotimia, ukalala na baba zako, nitainua mzao wako nyuma yako, atakayetoka viunoni mwako, nami nitaufanya imara ufalme wake. Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa jina langu, nacho kiti cha enzi cha ufalme wake nitakifanya imara milele. Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu; akitenda maovu nitamwadhibu kwa fimbo ya binadamu na kwa mapigo ya wanadamu; Na nyumba yako, na ufalme wako, vitathibitishwa milele mbele yako. Nacho kiti chako kitafanywa imara milele.

WIMBO WA KATIKATI: Zab.89:1-4,26,28(K)36
1. Fadhili za Bwana nitaziimba milele;
Kwa kinywa changu nitavijulisha vizazi vyote uaminifu wako.
Maana nimesema, Fadhili zitajengwa milele;
Katika mbingu utauthibitisha uaminifu wako.

(K) Wazao wake watadumu milele.

2. Nimefanya agano na mteule wangu,
Nimemuapia Daudi, mtumishi wangu.
Wazao wako nitawafanya imara milele,
Nitakijenga kiti chako cha enzi hata milele. (K)

3. Yeye ataniita, Wewe baba yangu,
Mungu wangu na mwamba wa wokovu wangu.
Hata milele nitamwekea fadhili zangu,
Na agano langu litafanyika amini kwake. (K)

SOMO 2:
Rum.4:13,16-18,22
Ahadi ile ya kwamba atakuwa mrithi wa ulimwengu alipewa Ibrahimu na uzao wake, si kwa sheria bali kwa haki aliyohesabiwa kwa imani. Kwa hiyo ilitoka katika imani, iwe kwa njia ya neema, ili kwamba ile ahadi iwe imara kwa wazao wote; si kwa wale wa torati tu, ila na kwa wale wa imani ya Ibrahimu; aliye baba yetu sisi sote; (k**a ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi); mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako. Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, k**a ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako. Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa ni haki.

SHANGILIO:
Mt.16:18
Aleluya, aleluya!
Heri wakaao nyumbani mwako,
ee Bwana, wanakuhimidi daima.
Aleluya!

INJILI:
Mt.1:16,18-21,24
Yakobo alimzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo. Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri. Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao. Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya k**a malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe;

Au,
Lk.2:41-51
Wazee wa Yesu huenda Yerusalemu kila mwaka, wakati wa sikukuu ya Pasaka. Na alipopata umri wake miaka kumi na miwili, walipanda k**a ilivyokuwa desturi ya sikukuu; na walipokwisha kuzitimiza siku, wakati wa kurudi kwao, yule mtoto Yesu alibaki nyuma huko Yerusalemu, na wazee wake walikuwa hawana habari. Nao wakadhani ya kuwa yumo katika msafara; wakaenenda mwendo wa kutwa, wakawa wakimtafuta katika jamaa zao na wenzao; na walipomkosa, wakarejea Yerusalemu, huku wakimtafuta. Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake. Na walipomwona walishangaa, na mama yake akamwambia, Mwanangu, mbona umetutenda hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni. Akawaambia, Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu? Nao hawakuelewa na neno hilo alilowaambia. Akashuka pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii.

MAOMBI
Ee Mungu, ulipenda kumchagua Yosefu awe Mume wa Bikira Maria, ili kuitimiza ahadi ya Mkombozi kutoka katika ukoo wa Daudi. Leo tunapofanya Sherehe yake, twakuomba.

1. Uwajalie Baba Mtakatifu F., Maaskofu na wote wenye Daraja takatifu neema ya kuzidi kuyatunza kiaminifu mafumbo matakatifu uliyowaaminisha.

2. Watu wa mataifa yote wajaliwe kumkiri Mwanao k**a Mungu na binadamu.

3. Uielekeze mioyo yetu kwenye ufalme wako na uwape watu wa ndoa mwamko wa kuishi kwa uaminifu, upendo na mshik**ano.

4. Mt. Yosefu aliliamini Neno lako; utujalie nasi imani thabiti k**a hiyo hasa tunaposongwa na majaribu makali.

5. Kwa maombezi ya Mtakatifu Yosefu, uwajalie wazazi wote fadhila ya mapendo kwa watoto wao na kwa wote wanaohitaji msaada wao.

6. Kwa sala za Mtakatifu Yosefu, marehemu wetu wapokelewe katika ushirika wa watakatifu huko mbinguni.

Ee Mungu, Mtakatifu Yosefu alimpokea Maria k**a mkewe na Yesu k**a mwanawe na akawatunza kwa upendo usio na mipaka. Utusaidie nasi kuyatimiza mapenzi yako kwa ndugu zetu wazima na wafu. Unayeishi na kutawala, daima na milele. Amina.

SALA YA KUOMBEA DHABIHU:
Ee Bwana, mtakatifu Yosefu alimtumikia kwa moyo mkuu Mwanao pekee aliyezaliwa na Bikira Maria. Tunakuomba utuwezeshe na sisi kuhudumia kwenye altare zako kwa moyo safi. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.

UTANGULIZI
Utume wa Mt. Yosefu.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele, na kukusifu kwa mbiu inayokustahili, na kukuhimidi na kukutangaza Wewe, katika adhimisho la sikukuu ya Yosefu mwenye heri.
Yeye alikuwa mtu mwenye haki, uliyependa awe Mume wake Bikira Maria Mama wa Mungu; na, k**a mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ulimweka juu ya Familia yako takatifu awe baba mlinzi wa Mwanao mpenzi, Yesu Kristo Bwana wetu, aliyetungwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Kwa njia yake Malaika husifu adhama yako, Enzi hukuabudu, na Mamlaka hukupigia magoti wakitetemeka.
Mbingu na Nguvu za mbinguni, na Maserafi wenye heri, wakuadhimisha pamoja kwa shangwe. Tunakusihi, utujalie tujiunge nao kwa wimbo wa sifa, tukisema kwa sauti ya unyenyekevu:

Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu...

ANTIFONA YA KOMUNYO: Mt.25:21
Vema, mtumishi mwema na mwaminifu, ingia katika furaha ya Bwana wako.

SALA BAADA YA KOMUNYO:
Ee Bwana, umetushibisha sisi familia yako kwa chakula cha altare hii, tukifurahia sherehe ya mtakatifu Yosefu. Tunakuomba utuhifadhi kwa ulinzi wako wa daima na kulinda ndani yetu baraka zako ulizotukirimia kwa hisani yako. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.

TAFAKARI YA MASOMO YA MISA JUMATANO, MACHI 18, 2026Jumatano ya Juma la 4 la KwaresimaMasomo: Isa 49:8–15; Zab 145:8–9,13...
17/03/2026

TAFAKARI YA MASOMO YA MISA JUMATANO, MACHI 18, 2026
Jumatano ya Juma la 4 la Kwaresima

Masomo: Isa 49:8–15; Zab 145:8–9,13–14,17–18; Yn 5:17–30

Utangulizi
Neno la Mungu la leo linatualika kufurahia na kuishi ndani ya mapenzi ya Mungu. Kwaresima ni safari ya kujifunza kumtegemea Mungu zaidi na kuacha mapenzi yetu ili kuingia katika mpango wake. Ndani ya mapenzi ya Mungu ndipo kuna amani ya kweli na furaha ya kudumu.

Katika somo la kwanza kutoka Kitabu cha Isaya, Mungu anaonyesha upendo wake usioyumba kwa watu wake: “Je, mama aweza kumsahau mtoto wake?... hata akimsahau, mimi sitakusahau wewe.” Huu ni ujumbe wa faraja—kwamba hata tukipitia changamoto, Mungu hatuachi. Mapenzi yake kwetu ni ya upendo na wokovu, si ya kutuangamiza.

Katika Injili kutoka Injili ya Yohane, Yesu anaonyesha umoja wake wa ndani kabisa na Baba: “Mwana hawezi kufanya neno mwenyewe ila lile amwonalo Baba akilifanya.” Yesu anaishi kwa kufanya mapenzi ya Baba yake kikamilifu. Hapa ndipo tunajifunza kwamba maisha ya kweli ya Kikristo ni kuiga mtindo huu wa Yesu—kuishi si kwa matakwa yetu binafsi, bali kwa kuyatafuta na kuyafuata mapenzi ya Mungu.

Katika maisha ya kila siku, changamoto ni kwamba kuna sauti nyingi zinatuita: tamaa, hofu, shinikizo la jamii na matarajio ya dunia. Lakini Mkristo anaitwa kuchagua sauti ya Mungu. Tunapochagua mapenzi ya Mungu hata katika mambo madogo, tunaanza kuingia katika umoja wa karibu naye. Na hapo ndipo tunapopata furaha ya kweli—furaha ya kujua kwamba tunaishi kulingana na kusudi la Mungu.

Sala
Ee Baba wa mbinguni, nisaidie nitambue na kuyapenda mapenzi yako katika maisha yangu. Nipe neema ya kuchagua mema na kuacha yale yasiyokupendeza. Nivute karibu nawe ili niishi katika furaha ya kufanya mapenzi yako.
Yesu, nakuamini wewe. Amina.

Address

P.O.PERAMIHO
Peramiho

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Parokia ya Mtakatifu Benedikto Peramiho posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share