St.Benedict's Abbey Peramiho

St.Benedict's  Abbey Peramiho Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from St.Benedict's Abbey Peramiho, Convent and monastery, P. O. PERAMIHO, Peramiho.

Monastery founded as a mission station in 1898 Eerected as Abbatia Nullius on 23 December 1931
Raised to Diocese of Songea and reduced to status as simple Abbey on 6 February 1969

14/08/2026

MASOMO YA MISA, JUMAPILI, AGOSTI 16, 2026
JUMA LA 20 LA MWAKA

________

SOMO I
Isa. 56:1, 6-7

Bwana asema hivi, Shikeni hukumu, mkatenda haki; kwa maana wokovu wangu u karibu kuja, na haki yangu kufunuliwa. Na wageni, walioandamana na Bwana ili wamhudumu, na kulipenda jina la Bwana, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu; Nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.

Neno la Bwana...Tumshukuru Mungu
________

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 67:1-2, 4-5, 7 (K) 5

(K) Watu na wakushukuru, Ee Mungu,
Watu wote na wakushukuru.

Mungu na atufadhili na kutubariki,
na kutuangazia uso wake.
Njia yake ijulikane duniani,
wokovu wake katikati ya mataifa yote. (K)

mataifa na washangilia,
naam, waimbe kwa furaha.
Maana kwa haki utawahukumu watu,
na kuwaongoza mataifa walioko duniani. (K)

watu na wakushukuru, Ee Mungu,
watu wote na wakushukuru.
Mungu atatubariki sisi;
miisho yote ya dunia itamcha Yeye. (K)
________

SOMO 2
Rum. 11:13-15, 29-32

Nasema na ninyi, mlio watu wa Mataifa. Basi, kwa kadiri nilivyo mtume wa watu wa Mataifa. Basi, naitukuza huduma iliyo yangu? Huenda nikapata kuwapatia wivu walio damu moja na mimi na kuwaokoa baadhi yao. Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je! Kukubaliwa kwao kutakuwa nini k**a si uhai baada ya kufa. Kwa sababu karama za Mungu hazina majuto, wala mwito wake. Kwa maana k**a ninyi zamani mlivyomwasi Mungu, lakini sasa mmepata rehema kwa kuasi kwao; kadhalika na hao wameasi sasa, ili kwa kupata rehema kwenu wao nao wapate rehema. Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote.

Neno la Bwana...Tumshukuru Mungu
________

SHANGILIO
Mdo. 16:14

Aleluya, aleluya,
Fungua mioyo yetu, Ee Bwana,
Ili tuyatuze maneno ya Mwanao.
Aleluya
________

INJILI
Mt. 15:21-28

Yesu aliondoka huko, akaenda kando pande za tiro na Sidoni. Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo. Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu. Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Naye akaja akamsujudia, akisema, Bwana unisaidie. Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa. Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao. Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako k**a utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile.

Neno la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo
________

10/07/2026

MASOMO YA MISA, JUMAPILI, JULAI 12, 2026
JUMA LA 15 LA MWAKA

SOMO 1
Isa 55:10-11

K**a vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 65:9-13

(K) Mbegu nyingine zikaanguka penye udongo mzuri zikamea, zikazaa.

Umeijilia nchi na kuisitawisha,
Umeitajirisha sana;
Mto wa Mungu umejaa maji;
Wawaruzuku watu nafaka Maana ndiwe uitengenezaye ardhi.

Matuta yake wayajaza maji; Wapasawazisha palipoinuka,
Wailainisha nchi kwa manyunyu; Waibariki mimea yake.

Umeuvika mwaka taji ya wema wako;
Mapito yako yadondoza unono.
Huyadondokea malisho ya nyikani,
Na vilima vyajifunga furaha.

Na malisho yamevikwa kondoo,
Na mabonde yamepambwa nafaka,
Yanashangilia, naam, yanaimba.

SOMO 2
Rum 8:18-23

Ndugu, nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu k**a utukufu ule utakaofunuliwa kwetu. Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu. Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye atiyevitiisha katika tumaini; kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, hata viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu. Kwa maana twajua ya kuwa viumbe vyote pia vinaugua pamoja, navyo vina utungu pamoja hata sasa. Wala si hivyo tu; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia kufanywa wana, yaani, ukombozi wa mwili wetu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO
Efe 1:17, 18

Aleluya, aleluya
Baba wa Bwana wetu Yesu Kristu, Ayatie nuru macho ya mioyo yetu, Ili tujue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo.
Aleluya.

INJILI
Mt 13:1-23

Siku ile Yesu akatoka nyumbani, akaketi kando ya bahari. Wakamkusanyikia makutano mengi, hata akapanda chomboni, akaketi; na ule mkutano wote wakasimama pwani. Akawaambia mambo mengi kwa mifano, akisema, Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda. Hata alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila; nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara zikaota, kwa udongo kukosa kina; na jua lilipozuka ziliungua; na kwa kuwa hazina mizizi zikanyauka. Nyingine zikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea, ikazisonga; nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini Mwenye masikio na asikie. Wakaja wanafunzi, wakamwambia, Kwa nini wasema nao kwa mifano? Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa. Kwa maana ye yote mwenye kitu atapewa, naye atazidishiwa tele; lakini ye yote asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa. Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa. Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; K*tazama mtatazama, wala hamtaona. Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya. Lakini, heri macho yenu, kwa kuwa yanaona; na masikio yenu, kwa kuwa yanasikia. Kwa maana, amin, nawaambia, Manabii wengi na wenye haki walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi, wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi, wasiyasikie. Basi ninyi sikilizeni mfano wa mpanzi. Kila mtu alisikiapo neno la ufalme asielewe nalo, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia. Naye aliyepandwa penye miamba, huyo ndiye alisikiaye lile neno, akalipokea mara kwa furaha; lakini hana mizizi ndani yake, bali hudumu kwa muda; ikitukia dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara huchukizwa. Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai. Naye aliyepandwa penye udongo mzuri, huyo ndiye alisikiaye lile neno, na kuelewa nalo; yeye ndiye azaaye matunda, huyu mia, na huyu sitini, na huyu thelathini.

Neno la Bwana........Sifa kwako Ee Kristo

26/06/2026

MASOMO YA MISA, JUNI 28, 2026
DOMINIKA LA 13 LA MWAKA

MWANZO:
Zab. 47:2
Enyi watu wote, pigeni makofi, mpigieni Mungu kelele kwa sauti ya shangwe.

SOMO 1
2 Fal 4:8-11,14-16

Ilikuwa siku moja, Elisha alikwenda Shunemu; na huko kulikuwa na mwanamke mmoja mwenye cheo; nave akamshurutisha aje ale chakula. Ikawa kila alipopita njia ile, huingia kula chakula. Yule mwanamke akamwambia mumewe, Tazama, mimi naona ya kuwa mtu huyu apitaye kwetu mara kwa mara ni mtu mtakatifu w’a Mungu. Nakuomba, tumfanyie chumba kidogo ukutani; na ndani yake tumwekee kitanda, na meza, na kiti, na kinara cha taa na itakuwa, atujiapo, ataingia humo. Ikawa siku moja akafikia huko, akaingia katika chumba kile akalala. Akasema, Basi, atendewe nini? Gehazi akajibu, Hakika hana mwana, na mumewe ni mzee. Akamwambia, Kamwite. Naye alipokwisha kuitwa, akasimama mlangoni. Akasema, Panapo wakati huu mwakani, utamkumbatia mwana.

Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 89 : 1-2, 15-18 (K) 1

(K) Fadhili za Bwana nitaziimba milele.
Fadhili za Bwana nitaziimba milele;
Kwa kinywa changu nitavijulisha vizazi vyote uaminifu wako.
Maana nimesema, Fadhili zitajengwa milele;
Katika mbingu utauthibitisha uaminifu wako. (K)

Heri watu wale waijuao sauti ya shangwe,
Ee Bwana, kuenenda katika nuru ya uso wako.
Kwa jina lako hufurahi mchana kutwa,
Na kwa haki yako hutukuzwa. (K)

Maana fahari ya nguvu zao ni Wewe,
Na kwa radhi yako pern be yetu itatukuka.
Maana ngao yetu ina Bwana,
Na mfalme wetu ni wake Mtakatifu wa Israeli. (K)

SOMO 2
Rum. 6:3-4,8-11

Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi k**a Kristo alivyofufuka katika

wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. Lakini tukiwa tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye; tukijua ya kuwa Kristo akiisha kufufuka katika wafu hafi tena, wala mauti haimtawali tena. Maana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake, amwishia Mungu. Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi, na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu.

Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO
Mt. 11:25

Aleluya, aleluya,
Nakushukuru, Baba, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.
Aleluya.

INJILI
Mt. 10:37-42

Yesu aliwafundisha mitume wake hivi: Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili. Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili. Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona.

Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma. Ampokeave nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; naye ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki. Na mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa ngaa kikombe cha maji ya baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, amin, nawaambia. haitampotea kamwe thawabu yake.

Neno la Bwana........Sifa kwako Ee Kristo

09/06/2026
05/06/2026

MASOMO YA MISA, JUNI 7, 2026
SHEREHE YA MWILI NA DAMU TAKATIFU YA BWANA WETU YESU KRISTU
MWANZO:
Zab. 80:17
Nimewalisha kwa unono wa ngano na kuwashibisha asali itokayo mwambani.
SOMO 1
K*m. 8:2-3;14-16
Musa aliwaambia makutano: Nawe utaikumbuka njia ile yote Bwana, Mungu wako, aliyokuongoza miaka hii arobaini katika jangwa, ili akutweze, kukujaribu, kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo. Akakutweza, akakuacha uone njaa, akakulisha kwa mana, usiyoijua wewe wala baba zako hawakuijua; apate kukujulisha ya kuwa mwanadamu haishi kwa mkate tu, bali huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha Bwana. Basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau Bwana, Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa; aliyekuongoza katika jangwa lile kubwa lenye kitisho, lenye nyoka za moto na nge, nchi ya kiu isiyokuwa na maji; aliyekutolea maji katika mwamba mgumu, aliyekulisha jangwani kwa mana, wasiyoijua baba zako.
Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 147:12-15,19-20 (K) 12
(K) Msifu Bwana, Ee Yerusalemu.
Msifu Bwana, Ee Yerusalemu;
Msifu Mungu wako, Ee Sayuni.
Maana ameyakaza mapingo ya malango yako,
Amewabariki wanao ndani yako. (K)
Ndiye afanyaye amani mipakani mwako,
Akushibishaye kwa unono wa ngano.
Huipeleka amri yake juu ya nchi,
Neno lake lapiga mbio sana. (K)
Humhubiri Yakobo neno lake,
Na Israeli amri zake na hukumu zake.
Hakulitendea taifa lolote mambo k**a hayo,
Wala hukumu zake hawakuzijua.
aleluya. (K)
SOMO 2
1Kor. 10:16-17
Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja.
Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.
SHANG1LIO
Yn. 6:51
Aleluya, aleluya,
Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; asema Bwana; mtu akila chakula hiki, ataishi milele.
Aleluya.
INJILI
Yn. 6:51-58
Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu. Basi Wayahudi walishindana wao kwa wao wakisema, Awezaje mtu huyu kutupa sisi mwili wake ili tuule? Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. K**a vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi. Hiki ndicho chakula kishukacho kutoka mbinguni; si k**a mababa walivyokula, wakafa; bali akilaye chakula hicho ataishi milele.
Neno la Bwana... Sifa kwako Ee Kristo.

Bleibt in meiner Liebe 🫶 John 15:9. 🇹🇿💒🇹🇿
03/06/2026

Bleibt in meiner Liebe 🫶
John 15:9. 🇹🇿💒🇹🇿

29/05/2026

MASOMO YA MISA, JUMAPILI MEI 31, 2026
SHEREHE YA UTATU MTAKATIFU
JUMAPILI BAADA YA PENTEKOSTE - MWAKA A
SOMO 1
K*t. 34 : 4-6, 8-9
Musa aliinuka na mapema asubuhi, naye akakwea katika mlima wa Sinai, k**a Bwana alivyomwamuru, akazichukua hizo mbao mbili za mawe mkononi mwake.
Bwana akashuka ndani ya lile wingu, akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina la Bwana. Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; Musa akafanya haraka, akainamisha kichwa chake hata nchi, akasujudu. Akasema, Ikiwa sasa nimepata neema mbele zako, Bwana, nakuomba, Bwana, uende kati yetu maana ni watu wenye shingo ngumu; ukasamehe uovu wetu na dhambi yetu, ukatutwae tuwe urithi wako.
WIMBO WA KATIKATI
Dan. 3:52-56. (K) 52
(K) Wastahili kusifiwa na kutukuzwa milele.
Umehimidiwa, Ee Bwana, Mungu wa baba zetu:
Wastahili kusifiwa na kutukuzwa milele.
Limehimidiwa jina lako takatifu, tukufu;
Wastahili kusifiwa na kutukuzwa milele. (K)
Umehimidiwa katika hekalu la fahari yako takatifu;
Wastahili kusifiwa na kutukuzwa milele.
Umehimidiwa juu ya kiti cha ufalme wako;
Wastahili kusifiwa na kutukuzwa milele. (K)
Umehimidiwa utazamaye vilindi, uketiye juu ya makerubi;
Wastahili kusifiwa na kutukuzwa milele.
Umehimidiwa katika anga la mbinguni
Wastahili kusifiwa na kutukuzwa milele. (K)
SOMO 2
2 Kor. 13 :11-14
Hatimaye, ndugu, kwaherini; mtimilike, mfariji- ke, nieni mamoja, mkae katika amani; na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi. Sali- mianeni kwa busu takatifu. Watakatifu wote wawasalimu. Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu. na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote.
SHANG1LIO
Ufu. 1 :8
Aleluya, Aleluya, Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, Mungu ambaye yupo, aliyekuwako, na atakayekuja. Aleluya.
INJILI
Yn. 3:16-18
Yesu alimwambia Nikodemu: Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhu- kumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.

MASOMO YA MISA, JUMAPILI, MEI 24, 2026SHEREHE YA PENTEKOSTESOMO 1 Mdo. 2:1-11Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwa...
22/05/2026

MASOMO YA MISA, JUMAPILI, MEI 24, 2026
SHEREHE YA PENTEKOSTE

SOMO 1
Mdo. 2:1-11

Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi k**a uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, k**a ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, k**a Roho alivyowajalia kutamka.

Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu. Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe. Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya? Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo? Waparthi na Wamedi na Waelani, nao wakaao Mesopotamia, Uyahudi na Kapadokia, Ponto na Asia, Frigia na Pamfilia, Misri na pande za Libia karibu na Kirene, na wageni watokao Rumi, Wayahudi na waongofu, Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu.

Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATI KATI
Zab. 104:1, 24, 29-31, 34, (K) 30

(K) Waipeleka roho yako, Ee Bwana, Nawe waufanya upya uso wa nchi. au: Aleluya.

Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana,
Wewe, Bwana, Mungu wangu,
Umejifanya mkuu sana;
Ee Bwana, jinsi yalivyo mengi matendo yako!
Dunia imejaa mali zako. (K)

Waiondoa pumzi yao, wanakufa,
Na kuyarudia mavumbi yao,
Waipeleka roho yako, wanaumbwa,
Nawe waufanya upya uso wa nchi. (K)

Utukufu wa Bwana na udumu milele;
Bwana na ayafurahie matendo yake.
K*tafakari kwangu na kuwe kutamu kwake;
Mimi nitamfurahia Bwana. (K)

SOMO 2
1 Kor. 12 :3-7, 12-13

Hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu. Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.

Maana k**a vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo. Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.

Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO

Aleluya, aleluya, Uje Roho Mtakatifu, uzienee nyoyo za waamini wako uwatie mapendo yako. Aleluya.

INJILI
Yn. 20 :19-23

Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu. Naye akiisha kusema hayo, akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Basi wale wanafunzi wakafurahi walipomwona Bwana.

Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; k**a Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu. Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.

Neno la Bwana... Sifa kwako Ee Kristo.

This is a Catholic Blog with faith related content both in English and Swahili

On 16th May 2026 at St Dominic Major Seminary Lusaka  Zambia 🇿🇲 Our confrère Br Francis Mkiwa OSB was ordained Deacon. W...
17/05/2026

On 16th May 2026 at St Dominic Major Seminary Lusaka Zambia 🇿🇲
Our confrère Br Francis Mkiwa OSB was ordained Deacon. We bless him and wish him endeavors blessings towards the ahead Ministry 👏👏👏

Address

P. O. PERAMIHO
Peramiho

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when St.Benedict's Abbey Peramiho posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to St.Benedict's Abbey Peramiho:

Shortcuts

Share