Kilimanjaro Gospel Fire

Kilimanjaro Gospel Fire Mathayo
28:19-20 "basi enendeni
mkawafanye mataifa yote kuwa
wanafunzi mkiwabatiza kwa jina la
Baba Allen E.

Hii ni huduma iliyoko chini ya kanisa la T.A.G Inayoongozwa na Mch. Lekey wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Betheli Mdawi, ambaye pia ni Mwinjilisti anayehubiri maeneo mbalimbali nchini katika nchi nzima ya Tanzania na nje ya nchi.

Picha katika matukio mkutano uliofanyika Rombo wiki chache zilizopita.
29/03/2019

Picha katika matukio mkutano uliofanyika Rombo wiki chache zilizopita.

KADRI DHAHABU INAVYOPITA KWENYE MOTO NDIVYO AMBAVYO THAMANI YAKE INAONGEZEKA.
29/03/2019

KADRI DHAHABU INAVYOPITA KWENYE MOTO NDIVYO AMBAVYO THAMANI YAKE INAONGEZEKA.

KADRI DHAHABU INAVYOPITA KATIKA MOTO NDIVYO AMBAVYO THAMANI YAKE INAONGEZEKA. Na Steven Mshiu. Habari rafiki. Hongera kwa kuianza vyema siku yako ya leo. Inawezekana imekuwa ni siku ya changamoto k…

KADRI DHAHABU INAVYOPITA KATIKA MOTO NDIVYO AMBAVYO THAMANI YAKE INAONGEZEKA. Na Steven Mshiu. Habari rafiki. Hongera kw...
29/03/2019

KADRI DHAHABU INAVYOPITA KATIKA MOTO NDIVYO AMBAVYO THAMANI YAKE INAONGEZEKA. Na Steven Mshiu. Habari rafiki. Hongera kwa kuianza vyema siku yako ya leo. Inawezekana imekuwa ni siku ya changamoto kubwa sana kwako, au labda umeshindwa kufikia lengo ulilokuwa umejiwekea, nikutie moyo kuwa hujafikia mwisho wako, bado Mungu amekupa nafasi ya kipekee amini kuwa utafikia lengo lako tu. Binafsi nina moyo wa shukrani kwako utakaetumia muda wako japo dakika tano kusoma hiki ninachokiandika hapa. [ 574 more words ]

KADRI DHAHABU INAVYOPITA KATIKA MOTO NDIVYO AMBAVYO THAMANI YAKE INAONGEZEKA. Na Steven Mshiu. Habari rafiki. Hongera kwa kuianza vyema siku yako ya leo. Inawezekana imekuwa ni siku ya changamoto k…

UFANYE NINI PALE UNAPOFIKWA NA HALI YA KUKOSA TENA TUMAINI? Na Steven Mshiu. Kuna hali inaweza kumpata mtu yeyote, haija...
25/03/2019

UFANYE NINI PALE UNAPOFIKWA NA HALI YA KUKOSA TENA TUMAINI? Na Steven Mshiu. Kuna hali inaweza kumpata mtu yeyote, haijalishi kwamba ana nguvu za Mungu kiasi gani, au hata ana upako kiasi gani, mtu huyo anaweza kukosa tumaini la kusonga mbele aidha ni kwa sababu tu ya hali anayoipitia. Kipindi hicho ndicho ambacho shetani huwa anafanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha kuwa mtu huyo anabaki katika hali ya kukosa tumaini. [ 721 more words ]

UFANYE NINI PALE UNAPOFIKWA NA HALI YA KUKOSA TENA TUMAINI? Na Steven Mshiu. Kuna hali inaweza kumpata mtu yeyote, haijalishi kwamba ana nguvu za Mungu kiasi gani, au hata ana upako kiasi gani, mtu…

MTAZAMO WA MUNGU NA MTAZAMO WA WANADAMU. Na Steven Mshiu. Nakusalimu kupitia jina la Kristo Yesu ambaye ni Bwana na Mwok...
25/03/2019

MTAZAMO WA MUNGU NA MTAZAMO WA WANADAMU. Na Steven Mshiu. Nakusalimu kupitia jina la Kristo Yesu ambaye ni Bwana na Mwokozi wa maisha yetu. Ni matumaini yangu kuwa bado una uzima wa kutosha. Nina kila sababu ya kumtukuza Mungu kwa hilo. Karibu katika blog hii tujifunze na kukimbushana mambo mbalimbali yatakayotujenga kiroho na kimwili. Lengo letu ni kuihubiri injili ya Kristo inayoleta wokovu kwa wanadamu. [ 706 more words ]

MTAZAMO WA MUNGU NA MTAZAMO WA WANADAMU. Na Steven Mshiu. Nakusalimu kupitia jina la Kristo Yesu ambaye ni Bwana na Mwokozi wa maisha yetu. Ni matumaini yangu kuwa bado una uzima wa kutosha. Nina k…

23/03/2019

UFANYE NINI PALE UNAPOFIKWA NA HALI YA KUKOSA TENA TUMAINI?

Na Steven Mshiu.

Kuna hali inaweza kumpata mtu yeyote, haijalishi kwamba ana nguvu za Mungu kiasi gani, au hata ana upako kiasi gani, mtu huyo anaweza kukosa tumaini la kusonga mbele aidha ni kwa sababu tu ya hali anayoipitia.

Kipindi hicho ndicho ambacho shetani huwa anafanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha kuwa mtu huyo anabaki katika hali ya kukosa tumaini. Humletea hofu na mashaka. Humletea hali ya kuona umauti tuu. Humletea hali ya kuona hakuna tena uzima.

Alikuwepo mfalme mmoja aliyeitwa Hezekia. Mfalme huyu alifanya mambo mengi sana yaliyompendeza Mungu. Katika siku za utawala wake k**a mfalme wa Yuda, hakumuacha Mungu wala kuabudu miungu. Alimtumikia Mungu kwa nguvu zake zote.

Licha ya kutokumtenda Mungu dhambi, Neno la Mungu linakuja kupitia nabii Isaya kwenda kwa Hezekia kuwa atengeneze mambo ya nyumba yake maana atakufa wala hatapona. Mfamle huyu alijikuta katika hali ya kuugua, na kwa kuwa alimuamini Mungu hivyo aliamini kuwa Mungu hataacha kumponya. Mbaya zaidi ugonjwa huo ulimfikisha katika hatari ya kufa.

Ujumbe huu wa Mungu kupitia Isaya inawezekana ulikosesha mfalme huyu tumaini kabisa. Kwa hali ya kibinadamu Hezekia inawezekana alifika mbali sana kimawazo, k**a mtu mwingine angeweza kulalamika sana, mwingine angefikia hatua hata ya kumkufuru Mungu, labda mwingine angetumia na kugawa mali zake zote maana hana tumaini la kuishi tena, na mambo mengine kadha wa kadha.

Lakini kupitia kisa hiki, HEZEKIA anatufundisha mambo kadhaa ya kufanya hususani pale tunapojikuta tumefika katika hali ya kukata tamaa na kukosa matumaini.

Jambo la kwanza la kufanya pale unapofika katika hali ya kukosa tena tumaini ni KUJIGEUZA na KUELEKEZA USO KWA MUNGU na KUMUOMBA MUNGU. Isaya 38:2, Hapa tunajifunza kuwa hakuna sehemu yoyote tunapoweza kupata tumaini isipokuwa kwa Mungu. Nimewahi kushudia baadhi ya watu wanapopita katika hali ngumu, huwa wanaenda kwa waganga na wachawi kutafuta kinga, wanamsahau Mungu, Lakini Hezekia anakua ni kielelezo bora kwetu kuwa tufanye nini pale tunapofikia katika hali ambayo yeye mwenyewe aliipitia.

Lakini jambo la pili alilolifanya Hezekia ni KUMKUMBUSHA BWANA, Isaya 38:3, Alikumbusha Bwana jinsi ambavyo alikwenda mbele zake katika kweli yote na kwa moyo mkamilifu. Alimkumbusha jinsi alivyotenda mema machoni pake(Mungu) Tena hapa anazidi kulia sana. Sio kwamba Mungu ni msahaulifu. La hasha. Sio kwamba alikuwa amesahau mambo ambayo Hezekia aliyatenda. Hapana. Lengo lake alitaka kupima imani ya Hezekia. Je Hezekia angejihesabia haki? Je angekuwa na kiburi cha uzima?

Ni kweli kwamba tuna wajibu wa kumkumbusha Bwana juu ya uhitaji wetu. Sio kwamba yeye hajui uhitaji wetu. Lakini yeye k**a Baba kwetu anataka kutuona sisi k**a watoto wake tukienda mbele zake na kumbusha juu ya uhitaji wetu. Lakini yale ambayo tunayafanya au ile kazi ya Mungu tunayoifanya ndio inayotupa nguvu zaidi ya kuzidai ahadi na Baraka zetu kwake. K**a Hezekia angekuwa ni mlegevu kwenye kazi ya Mungu asingekuwa na ujasiri wa kumlilia na kumkumbusha Mungu juu ya hitaji lake la kurejeshewa uponyaji.

Jambo la tatu, Jifunze kuwa mtu wa shukrani na kujishusha. Isaya 38:9-22. Licha ya Hezekia kurejeshewa tena tumaini la uhai wake hakujikweza wala kuchukua utukufu wa Mungu, bado alizidi kuwa mtu wa shukrani mbele za Mungu. Bado alijishusha hadi chini kabisa. Hakuhesabu ni kwa ajili ya matendo mema aliyotenda ndio maana Mungu amemuongezea miaka.

Kuna watu wengine Mungu akiwabariki kwa kidogo tu, mabega yanapanda juu. Wanajiona k**a walistahili. Wanakuwa na kiburi, wanajivuna. Sio hivyo. Kuna mambo Mungu anatutendea sio kwamba tunastahili, ila ajitukuze kupitia sisi. Vyeo vyetu na nafasi zetu havifai wala haviwezi kulirejesha tumaini letu ambalo ni faraja kwetu.

Lakini jambo lingine ni kutambua Mungu yuko tayari kukupatia tumaini jipya. Vs 20. Mwanadamu anaeishi katika ulimwengu huu uliopotoka na kuanguka anategemea tumaini moja tu la WOKOVU. Ili uweze kuwa mshindi kwenye hii dunia inayokwenda kasi katika zama za ujuaji na uovu ni lazima uwe na TUMAINI la wokovu tu. Kwamba hata katika mambo yote bado Mungu aweza kukuokoa. TUMAINI ni ile hali ya kutegemea na kuuona USHINDI hata k**a hakuna dalili za kibinadamu zinazoashiria USHINDI.

Mwisho kabisa mtegemee Mungu aliye chanzo cha tumaini lako. Wakati Daniel anatupwa kwenye shimo la samba wenye njaa kali bado Tumaini lake lilikuwa kwa Mungu wake kuwa anaweza kumuokoa na samba wenye njaa kali. Kina Meshaki na Shedraki walipotupwa ndani ya tanuru la moto mkali bado walikuwa na Tumaini la kuokolewa na Mungu katika moto ule. Ayubu licha ya kupoteza kila kitu kuanzia mali hadi watoto bado alikuwa na tumaini kwa Mungu wake kuwa anaweza kufanya jambo lingine kubwa zaidi.

Mpendwa rafiki, haijalishi unapitia katika hali gani. Umekata tama kiasi gani. Huoni njia kabisa. Huoni mpenyo. Kila kitu kimekwama. Nakuhakikishia kuwa bado liko tumaini la kuinuka tena. K**a shina la mti laweza kuchipua tena na kutoa matunda na watu wakayala. Hata kwako Mungu aweza kukurejeshea tena yale unayoyaona kuwa haiwezekani tena kutokea.

Mungu akuinue viwango viwango vingine.

Rafiki yako,
Steven Mshiu.
0655-882074
March 23, 2019

Na Steven Mshiu Miongoni mwa vitu ambavyo Mungu anavisimamia na kuviangalia kwa jicho la kipekee ni ile hali ya IBADA ya...
20/03/2019

Na Steven Mshiu Miongoni mwa vitu ambavyo Mungu anavisimamia na kuviangalia kwa jicho la kipekee ni ile hali ya IBADA ya mwanadamu mbele zake. Ibada ndiyo njia pekee ya kupeleka sifa zetu kwa Mungu, Ni namna gani yeye ni wa tofauti, asiyefananishwa wala kulinganishwa na chochote. Ndani ya ibada kuna sifa. Mungu anaposifiwa na kuabudiwa katika hali ya uchaji, huwa anashindwa kuvumilia hivyo hushuka kwa njia ya Roho Mtakatifu na kuwahudumia watu wanapokuwa wanafanya ibada ya kweli. [ 502 more words ]

Na Steven Mshiu Miongoni mwa vitu ambavyo Mungu anavisimamia na kuviangalia kwa jicho la kipekee ni ile hali ya IBADA ya mwanadamu mbele zake. Ibada ndiyo njia pekee ya kupeleka sifa zetu kwa …

Na Steven Mshiu.Hakuna kitu kisichokuwa na tafsiri. Tafsiri yaweza kuwa nzuri au mbaya. Inategemea na yule aliyeitengene...
20/03/2019

Na Steven Mshiu.Hakuna kitu kisichokuwa na tafsiri. Tafsiri yaweza kuwa nzuri au mbaya. Inategemea na yule aliyeitengeneza hiyo tafsiri ameitengenezaje, aidha watu watoe tafsiri nzuri au watoe tafsiri mbaya. Kabla hujaanza kuwakilisha kile kilichopo ndani yako au ujumbe ulioubeba, fahamu kuwa kabla ya yote ile hadhira iliyoko mbele yako imeshaanza kujenga na kutoa tafsiri yako hata kabla hujawakilisha kile ulichobeba. [ 501 more words ]

Na Steven Mshiu.Hakuna kitu kisichokuwa na tafsiri. Tafsiri yaweza kuwa nzuri au mbaya. Inategemea na yule aliyeitengeneza hiyo tafsiri ameitengenezaje, aidha watu watoe tafsiri nzuri au watoe tafs…

Na Steven Mshiu. Kila siku huwa najitahidi kuzisoma ahadi za Mungu ndani ya Biblia juu yetu, na mara nyingi huwa naishia...
20/03/2019

Na Steven Mshiu. Kila siku huwa najitahidi kuzisoma ahadi za Mungu ndani ya Biblia juu yetu, na mara nyingi huwa naishia tu kukutana na maandiko kuwa, "NITAKUBARIKI", "NITAKUPONYA", n.k. Sikuwahi kukuta mahali palipoandikwa kuwa siku fulani, tarehe fulani na saa fulani katika mwaka fulani nitakubariki. Labda wewe ulishakuta uniambie ili nibadilishe topic. Sababu kubwa ya MUNGU kutoweka muda wa kukubariki, ni ili mwanadamu aendelee kuweka tumaini na imani yake kwa Mungu wake. [ 334 more words ]

Na Steven Mshiu. Kila siku huwa najitahidi kuzisoma ahadi za Mungu ndani ya Biblia juu yetu, na mara nyingi huwa naishia tu kukutana na maandiko kuwa, “NITAKUBARIKI”, “NITAKUPONYA…

Unaweza Ku download Nyimbo hizi zikubariki kwenye maisha yako. INJILI MOTO ALBUM Karibu Sana Na Ubarikiwe.
20/03/2019

Unaweza Ku download Nyimbo hizi zikubariki kwenye maisha yako. INJILI MOTO ALBUM Karibu Sana Na Ubarikiwe.

Unaweza Ku download Nyimbo hizi zikubariki kwenye maisha yako. INJILI MOTO ALBUM Karibu Sana Na Ubarikiwe.

Address

Moshi
Old Moshi

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kilimanjaro Gospel Fire posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share