Wingu la Bwana International church- Nzega

Wingu la Bwana International church- Nzega we are a prophetic church ! we believe in the power of the living God , Holy spirit and Jesus Christ.

08/10/2024

NITAJUAJE K**A NIMEACHA AU NIMEPOTEZA WITO WANGU.

Naitwa Peter Maboja, ninamshukuru sana Mungu kwaajili ya Neema hii aliyonipa siku ya leo kusema na wewe juu ya ujumbe huu.Unaosema " NITAJUAJE K**A NIMEACHA AU NIMEPOTEZA WITO WANGU"
Na mimi ninge penda kuitumia fursa hii kukukaribisha ili tuweze kushirikiana kwa ukaribu kabisa katika ujumbe huu.

Nataka nikuhakikishie tu ya kwamba kila mtu hapa duniani ana wito maalum alioitiwa na Mungu kuutimiza ili kuleta matokeo yaliyokusudiwa na Mungu. Unaweza ukaniuliza peter kwani wito ni nini, swali hili ni la muhimu sana na linapaswa kujibiwa.

Neno wito kwa lugha ya kawaida ni hali ya kuita au kuitwa. Kwa maana hiyo wito unahusisha pande mbili, kuna anaeita na kuna anaeitwa. K**a kuna mazingira ya namna hiyo maana yake wito au mtu anapoitwa ataitikia na baada ya kuitikia ataambiwa nini cha kufanya na namna gani kifanyike, wakati gani na mazingira gani na kisha atalazimika kukipokea.

Kwa ujumbe huu, ni muhimu tumjue ni nani anayeita na anayeitwa.
Anayeita ni Mungu na anayeitwa ni kila mtu aliyepo hapa duniani hasa aliyempokea Bwana Yesu k**a Bwana na Mwokozi wa maisha yake; zingatia hii kuitwa ni jambo moja na kuitika ni jambo lingine, unaweza ukaitwa na usiitike au ukaitika; hivyo siyo kila aliyeitwa ameitika yupo aliyeitwa lakini hajaitika. Mimi ninaemlenga hapa ni yule aliyeitwa akaitika na amepoteza wito wake.
Na msukumo wangu zaidi ni yule ambaye hajui kuwa amepoteza wito wake na lengo likiwa kwamba, ajue na achukue hatua ya kurejea kwenye wito wake, kwani kuna faida kubwa ukitumikia wito wa Mungu ulioitiwa hapa duniani na hata katika ulimwengu ujao. Na kuna hasara kubwa sana k**a ukiuacha wito wako. Kumbuka wito ni jukumu ambalo Mungu anataka ulitimize uwapo hapa duniani.

Ingawa kuna sababu mbalimbali zinazopelekea mtu kuacha au kupoteza wito wake, natamani kuzungumzia zaidi dalili za kukusaidia kujua kuwa umeacha au umepoteza wito wako.

DALILI YA KWANZA:

Utaandamwa na roho ya bora tukose wote.
Hii ni roho inayofanya kazi kwa nguvu sana kwa mtu aliyepoteza wito, hii ni kwa sababu yeye hana wito tena atatamani na wengine wakose. Atawavuruga kwa kadri anavyoweza, atatumia kila njia kuhakikisha anawazuia wenzake wasitimize kile wanachokifanya katika wito wao.

Hebu tusome katika kitabu cha 1falme3:16-27.
16 𝘕𝘥𝘪𝘱𝘰 𝘸𝘢𝘯𝘢𝘸𝘢𝘬𝘦 𝘸𝘢𝘸𝘪𝘭𝘪, 𝘮𝘢𝘬𝘢𝘩𝘢𝘣𝘢, 𝘸𝘢𝘭𝘪𝘮𝘸𝘦𝘯𝘥𝘦𝘢 𝘔𝘧𝘢𝘭𝘮𝘦, 𝘸𝘢𝘬𝘢𝘴𝘪𝘮𝘢𝘮𝘢 𝘮𝘣𝘦𝘭𝘦 𝘺𝘢𝘬𝘦.
17 𝘕𝘢 𝘮𝘸𝘢𝘯𝘢𝘮𝘬𝘦 𝘮𝘮𝘰𝘫𝘢 𝘢𝘬𝘢𝘴𝘦𝘮𝘢, 𝘌𝘦 𝘣𝘸𝘢𝘯𝘢 𝘸𝘢𝘯𝘨𝘶, 𝘮𝘪𝘮𝘪 𝘯𝘢 𝘮𝘸𝘢𝘯𝘢𝘮𝘬𝘦 𝘩𝘶𝘺𝘶 𝘵𝘶𝘯𝘢𝘬𝘢𝘢 𝘬𝘢𝘵𝘪𝘬𝘢 𝘯𝘺𝘶𝘮𝘣𝘢 𝘮𝘰𝘫𝘢; 𝘯𝘢𝘮𝘪 𝘯𝘢𝘭𝘪𝘻𝘢𝘢 𝘯𝘪𝘭𝘪𝘱𝘰𝘬𝘶𝘸𝘢 𝘱𝘢𝘮𝘰𝘫𝘢 𝘯𝘢𝘺𝘦 𝘯𝘺𝘶𝘮𝘣𝘢𝘯𝘪.
18 𝘒𝘪𝘴𝘩𝘢, 𝘴𝘪𝘬𝘶 𝘺𝘢 𝘵𝘢𝘵𝘶 𝘣𝘢𝘢𝘥𝘢 𝘺𝘢 𝘬𝘶𝘻𝘢𝘢 𝘬𝘸𝘢𝘯𝘨𝘶, 𝘪𝘬𝘢𝘸𝘢 𝘮𝘸𝘢𝘯𝘢𝘮𝘬𝘦 𝘩𝘶𝘺𝘶 𝘯𝘢𝘺𝘦 𝘢𝘬𝘢𝘻𝘢𝘢; 𝘯𝘢 𝘴𝘪𝘴𝘪 𝘵𝘶𝘭𝘪𝘬𝘶𝘸𝘢 𝘱𝘢𝘮𝘰𝘫𝘢; 𝘩𝘢𝘱𝘢𝘬𝘶𝘸𝘢 𝘯𝘢 𝘮𝘵𝘶 𝘮𝘸𝘪𝘯𝘨𝘪𝘯𝘦 𝘱𝘢𝘮𝘰𝘫𝘢 𝘯𝘢𝘴𝘪 𝘯𝘺𝘶𝘮𝘣𝘢𝘯𝘪, 𝘪𝘴𝘪𝘱𝘰𝘬𝘶𝘸𝘢 𝘴𝘪𝘴𝘪 𝘸𝘢𝘸𝘪𝘭𝘪 𝘵𝘶.

19 𝘕𝘢 𝘮𝘵𝘰𝘵𝘰 𝘸𝘢 𝘮𝘸𝘢𝘯𝘢𝘮𝘬𝘦 𝘩𝘶𝘺𝘶 𝘢𝘬𝘢𝘧𝘢 𝘶𝘴𝘪𝘬𝘶, 𝘮𝘢𝘢𝘯𝘢 𝘢𝘭𝘪𝘮𝘭𝘢𝘭𝘪𝘢.
20 𝘈𝘬𝘢𝘰𝘯𝘥𝘰𝘬𝘢 𝘬𝘢𝘵𝘪 𝘺𝘢 𝘶𝘴𝘪𝘬𝘶, 𝘢𝘬𝘢𝘮𝘸𝘰𝘯𝘥𝘰𝘢 𝘮𝘵𝘰𝘵𝘰 𝘸𝘢𝘯𝘨𝘶 𝘶𝘣𝘢𝘷𝘶𝘯𝘪 𝘱𝘢𝘯𝘨𝘶, 𝘮𝘪𝘮𝘪 𝘮𝘫𝘢𝘬𝘢𝘻𝘪 𝘸𝘢𝘬𝘰 𝘯𝘪𝘭𝘪𝘱𝘰𝘬𝘶𝘸𝘢 𝘶𝘴𝘪𝘯𝘨𝘪𝘻𝘪𝘯𝘪, 𝘢𝘬𝘢𝘮𝘸𝘦𝘬𝘢 𝘬𝘪𝘧𝘶𝘢𝘯𝘪 𝘱𝘢𝘬𝘦, 𝘯𝘢 𝘮𝘵𝘰𝘵𝘰 𝘸𝘢𝘬𝘦 𝘮𝘸𝘦𝘯𝘺𝘦𝘸𝘦, 𝘢𝘭𝘪𝘺𝘦𝘬𝘶𝘸𝘢 𝘢𝘮𝘦𝘬𝘶𝘧𝘢 𝘢𝘬𝘢𝘮𝘸𝘦𝘬𝘢 𝘬𝘪𝘧𝘶𝘢𝘯𝘪 𝘱𝘢𝘯𝘨𝘶.
21 𝘕𝘪𝘭𝘪𝘱𝘰𝘰𝘯𝘥𝘰𝘬𝘢 𝘢𝘴𝘶𝘣𝘶𝘩𝘪 𝘯𝘪𝘮𝘯𝘺𝘰𝘯𝘺𝘦𝘴𝘩𝘦 𝘮𝘵𝘰𝘵𝘰 𝘸𝘢𝘯𝘨𝘶, 𝘬𝘶𝘮𝘣𝘦? 𝘈𝘮𝘦𝘬𝘶𝘧𝘢. 𝘏𝘢𝘵𝘢 𝘢𝘴𝘶𝘣𝘶𝘩𝘪 𝘯𝘪𝘭𝘪𝘱𝘰𝘮𝘵𝘢𝘻𝘢𝘮𝘢 𝘴𝘢𝘯𝘢, 𝘬𝘶𝘮𝘣𝘦! 𝘚𝘪𝘺𝘦 𝘮𝘵𝘰𝘵𝘰 𝘸𝘢𝘯𝘨𝘶 𝘯𝘪𝘭𝘪𝘺𝘦𝘮𝘻𝘢𝘢.
22 𝘕𝘥𝘪𝘱𝘰 𝘺𝘶𝘭𝘦 𝘮𝘸𝘢𝘯𝘢𝘮𝘬𝘦 𝘸𝘢 𝘱𝘪𝘭𝘪 𝘢𝘬𝘢𝘴𝘦𝘮𝘢, 𝘴𝘪𝘷𝘺𝘰 𝘩𝘪𝘷𝘺𝘰; 𝘣𝘢𝘭𝘪 𝘮𝘵𝘰𝘵𝘰 𝘸𝘢𝘯𝘨𝘶 𝘯𝘥𝘪𝘺𝘦 𝘢𝘭𝘪𝘺𝘦 𝘩𝘢𝘪, 𝘯𝘢 𝘮𝘵𝘰𝘵𝘰 𝘸𝘢𝘬𝘰 𝘯𝘥𝘪𝘺𝘦 𝘢𝘭𝘪𝘺𝘦𝘬𝘶𝘧𝘢...
23 𝘕𝘥𝘪𝘱𝘰 𝘮𝘧𝘢𝘭𝘮𝘦 𝘢𝘬𝘢𝘴𝘦𝘮𝘢 , 𝘏𝘶𝘺𝘶 𝘢𝘯𝘢𝘴𝘦𝘮𝘢, 𝘔𝘵𝘰𝘵𝘰 𝘸𝘢𝘯𝘨𝘶 𝘺𝘶 𝘩𝘢𝘪 , 𝘯𝘢 𝘮𝘵𝘰𝘵𝘰 𝘸𝘢𝘬𝘰 𝘢𝘮𝘦𝘬𝘶𝘧𝘢. 𝘕𝘢 𝘩𝘶𝘺𝘶 𝘢𝘯𝘢𝘴𝘦𝘮𝘢, 𝘚𝘪𝘷𝘺𝘰 𝘩𝘪𝘷𝘺𝘰; 𝘣𝘢𝘭𝘪 𝘮𝘵𝘰𝘵𝘰 𝘢𝘭𝘪𝘺𝘦𝘬𝘶𝘧𝘢 𝘯𝘪 𝘸𝘢𝘬𝘰, 𝘯𝘢 𝘮𝘵𝘰𝘵𝘰 𝘢𝘭𝘪𝘺𝘦 𝘩𝘢𝘪 𝘯𝘪 𝘸𝘢𝘯𝘨𝘶.
24 𝘔𝘧𝘢𝘭𝘮𝘦 𝘢𝘬𝘢𝘴𝘦𝘮𝘢, 𝘕𝘪𝘭𝘦𝘵𝘦𝘦𝘯𝘪 𝘶𝘱𝘢𝘯𝘨𝘢. 𝘞𝘢𝘬𝘢𝘭𝘦𝘵𝘢 𝘶𝘱𝘢𝘯𝘨𝘢 𝘮𝘣𝘦𝘭𝘦 𝘺𝘢 𝘮𝘧𝘢𝘭𝘮𝘦.
25 𝘔𝘧𝘢𝘭𝘮𝘦 𝘢𝘬𝘢𝘴𝘦𝘮𝘢, 𝘔𝘬𝘢𝘵𝘦 𝘮𝘵𝘰𝘵𝘰 𝘢𝘭𝘪𝘺𝘦 𝘩𝘢𝘪 𝘷𝘪𝘱𝘢𝘯𝘥𝘦 𝘷𝘪𝘸𝘪𝘭𝘪, 𝘬𝘢𝘮𝘱𝘦 𝘩𝘶𝘺𝘶 𝘯𝘶𝘴𝘶, 𝘯𝘢 𝘩𝘶𝘺𝘶 𝘯𝘶𝘴𝘶.
26 𝘕𝘥𝘪𝘱𝘰 𝘮𝘸𝘢𝘯𝘢𝘮𝘬𝘦 𝘺𝘶𝘭𝘦, 𝘢𝘮𝘣𝘢𝘺𝘦 𝘮𝘵𝘰𝘵𝘰 𝘸𝘢𝘬𝘦 𝘢𝘭𝘪𝘺𝘦 𝘩𝘢𝘪 𝘯𝘪 𝘸𝘢𝘬𝘦, 𝘢𝘬𝘢𝘮𝘸𝘢𝘮𝘣𝘪𝘢 𝘮𝘧𝘢𝘭𝘮𝘦 𝘬𝘸𝘢 𝘮𝘢𝘢𝘯𝘢 𝘮𝘰𝘺𝘰𝘯𝘪 𝘮𝘸𝘢𝘬𝘦 𝘢𝘭𝘪𝘮𝘸𝘰𝘯𝘦𝘢 𝘮𝘵𝘰𝘵𝘰 𝘸𝘢𝘬𝘦 𝘩𝘶𝘳𝘶𝘮𝘢, 𝘢𝘬𝘢𝘴𝘦𝘮𝘢, 𝘌𝘦 𝘣𝘸𝘢𝘯𝘢 𝘸𝘢𝘯𝘨𝘶, 𝘮𝘱𝘦 𝘩𝘶𝘺𝘶 𝘮𝘵𝘰𝘵𝘰 𝘢𝘭𝘪𝘺𝘦 𝘩𝘢𝘪, 𝘸𝘢𝘭𝘢 𝘶𝘴𝘪𝘮𝘸𝘶𝘦 𝘬𝘢𝘮𝘸𝘦. 𝗟𝗮𝗸𝗶𝗻𝗶 𝘆𝘂𝗹𝗲 𝗺𝘄𝗶𝗻𝗴𝗶𝗻𝗲 𝗮𝗸𝗮𝘀𝗲𝗺𝗮, 𝗔𝘀𝗶𝘄𝗲 𝘄𝗮𝗻𝗴𝘂 𝘄𝗮𝗹𝗮 𝘄𝗮𝗸𝗼; 𝗮𝗸𝗮𝘁𝘄𝗲.
27 𝘕𝘥𝘪𝘱𝘰 𝘮𝘧𝘢𝘭𝘮𝘦 𝘢𝘬𝘢𝘫𝘪𝘣𝘶, 𝘢𝘬𝘢𝘴𝘦𝘮𝘢, 𝘮𝘱𝘦 𝘩𝘶𝘺𝘶 𝘸𝘢 𝘬𝘸𝘢𝘯𝘻𝘢 𝘮𝘵𝘰𝘵𝘰 𝘢𝘭𝘪𝘺𝘦 𝘩𝘢𝘪, 𝘮𝘢𝘢𝘯𝘢 𝘺𝘦𝘺𝘦 𝘯𝘥𝘪𝘺𝘦 𝘮𝘢𝘮𝘢 𝘺𝘢𝘬𝘦.

Bwana Yesu atusaidie sana, kwenye mistari hii tunawaona wana wake wawili ambao kwa Neema ya Mungu walipata watoto, k**a tunavyojua mtoto ni baraka na anaweza kukusabishia mambo makubwa baadae katika maisha yako k**a atalelewa vizuri.

Wito pia hauko mbali sana kile mtoto anaweza kuleta na kikawa matunda mema kwa mzazi, kumbuka tulikotoka nimesema wito wowote unamazingira ya kuita kwanza na kisha anayeitwa kuitikia wito. Na akisha itika wito anaingia kwenye mchakato ili kuuishi na kuutumikia na mwisho wa siku kumzalia matunda.

Ukiongea au ukiwasikiliza watu ambao wanaonekana kuwa na matokeo makubwa katika wito walio nao utagundua hakuna hata mmoja ambaye aliibuka tu. Kwenye wito wa kila mmoja kuna mambo mapya na yakipekee yanayomtengeneza kuwa alivyo, lakini kanuni siku zote ni zile zile zilizomsaidia kila mmoja.

Hakuna wito usio kuwa na vita, kila mwenye wito ni lazima atakutana na upinza ili ikiwezekana aache au apoteze wito wake.

K**a nilivyozungumza, hapo mwanzo kutokana na sababu mbalimbali, mtu anaweza kuacha au kupoteza wito wake. Na lengo la somo hili ni kumsaidia yule ambaye tayari amepoteza au kuacha wito wake.

Kila kitu kina dalili yake zinazo ashiria uwepo wa hicho kitu, Waswahili wanasema " dalili yamvua ni mawingu" . Hivyo ni muhimu tukazifahamu dalili za mtu kupoteza au kuacha wito wake.
Kwenye matari wa ishiri na sita katika mistari yenye mwansiko mkolezo, tunaona baada ya hawa watu wawili kuwa wamepata watoto mmoja alizembea akamlalia mtoto wake akafa na kumbadilishia mwenzake. Na mwenzake, alipochunguza akagundua kuwa amewekea mtoto ambaye siyo wake na kuamua kuwasilisha malalamiko yake kwa mfalme.
Mfalme kwa hekima aliyokuwa nayo alijua aliyepoteza siku zote ana roho ya bora tukose wote.

Dalili hii ni muhimu sana kwa kila mwenye wito kwani itamsaidia kujitambua mapema na kushughulikia hii hali ili kurudisha wito wake. Kila mwenye wito ukiona, ndani yako kuna msukumo wa nguvu unaokusukuma kiasi kwamba unatamani kwa sababu wewe kuna namna umepoteza unatamani hata kutumia gharama, ili tu uhakikishe mnakosa wote. Jua hii ni dalili inayokuonyesha kuwa tayari umepozeza au umeacha wito wako. Na unatakiwa kurudi kwa Mungu kwa toba kisha uombe kurejeshewa.

Aliyepoteza yuko tayari kuangamiza cha wale anaoona wanaendelea mbele, kwa mfano mtu alikuwa mwimbaji na amepoteza huo wito atahakikisha anapambana na waimbaji wenzake hata kwa kuwachafua ili tu ahakikishe wanakosa wote. Roho hii ya tukose wote ikimshika mtu ina lengo moja tu la kuwaharibia watu wengine waliosimama na wito wao.
Mtu mwenye roho hii atajaribu kunyang' anya wito wa mwingine na akishindwa atatamani ufe lengo likiwa tukose wote.

Uonapo dalili hii rudi angalia wapi umeanguka ukatengeneze na Mungu ni mwaminifu utasimama tena kwenye wito wako.

Ninaamini umejifunza nitakuletea hapa hapa dalili nyingine itakayokusaidia kujua kuwa umeacha au umepoteza wito wako.
Naitwa peter Maboja.
0744 956 919.

10/03/2024
Ujenzi wa choo cha kanisa unaendelea tusaidiane kwa kuchangia kazi hiyo kupitia namba ya huduma 0756914466
26/12/2021

Ujenzi wa choo cha kanisa unaendelea tusaidiane kwa kuchangia kazi hiyo kupitia namba ya huduma 0756914466

03/05/2019

Jana tulijifunza kumbe mtumishi wa mungu anaweza kuwa katika position yoyote ya KAZI sio kutumika madhabahuni tuu tulimuangalia yusuph alikuja kuwa waziri mkuu wa misri kutokea gerezani Kwa kutafsiri ndoto ya farao Kwa mungu akupe kufanikiwa popote kwenye KAZI yoyote unayofanya. Jina la yesu likutetee na kukupa kibari soma mwanzo 41:1.................

03/05/2019

Mungu awabariki mpitao kwenye page yeti.

23/12/2018

kwa huduma au kuchangia huduma +255756914466

29/08/2018

Nawasilimu katika jina la yesu aliye hai. ndugu msisahau kusikiliza wimbo wa mwimbaji wetu kwenye youtube jina ni mary iseke

karibu sana
13/07/2018

karibu sana

18/02/2018

Shalom watu wa Mungu ! Nawakaribisha kwenye ibada ya leo Wingu la Bwana International church- Nzega church, Kitangili Nzega.
Ibada itaanza saa 8:00 mchana hadi saa 12:00 jioni,
Wote mnakaribishwa kuja kusikia ujumbe wa neno la Mungu kutoka kwa watumishi wa Mungu aliye hai maombi na maombezi yatafanyika pia.
Ratiba yetu nyingine ni kila Alhamisi na Jumanne kuanzia saa 10:00 jioni hadi saa 12:30 jioni.
Ubarikiwe na karibu sana huduma ya Wingu la bwana International churchKitangili Nzega Mjini !

Address

Nzega

Telephone

+255756547218

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Wingu la Bwana International church- Nzega posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Wingu la Bwana International church- Nzega:

Share