Neno Kwanza

Neno Kwanza Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Neno Kwanza, Church of Christ, Njombe.

K**a una kiu ya kumjua Mungu, mpango wako ni kwenda mbinguni, na kuishi maisha ya ushindi hapa duniani mbali na dhambi :
Follow hii page;
facebook; Neno kwanza
Au jiunge whatsapp group kwa usomaji biblia na kujifunza Neno
https://chat.whatsapp.com/GcN2LY

MWALIKO WA MUNGULeo sitahubiri sana, haya maandiko ni mahubiri tosha, niambie wewe umeelewaje hapo, ni kweli unakataa hu...
28/10/2024

MWALIKO WA MUNGU

Leo sitahubiri sana, haya maandiko ni mahubiri tosha, niambie wewe umeelewaje hapo, ni kweli unakataa huo mwaliko? Kwa sababu gani? Kwa ajili ya starehe hizi za dunia? Unakubali ukose hii ahadi ya Mungu?

Ufunuo 21: 1-8.
1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, k**a bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
5 Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.
6 Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure.
7 Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.
8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.

Kuna rafiki yangu mmoja aliniambia Mtumishi subiri kwanza nile ujana nitaokoka baadae uzeeni, khaa, nikajiuliza hivi ana uhakika gani kwamba hata huko uzeeni atafika? Je ana mkataba na Mungu au? Na dunia hii ya sasa inavyozidi kuharibika na uovu kuongezeka, unapata wapi ujasiri wa kusema hivyo, sio k**a nataka kukutisha, hapana ila natamani ufikiri mara mbili, linalowezekana leo lifanye leo, wakati wa wokovu uliokubalika ni sasa.

Dunia hii na mambo yake yote yatapita ila Neno la Mungu na ahadi zake vyote vitatimia, k**a ujio wa Yesu ulitabiriwa miaka zaidi ya 5000 iliyopita ukatimia na mambo mengi tu tunaona katika biblia yaliyotabiriwa yametimia basi na hilo andiko tulilosoma hapo litatimia tu, dunia hii itaondoshwa itakuja mbingu mpya na nchi mpya.

Rafiki yangu usidanganywe na dunia hii na starehe zake, yote yatapita hayo, wako wapi akina Michael jackson, R.kelly au P.diddy, watu ambao nilikuwa mshabiki wao sana enzi za ujinga, mmoja alijulikana k**a mfalme wa pop, mwingine mfalme wa rnb, niliwapenda sana, nilitamani kuwa k**a wao, nilikariri na kuimba sana nyimbo zao, k**a starehe wamefanya sana hadi wamepitiliza, hakuna starehe wasiyoijua, wewe mwenzangu na mimi sidhani k**a unajua starehe yoyote ukifananisha na hao jamaa, huwezi kuwafikia hata kidogo, lakini pamoja na hayo, je mwisho wao umekuwaje, au utakuwaje? ndio swali la msingi la kujiuliza, Au unafikiri wataishia wapi, peponi au jehanamu? Walikuwa na vipaji vikubwa lakini walikubali kutoa kumpa na kumtumikia mkuu wa giza, sasa wanavuna walichopanda, ndugu yangu TAFAKARI NA CHUKUA HATUA.

(Ufunuo 3:20) Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

Hii ni Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake, Bwana Yesu yu karibu kuja.

Mwalimu Gadi Mbajo.

15/10/2024

ASILI YA JINA LA YESU.

Jina la Yesu maana yake ni mwokozi, pia linatambulika k**a Yoshua katika agano la kale, maana yake ni ile ile moja mwokozi, wayahudi au waebrania au waisrael walikuwa na kawaida au utamaduni wa kumpa mtu jina kutokana na wito aliokuwa nao, majina yote waliyokuwa wanatoa yalikuwa yana maana, walikuwa hawampi mtoto jina kwa sababu wanajisikia kumpa, hapana, ilikuwa inategemea sana wito au jukumu alilopewa au kusudiwa na Mungu kuja kufanya hapa duniani.

Kwa hiyo wale watoto waliopewa majukumu makubwa muda mwingine Mungu alikuwa anaingilia kati na kutoa majina Yeye mwenyewe kwa mfano tunaona kwa Ibrahimu, Israel, Yohana mbatizaji na hata Yesu mwenyewe.

Kwa hiyo tunajifunza hapo kabla ya kutoa jina kwa mtoto wako embu fikiri mara mbili, lakini itapendeza zaidi na itakuwa ni busara sana kumuuliza Mungu mwenyewe aliyekupa huyo mtoto, sababu ndiye anayejua amemkusudia huyo mtoto kuja kuwa nani.

Kwa hiyo Yesu aliitwa mwokozi kwa sababu kazi yake kubwa ilikuwa kuja kuuokoa ulimwengu na dhambi yao, alikuja kutuokoa mimi na wewe ili tusiangamie na kuishia jehanamu kwenye moto wa milele, alikuja kutuokoa na mauti na kutupatia uzima wa milele, kivipi? Kwa njia ya kuchukua dhambi zetu na adhabu zake ili sisi turithi uzima wa milele.

Yohana 3:16
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

2Petro 3:9
Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, k**a wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.

Picha inaanzia hapa, huu ulikuwa ni mpango kamili wa Mungu, uliosukumwa na nguvu ya upendo aliokuwa nao, ambao ndiyo msingi mkuu au unatakiwa uwe msingi mkuu wa dini zote au imani zote, kwa sababu Mungu aliupenda ulimwengu ulioasi, hakutaka watu aliowaumba waangamie, upendo ukazaa nia, nia yake kubwa ni kuwa watu wote waokolewe, japo huwa hamlazimishi mtu,

Hakuishia kupenda tu na kuwa na nia hapana, upendo huwa unakamilishwa na kitendo, kwa hiyo akamtuma Yesu, na ndiye na aliyetoa jina la Yesu, lenye maana ya mwokozi, kulingana na kusudi alilobeba.

Kwa hiyo nia hii aliyokuwa nayo Mungu Baba akamuambukiza na mwanae pia, kwa hiyo Mungu aliupenda ulimwengu akamtuma mwanae, mwanae pia aliupenda ulimwengu akakubali kuja kutuokoa, kwa hiyo ujio wake duniani ulikuwa maalumu kwa lengo moja tu, kukamilisha mission/mpango wa Mungu Baba, nao ni kutuokoa wanadamu.

Mathayo 1:21
Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.

Yohana 1:29
Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!

Isaya 53:5
Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

Mathayo 18:11
[Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea.]

Luka 9:56
Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.

1Thesalonike 1:10
na kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye alimfufua katika wafu, naye ni Yesu, mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayokuja.

Yohana 12:47b
sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu.

Lakini mtu yoyote akishaokolewa na Kristo Yesu, anapewa nia ile ile aliyokuwa nayo Bwana Yesu, ya kusaidia au kutaka watu wengine pia waokolewe, inakuwa ni mwendelezo, kutoka kwa Mungu, kwa Yesu hadi kwetu, ndio wito mkuu tuliokuwa nao watumishi, kwa sababu Roho mtakatifu yule yule aliyekuwa anatenda kazi ndani ya Kristo Yesu ndiye tuliyepewa k**a zawadi kwa kumuamini Yeye, huyo Roho mtakatifu anatenda hata sasa ndani yetu, wito ni ule ule, kazi ni ile ile, nia ni ile ile kuokoa.

1 Wakorintho 2:16
Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.

Wafilipi 2:5
Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;

Watumishi wanaotoka ndani ya wito na nia hiyo na kuanza kutafuta mali na fedha na vitu vingine vya kidunia wanakuwa wametoka nje ya reli, nje ya mpango wa Mungu, wanakuwa wametoka kwenye nia ya Kristo, kunakuwa hakuna nguvu ya upendo nyuma yao inaowasukuma kuanisha na kuendesha huduma zao, bali tamaa ya mali na fedha, uwe na uhakika hata mahusiano na aliyewatuma yanakuwa hayapo tena, ndio hao anaosema siku ya mwisho atawakataa, akisema hawajui, maana kazi yao ilikuwa kujilimbikizia mali na starehe za dunia, ila sio kuokoa watu.

Mathayo 7:21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, 22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.

Binafsi huu ndio wito wangu mkuu kutaka watu wote waokolewe, na mtumishi wa hivi huwezi kumzuia kwa namna yoyote kwa sababu anatembea na nguvu na uweza na kujitoa k**a alivyokuwa Bwana Yesu, na huwezi kumzuia wala kumkatisha tamaa kwa chochote sababu anajua ni nini anafanya na wito wake ni nini.

Unaweza ukashangaa kwanini mtumishi wa hivi anaweza kukutana na mambo mengi ya kumkatisha tamaa lakini akasonga mbele, watu wanaweza kumsema vibaya, kumdharau, kumkatisha tamaa kwanamna tofauti lakini akasonga mbele, na muda mwingine, pengine watu hao hao anaowasaidia ndio wanaweza kutumika kumkatisha tamaa, lakini akavumilia na kusonga mbele na wala asiwe na kinyongo nao ni kwa sababu hii, ya wito na nia ya Kristo Yesu ndani yetu.

Hata Yeye Bwana Yesu alivumilia mengi, kukataliwa, kutukanwa, kusemwa vibaya, alitemewa hadi mate, alipigwa na kusulubiwa tena na watu hao hao aliotumwa awaokoe, lakini hakukasirika, hakuzira , hakulalamika wala hakuacha, sababu yeye ni mwokozi na alikuja duniani kwa sababu hiyo tu, kuokoa, naye alijua, alitambua amekuja kufanya nini duniani, kwa mfano, k**a kweli wewe wito wako ni udaktari huwezi kulalamika ukiletewa wagonjwa sababu ni kazi pia ni wito wako, kuona watu wanapona, mtu anayelalamikia kazi anayofanya ujue kabisa huyo huo sio wito wake, Bwana Yesu naye pia alitambua hilo, kwa hiyo alivumilia yote, aliishia kusema Mungu wasamehe maana hawajui walifanyalo.

Isaya 53:3
Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na k**a mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.

Luka 9:22
akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi, na kukataliwa na wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, na kuuawa na siku ya tatu kufufuka.

Luka 17:25
Lakini kwanza, hana budi kupata mateso mengi, na kukataliwa na kizazi hiki.

Luka 18: 32-33.
32 Kwa kuwa atatiwa mikononi mwa Mataifa, atafanyiwa dhihaka; atatendwa jeuri, na kutemewa mate; 33 nao watampiga mijeledi, kisha watamwua; na siku ya tatu atafufuka.

Luka 23:34
Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura.

Kiukweli huwezi kumchukia au kumkasirikia mtu anayehitaji msaada na hajui k**a anahitaji msaada, sababu anakuwa hajui afanyalo.

Nitoe mfano huu wanasema mtu anayetaka kuzama majini, ukienda kumuokoa msubiri kwanza mpaka aishiwe nguvu ndio umbebe, kwa sababu akiwa na nguvu zake huwa ana tapa tapa anaweza kukuzamisha nawewe pia, sasa hapo inahitajika hiyo busara kwa sababu huwezi kujaribu mara moja akakusumbua ukamuacha sio sawa, sababu kwa muda ule anakuwa hajui afanyalo, au ni sawa na mtoto mdogo unaweza kumbeba mgongoni akakuchana na viwembe huwezi kukasirika na kumtupa sababu anakuwa hajui afanyalo, ndivyo Bwana Yesu alivyokuwa anatutizama, nasisi tunatakiwa kutazama hivyo kwa wengine pia ambao hawajamjua Yesu.

Kwa hiyo na wale anaowaokoa anawapa nia, nguvu na kiu hiyo hiyo ya kutaka watu wengine waokolewe pia, mtumishi wa kweli anayefahamu wito wake hawezi kukata tamaa au kukatishwa tamaa kirahisi, ukifunga mlango mmoja atafungua mwingine, sababu ndio kazi aliyobakiwa nayo kufanya hapa duniani, kuna muda Bwana Yesu aliacha hadi chakula sababu ya wito wake na moto uliokuwa unawaka ndani yake, kiu yake ilikuwa akachape injili ili watu wote waokolewe.

Yohana 4:31
31 Huko nyuma wanafunzi wakamsihi wakisema, Rabi, ule, 34 Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake.

Kati ya silaha alizokuwa nazo kwa msaada wa Roho mtakatifu, ametupatia nasisi pia watumishi wake ni uvumilivu, upole na subira, sababu muda mwingine hao hao uliotumwa uwasaidie wanaweza kukupiga mawe, huwezi kukasirika wala kuacha sababu ndio kazi yako, ndio wito wako, yanaweza pia kutokea mambo mengi ya kutukatisha tamaa, lakini Bwana Yesu alishatutahadharisha mapema,

Mathayo 20:22-23a.
22 Yesu akajibu akasema, Hamjui mnaloliomba. Je! Mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi? Wakamwambia, Twaweza, 23 Akawaambia, Hakika mtakinywea kikombe changu;

Mathayo 10:17, 22.
17 Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga; 22 Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.

Mathayo 24:9
Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu.

Yohana 15:18
18 Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi, 19 K**a mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia.
(Yohana 16:4a) Lakini nimewaambia hayo, ili makusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi naliwaambia.

1Thesalonike 3:3
mtu asifadhaishwe na dhiki hizi; maana ninyi wenyewe mnajua ya kuwa twawekewa hizo.

Kwa hiyo ukiona mtumishi anakata tamaa au anakatishwa tamaa kirahisi na watu au mazingira basi hajajua bado wito wake.

2Timotheo 2:24-26.
24 Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi; bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha, mvumilivu; 25 akiwaonya kwa upole wao washindanao naye, ili k**a ikiwezekana, Mungu awape kutubu na kuijua kweli; 26 wapate tena fahamu zao, na kutoka katika mtego wa Ibilisi, ambao hao wametegwa naye, hata kuyafanya mapenzi yake.

Mtumishi wa kweli wa Mungu haiwezekani kabisa kumkatisha tamaa, moto ukishawaka umewaka hakuna awezaye kuuzima, Bwana Yesu alisema,

Luka 12:49
Nimekuja kutupa moto duniani; na ukiwa umekwisha washwa, ni nini nitakalo zaidi?

Silaha nyingine aliyotumia na aliyotupatia Bwana Yesu ni kweli na ujasiri, kuna muda watu wengi walimuacha sababu hawakuwa tayari kusikia kweli na wengine walimchukia sababu ya kuzungumza ukweli lakini yeye hakujali, baadhi ya wanafunzi wake walipoondoka aliwauliza wale waliobaki na nyie mnataka kuondoka? Kwa sababu alikuwa yupo tayari kubaki hata peke yake na kusimamia kweli hata k**a dunia yote ingemkataa,

Muda mwingi alipingana na mafarisayo sababu walikuwa wanafiki watu wasio na kweli, mdomoni wanasema hivi, ila moyoni hawamaanishi, sababu matendo yao ni tofauti na wanachosema, aliwakemea hadharani bila woga,

Mathayo 15: 7-9.
7 Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema, 8 Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami, 9 Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.

Yohana 8:40 -44.
40 Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, mtu ambaye nimewaambia iliyo kweli, niliyoisikia kwa Mungu. Ibrahimu hakufanya hivyo, 41 Ninyi mnazitenda kazi za baba yenu. Ndipo walipomwambia, Sisi hatukuzaliwa kwa zinaa; sisi tunaye Baba mmoja, yaani, Mungu, 42 Yesu akawaambia, K**a Mungu angekuwa baba yenu, mngenipenda mimi; kwa maana nalitoka kwa Mungu, nami nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma, 43 Mbona hamyafahamu hayo niyasemayo? Ni kwa sababu ninyi hamwezi kulisikia neno langu, 44 Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.

Yohana 3: 20-21
20 Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa, 21 Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu.

Huo msimamo na huo ujasiri ndio aliotuachia watumishi wake pia, mtumishi wa kweli wa Bwana Yesu yupo tayari kusimamia kweli mpaka mwisho hata k**a watu wote watamchukia, watamkataa na akabaki peke yake, lakini pia anakuwa na ujasiri k**a simba.

Kizazi cha sasa wengi wanapenda injili za mafanikio na miujiza, wanapenda wahubiriwe kile wanachopenda kusikia, ukiwahubiria kweli, ukiwakaripia na kuwaonya hawatakupenda, ndio maana manabii wa uongo wanapata watu wengi sana, wanahubiri na kufanya kile watu wanapenda kusikia.

Lakini nisisitize njia inayoweza kuonekana ni njema na ina watu wengi inaelekea upotevuni, njia iendayo uzimani ni nyembamba na imesonga sio wengi wataiona au kuipenda kuifata, Mungu akusaidie uweze kutambua hili nilisemalo.

Mathayo 7:13-14
13 Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo, 14 Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.

Tuishie hapa kwa leo, hiyo ndiyo asili ya jina la Yesu, na Bwana Yesu aliyowaachia pia wale wote waliomuamini, waliozaliwa mara ya pili, jina limebeba wito na utume huo.

Mwl. Gadi J Mbajo.

30/08/2024

Tafadhali uliyekuwa umefollow hii page kwa ajili ya mafundisho, hamia kwenye page hii Gady John Mbajo
ndio nitakuwa naweka huko mafundisho kwa sasa, pole kwa usumbufu, Mungu akubariki.

30/08/2024

Tuingie darasani;
ELEWA AU FAHAMU VIZURI MAAGANO YALIYOPO KATI YA MUNGU NA MWANADAMU.
PART 4:

Somo lililopita tumejifunza historia ya agano ilipoanzia, tumeona Mungu alipomuumba tu mwanadamu kwa sababu alimuumba kwa sura na mfano wake, akampa utashi na akili ya kuweza kuamua, kiasi kwamba anaweza kuamua hata kutomtii yeye Mungu aliyemuumba, ilibidi aingie naye agano/mkataba, kwamba unaweza kuamua kutonitii japo nimekuumba, ila nakushauri unitii, Mungu akaainisha faida na hasara za kutomtii, agizo kuu lilikuwa hili, kwamba ukinitii utaishi usiponitii utakufa, lakini pia utaharibu mfumo wako wote wa maisha hapa duniani.

Leo tutajadili aina za maagano yaliyopo, tutaangalia,
Maagano makuu manne,

AGANO LA KWANZA.
AGANO LA MUNGU NA ADAMU.

Agano la Mungu na adamu katika bustani ya edeni, Adamu ni jina la uwingi, Mungu alipoingia agano/mkataba na Adamu, wanadamu wote walikuwa ndani ya adamu, kwa hiyo na sisi tunahusika sana na yale mapatano, ukisoma mwanzo sura ya 1 na ya 2, adamu na Mungu walienda vizuri, ndio maisha halisi Mungu aliyoyakusudia kwa mwanadamu,

kuanzia sura ya 3 shetani anaingia anamshawishi hawa, naye anamshawishi adamu, wanakula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya, kwa lugha rahisi wanavunja agano, kwamba hawataki kumtegemea Mungu tena, wanataka kuishi kwa mtizamo wao, watafsiri maisha wanavyoona wao, wakakataa kuishi kwa maelekezo ya Mungu, na ndio wanadamu wengi wanaishi hivyo sasa kwa kutegemea akili zao, Mungu wamemuweka mbali.

Na ndio chanzo cha matatizo yote tunayoyaona duniani, kwa sababu Mungu hakumuumba mwanadamu ajitegemee mwenyewe au ategemee akili yake tu, mwanadamu kujitegemea, ni sawa na umwambie mtoto mdogo aliyezaliwa leo ajitegemee mwenyewe haiwezekani.

Mithali 3:5.
Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;

Mwanzo 3: 4-5.
4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa k**a Mungu, mkijua mema na mabaya.

Mti wa uzima unamuwakilisha Yesu au Neno la Mungu, au hekima ya Mungu au sheria na maagizo ya Mungu, mti wa ujuzi wa mema na mabaya, Mwandishi ni k**a alitumia lugha nzuri kidogo akapunguza makali ila ni mti wa kifo, ni kinyume cha mti wa uzima, ni kukataa kuishi kwa Neno la Mungu, au muongozo wa Mungu, kwa lugha rahisi ni kukataa mkataba au agano au offer aliyotoa Mungu ya kufunga agano na yeye, ni kuasi au kutenda dhambi, dhambi ni uasi ni kukataa kumtambua aliyekuumba na kufata maelekezo yake.

Mti wa uzima.
Mithali 3:13,18
13 Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu.
18 Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu ashik**anaye naye.

Ufunuo 22:14
Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.

Yohana 14:6
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

Baada ya adamu kuvunja agano, kwa kuchagua kutofata maelekezo ya Mungu, baada ya kushawishiwa na kudanganywa na shetani, akatolewa katika bustani ya edeni, alitolewa katika uwepo wa Mungu, na Mungu akawa hana shirika naye tena, akaanza kuishi maisha ya taabu yaliyojaa huzuni na mauti ilitawala,

sasa ili Mungu kumsaidia huyu mwanadamu kwa sababu ya upendo wake mkuu, akaanza kuandaa mpango mwingine wa kumsaidia mwanadamu, akatafuta mtu aliye tayari kumtii, afanye naye agano atengeneze taifa kupitia yeye, ndio tunaona agano linalofatia sasa, tumejifunza katika somo lililopita kuwa kazi kubwa ya agano/mkataba ni kuimarisha mahusiano na ushirika baina ya pande mbili, Mungu alikuwa anataka kutengeneza mahusiano yaliyoharibika.

AGANO LA 2
AGANO LA MUNGU NA IBRAHIMU NA UZAO WAKE.
Wanadamu walikuwa wametawanyika juu ya dunia, lakini hawana Mungu, wamemuasi Mungu, ili Mungu aweze kuwasaidia mpango wake ulikuwa atafute mtu, kupitia mtu huyo mmoja atakayemtii aunde taifa litakalomtii kupitia mtu huyo mmoja, afanye nalo agano/mkataba, na mkataba huo ni ule ule aliofanya nao na adamu akaurudisha tena, na alikusudia kupitia hilo taifa ajifunue, kwa kuwasaidia na kuwafanikisha sana, ili awatie wivu na watoto wake wengine waliotawanyika huko na huko wamrudie yeye, mpango wake Mungu ulikuwa kurudisha mahusiano na watu wake wote aliowaumba, ila alitaka afanye hivyo kupitia taifa moja, ambalo ndilo israel alilolichagua,

Kwa bahati mbaya, uzao wa Ibrahimu ambao ndio taifa la israel, hawakumuelewa bado Mungu, wakawa wanaasi na kutenda dhambi, na wakati Mungu alitaka wawe mfano, kwa hiyo, ikawapelekea kuingia utumwani katika nchi ya misri, Mungu akaandaa mpango mwingine wa kuwatoa baada ya kumlilia, ili akafunge nao agano jingine.

AGANO LA 3.
AGANO LA MUNGU NA WANA WA ISRAEL-MLIMA SINAI KUPITIA MUSA.
Mungu akafanya agano lingine na Musa baada ya kuwatoa utumwani, akajifunua zaidi kwao, ukifatilia kila agano linalofatia Mungu alikuwa anazidi kujifunua zaidi, anachotaka watu wajue agano/mkataba ili waweze kufanya wajibu wao, akawapa na torati au sheria au wajibu wao wanaotakiwa kufanya ili Mungu naye aweze kuwasaidia na kuwafanikisha.

Kutoka 19:5-6
[5]Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu,

[6]nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli.

Kwa bahati mbaya wakavunja tena agano hili, kwa sababu walizidisha uasi na kutenda dhambi, tena zaidi ya mataifa ya nje ambao wao walitakiwa wawe mfano kwao, Mungu naye akavunja agano, akasema hawatambui tena, akaja na mpango wa mwisho, ambao ni agano la mwisho,

2 wafalme 21:9
Walakini hawakusikia; naye Manase akawakosesha wafanye mabaya, kuliko mataifa Bwana aliowaharibu mbele za wana wa Israeli.

Zekaria 11: 9-10.
9 Ndipo nikasema, Sitawalisheni; afaye na afe; atakayekatiliwa mbali na akatiliwe mbali; nao waliosalia, kila mmoja na ale nyama ya mwili wa mwenziwe, 10 Nikaitwaa hiyo fimbo yangu, iitwayo Neema, nikaikata vipande viwili, ili nipate kulivunja agano langu nililolifanya na watu wa kabila zote.

Lakini jambo zuri au jema, ni kuwa Mungu aliondoa lile la kwanza, akaleta agano jipya lililo bora zaidi,

waebrania 10: 9.
Ndipo aliposema, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili.

Kwa hiyo maagano yote hayo ya mwanzo kabla ya ujio wa Yesu yanatambulika k**a agano la kale, baada ya ujio wa Yesu, ndio analeta agano jipya, agano bora kupita yote, na agano la mwisho, baada ya hili k**a watu hawataelewa k**a mwanzo na kujiingiza hapo, Mungu hana mpango wa kuleta agano jingine, au wokovu mwingine au msaada mwingine tena.

AGANO LA MWISHO- AGANO JIPYA.
akamtuma mwanaye mpendwa Yesu, akasema kupitia yeye sasa ataunda hilo taifa (KANISA), mwanzo alitaka atumie waisrael hao tena, wakamkataa kisha wakamsulubisha, kufika hapa Mungu hakuchagua tena taifa flani au mtu flani au kabila flani, hapa akafungua geti wazi, ili sasa yoyote ajiingize, akasema yoyote atakayemuamini mwanaye anaingia katika agano na yeye, na anakuwa mwakilishi wake au taifa lake teule, haijalishi unatoka kabila gani au nchi gani ilimradi ukimuamini Yesu unaingia katika agano unakuwa taifa la Mungu ili utumike sasa kuwavuta wengine, hao watu wa Mungu waliopotea, waingie katika agano, ndio kazi kubwa aliyopewa mtume Paulo akafanye utume kwa mataifa.

Luka 22: 19-20.
19 katwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.
20 Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.]

Na ukimuamini Bwana Yesu, haki zote na ahadi zote njema katika maagano ya nyuma hayo yanakuwa haki yako pia, kwanini? Kwa sababu Mungu alipoingia maagano na wana wa israel hakuwa amewalenga wao tu, ila alikusudia kuwatumia k**a chombo, ndio maana alimwambia Ibrahimu hutakuwa baba wa taifa tu ila utakuwa baba wa mataifa mengi, baraka za Ibrahimu na Israeli zilikusudiwa kwa watu wote dunia nzima wale watakaoamua kumrudia Mungu na kuingia kwenye agano na Mungu tena, na hiyo inafanyika hivyo kupitia kwa Bwana wetu Yesu, ukimuamini yeye unaingia katika agano jipya.

Mwanzo 17:4
Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi,

Wagalatia 3:14.
ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.

Somo linalofata tutaangalia faida/baraka zinazopatikana mwanadamu anapoamua kurudi na kuingia agano tena na Mungu, ni mambo gani ambayo Mungu ameahidi au amemkusudia mtu aliyeamua kurudi katika agano na yeye Mungu, Mungu yeye hana shida mkataba upo mezani, ni uamuzi wa mwanadamu kuamua kurudi kwake na kuangusha sign pale, aanze kupata mema Mungu aliyomkusudia, dini zilitakiwa ziwe msaada katika hili, japo dini tena zimekuwa kikwazo kikubwa kwa mtu kurudisha mahusiano yake na Mungu, halikuwa kusudi la Mungu kuleta dini bali kurudisha mahusiano na mwanadamu kupitia agano.

Maagano hayo yote manne nimeyaeleza na nimeyachambua kwa undani, yote yanapatikana katika youtube, channel jina,
Gadi John Mbajo.

Itaendelea…

Taarifa.
Kwa uliyekuwa umenifollow page hii ya Neno Kwanza tafadhali nifollow page hii kwa sasa ndiyo naitumia kuachilia mafundisho, Fb
Gady John Mbajo

Na Mwl. Gadi J Mbajo.

01/07/2024

USOMAJI WA BIBLIA
Usomaji wa biblia sio kitu kinachovutia kwa wengi ila wacha nikushauri kitu.

Usomaji biblia ni sawa na kupanda mbegu, huwezi kuvuna muda huo huo, wakati wa kulima wengi huwa wanapata shida, lakini ukifika wakati wa mavuno huwa ni furaha, panda mbegu sasa faida yake utaiona baadae.

Kazi moja kuu ya Roho wa Mungu ni kutukumbusha na kutuongoza, hasa ikifika kipindi flani una shida, huwa anapenda kutumia Neno kutukumbusha, kututia moyo, kutufariji na kutuongoza, lakini sasa hataweza kufanya hivyo k**a huna Neno la kutosha ndani yako, hawezi kukumbusha kitu ambacho hukijui, hakipo ndani yako.

Kwa hiyo nakushauri soma Neno, unapanda mbegu kwa faida yako ya baadae, hata k**a hupendi jilazimishe, hakuna mkulima anayefurahia sana wakati wa kupanda😊 isipokuwa wakati wa mavuno.

Hizi siku za mwisho tunazoenda utahitaji Neno kuliko kitu chochote, niamini mimi.

Follow hii page kwa mafundisho zaidi.
Gady John Mbajo

Unaweza kujiunga pia na group letu la whatsapp kwa usomaji biblia na mafundisho zaidi.

10/06/2024

Unapochagua mambo ya dunia na starehe zake, maanake umeamua kujifurahisha kwa kitambo tu, ili uje uangamie milele, miaka 80 si kitu ukifananisha na uzima wa milele, choose wisely, tumia akili yako sawa sawa kuamua, ujifurahishe kwa kitambo tu uje uishie jehanamu ya moto, au umtii Mungu uje kurithi uzima wa milele? The choice is yours, uamuzi ni wako.

Warumi 6:23
[23]Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Marko 8:36
[36]Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?
Ufunuo wa Yohana 21:8
[8]Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.

Ila Mungu anashauri hapa,

Kumbukumbu la Torati 30:19
[19]Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;

john mbajo #
wa kanuni za ufalme #

Address

Njombe

Telephone

+255752282884

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Neno Kwanza posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share