13/04/2023
*CHANJO YA MBEGU*
Agronomist Emmanuel Mwakabana anaandika nakala hii fupi kuwaelewesha wakulima na kuwaongeza ufahamu.
Chanjo ya mbegu ni sumu (kiuatilifu) kinachoongezwa juu ya mbegu. Sumu hii inaweza kuwekwa pia rangi ili kutofautisha mbegu ambazo teyari zimeshakingwa na ambazo bado hazijapata huduma hiyo.
Rangi ambazo utumika sana kwa masoko ya Tanzania kwenye mbegu za mahindi ni *Nyekundu na Kijani*.
Mara baada ya mbegu kuchanganywa na hizi sumu, mbegu hizo zinakuwa hazifahi tena kwa matumizi ya chakula kwa wanadamu ama mifugo.
π Kila pakiti ya mbegu (mahindi, mbogamboga, n.k) ambazo zimeshachanganya na sumu hizi (Seed dresser) uwekwa alama ya ONYO kwenye pakiti. Mfano.
*ONYO*
*Sumu: Mbegu hii imetiwa dawa ya Maxim na Chlorbyriphos. Usiitumie kwa madhumuni ya chakula cha binadamy, mifugo au kukamua mafuta ya kula* tahadhari hii utaiona kwenye mbegu SC 403 Tumbili nyuma ya pakiti.
*SUMU. Mbegu hii imehifadhiwa na dawa na haifai kwa kuliwa au kutumika kuwalisha mifugo au kazi nyingine yeyote isipokuwa kuoanda shambani* Tahadhari hii utaiona kwenye Pakiti ya Mbegu ya Alizeti - Record ya kampuni ya Singidani Seed Company Ltd.
Mifano ya chanjo hizo ni pamoja na...
Maxim
Apron Star
Gaucho
Thirum
Cruiser
Chlorbyriphos nimetaja kwa uchache. Soma vibandiko vya maelezo kwenye pakiti za mbegu utaona mifano mingine ya chanjo za mbegu.
*Kwanini mbegu zinachangangwa ama kupakwa sumu kabla ya kutumika mashambani*.
Yafuatayo ni malengo ya kuchanganya mbegu na sumu tajwa hapo juu.
π Kulinda na kukinga mbegu isibunguliwe na wadudu wa gharani kwa urahisi.
π Kuziongezea uwezo wa uotaji na uchomozaji kutoka kwenye ardhi baada ya kupanda.
π Kuzinginga na magonjwa ya ukungu / kuvu zikiwa katika kuifadhiwa.
Mf. Dumping off, Blight (ukungu)
π Kuzilinda dhidi ya wadudu wavamiao miche katika hatua za awali.
π Kuzikinga dhidi ya kusambaa kwa magonjwa ya ukungu.
π Kudhibiti wadudu wa ardhini waaribifu kwa mazao.
- Minyoo fundo.
Napozitaja kazi hizo tajwa hapo juu sina maana kila sumu iliyochanganywa na mbegu basi inafanya kazi hizo zote; HAPANA.
Chanjo ya mbegu inaweza kufanya kazi moja, mbili ama zaidi kulingana na kiambata amilifu kilichopo kwenye sumu.
Mbegu zinaweza kupata magonjwa, kuvamiwa na wadudu ama mbegu chache kusambaza ugonjwa kwa mbegu zingine.
Ili kutunza na kuakikisha ubora wa mbegu ni vema mbegu zikachanganywa na sumu ili kuakikisha zinabaki katika ubora.
Sumu hizi zinaweza pia kuangamiza magonjwa ambayo teyari yameshavamia baadhi ya mbegu pia kudhibiti uanzishwaji wa vimelea vya kuvu (fungal spores) na kufanya mkusanyiko wako wa mbegu unakuwa salama.
πChanjo za mbegu ni sumu, zaweza kuwa sumu kwa mbegu na hata kwa wanyama na binadamu; hivi matumizi yake yanapaswa kuwa ya umakini na kwa usahihi ili kuepuka madhara.
Umakini huo ni pamoja na kutumia kiasi sahihi cha sumu na kiasi sahihi cha mbegu, na uvaaji wa vifaa kinga wakati wa uchanganyaji wa sumu na mbegu.
*Mfano wa chanjo ya mbegu na namna ya kutumia*
πApron Star 42WS.
βNi chanjo ya uhakika kwa mbegu za mahindi,Soya na Maharage, viazi, pia na mboga mboga.
πSumu hii uchanganywa na mbegu kisha utoa kinga kwa mmea dhidi ya wadudu wote wanaofyonza majani mateke na miche michanga, inzi wa mazao (maharage), inzi weupe, viroboto (Thrips), minyoo ya ardhini (wireworms), panzi (grasshopper), teemites na wadudu wengine.
πPia ni kinga ya magonjwa ya ukungu, kata kiuno (dumping off), ubwiri unga, ukungu, n.k.
πPia uboresha mizizi, na kuwezesha mmea uwe na mizizi mingi na yenye afya.
πUsaidia sana mimea kuota kwa pamoja na kwa kasi na nguvu maradufu.
πPia uzuia matatizo yakuoza mbegu na miziz ama mashina machanga.
πChanjo hii hudumu katika mmea kwa mwezi mzima toka siku ya kupanda mbegu zako.
Upenya kwenye mmea mara baada ya mbegu kupasuka na kuanza kuota.
Hivyo ni kinga yakutosha shambani na hata kitaruni.
Hii ndio maana wataalum tunaita chanjo ya mbegu, ambayo utuakikishia afya ya mazao na ubora wa mavuno yetu.
*NAMNA YAKUTUMIA.*
Changanya 8g za Apron Star na 30 - 40ml za maji changanya vizuri kisha changanya na 4kg za mbegu ( mahindi/soya/Mpunga/maharage n.k) kwenye mfuko ama plastic.
π *Unaweza pia kutumia 5g za sumu hii Apron Star, 20ml za maji na 2kg za mbegu yako (mahindi, Soya, maharage, kunde, mpunga, n.k)*
Acha kidogo ikauke na baada ya kukauka, mbegu hizo zinakuwa teyari zimeshapewa chanjo na teyari kwa kusia/kupanda shambani.
Pia kwa mbegu ndogondogo k**a za vitunguu, hoho, nyanya, pilipili, n.k mchanganyo wake hautahitaji maji na ni kiasi kidogo cha dawa kitaitajika.
Kwa hili nivema kufanya mawasiliano na wataalum kwakua ni ngumu kupata 4kg za mbegu hizi kwa wakulima wadogo wadogo.
Vaa groves wakati wa uchanganyaji epuka kunusa ama kuruhusu hewa ya dawa kuingia puani ama mdomoni. Epuka kushika sumu kwa mikono, hakikisha unavaa mavazi kinga kwa kulinda afya yako.
Ni vema kulinda mwili na afya yako wakati wote unapotumia sumu za kilimo.
Soma maelekezo yaliyopo katika vifungashio vya viuatilifu.
Nimalizie kwa kusema, usipande mbegu bila kuzipa chanjo.
Chanjo itakupa faida nyingi kwa mavuno na afya ya mimea yako.
Ni mimi Bwanashamba nguli.
Agronomist.
Emmanuel Mwakabana.
+255754998944 WhatsApp
ππΎππΎππΎ π π½ πΈ