27/08/2026
BIBLIA INASEMA NINI KUHUSU UFUFUKO WA WAFU SIKU YA MWISHO.
Utukufu kwa Yesu kristo, aliye Alfa na Omega, Mungu wa milele nakuarika kusoma Makala hii inayohusu kufufuka kwa watu waliokufa siku ya Mwisho.
Biblia Inasema kwamba maisha ya watu duniani hayaishii pale mtu akifa na kuzikwa kaburini bali maisha ya mtu aliyekufa huwa yanaendelea.
Watu wameshindwa kuelewa kwamba Miili tuliyonayo ndiyo huwa inazikwa kaburini kwa sababu, Miili ni udongo tu.
Mwanzo 3:19b kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.
Mungu alivyomuumba mwanadamu alimuumba akiwa na Vipande Viwili Yaani Mwili pamoja na Pumzi yaani Roho.
Mtu ni roho(sio Roho Mtakatifu) roho yako, inayokaa ndani ya nyumba inaitwa mwili.
Mwanzo 2:7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi(mwili), akampulizia puani pumzi ya uhai(roho); mtu akawa nafsi hai.
Maneno ya u mavumbi wewe na mavumbini utarudi aliyeambiwa ni Mwili uliotengenezwa kwa udongo.
Na ndio Maana sote mashahidi Mtu akifa huzikwa kaburini Ila kinachozikwa ni Mwili wa mtu na sio roho ya mtu.
Kifo sio tukio bali ni utengano wa Roho ya Mtu na Mwili wa Mtu, Roho ikichomoka ndani ya mwili, Mwili huwa haufai tena hauna nguvu, hauwezi kutembea wala kukaa unaanguka unaenda kuzikwa.
Yohana 6:63a Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu;
Sasa kwa kawaida mwili wa mtu ukizikwa kaburini, Roho huendelea kuwa hai na hurudi kwa Mungu kwa ajiri ya Hukumu.
Waebrania 9:27 Na k**a vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;
Hukumu hii hutoa Mungu mwenyewe na hii hukumu sio ile ya mwisho wa dunia atakayohukumu Mwanakondoo Yaani Yesu kristo bali, hukumu hii ni mwanzo tu wa kuamua huyo mtu aende wapi.
Ukifa hakuna mapumziko bali Roho yako inaenda kukutana na Mungu mwenyewe na anatoa hukumu kwa haki.
K**a ulikuwa ujamwamini Yesu Yaani kuokoka Basi, Unahukumiwa kwenda kuzimu kwenye mateso makali, na K**a ulikuwa umeokoka Duniani ulimwamini Yesu kristo basi, utapelekwa paradiso Yaani eneo la mapumziko au kifuani pa Ibrahim.
Mtu anayehukumiwa na kutupwa kuzimu ananza kulipia hukumu yake kwa mateso makali sana na huu sio Mwisho wa yote ni mwanzo tu,
Luka 16:23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
Tajiri huyu alivyokufa alizikwa mwili wake kaburini lakini Roho yake ilienda kwa Mungu na ikahukumiwa kutupwa kuzimu na kuzimu kule alipata mateso.
Lakini mtu ambaye anahukumiwa kuingia paradiso Basi kule anapata pumziko la kweli na huu ni mwanzo wa raha na atapata raha zaidi, Lazaro Masikini alipokufa alichukuliwa na Malaika akapelekwa kupumzika.
SASA BIBLIA INASEMA NINI KUHUSU UFUFUKO WA WAFU.
Siku yaja ambayo Mambo yote yataisha duniani,
1 Wakorintho 15:52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. 53 Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.
Japo linaloongelewa hapa ni:
🔹 Wafu watafufuliwa.
Huu ndio unaitwa ufufuko wa wafu, Maana yake kinachotokea Zile Roho zilizokufa zitapewa miili tena isiyoharibika na kurudi hai kwa ajiri ya Hukumu ya Siku ya Mwisho.
Roho ambazo zilikuwa kuzimu zitapewa miili na zitahukumiwa Sasa hukumu ya Pili yaani kutupwa Jehanamu kwenye ziwa la Moto na huu ndio utungu wenyewe.
Ufunuo wa Yohana 20:12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.
Hukumu hii ni kutupwa Motoni, kuendelea na mateso, mateso ya Jehanamu ni mara mia ya mateso ya kuzimu.
Lakini na zile Roho za watu zilizoingia Paradiso na zenyewe zitaingia Mbinguni na huko kutakuwa na sherehe na shangwe.
Na huu ndio Mwisho wa maisha ya wanadamu Yaani ama utupwe Motoni uishi milele Motoni, au uingie Mbinguni uishi milele kwa starehe.
Ili uingie Mbinguni fanya Mambo haya:
🔹 Okoka
Yaani mwamini Yesu wewe binafsi ndani ya Moyo wako.
🔹 Maisha matakatifu
Acha dhambi ishi kwa usafi.
Wagalatia 5:19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, k**a nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Tuishie Hapa, Mungu akubariki na akupe Neema ya Wokovu.
Kwa Sala ya Toba na Ushauri
Namba: WhatsApp au 0621002308.
Njoo nikuunge group la Whatsapp la Neno la Mungu, weka namba yako hapa.
Share kwa marafiki
✍
Na Pastor Kijana Zaidi.
Pastor Emmanuel Chatanda