Ludewa SDA church SHC

Ludewa SDA church SHC Hii ni page maalumu ya kanisa la Waadventista wa Sabato wilaya ya Ludewa ,Jimbo la Nyanda za juu Kusini SHC

29/05/2025
09/03/2024

*KESHA LA ASUBUHI.*

*JUMAMOSI, 09/03/2024.*

*NJIA YA WAKOSAJI.*

*Ufahamu mwema huleta upendeleo, bali njia ya haini huparuza. - Mithali 13:15.*

✍️ Taarifa za anguko la mwanadamu zilienea kila kinubi kiliwekwa chini. Malaika mbinguni kote kutoka vichwani mwao kwa huzuni. Mbingu yote ilikuwa katika mtikisiko. Halmashauri iliitishwa kuamua kile ambacho lazima kifanyike kwa kosa la wawili hawa. Malaika walihofu kuwa wanaweza kunyoosha mkono na kula tunda la mti wa uzima, na kuwa wenye dhambi wasioweza kufa. Lakini Mungu alisema angewafukuza wakosaji hao kutoka bustanini. Haraka sana Malaika waliagizwa kuilinda njia ya kuuendea mti wa uzima. Ilikuwa ni mpango wa makusudi wa Shetani kwamba Adamu na Hawa wamwasi Mungu, wapokee hasira Yake, na kisha waongozwe kula matunda ya mti wa uzima, ili waweze kuishi milele katika dhambi na kutokutii, na kwa njia hiyo dhambi iwe ya milele. Lakini malaika watakatifu walitumwa kuwatoa nje ya bustani, wakati kundi lingine la malaika wakiagizwa kuilinda njia ya kuuendea mti wa uzima...

✍️ Shetani alishinda. Aliwafanya wengine kuteseka kwa anguko lake. Alikuwa amefukuzwa mbinguni, wako nje ya Paradiso.

✍️ Kwa uasi Adamu aliipoteza Edeni. Kwa kuziasi amri za Mungu mwanadamu ataikosa mbingu, na furaha kamili ya umilele. Hivi sio visasili vya uongo, bali ni ukweli... Nauliza swali, wewe unasimama upande gani?

✍️ Ni kweli kwamba njia ya Shetani imefanywa kuonekana ya kuvutia, lakini yote hii ni udanganyifu; katika njia ya uovu kuna majuto machungu na maumivu mabaya... Katika njia ya uharibifu lango linaweza kung'aa kwa maua, lakini miiba imetanda njiani...

✍️ *"Njia ya haini huparuza," lakini "Njia zake ni njia za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani" (Zaburi 13:15; 3:17). Kila tendo la utii kwa Yesu, kila tendo la kujikana nafsi kwa ajili Yake, kila jaribio lililostahimiliwa vyema, kila ushindi uliopatikana dhidi ya jaribu, ni hatua katika mwendo kuuelekea utukufu etu ushindi wa mwisho. Ikiwa tunamfanya Yesu kuwa kiongozi wet

Ni Kesho .Karibu Sana
26/01/2024

Ni Kesho .Karibu Sana

Karibu Katika Ibada Ya Leo
13/01/2024

Karibu Katika Ibada Ya Leo

Sabato ya Shukrani, Sifa, shuhuda,uimbaji, Nyimbo na Kujiweka Wakfu 2023
29/12/2023

Sabato ya Shukrani, Sifa, shuhuda,uimbaji, Nyimbo na Kujiweka Wakfu 2023

Karibuni sana sana Katika Mkutano Huu Makini
06/06/2023

Karibuni sana sana Katika Mkutano Huu Makini

25/10/2022

*KESHA LA ASUBUHI.*

Jumanne, 25/10/2022.

*KAZI YA KIMWILI INASAIDIA KUKUZA AKILI NA TABIA.*

*Nao watajenga nyumba, na kukaa ndani yake; watapanda mizabibu, na kula matunda yake. Hawatajenga akakaa mtu mwingine ndani yake; hawatapanda, akala mtu mwingine; maana k**a siku za mti ndivyo zitakavyokuwa siku za watu wangu, na wateule wangu wataifurahia kazi ya mikono yao muda wa siku nyingi. Isaya 65:21, 22.*

▶️ Leo, k**a ilivyokuwa katika siku za wana wa Israeli, kila kijana anapaswa kufunzwa majukumu ya maisha ya vitendo. Kila mmoja anapaswa kupata ujuzi wa baadhi ya tawi la kazi ya mikono ambayo, k**a ikihitajika, itasaidia kupata riziki. Hili ni muhimu, si tu k**a ulinzi dhidi ya misukosuko ya maisha, bali kutokana na athari yake juu ya ukuaji wa kimwili, kiakili na kimaadili. Hata k**a ingekuwa hakika kuwa mtu hangehitaji kamwe kukimbilia kazi ya mikono ili kupata msaada, bado wanapaswa kufundishwa kufanya kazi. Bila mazoezi ya mwili hakuna mtu anayeweza kuwa na umbile zuri na afya njema; na nidhamu ya kazi iliyodhibitiwa vizuri pia ni muhimu katika kujipatia akili thabiti, hai na tabia ya kiungwana.

▶️ Wanafunzi ambao wamepata ujuzi wa kitabu bila kupata ujuzi wa kazi ya vitendo hawawezi kudai kuwa na ulinganifu wa elimu. Nguvu ambazo zilipaswa kutolewa katika kazi za namna mbali mbali zimepuuzwa. Elimu haitegemei kutumia ubongo pekee. Kuufanyisha kazi mwili ni sehemu ya mafunzo muhimu kwa kila kijana. Sehemu muhimu ya elimu inakosekana ikiwa mwanafunzi hatafundishwa jinsi ya kujishughulisha na kazi muhimu.

▶️ Zoezi la afya la kiumbe chochote litatoa elimu ambayo ni pana na ya kina. Kila mwanafunzi anapaswa kutoa sehemu kila siku kwa kazi ya bidii. Hivyo basi tabia ya uzalishaji itaundwa na moyo wa kujitegemea utahimizwa, huku vijana wakilindwa dhidi ya mazoea mengi maovu na ya udhalilishaji ambayo mara nyingi ni matokeo ya uvivu. Na haya yote yanaendana na lengo la msingi la elimu; kwa maana katika shughuli za kutia moyo, bidii, na usafi, tunapata upatanifu.

20/10/2022

📖 *SOMO LA ASUBUHI*

*ALHAMISI, OKTOBA 20 2022 SIKU YA TANO YA JUMA*

*KICHWA CHA SOMO >>>* 👇🏼

*KUPITIA YESU HUJA AFYA NA TULIZO KUTOKA KATIKA MASHAKA*

*FUNGU LA MAANDIKO MATAKATIFU >>>* 👇🏼

*Kutoka 15:23, 24.*
Walipofika mahali palipoitwa Mara hawakupata kuyanywa yale maji ya Mara, kwa kuwa yalikuwa machungu; kwa ajili ya hayo jina lake likaitwa Mara. Ndipo watu wakamnung'unikia Musa, wakisema, Tunywe nini?

✍🏼
Bwana alikuwa na somo la kuwafundisha wana wa Israeli. Maji ya Mara yalikuwa ni somo kielelezo, yakiwakilisha magonjwa yaliyoletwa kwa wanadamu kwa sababu ya dhambi. Sio siri kwamba wakaaji wa dunia wanaugua magonjwa ya kila mtindo na kila aina. Ni kwa sababu wanaiasi sheria ya Mungu.
🖊️
Hivyo ndivyo walivyofanya wana wa Israeli. Walivunja vizuizi ambavyo Mungu katika ubunifu Wake alikuwa ameviweka ili kuwalinda na magonjwa, ili waweze kuishi katika afya na utakatifu, na hivyo kujifunza utii katika kusafiri kwao jangwani. Walisafiri chini ya uongozi maalum wa Kristo, ambaye alikuwa Amejitolea Mwenyewe kuwa kafara ili kuhifadhi watu ambao daima watamweka Mungu katika kumbukumbu zao, licha ya majaribu makuu ya shetani. Akiwa amefunikwa katika nguzo ya wingu, ilikuwa ni shauku ya Kristo kuwaweka chini ya bawa Lake la kuwahifadhi wale wote ambao wangefanya mapenzi Yake.
🖍️
Haikuwa kwa bahati kwamba katika safari yao wana wa Israeli walikuja mpaka Mara. Kabla hawajaondoka Misri Bwana alianza masomo Yake ya mafundisho, ili awaongoze kutambua kuwa Yeye ndiye Mungu wao, Mwokozi wao, na Mlinzi wao. Walinung'unika dhidi ya Musa na dhidi ya Mungu, lakini bado Bwana alitaka kuwaonyesha kwamba angewaondolea wasiwasi wao wote ikiwa watamtazama Yeye. Maovu waliyokutana nayo na kuyapitia yalikuwa sehemu ya mpango mkuu wa Mungu, ambapo alitamani kuwathibitisha.
🖊️
Walipofika kwenye maji ya Mara, "Ndipo watu wakamnung'unikia Musa, wakisema, Tunywe nini? Naye akamlilia BWANA; BWANA akamwonesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawaweke

19/10/2022

*KESHA LA ASUBUHI.*

Jumatano, 19/10/2022.

*VICHOCHEA MWILI HATIMAE HUTOA MATOKEO MAOVU.*

*Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo, lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili. 1 Wakorintho 10:13.*

✍️ Sisi watu, pamoja na kukiri kwetu matengenezo ya afya, tunakula kupita kiasi. Kujihusisha na uchu wa kula ndio sababu kuu ya kudhoofika kwa mwili na akili, na ndio msingi wa udhaifu ambao unaonekana kila mahali.

✍️ Kukosa kiasi kunaanzia katika meza zetu katika matumizi ya chakula kisichokuwa cha afya. Baada ya muda, kwa njia ya kuendelea kula ovyo, viungo vya utumbo huwa dhaifu, na chakula kilicholiwa hakikidhi hamu ya kula. Hali zisizokuwa za afya zinaanzishwa, na kunakuwa na uhitaji sana wa chakula kinachochangamsha mwili zaidi. Chai, kahawa, minofu ya nyama huleta madhara kwa haraka. Katika mvuto wa sumu hizi mfumo wa neva unasisimuliwa, na, katika baadhi ya matukio, kwa wakati huu, akili inaonekana kuwa na nguvu na mawazo kuwa wazi zaidi. Kwa sababu vichocheo hivyo huzalisha matokeo yanayokubalika kwa wakati huo, wengi wanahitimisha kuwa wanavihitaji sana na kuendelea kuvitumia.

✍️ Lakini daima kuna athari. Mfumo wa neva, ukiwa na msisimko usiofaa, ulikopa nguvu kwa matumizi ya sasa kutoka kwenye rasilimali zake za nguvu za baadaye. Uimarishaji huu wote wa mfumo ni wa kitambo tu na unafuatiwa na mfadhaiko. Kwa kadiri vichocheo hivi vinavyochangamsha kwa kitambo, mfumo huo utakuwa wa kushusha nguvu za viungo vilivyosisimka baada ya kichocheo kupoteza nguvu yake. Uchu wa kula unaelimishwa kutamani kitu chenye nguvu zaidi ambacho kitakuwa na tabia ya kuendelea na kuongeza msisimko unaokubalika, hadi anasa inakuwa mazoea, na kunakuwa na hamu ya kuendelea kutaka sana kichocheo chenye nguvu zaidi, k**a vile tumbaku, mvinyo, na vileo....

✍️ *Mwisho mkuu ambao Kristo alistahimili mfungo huo mrefu jangwani ulikuwa ni kutufundisha ulazima

21/09/2022

*KESHA LA ASUBUHI*

_Jumatano, Septemba 21, 2022._

*" Wafuasi Wa Kristo Kutofautiana Na Ulimwengu,*

*_“Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu.”_ 1 Petro 2:9.*

*Tunaposoma Neno la Mungu, inaonekana wazi kuwa watu Wake wanapaswa kuwa wapekee na tofauti na ulimwengu usioamini unaowazunguka*. Msimamo wetu ni wa kuvutia na wa kutisha; tunaishi katika siku za mwisho, *basi ni muhimu sana kwetu kuiga mfano wa Kristo, na kutembea k**a Alivyotembea. _“Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.”_ (Mathayo 16:24)*. Mitazamo na hekima ya wanadamu haipaswi kutuongoza au kututawala. Wakati wote vinatuongoza mbali na msalaba.

*Watumishi wa Yesu Kristo hawana makazi yao wala hazina zao hapa*. Ningependa wote waelewe kuwa ni kwa sababu tu Bwana anatawala ndio maana hata tumeruhusiwa kuishi kwa amani na usalama baina ya adui zetu. Sio nafasi yetu kudai upendeleo maalum wa ulimwengu huu. Lazima tukubali kuwa masikini na kudharauliwa kati ya wanaume na wanawake, mpaka pale pambano litakapoisha na ushindi umepatikana. *Waumini wa Kristo wanaitwa kutoka na kutengwa na urafiki na roho ya kidunia; uwezo na nguvu zao zinategemea kuchaguliwa na kukubaliwa na Mungu*....

Ulimwengu unakuwa tayari kwa ajili ya uharibifu wake. Mungu anaweza kuwavumilia wenye dhambi lakini ni kitambo tu. Lazima wanywe masimbi ya kikombe cha hasira Yake isiyochanganywa na rehema. *Wale ambao watakuwa warithi wa Mungu, na warithi pamoja na Kristo katika urithi wa milele, watakuwa watu wapekee. Naam, wa pekee sana kiasi kwamba Mungu ataweka alama juu yao kuwa Wake, watu Wake Kabisa*. Je! Unadhani kuwa Mungu atapokea, heshima, na kuwakubali watu waliochanganyika sana na ulimwengu kiasi kwamba wanatofautiana kwa jina tu? *_“Tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu.

Address

Ludewa
Njombe

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ludewa SDA church SHC posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Ludewa SDA church SHC:

Share