Viwawa Jimbo la Rulenge-Ngara

Viwawa Jimbo la Rulenge-Ngara Ukurasa huu ni maalumu kwa ajili ya kupeana elimu mbalimbali zinazohusu Imani yetu Katoliki.

Swali: Je, padre sakramenti saba za Kanisa Katoliki ziliasisiwa kweli na Yesu Kristo au ni utunzi na ubunifu wa Kanisa K...
07/09/2025

Swali: Je, padre sakramenti saba za Kanisa Katoliki ziliasisiwa kweli na Yesu Kristo au ni utunzi na ubunifu wa Kanisa Katoliki tu? Je, unaweza kuonesha nukuu zozote za Biblia?

Jibu na mzee wenu Pd. Titus Amigu.
Sakramenti saba za Kanisa Katoliki ziliasisiwa kweli na Yesu Kristo na hivyo siyo utunzi na ubunifu wa Kanisa Katoliki. Sasa naonesha nukuu za Biblia zinazohusika k**a ifuatavyo:
1. Ubatizo
Sakramenti ya ubatizo iliasisiwa na Yesu pale alipobatizwa mwenyewe mtoni Yordani hivyo akayabariki maji kwa ubatizo wa wanadamu (Mt 3:13-17, Mk 1:9-11, Lk 3:21-22) na baadaye akaamuru mitume wakabatize watu (Mt 28:18-20).
Kuhusu kiasi cha maji, wafuasi walishaelewa kwamba hata maji kidogo yalitosha ndiyo maana watu 3000 siku ya Pentekoste walibatizwa kwa maji machache (Mdo 2:41-42). Si wao tu, Mtume Paulo alibatizwa kwa maji kidogo (Mdo 9:17-19) na bwana jela na familia yake walibatizwa pia kwa maji kidogo (Mdo 16:33). Maji mengi yakiwapo yanaweza kutumika (Mdo 8:34-39) lakini si lazima kwa sababu ubatizo si maji wala suala la kuoshana uchafu wa nje isipokuwa ni nia ya rohoni kumfuasa Mungu (1 Pet 3:21). Tupeane onyo la kiroho: mtu asibatizwe kwa maji mengi siku hizi na kukufuru kwa kutaka kusema ubatizo wake ni bora kuliko ubatizo wa Wakristo 3000 wa siku ya Pentekoste au bora zaidi ya ubatizo wa Mtume Paulo na wa bwana jela na familia yake.

2. Kipaimara
Sakramenti hii iliasisiwa pale mitume walipopewa Roho Mtakatifu ambaye waliweza kuwapokeza wengine kwa kuwawekea mikono, rejea Yn 20:22 na Mdo 8:14-24). Waliadhimisha sakramenti hii kwa namna bayana kabisa kwa watu wa Samaria k**a tunavyosoma katika Mdo 8:14-24.

3. Ekaristi Takatifu
Sakramenti hii ilidokezwa kwa mbali katika chakula cha ajabu kilichoitwa manna walichopewa Waisraeli kwa miaka arobaini jangwani (K*t 16:1-36); iliashiriwa kwa karibu katika miujiza ya kuwalisha watu wengi mikate (Mt 14:13-21, Mk 6:30-44, Lk 9:10-17, Yn 6:1-15); ILIASISIWA KATIKA KARAMU YA MWISHO (Mk 14:12-26, 1Kor 11:23-32) na iliamriwa itumike na Wakristo wote. Yesu alisema watakaokula mwili wake na kunywa damu yake watakuwa na uzima wa milele naye atawafufua siku ya mwisho (Yn 6:35.47-69). Yesu hawatanii wanadamu, hivyo maneno yaliyo katika Yn 6 hakutania bali alimaanisha hivyo hivyo alivyosema.
Watu wasio na sakramenti ya Ekaristi Takatifu na wasiokula mwili wa Yesu na kunywa damu yake wanayaweka maisha yao wenyewe rehani. K**a wanajua alichosema Yesu na wanapuuza ni wakaidi; k**a hawajui alichosema Yesu ni wajinga, ila wana ujinga unaoshindika. Lakini basi hata wasio na Ekaristi Takatifu na wasioipokea wataweza kuupata uzima wa milele kwa sababu ya uwingi na ukuu wa rehema ya Mungu tu kwa vile atawapima kwa huruma kwa kigezo cha pekee, ndicho kigezo cha kusikiliza dhamiri zao tu (Rum 2:12-15). Kisingelikuwapo kigezo hiki, watu hao wasingekuwa na chao tena.

4. Kitubio
Mintarafu sakramenti hii tunaeleza ifuatavyo. Nguvu ya kuondoa dhambi ni ya Mungu (Mk 2:1-12) lakini kwa hiyari yake aliwapasia wanadamu nguvu (ufunguo) hiyo waitumie kwa niaba yake na hivyo kuasisi sakramenti ya Kitubio (Yn 20:19-23). Kwa kuwa ufunguo amewapatia wanadamu, wanadamu hawana budi kwenda kuungama kwa hao waliokabidhiwa ufunguo (Isa 1:18-20). Kuwakimbia au kugoma kuwatumia waliokabidhiwa ufunguo ni ukaidi.

5. Mpako wa Wagonjwa
Yesu aliasisi sakramenti hii pale alipowaamuru mitume na wafuasi wake wakawawekee mikono wagonjwa na kuwapaka mafuta (Mt 10:8, Mk 6:7-13, Lk 9:2). Baada ya kupaa Yesu mbinguni, mitume waliendelea kuiadhimisha sakramenti hiyo kwa wagonjwa kwa ufahamu kamili (Yak 5:13-18).

6. Ndoa
Yesu aliiasisi sakramenti ya ndoa pale alipohudhuria harusi ya Kana na kwa uwapo wake kuikubali taasisi ya ndoa na kuleta baraka juu yake (Yn 2:1-12).

7. Upadre
Yesu aliiasisi sakramenti ya Upadre au Daraja pale alipoamuru mitume wawe wanarudia adhimisho la Ekaristi Takatifu, yaani kwa kule kusema β€œFANYENI HIVI KWA UKUMBUSHO WANGU” k**a anavyotueleza vizuri mtume Paulo kwamba ndivyo ilivyopokezwa na wale waliokuwapo sakramenti hiyo inaasisiwa (1Kor 11:23-25). Huwezi kuwaamuru watu warudie kitu kwa kudumu k**a watu hao si wa kudumu. Hapa rejea muktadha wa karamu ya mwisho yenyewe (Mt 26:26-28, Mk 14:22-24, 1Kor 11:23-25).

Hatima
Hadi hapa natumaini jibu limekaa vizuri na limekutosheleza msomaji wangu. Watu wanaodhani kwamba sakramenti zilibuniwa na Kanisa Katoliki wanasigina aya hizo zote na wanasoma Biblia kwa raghba wakimfuata Padre Martin Luther aliyekuwa akisoma Biblia kwa makengeza ilmradi asimame kinyume na mafundisho ya Kanisa Katoliki. Ulikuwa mkasa mbaya wa kati ya mwaka 1517-1520. Ushahidi wa jazba yake ni kukosa kuziona na kushonanisha aya hizo za Biblia zilizokuwa wazi kabisa katika Biblia iliyokuwa mkononi mwake. Unapata picha? K**a si jazba ya ubishi, hivi Martin Luther alishindwaje kuziona aya hizo huku akijinasibu kuisoma sana Biblia? Lakini ukiona mtu halioni gari kubwa lililosimama mbele yake ila anakwambia anaweza kuiona sindano iliyolala mchangani ujue umekumbana na kiroja. Lakini mbaya zaidi ni pale wafuasi wa mtu aliyezifunika aya za wazi za Biblia wanapodai kwamba na wao pia hawazioni. Alahaula! Akili ya kuambiwa ilipasa kuongezewa na yako mwenyewe!

IMANI KATOLIKITulidadavue kidogo neno hilo tamu masikioni na mioyoni  mwetu.Ni mafundisho ya Kikatoliki yanayowaunganish...
04/09/2025

IMANI KATOLIKI

Tulidadavue kidogo neno hilo tamu masikioni na mioyoni mwetu.

Ni mafundisho ya Kikatoliki yanayowaunganisha pamoja waamini wote, kila mahali na kutenda kazi iliyo moja kwa ushirika na ushirikishaji, ni
K*tembea pamoja.

Ni kushika mafundisho yote yafundishwayo na Mama Kanisa

Ni imani inayotokana na Mafundisho ya Mitume. Mdo.14:22.

Tumejengwa juu ya msingi wa Mitume na Manabii. Efe.2:20-22.
πŸ“ΏImani Katoliki Ni Mafundisho na Maagizo yote ya Mungu tunayopata kutoka Neno lake kupitia Mababa wa Kanisa. (Mitume.) Mt.28:20; 2Tim.3:10-13.

Ni Kuwachagua Mitume maana ndio Msingi. Lk.6:12-16. Na Kristo ni jiwe kuu la pembeni. Maana Bwana ndiye aliyelianzisha mwenyewe:
Kuna Bwana Mmoja, Imani Moja, na Ubatizo Mmoja, na Mungu Mmoja ambaye ni Baba wa wote aliye juu ya wote. Efe.4:5-6.

πŸ“ΏKatika Imani Katoliki kila mmoja anapewa Neema kwa kadiri ya kipimo alichogawiwa na Kristo. Efe.4:7.

Ndio maana ninasema, nikiungama, ninasadiki maneno yote linayosadiki na Kufundisha Kanisa Katoliki.

Kanisa Katoliki Ni Kuungama Imani Moja. Fil.1:27.

πŸ“ΏImani Katoliki ninaweza kusema, ni Mitume, Bila Mitume tusingelipokea Imani Katoliki Ndani ya Kanisa Katoliki. Mdo. 8:1, 4-8.

πŸ“ΏImani Katoliki ni mwelekeo mmoja, Mshik**ano, na Ushirika Mmoja pamoja na Yesu tukinia mamoja 1Kor.1:10.

πŸ“ΏImani Katoliki Kanisa haligawanyiki 1Tim.3:13. japo watu wanagawanyika.

πŸ“ΏImani Katoliki Ni ya popote, kila mahali na kwa kila kiumbe. Enendeni duniani mwote..Mk.16:15-18.

πŸ“ΏImani Katoliki inatiisha kwa mamlaka kila kiumbe katika nchi, wanyama, ndege n.k, kumwabudu Mungu. Kumb.26:1-11; Mwa.1:28.

πŸ“ΏImani Katoliki Ni watu wote wawe na umoja. Yh.17:21-23.

πŸ“ΏImani Katoliki Ni kuwa na Umoja, Furaha na Amani. Fil.4:1-9; Yh.17:9-19.

πŸ“ΏImani Katoliki ni Imani ya Kanisa (Fides ecclesiae) si imani ya mtu binafsi bali ya Kanisa lote kwa pamoja.

πŸ“ΏImani Katoliki ina misingi mikuu miwili, Maandiko Matakatifu na Mapokeo Mat. 1Pet.1:10; Mdo.17:10-12; Zab.44:1.

πŸ“ΏImani Katoliki Ina Nguzo nne: -Imani, Sakramenti, Amri za Mungu na za Kanisa na Sala ya BWANA.

πŸ“ΏImani Katoliki ina sifa Nne: -Ni Moja, Takatifu, Katoliki na la Mitume.

πŸ“ΏImani Katoliki Pia ina Muundo huu: Kanisa linaendelea kutumwa; Mt.10:5-15; Mk.6:7-13.
-Baba Mtakatifu (Papa)=Kanisa Zima la ulimwengu, Askofu=Jimbo, Paroko=Parokia, Katekista =Jumuiya-Kigango.

Niseme nini!
Imani Katoliki, Ni Kanisa Katoliki ikimaanisha Kanisa la Kristo, Kanisa la Mungu linalokubali Mamlaka ya kiroho chini ya Papa wa Roma akiwa Mkuu wa urika wa Maaskofu juu yake.
Wewe ndiwe Petro.. Mt.16:18.

πŸ“ΏImani Katoliki Inafunuliwa na Mungu uliotolewa na kupitia wana wa Israeli na kukamilishwa kwa kutambulishwa na Yesu ambaye alimfunua k**a Baba kwa kulianzisha Kanisa kwa njia ya RohoMtakatifu aliyetumwa juu ya Mitume wake. Mdo.2:1-13.

πŸ“ΏImani Katoliki Ni imani katika Ubatizo, ambao ndio Muhuri unaoungamwa ndani ya mioyo yetu. Sakramenti ya kwanza kati Saba iliyo mlango ikiangazia kuwa, Mungu ni Mmoja tu. Mungu Baba, Mungu Mwana, Mungu Roho Mtakatifu.

Na mwisho kwa uchache, Tuiungame Imani Yetu Katoliki, Tuipende, Tuilinde, Tuitunze Tuichochee na Kuieneza. 2Tim.4:7-8; Mwa.15:6.

πŸ“ΏImani Katoliki Ni kutumwa k**a kondoo kati ya Mbwa mwitu. Mt.10:16-20.

Imani Katoliki Ni kutangaza kifo cha BWANA, mpaka atakapokuja. 1Kor.11:26.

Amina na Mungu awabariki. Amina

.KANISA KATOLIKI LIMEGAWANYIKA KATIKA SEHEMU KUU TATUKanisa la Mbinguni ambako tunaamini Mungu hutukuzwa na watakatifu w...
02/11/2024

.

KANISA KATOLIKI LIMEGAWANYIKA KATIKA SEHEMU KUU TATU

Kanisa la Mbinguni ambako tunaamini Mungu hutukuzwa na watakatifu wake.

Kanisa lililoko Toharani ambalo kuna waamini wamekufa katika hali ya neema lakini wako Toharani kufanya malipizi ya madhambi,

Kanisa hili hutegemea zaidi maombi ya watakatifu na sisi waamini tulioko duniani kwa ajili ya utakaso wao na ndio maana Kanisa Katoliki linaadhimisha siku ya Marehemu wote kwa ajili ya kuwaombea hawa na vilevile huwaombea katika kila Misa wapate Neema ya utakaso na kujumuika katika Kanisa la mbinguni.

Kanisa la tatu ni letu sisi tulioko hapa duniani amba oni wasafiri kuelekea mbinguni na tunatafuta Utakatifu katika Maisha yetu ya kila siku kwa kuishi katika sala na kufanya yale yanayompendeza Mungu chini ya maongozi ya Mama Kanisa yaani Kanisa aliloanzisha Kristo na kulikabidhi kwa mitume wake na ndio hili tunaliliamini moja, Takatifu, Katoliki na la Mitume.

MATUKIO KATIKA PICHA- RULENGE NGARA. β–ͺ︎Picha mbalimbali wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Uzinduzi wa Grotto la Ma...
31/10/2024

MATUKIO KATIKA PICHA- RULENGE NGARA.

β–ͺ︎Picha mbalimbali wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Uzinduzi wa Grotto la Mama Bikira Maria Parokia ya Watakatifu Petro na Paulo - Buziku , Jimbo Katoliki Rulenge Ngara.

β–ͺ︎Katika Misa hiyo kulikuwa na utoaji Sakramenti ya Kipaimara kwa waimarishwa 105 pamoja na Sakramenti ya Ndoa kwa jozi 23.

Misa Takatifu imeadhimishwa na Dekano wa Dekania ya Bwanga Padre Pamphilius Kitondo wa Jimboni humo.

HABARI PICHA -  BUSERESERE, JIMBO KATOLIKI RULENGE-NGARA. Matukio mbalimbali wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya uto...
21/10/2024

HABARI PICHA - BUSERESERE, JIMBO KATOLIKI RULENGE-NGARA.

Matukio mbalimbali wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya utolewaji wa Sakramenti ya Kipaimara katika Parokia ya Mtakatifu Theresia Mtoto Yesu Buseresere, Jimbo Katoliki Rulenge Ngara.

Misa Takatifu imeadhimishwa na Mhashamu Severine Niwemugizi, Askofu wa Jimbo Katoliki Rulenge Ngara.

07/07/2024

TAFAKARI: DOMINIKA YA 14 MWAKA B WA KANISA

Na Pd. Luoga MT. Mtitu

"Mwanadamu, nakutuma kwa wana wa Israeli, kwa mataifa wanaoasi, walioniasi mimi, wao na baba zao wamekosa juu yangu, naam, hata hivi leo"(Eze 2:2-5).

"Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake? Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni? na maumbu yake hawapo hapa petu?" (Mk 6: 1-6)

Masomo
I:Eze 2:2-5
II: 2 Kor 12: 7-10
Inj. Mk 6: 1-6

Dominika ya 14 ya kawaida mwaka B wa kanisa. Masomo ya dominika hii yanatoa ujumbe unaofanana; kuwahubiria watu wongofu. Katika injili Yesu anahubiri juu ya wongofu kwa watu wake ambao wanamkataa wakidhani kuwa wanamfahamu sana. Hata hivyo Yesu hakubali kukatishwa tamaa anaendelea kuhubiri. Nasi tunafundishwa kutokubali kukatishwa tamaa na mtu yeyote, historia yetu wala udhaifu wetu.

Katika somo la kwanza
(Eze 2:2-5 ), Ezekiel anasema "Bwana Akaniambia, Mwanadamu, nakutuma kwa wana wa Israeli, kwa mataifa wanaoasi, walioniasi mimi, wao na baba zao wamekosa juu yangu, naam, hata hivi leo". Roho wa Mungu anamtuma Ezekieli kutangaza neno la Mungu. Nabii anahitaji nguvu ya Mungu kupeleka imani, mwaliko mgumu kwa watu kuongoka. Anapaswa kubaki imara katikati ya kutoeleweka na upinzani.

Mwinjili Marko (Mk 6: 1-6)
anatueleza kuwa watu wa kijijini kwa Yesu walimkataa Yesu wakidhani walimjua kwa undani. Hawakutambua kwamba mahusiano yake ya familia hayakufunua utambulisho wake halisi. "wengi waliposikia wakashangaa, wakisema...Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake? Huyu si yule seremala, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni? na maumbu yake hawapo hapa petu?"

6:1.Yesu anakataliwa na watu wa kwao, jambo ambalo ni picha ya mwanzo ya kukataliwa mjini Yerusalemu wakati wa mateso na kifo.
6:2. Hekima: K*tokana na hekima yake Yesu alitenda kwa upekee hivyo mara nyingi Wayahudi walimkataa. Rej. Mt 11:19; 12:42; 13:54; Lk 2:52; 7:35; 11:3149; Yn 7:15; 1 Korl:24.30.
Mtindo wa Yesu wa kufundisha, mambo anayoyanena na maisha yote yanamtangaza kuwa katika mlolongo wa wenye busara walioongea kwa sauti ya hekima. Utambulisho wa Yesu na Hekima ulikuwa na maana kubwa. Yesu alikuwa mwanamageuzi aliyetangaza mapenzi ya Mungu kwa ustawi wa watu akishindana na taasisi, hierarkia na sheria. Yesu alikuwa nabii aliyejazwa na Roho Mtakatifu aliyewezesha kufika kwa upendo wa msamaha wa Mungu ulimwenguni kwa kupitia huduma yake na utii wa kujitoa sadaka.

6:3. Huyu si yule seremala: Yesu haitwi seremala katika Injili nyingine. Anashiriki matatizo ya wafanyakazi na anachukua mashaka yao na kuyatunza moyoni mwake. Ukweli ni kwamba Masiya anaonekana k**a seremala wa kimapinduzi. Mwana wa Maria: Hakuna uwezekano kabisa kwa Yesu kuelezwa kwa kumpitia mama yake badala ya baba yake k**a haimaanishi kumtukana. Bila shaka hapa panaweza kusomwa vizuri zaidi k**a makala ni "mwana wa seremala na Maria".

Yesu anatufundisha kuwa tusikubali kuvunjwa moyo/ kukatishwa tamaa na kamwe tusiwe watumwa wa Historia za zamani, mfano umasikini, upagani, kutokuwa wasomi, maradhi hata tabia zetu za zamani zisiturudishe nyuma. Tumebatizwa na kuwa wakristo basi tuanze kuishi upya, hata k**a tulitenda dhambi.

Kila mtu ana vipaji vingi anavyovijua na asivyovijua, pamoja na hilo kila mtu ana mapungufu fulani ambayo yapo pale kwa makusudi kabisa ili kumzuia mtu huyo asije akajivuna kupita kiasi. "Makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili;" (2 Kor. 12 :7-10). Unaweza ukaona mtu fulani ana akili sana darasani mara nyingi anaweza akapata alama za juu kwenye mtihani. Lakini mara nyingine huyohuyo ana uwezo mdogo katika maisha halisi. Mungu hutupunguzia vitu vingine ili tusijivune na tuweze kutegemeana. Mtume Paulo anasema "niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu"( 2 Kor.12:10).

Tunaweza kutumia mapungufu yetu kijiimarisha. Unapojua mapungufu yako ni hatua muhimu ya kuyashinda ili yasikuyumbishe tena. Mfano una mapungufu ya majivuno basi utajitahidi kujizoeza unyenyekevu na kuomba neema ya Mungu.

Sala: Ee Yesu naomba unipe unyenyekevu wa kupokea wito wako wa kuhubiri wongofu kwa watu wote. Nisikubali kukatishwa tamaa na mtu yoyote, historia yangu, umaskini wangu wala hali yangu ya kiuchumi na kielimu. Nakuomba ee Mungu unipe hekima ya kuyatumia mapungufu yangu kupata ushindi kwa wakati ujao. Amina

πŒπ€π’πŽπŒπŽ π˜π€ πŒπˆπ’π€ - π‰π”ππˆ πŸπŸ‘, πŸπŸŽπŸπŸ’πƒπŽπŒπˆππˆπŠπ€ π˜π€ 𝟏𝟐 π˜π€ πŒπ–π€πŠπ€ (𝐁) Na Pd. Victor Orwa OFMSOMO 1Ayu. 38:1,8-11 Bwana alimjibu Ayub...
23/06/2024

πŒπ€π’πŽπŒπŽ π˜π€ πŒπˆπ’π€ - π‰π”ππˆ πŸπŸ‘, πŸπŸŽπŸπŸ’
πƒπŽπŒπˆππˆπŠπ€ π˜π€ 𝟏𝟐 π˜π€ πŒπ–π€πŠπ€ (𝐁)

Na Pd. Victor Orwa OFM

SOMO 1
Ayu. 38:1,8-11

Bwana alimjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema, Ni nani aliyeifunga bahari kwa milango, Hapo ilipofurika kana kwamba imetoka tumboni. Nilipolifanya wingu kuwa vazi lake, Na giza zito kuwa nguo ya kuifungia, Nikaiagiza amri yangu; Nikaiwekea makomea na milango, Nikasema, Utafika mpaka hapa, lakini hutapita, Na hapa mawimbi yako yanyetayo yatazuiliwa?

Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 107 : 23-26, 28-31 (K)1

(K) Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Washukao baharini katika merikebu,
Wafanyao kazi yao katika maji mengi,
Hao huziona kazi za Bwana,
Na maajabu yake vilindini.

Maana husema, akavumisha upepo wa dhoruba,
Ukayainua juu mawimbi yake.
Wapanda mbinguni, watelemka vilindini,
Nafsi yao yayeyuka kwa hali mbaya. (K)

Wakamlilia Bwana katika dhiki zao,
Akawaponya na shida zao.
Huituliza dhoruba, ikawa shwari,
Mawimbi yake yakanyamaza. (K)

Ndipo walipofurahi kwa kuwa yametulia;
Naye huwaleta mpaka bandari waliyoitamani.
Na wamshukuru Bwana kwa fadhili zake,
Na maajabu yake kwa wanadamu. (K)

SOMO 2
2 Kor. 5 :14-17

Upendo wa Kristo watubidisha; maana tumehukumu hivi, ya kwamba mmoja alikufa kwa ajili ya wote, basi walikufa wote; tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao. Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili. lakini sasa hatumtambui hivi tena. Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita; tazama! yamekuwa mapya.

Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO
Yn. 14 : 6

Aleluya, aleluya, Mimi ndimi Njia, na Ukweli, na Uzima, asema Bwana; Mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. Aleluya.

INJILI
Mk. 4:35-41

Siku ile kulipokuwa jioni, Yesu aliwaambia, Na tuvuke mpaka ng’ambo. Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye. Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji. Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia? Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu. Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado? Wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, Ni nani huyu, basi, hata upepo na bahari humtii?

Neno la Bwana... Sifa kwako Ee Kristo.

π“π€π…π€πŠπ€π‘πˆ

- Mtakatifu Bede, anaeleza Injili ya leo kwamba mashua ambayo Yesu alivuka bahari inawakilisha Msalaba ambao njia salama hupatikana ili kufika kwenye ufuo wa Mbingu. Mashua nyingine zilizofuata zinawakilisha wale walio na imani katika Msalaba wa Kristo na kuufuata. Na ingawa wanateseka na mawimbi ya majaribu na magumu, wanasonga mbele, wakitegemea nguvu ya wokovu ya Msalaba.

- Yesu akiwa amelala huwakilisha usingizi Wake wa kifo, na kuamka Kwake kunawakilisha ufufuo Wake. Maombi ya wanafunzi yanawakilisha hitaji letu la kumgeukia Yesu wakati wa dhoruba na majaribu ya maisha. Kukemewa kwa mawimbi na utulivu unaofuata hudhihirisha neema iliyopatikana kwa kifo na ufufuo wake, ambayo inaweza kunyamazisha pepo na tamaa zisizo na utaratibu. Hofu ambayo wanafunzi walikumbana nayo inaelekeza kwenye woga wetu wenyewe unaotokana na ukosefu wa imani na tumaini katika Mungu.

- Mungu anaweza kusema haya na kweli nyingine nyingi kwetu kupitia matendo na maneno yake yaliyomo katika Maandiko. Hakuna kikomo kwa kina na maana tunaweza kupokea kupitia Neno lake takatifu. Kwa hiyo, ingawa ni muhimu kutafakari juu ya tafsiri mbalimbali ni muhimu pia kutafakari juu ya vifungu hivi sisi wenyewe, ili kuruhusu Bwana wetu aseme nasi ujumbe tunaohitaji kusikia.

Kristo….

16/02/2024
17/01/2024
TOKEO LA BWANA /EPIFANIA"Nao Mamajusi walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno... Wakaingia nyumbani, wakamwona...
07/01/2024

TOKEO LA BWANA /EPIFANIA
"Nao Mamajusi walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno... Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia ... wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane. Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine."(Mt.2:1-12)

Masomo
I:Isa.60:1-6
II:Efe.3:2-3,5-6
Inj Mt.2:1-12

Leo, kanisa linaadhimisha sherehe ya Epifania: Yesu Kristo kujidhihirisha kwa mataifa k**a inavyowakilishwa na Mamajusi (Mathayo 2:1–12). Hii ndiyo siku ambayo mamajusi walifanya ziara kwa mtoto Yesu. Mamajusi hao walikuwa ni watu toka mataifa mbalimbali ambao hawakuwa wayahudi, hao waliwakilisha watu wa mataifa yote. Pia katika ubatizo wake Yesu, Mungu baba alimdhihirisha kwa kusema "... Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe..."(Mk 1:11) Hivyo, Epifania ni udhihirisho wa Yesu Kristo kwa mataifa: Yesu Kristo Mwana wa Mungu, ni mfalme na masihi amekuja kuwakomboa wanadamu wote toka katika dhambi.

Alama za Epifania ni Mamajusi watatu; Gaspari, Melkiori na Baltazari ambao walipeleka zawadi za aina tatu; dhahabu, manemane na ubani. Dhahabu inawakilisha ufalme (mwenye kuletewa ni mfalme), ubani huwakilisha ukuhani na manemane sadaka ya kuwakomboa watu. Maana yake mtoto huyo anayeletewa zawadi hizo ni mfalme, kuhani na masihi ambaye atatolewa sadaka kukomboa watu wake.

Pia ni sikukuu ambayo Kanisa linaadhimisha kubatizwa kwa Yesu na Yohana Mbatizaji. Katika tamaduni za Mashariki, huita sikukuu ya Theofania, ambapo ubatizo wa Yesu, unaoonekana k**a udhihirisho wa Kristo k**a mwanadamu kamili na Mungu pia. Wapagani sasa wanashiriki urithi sawa katika Kristo Yesu. "Tuliiona nyota yake ilipochomoza na tumekuja kumsujudia."

Wakati Waisraeli walikuwa wametoka Misri na walipokuwa wakisonga mbele kuelekea Kanaani, walichukua kila kitu katika njia yao. Baleki mfalme wa Moabu alimwita Balaamu ili awalaani. Balaamu alikuwa mtu wa Mungu lakini alifanya kosa na Mungu akasimama katika njia yake. Balaamu hakuweza kuwalaani Israeli, badala yake aliwabariki. Nyota ikatoka kwa Yakobo. Anainuka akiwa na fimbo mkononi mwake. Sasa nyota imechomoza na inasimama juu ya Yesu ikiwavutia watu kutoka sehemu zote za dunia. Wao pia walifanya makosa lakini Mungu akawaongoza kwenye nyota ya Yakobo, kwa Bwana Yesu.
Wale waliopaswa kufurahia ujio wa masihi hawakufurahia, badala yake walikasirishwa na kujaa chuki mioyoni. Herode, makuhani wakuu na Yerusalemu yote walipaswa kufurahia, kinyume chake, walifadhaika na Herode alipanga kumuua.

Wa kwanza watakuwa wa mwisho na wa mwisho watakuwa wa kwanza. Hadithi ya Mamajusi inaakisi historia ya kanisa la kwanza. Wayahudi walikuwa wamewatenga Wakristo lakini watu wa mataifa mengine walikuwa wakimiminika kwa Yesu na kubatizwa - "...na wakaingia ndani wakapiga magoti na kumsujudia." Katika hadithi hii, uko wapi? Je, wewe ni miongoni mwa makuhani wakuu ambao walipaswa kuhangaika sana kumkaribisha mfalme mchanga wa Wayahudi lakini hawakupendezwa au unaungana na mamajusi?

Tumruhusu Yesu afanye kazi katika maisha yetu na tumtafute Yesu kwa gharama yoyote ile. Mungu hayuko mbali na yeyote kati yetu. Kila siku lazima tumtafute katika maandiko matakatifu, kanisani na katika sala zetu. Kumfikia Yesu ni safari ndefu na tunapaswa kuendelea nayo kila siku. Hata hivyo, tukidumu katika kusali, kila siku na kuliishi neno la Mungu, tutampata Yesu k**a vile mamajusi walivyomwona. Tutafurahi katika yeye na tutaacha ya kale na kuwa viumbe vipya.

πΉπ‘Ÿ.πΏπ‘’π‘œπ‘”π‘Ž 𝑀.𝑇.𝑀𝑑𝑖𝑑𝑒,

Address

Rulenge
Ngara

Telephone

+255625683969

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Viwawa Jimbo la Rulenge-Ngara posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share