TMCS_MZUMBE UNIVERSITY

TMCS_MZUMBE UNIVERSITY Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from TMCS_MZUMBE UNIVERSITY, Religious organisation, Mzumbe.

๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™
06/04/2026

๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™

โœ๏ธโœ๏ธโœ๏ธ
04/01/2026

โœ๏ธโœ๏ธโœ๏ธ

18/10/2025

Kwanini MTIKISIKO KIDOGO TU, ?? ๐Ÿฅบ

18/10/2025

Never Ever....๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™

๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ™
21/04/2025

๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ™

๐ŸŒธNaye Maria aliyefanyika Mama wa Israeli, akafanyika Mama wa Ulimwengu wote, kwaye ni Mtakatifu sana wala uharibifu hauk...
27/10/2023

๐ŸŒธNaye Maria aliyefanyika Mama wa Israeli, akafanyika Mama wa Ulimwengu wote, kwaye ni Mtakatifu sana wala uharibifu haukuhimili mwili wake naye akapalizwa Mbinguni, ni Mama wa Kristo, ni Mama wa Mungu, ni Mama wa Ulimwengu wote naye Kristo amemketisha mahali pazuri sana, huko hajawahi kosa neno juu ya Ulimwengu, yeye atuombea.

๐ŸŒธIkiwa wanadamu kwa mapungufu yao huombeana msamaha kwa wakubwa wao iweje kwa mama aliyefanyika mama wa Mungu, Je si atafanya zaidi? Maana zaidi ni yeye.


AGANO JIPYA NI LIPI? โœ๐ŸพIkiwa sisi ni wakiristo basi tunakiri kuwa sisi ni wa Agano Jipya sababu tumefanyika kutokana na ...
23/08/2023

AGANO JIPYA NI LIPI?

โœ๐ŸพIkiwa sisi ni wakiristo basi tunakiri kuwa sisi ni wa Agano Jipya sababu tumefanyika kutokana na yeye aliyefanya Agano Jipya ndiye Kristo.

โœ๐ŸพNa Agano Jipya ni Lipi? nalo ni hili kumpenda Mungu na Jirani, Mungu yupo katika watu, unavyoishi na watu hasa kusaidia wenye uhitaji ndivyo Mungu anavyokuwa na kuonekana katik maisha yako.

โœ๐ŸพYeye Mwenyewe alisisitiza pale palipo na wawili au watatu kwa ajili yake YEYE YUPO. Majirani wanapokutana Kijumuiya yupo.

โœ๐ŸพAlimwambia yule tajiri auze kila kitu amgawie jirani mhitaji..sababu akifanya hivyo amemfanyia aliye Juu.

Agano la Kale Waisraeli waliingia Mkataba na Bwana nao ni kumpenda Mungu kwa Roho, Moyo na nguvu zote,Kumwabudu yeye Peke yake, Lakini kuna ukimya katika Jirani, Agano lilikosa mapendo ya Jirani, Israeli zaidi alijiangalie yeye peke yake na Mungu wake na Jirani akabaki kuwa najisi.

Ikiwa wewe leo ni wa Agano Jipya na unamtafuta Mungu yuko wapi, MPENDE JIRANI yako, kwayo umemfanyia Bwana, Na Jirani ni yoyote aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu bila kujali Dini wala Kabila

Mwanakondoo wa Mungu,ย  uondoaye dhambi za ulimwengu, utuhurumie x 3Yesu, mwenye Moyo mpole na mnyenyekevu,Uzilinganishe ...
02/08/2023

Mwanakondoo wa Mungu,ย  uondoaye dhambi za ulimwengu, utuhurumie x 3
Yesu, mwenye Moyo mpole na mnyenyekevu,
Uzilinganishe nyonyo zetu na moyo wako.
Tuombe. Ee Mungu, mwenyezi wa milele, uuangalie Moyo wa mwanao mpendelevu, pia na heshima na malipo aliyokutoleaย  kwa ajili ya wenye dhambi, uridhike, uwaondolee wenye kuomba toba kwako kwa njia ya huyo Mwanao Yesu Kristo, anayeishi na kutawala nawe pamoja na Roho Mtakatifu, Mungu, milele na milele. Amina.

๐Ÿคฒ๐Ÿคฒ๐Ÿคฒ๐Ÿคฒ๐Ÿ™
02/08/2023

๐Ÿคฒ๐Ÿคฒ๐Ÿคฒ๐Ÿคฒ๐Ÿ™

Tunamkabidhi kwa Bwana Aliyesema njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kuelemewa na mizigo nami nitawapumzisha Ap...
02/08/2023

Tunamkabidhi kwa Bwana Aliyesema njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kuelemewa na mizigo nami nitawapumzisha Apumzike kwa Amani Amina ๐Ÿ™

02/07/2023

๐—›๐—œ๐—ฉ๐—œ ๐—ช๐—”๐—๐—จ๐—” ๐—ž๐—ช๐—”๐—ก๐—œ๐—ก๐—œ ๐—ง๐—จ๐—ก๐—”๐—”๐—ก๐——๐—”๐— ๐—”๐—ก๐—” ๐—ช๐—”๐—ž๐—”๐—ง๐—œ ๐—ช๐—” ๐— ๐—œ๐—ฆ๐—”?

Kwanza kabisa nianze kwa kusema kwamba, neno "Maandamano" limetokana na neno la Kiingereza "Procession" yaani "Kundi la watu wanaotembea pamoja kwa lengo fulani."

Katika Kanisa Katoliki, maandamano hutafsiriwa k**a msafara wa Waamini wanaotembea pamoja kutoka eneo moja na kwenda eneo lingine, huku wakiimba na kucheza kwa furaha kwa ajili ya kumsifu na kumwabudu Mungu.

Licha ya Kanisa kukopi maandamano yanayofanywa na watu katika jamii zetu, lakini maandamano yanayofanywa na Wakatoliki asili yake ni kutoka kwenye Biblia kabisa, hasa pale Waisraeli walipokuwa wakitembea pamoja kwa furaha kuelekea Kanaani, baada ya kukombolewa kutoka utumwani Misri (Kutoka 13:1-10). Wakiwa njiani, walimchezea Mungu na kumshangilia kutokana na matendo makuu aliyowafanyia (Kutoka 15:1-19).

๐—ฆ๐—ช๐—”๐—Ÿ๐—œ: ๐—ž๐—ช๐—”๐—ก๐—œ๐—ก๐—œ ๐—ช๐—”๐—ž๐—”๐—ง๐—ข๐—Ÿ๐—œ๐—ž๐—œ ๐—›๐—จ๐—”๐—ก๐——๐—”๐— ๐—”๐—ก๐—” ๐—ช๐—”๐—ž๐—”๐—ง๐—œ ๐—ช๐—” ๐— ๐—œ๐—ฆ๐—”?

๐—๐—œ๐—•๐—จ: Mpendwa kabla sijajibu swali hili, naomba nielezee kwanza aina za maandamano yanayofanyika wakati wa Misa, ili wale wasiojua nao pia waweze kujua. Na kupitia maelezo hayo nitakayoyatoa hapo chini, basi na majibu yake yatakuwepo. Hivyo jitahidi kusoma kwa umakini, ili uweze kuelewa.

1. ๐— ๐—”๐—”๐—ก๐——๐—”๐— ๐—”๐—ก๐—ข ๐—ฌ๐—” ๐—ž๐—จ๐—œ๐—ก๐—š๐—œ๐—”

= Hili ni andamano la kwanza kabisa kati ya matano yanayofanyika katika Misa. Kikawaida kabla ya Misa kuanza kwa ishara ya Msalaba, Kuhani pamoja na Watumishi wa Altare, Wanakwaya, Wasomaji na Waamini baadhi kutoka Jumuiya inayohudumia, huandamana kutoka nje ya Kanisani hadi ya Altareni.

= Lengo kuu la maandamano hayo, ni kumshangilia Kristo ambaye anakuja tena kwetu na kuirudia Sadaka yake ya wokovu, aliyoitoa pale Kalvari kwa njia ya Misa Takatifu, huku akitualika tuungana nae na kumpokea katika Karamu yake Takatifu. Na ndio maana katika mwaliko huo wa furaha na wa kipekee, Kanisa lote huandamana pamoja na Yesu kabla ya Misa kuanza.

2. ๐— ๐—”๐—”๐—ก๐——๐—”๐— ๐—”๐—ก๐—ข ๐—ฌ๐—” ๐—œ๐—ก๐—๐—œ๐—Ÿ๐—œ

= Hili ni andamano la pili kati ya matano yanayofanyika katika Misa. Mara nyingi maandamano haya hutokea wakati wimbo wa Aleluya ukiimbwa huku Padre au Shemasi akiweka ubani katika chetezo na kusema: "Bwana uitakase....." Halafu hukibeba juu kitabu cha Injili kwa taadhima kubwa kutoka Altareni au mlango mkuu wa Kanisa mpaka kwenye Ambo (Mimbari ya kusomea), akisindikizwa mbele na Watumishi wa Altare wenye chetezo na mishumaa.

= Lengo kuu la Maandamano haya, ni kuwafanya Waamini wakae tayari na kusikiliza kwa umakini ujumbe wa Neno la Mungu unaohubiriwa muda huo kutoka kwenye kitabu cha Injili. Na ndio maana muda huu unapofika, Kanisa lote linapaswa kukaa kimya, maana maneno yanayosomwa pale ni ya Kristo mwenyewe, akiongea nasi kwa kinywa cha Kuhani au Shemasi aliyeandaliwa kusoma.

3. ๐— ๐—”๐—”๐—ก๐——๐—”๐— ๐—”๐—ก๐—ข ๐—ฌ๐—” ๐—ฉ๐—œ๐—ฃ๐—”๐—๐—œ

= Hili ni andamano la tatu kati ya matano yanayofanyika katika Misa. Kikawaida, baada ya homilia na maombi kuisha, Waamini hutoa matoleo yao ya pesa, mazao, wanyama au kitu chochote kile na kisha hukusanywa pamoja na kupelekwa Altareni huku wakisindikizwa na Watumishi wa Altare wenye chetezo.

= Lengo kuu la maandamano hayo, ni kumuonyesha Mungu jinsi mioyo yetu ilivyo ya ukarimu k**a alivyo yeye, na kumshukuru kwa zawadi ya ridhiki na baraka mbalimbali alizotujalia. Na ndio maana tunaandamana kwa furaha, kumrudishia Mungu yale yote aliyotuneemesha japo ni kidogo, na kumwomba tena Mungu aweze kutubariki siku nyingine.

4. ๐— ๐—”๐—”๐—ก๐——๐—”๐— ๐—”๐—ก๐—ข ๐—ฌ๐—” ๐—ž๐—ข๐— ๐—จ๐—ก๐—ฌ๐—ข

= Hili ni andamano la nne kati ya matano yanayofanyika katika Misa. Mara nyingi baada ya Sala ya mageuzo kumalizika, Waamini Wakatoliki waliojiandaa, hupata fursa ya kushiriki Meza ya Bwana kwa mistari ili kuepuka vurugu na makelele. Kiukweli andamano hili, ni moja ya maandamano makubwa sana ambayo kusanyiko nzima huweza kushiriki kimwili na kiroho pia.

= Lengo kuu la maandamano hayo, ni kumpokea kwa furaha Kristo anayekuja kwetu katika Maumbo ya Mkate na Divai bila mastahili, na kukaa ndani mwetu. Na ndio maana wakati tunaandamana, tunapaswa wote tuimbe hata k**a tupo kwenye mstari, maana anayekuja ndani mwetu ni Mkuu sana, ni k**a vile unavyompokea mgeni mkubwa nyumbani kwako kwa bashishi.

5. ๐— ๐—”๐—”๐—ก๐——๐—”๐— ๐—”๐—ก๐—ข ๐—ฌ๐—” ๐—ž๐—จ๐—ง๐—ข๐—ž๐—”

= Hili ni andamano la mwisho kati ya matano yanayofanyika katika Misa. Kikawaida baada ya Misa kuisha kwa ishara ya Msalaba na maneno ya "Nendeni kwa amani" yanayotamkwa na Padre, Kuhani pamoja na Watumishi wa Altare ndio wanaoruhusiwa kwanza kutoka Kanisani, kisha Waamini wengine hufuata. Ni makosa makubwa sana Muumini kuondoka Kanisani, kabla ya Muongozaji Misa.

= Lengo kuu la maandamano haya, kwanza ni kumpa heshima Padre aliyechukua nafasi ya Kristo kuadhimisha Misa, na kuondoka Kanisani kwa ujasiri na furaha tele baada ya baraka ya mwisho ambayo, Kuhani hutualika huko tuendako tuwe Mabalozi wazuri wa Neno la Mungu tulilolisikia Kanisani. Na ndio maana baadhi ya Mapadre humaliza Misa kwa kusema hivi: "๐—ฆ๐—ฎ๐˜€๐—ฎ ๐— ๐—ถ๐˜€๐—ฎ ๐—ถ๐—บ๐—ฒ๐—ธ๐˜„๐—ถ๐˜€๐—ต๐—ฎ, ๐—บ๐—ป๐—ฎ๐˜๐˜‚๐—บ๐˜„๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐—ฒ๐—ป๐—ฒ๐—ป๐—ฒ๐˜‡๐—ฎ ๐—œ๐—ป๐—ท๐—ถ๐—น๐—ถ." Nasi tunajibu: "๐—ง๐˜‚๐—บ๐˜€๐—ต๐˜‚๐—ธ๐˜‚๐—ฟ๐˜‚ ๐— ๐˜‚๐—ป๐—ด๐˜‚".

๐—ง๐—จ๐— ๐—ฆ๐—œ๐—™๐—จ ๐—ฌ๐—˜๐—ฆ๐—จ ๐—ž๐—ฅ๐—œ๐—ฆ๐—ง๐—ข...

PUMZIKA KWA AMANI KAYETA Kanisa Katoliki Jimbo la Mbeya linaungana na Taifa lote la MUNGU kumkumbuka Mtunzi Mahiri wa Mu...
02/07/2023

PUMZIKA KWA AMANI KAYETA

Kanisa Katoliki Jimbo la Mbeya linaungana na Taifa lote la MUNGU kumkumbuka Mtunzi Mahiri wa Muziki Mtakatifu Marehemu Padri GREGORY FELIX KAYETA.

Historia inatueleza kuwa Fr Kayeta alifariki dunia tarehe k**a ya leo yaani Julai 2, 1992, Siku ya Alhamisi.

Baba yetu huyu ameondoka duniani lakini bado anaishi miongoni mwetu ndani ya Kanisa la Ulimwengu kupitia Muziki Mtakatifu ambapo tungo zake bado zinatesa katika anga ya uenjilishaji.

Tuendelee kumkumbuka katika sala zetu ili mkono wa huruma ya MUNGU uweze kuwa juu yake.

ROHO YA BABA KAYETA IPATE REHEMA KWA MUNGU APUMZIKE KWA AMANI !

Address

Mzumbe

Telephone

+255746111280

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TMCS_MZUMBE UNIVERSITY posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to TMCS_MZUMBE UNIVERSITY:

Share