Kiseke SDA Church

Kiseke SDA Church TO PREPARE PEOPLE FOR INTERNAL LIFE

26/06/2026

*MUHTASARI WA LESONI*

Robo ya Pili 2026 – Somo la 13:
*KATIKA UMILELE*

June 20–26, 2026

____🌹🌹____
Juma hili linahitimisha robo kwa *kuelekeza kwenye tumaini la milele.*
Tumejifunza kuwa,
- *Ingawa tunaishi katika ulimwengu uliojaa dhambi, mateso na majaribu, Mungu ametuandalia uzima wa milele kupitia Kristo.*
- *Wito mkuu ni kuishi leo katika uhusiano wa karibu na Yesu huku tukisubiri kesho kurudi kwake mkombozi.*

________ ________
*DONDOO*
- _Kuishi tayari kwa ujio wa Yesu._

- _Tumaini la mbingu mpya na nchi mpya._

- _Kumwona Yesu ana kwa ana._

- _Yerusalemu Mpya k**a makao ya waliokombolewa._

- _Wito wa kumfuata Mwana-Kondoo kila siku._

- _Mwaliko wa mwisho wa Mungu: *"Njoo."*_

____🌹🌹____
*MAUDHUI YA SOMO*

```Somo linaonyesha kuwa mwisho wa safari ya Mkristo si kaburi bali uzima wa milele pamoja na Kristo.```
Mungu anawaita watu wake kuendelea kukua katika uhusiano naye hadi watakapomwona uso kwa uso.

____🌹🌹____
*DHAMIRA*
Kuimarisha tumaini la uzima wa milele na kuwatia moyo waumini kuendelee kudumu katika Kristo tukisubiri kurudi kwake.

____🌹🌹____
*FUNGU LA KUKARIRI*

*_“Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona k**a alivyo.”_*
— 1 Yohana 3:2

*"Tutafanana naye"*
Tutafanywa wakamilifu katika tabia na utukufu, si kuwa miungu.

*"Tutamwona"*
Pasipo kizuizi cha dhambi, tukitazamana na Yesu, kuonana, kuongea na kukaa pamoja.

Ahadi hii inawahimiza waamini kuishi maisha ya utakatifu tukilitazamia tumaini hilo.

____🌹🌹____
*MATUMIZI MAISHANI LEO*

- _Dumisha uhusiano wa kila siku na Yesu Kristo Mkombozi._

- _Usiweke tumaini lako katika mali za dunia._

- _Ishi ukiwa tayari kwa kurudi kwa Kristo._

- _Washirikishe wengine tumaini la wokovu._

____🌹🌹____
*MUHTASARI WA KILA SIKU*

________ ________
Jumapili (21 June)
– *KUISHI LEO*

Zaburi 80
Ingawa tunatazamia mbingu, tunapaswa kuishi leo katika toba, maombi na uhusiano wa karibu na Mungu.

________ ________
Jumatatu (22 June)
– *HATIMAYE, ANA KWA ANA*

1 Wathesalonike 4:16-17

Kurudi kwa Yesu Kristo kutawaleta pamoja waliofufuliwa na walio hai ili kukutana na Kristo na kuwa naye milele.

________ ________
Jumanne (23 June)
– *BIBI HARUSI*

Ufunuo 21:9-27

Yerusalemu Mpya ni ishara ya makao ya milele ya waliokombolewa na uhusiano wa karibu kati ya Kristo na kanisa lake.

________ ________
Jumatano (24 June)
– *MFUATE MWANA-KONDOO*

Ufunuo 7:17; Isaya 25:8

Baraka kuu ya mbinguni si uzuri wake pekee bali kuwa na Yesu Kristo milele zote, ambaye ndiye Mchungaji wetu.

________ ________
Alhamisi (25 June)
– *NJOO!*

Mathayo 11:28-30; Yohana 6:44

Mungu bado anatoa mwaliko wa neema: *"Njoo."* kila mmoja anaalikwa kumjia Kristo kabla mlango wa rehema haujafungwa.

____🌹🌹____
*MASWALI NA MAJIBU*

________ ________
Swali 1:
*Ni nini kinakugusa katika maelezo ya mbinguni?*

Jibu:
Upendo wa Mungu, kutokuwepo kwa dhambi, mauti, machozi na kumwona Yesu uso kwa uso.

________ ________
Swali 2:
*Ni somo gani la robo unalotaka kulikumbuka?*

Jibu:
Kuendelea kukua katika uhusiano wa karibu na Mungu kila siku kwa njia ya Neno, maombi na imani.

________ ________
Swali 3:
*Ni nani unapaswa kumshirikisha tumaini hili?*

Jibu:
Wanafamilia, marafiki na wote ambao bado hawajampokea Kristo.

____🌹🌹____
*MASWALI YA ZIADA*

________ ________
*(a) Maswali ya Biblia*

1. Kwa nini Yesu anarudi?

- *Kuwachukua waliokombolewa kwake (Yohana 14:1-3).*

2. Kwa nini tumaini la mbinguni ni muhimu?

- *Hutupa nguvu ya kuvumilia majaribu (Warumi 8:18).*

3. Ni nani watakaoingia mbinguni?

- *Wote waliompokea Kristo Yesu kwa imani (Yohana 3:16).*

________ ________
*(b) Maswali ya Wapinzani*

1. Je, mbinguni ni hadithi?

- *Hapana. Yesu aliahidi kuandaa makao (Yohana 14:2-3).*

2. Kwa nini Yesu Kristo hajarudi bado?

- *Mungu anavumilia ili wengi wapate kutubu (2 Petro 3:9).*

3. Kwa nini waumini bado wanateseka?

- *Dhambi bado ipo duniani, lakini mateso yatakoma Kristo atakaporudi (Ufunuo 21:4).*

____🌹🌹____
*REJEA ZA FAFANUZI ZA ZIADA*
Ujisomee kwa kupata uelewa zaidi

________ ________
Pambano Kuu (The Great Controversy), uk. 354 – Yerusalemu Mpya na Bibi-arusi.

________ ________
Pambano Kuu, uk. 556 – *Utukufu wa mbingu hauwezi kuelezwa kikamilifu.*

________ ________
The Faith I Live By, uk. 363 – *Waamini wajifunze kuzungumza na kutafakari kuhusu mbingu.*

________ ________
________ ________
Na
EV. K. KUBOJA
0763740320
0656340320

*BARIKIWA*

25/11/2025

```DIRA YA UINJILISTI```

Usinyamaze ikiwa Bwana Mungu ametoa agizo, amka na fanyia kazi

____🌹🌹____
*Uinjilisti ni moyo wa injili na kiini cha wito wa kanisa la Mungu.* Kanisa halipo kwa ajili ya kujihudumia lenyewe bali kwa ajili ya *“kuhubiri injili kwa kila kiumbe”* (Marko 16:15).

*_Katika teolojia ya Waadventista wa Sabato, uinjilisti ni ushiriki wa mwanadamu katika kazi ya Kristo ya kuokoa wanadamu, kwa nguvu ya Roho Mtakatifu._*

____🌹🌹____

```DIRA KUU```

*“Kanisa la Mungu lipo duniani kwa kusudi moja kuu, kueneza nuru ya ukweli wa wokovu kwa ulimwengu mzima.”*
— Testimonies for the Church, Vol. 6, uk. 11.

Dira hii inatokana na agizo la Kristo:
*“Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza...”*
— Mathayo 28:19–20.

Kanisa k**a chombo cha uinjilisti:
*Kila muumini ni sehemu ya mwili wa Kristo na ameitwa kushiriki katika huduma ya injili*
(1 Wakorintho 12:27; Warumi 10:14–15).

____🌹🌹____

```MISINGI YA KIMAANDIKO YA UINJILISTI```

🌹🌹
Mathayo 28:18–20
Agizo Kuu la Kristo ambalo ni wito wa uinjilisti kwa wote.

🌹🌹
Marko 1:17
Yesu aliwaita wafuasi wake wawe *“wavuvi wa watu.”*

🌹🌹
Matendo 1:8
*Uwepo wa Roho Mtakatifu ni nguvu ya Uinjilisti.*

🌹🌹
2 Timotheo 4:2
Hubiri Neno kwa wakati ufaao na usiofaa.

🌹🌹
Ufunuo 14:6–12
*Ujumbe wa malaika watatu, ndiyo msingi wa uinjilisti wa Waadventista wa Sabato.*

____🌹🌹____

Ufafanuzi wa Biblia:

*Uinjilisti wa kweli ni matokeo ya kuishi kwa injili. Biblia inaonyesha kuwa wale waliokutana na Kristo walihubiri mara moja (Yohana 4:28–30). Uinjilisti sio tukio, ni mtindo wa maisha ya Mkristo.*

____🌹🌹____

*“Kila Mwana wa Mungu amewekwa wakfu kwa kazi ya uinjilisti. Yeye ambaye amepokea nuru anatakiwa kuifanya ing’ae kwa wengine.”*
— The Desire of Ages, uk. 822.

*“Kanisa limepewa kazi ya kuupeleka ulimwenguni ujumbe wa malaika watatu... Hii ndiyo kazi ya mwisho, kubwa, ya rehema.”*
— Evangelism, uk. 119.

*“Uinjilisti wa kweli unahusisha huduma ya mtu kwa mtu, moyo kwa moyo.”*
— Ministry of Healing, uk. 143.

*“Kama kanisa lingetenda kazi ambayo Mungu ameliamuru, ulimwengu wote ungepata onyo kwa siku chache, na Bwana Yesu angekuja haraka.”*
— Christian Service, uk. 111.

____🌹🌹____

*“Huduma ya uinjilisti ni wajibu wa kila mshiriki wa kanisa. Wote wameitwa kutoa ushuhuda wa imani yao katika Kristo, kwa maneno na matendo.”*
(Church Manual, 21st Edition, Kifungu cha 8, “Evangelism and Witnessing.”)

Kanisa linapendekeza aina za uinjilisti:
- Uinjilisti wa nyumbani na ujirani.
- Uinjilisti wa vikundi vidogo (small groups).
- Uinjilisti wa vijana, wanawake, na shule ya Sabato.
- Uinjilisti wa redio, televisheni, na mitandao ya kijamii.
- Uinjilisti wa wagonjwa (Medical Missionary Work).

*“Kazi ya Mungu duniani haitamalizika mpaka wanaume na wanawake wa kawaida, wanaojazwa na Roho Mtakatifu, wafanye kazi ya kuhubiri injili nyumbani na majirani.”*
Acts of the Apostles, uk. 111

____🌹🌹____

Mathayo 28:19–20
*“Amri hii ni ya wote wanaomwamini Kristo. Wale waliopokea wokovu hawapaswi kuutunza wao peke yao. Wameitwa kushirikisha wengine. Hivyo kanisa linakuwa ‘taifa takatifu’ linaloitwa kutoka gizani kwenda katika nuru ya ajabu.”*
— Seventh Day Adventist Bible Commentary, Vol. 5, uk. 641.

Ufunuo 14:6–12
*“Malaika watatu wanaashiria watu wa Mungu wanaotoa ujumbe wa onyo wa mwisho kwa ulimwengu kabla ya kurudi kwa Kristo. Ni uinjilisti wa dunia nzima unaolenga kumrudisha mwanadamu katika ibada ya kweli kwa Muumba.”*
— Seventh Day Adventist Bible Commentary, Vol. 7, uk. 823.

____🌹🌹____

```HUDUMA ZA KANISA```

🌹🌹
(a) Kwa Waumini Wote:

- *Kila mshiriki* aone uinjilisti k**a wajibu binafsi, si kazi ya wachungaji pekee.

- *Kila nyumba* iwe kituo cha nuru na ushuhuda (Mathayo 5:14–16).

🌹____🌹
(b) Kwa Viongozi wa Kanisa:

- *Waandae mpango wa Uinjilisti wa kudumu, si wa msimu.*

- *Wapewe mafunzo ya Uinjilisti wa vitendo kwa waumini.*

- Watumie Shule ya Sabato, kwaya, idara ya vijana, wanawake, na Watoto k**a vyombo vya uinjilisti.

🌹____🌹
(c) Kwa Vijana:

- Watumie vipaji vyao (muziki, michezo, mitandao ya kijamii) kufikisha injili.

- Wajifunze kuwa *“mishenari wa kisasa”* kwa kutumia teknolojia.

____🌹🌹____
Wito:
- Leo Kristo anaita kila Mwumini kuwa shahidi Wake.

*“Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache.”*
— Mathayo 9:37.

*Tuamke, tushike kazi, tuhubiri injili ya milele!*

____🌹🌹____
____🌹🌹____

Na
EV. K KUBOJA
0763740320
0656340320

*TUWE NA TAFAKARI NJEMA NA SIKU NJEMA WOTE*

Address

Kiseke
Mwanza

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kiseke SDA Church posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share