EAGT Nyakato - Canaan Gospel Center

EAGT Nyakato - Canaan Gospel Center GOSPEL CENTER

16/08/2026

KARIBU KATIKA IBADA YA WAMAMA.

16/08/2026

KATIBU KATIKA IBADA YA WAMAMA.

16/08/2026

KARIBU KATIKA IBADA YA HITIMISHO LA WIKI LA WAMAMA

02/08/2026

KARIBU KATIKA IBADA YA SHUKRANI KWA KUTIMIZA MIAKA 42

22/07/2026

CGM Week 2026 Recap

Kipekee kabisa tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha kufanikisha wiki ya Vijana kwa mafanikio makubwa. Wiki hii ya baraka na yenye udhihirisho wa nguvu za Mungu ilianza tarehe 15/07/2026 na kuhitimishwa siku ya Jumapili, tarehe 19/07/2026.

Hakika tumemwona Mungu akitenda makuu katikati yetu, akituongoza, akitulinda, na kutubariki katika kila hatua ya maandalizi na utekelezaji wa shughuli zote. Kwa yote aliyotutendea, sifa, heshima na utukufu vimrudie Mungu milele. Amina.

Ujumbe wa Wiki ya Vijana mwaka huu
ulitokana na Neno la Mungu lililopatikana katika kitabu cha

Isaya 60:1
Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja,
Na utukufu wa BWANA umekuzukia.
Arise, shine; for thy light is come, and the glory of the LORD is risen upon thee.

Ni muda wako wa kuondoka na kuangaza kwa kuwa majira yako yametimia.

01/06/2026

Tunamshukuru Mungu kwa ajili ya matendo yake makuu aliyoyatenda katika wiki hili la kwaya na kwenye wiki hili tulikuwa na semina kuanzia jumatano na jumapili ilikuwa ni hitimisho ya semina.

Mnenaji wa semina alikuwa ni mchungaji Shadrack Reuben kutoka kanisa la Mito Ya Baraka(Kishiri)......

Tumejifunza katika siku zote za semina(Jumatano,Ijumaa,Jumapili) somo kuhusu Nguvu ya Mungu Katika Uimbaji na andiko kuu la semina limetoka kitabu cha

Yohana 4:24

Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.

Ahsante sana kwa kuhudhuria semina hii na Mungu akubariki.

Nikukaribishe kwenye ibada ya kesho Jumapili 03/5/2026, Itakuwa ibada ya SIFA, MAABUDU NA SHUKRANI kwa Mungu wetu.Itaanz...
02/05/2026

Nikukaribishe kwenye ibada ya kesho Jumapili 03/5/2026, Itakuwa ibada ya SIFA, MAABUDU NA SHUKRANI kwa Mungu wetu.

Itaanza saa 3:00 asubuhi mpaka saa 7:30 mchana,
Kanisa lipo Nyakato, National jirani na shule ya msingi Mzigu (Almaarufu k**a kanisa la vioo)

Watu wote mnakaribishwa sana, tutafurahi kukuona.

Address

Mahango, Mhandu
Mwanza
33125

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when EAGT Nyakato - Canaan Gospel Center posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to EAGT Nyakato - Canaan Gospel Center:

Shortcuts

Share