22/08/2026
*_Sura za wiki hii kwa kifupi:_*
*Jumatatu:* Zaburi 54,63
Tafakari ya Daudi wakati anafuatiwa na Sauli na Wazifi wakamsaliti (1Sam 23 na 26) anaomba na kutambua msaada wa Mungu (Zab 53) na anamshukuru akiwa jangwani kwani hata hapo Mungu amemsadia (Zab 63)
*Jumanne:* 1Sam 29-31
Sura 29: Daudi anakataliwa kwenda vitani na wafilisti kupigana na Israeli wakihofia kusalitiwa
Sura 30: Baada ya kukataliwa, Daudi alirudi katika mji alikuwa amepewa na wafilisti kuishi (Siklagi) na kukuta mji umerejea na waamaleki, Daudi analaumiwa hata na watu wake. Lakini anajitia nguvu na kwenda kupambana na Mungu anampa ushindi
Sura 30: Sauli na wanawe wanauawa vitani
*Jumatano:* Zaburi 18
Daudi anatunga Zaburi ya shukrani kwa Mungu kwa ushindi mkuu.
*Alhamisi* Zaburi 121
Anaendelea kumshukuru Mungu kwa kumlinda na kumsaidia. Mungu ni mlinzi na msaada wa watu wake
*Ijumaa:* Zaburi 6,8-9
Sura 6: Daudi anamlilia Mungu kuomba msaada na Rehema, na hapa ni pengine alikuwa amekosea, na kuomba Mungu asimhukumu kwa hasira.
Sura 8: Anatangaza ukuu wa Mungu, muumba wa vyote, aliyekaa utukufu na kutaja nafasi ambayo Mungu amempa mwanadamu.
Sura 9: Anaendelea kumshukuru Mungu, namna alivyompigania dhidi ya adui zake, na anamsifu Mungu Kwa namna anavyotetea wanyonge na kukumbuka watu wake.
*Jumamosi:* Zaburi 10, 14
Sura 10: Katika kuendelea kumshukuru Kwa namna alivyomtetea, anataja pia watu wenye kiburi, wanavyoonea wanyonge, wakidhani kwamba wao ndio Kila kitu, wanavyomkashifu Mungu, Daudi anamwomba watu wa aina hiyo asiwaache waendelee kuonea walio chini. Akikumbuka Hali yake ilivyokiwa mbele ya Sauli.
Sura 14: Anaanza kuongelea namna wenye kiburi wanavyo mkataa Mungu na kuendelea kuonesha kuwa Mungu ni mtetezi na anahitimisha kwa kuomba wokovu wa Bwana
*Jumapili:* 19,21
Sura 19: anaendelea kuuelezea ukuu wa Mungu na namna viumbe vyote vinavuoutangaza, na anaelezea mamlaka ya Neno la Mungu na anamalizia kwa maombi ya unyenyekevu na Toba
Sura 21: Anaendelea kumshukuru Mungu kwa ushindi na kujibu haja ya moyo wake.