ELCT - ELVD

ELCT - ELVD East of Lake Victoria Diocese (ELVD) is part of the Lutheran Church in Tanzania (ELCT).

Contacts:
Bishop Andrew Petro Gulle: [email protected]
General Secretary Rogath Lewis Mollel: [email protected]
Assistant Bishop Oscar Lema: oscarlema11yahoo.com

*WANAFUNZI ZAIDI YA 2,000 WAFANYA MTIHANI WAO WA KUHITIMU MASOMO YA KIPAIMARA KKKT-DMZV (Mwanza)*Zaidi ya Wanafunzi 2,00...
06/09/2026

*WANAFUNZI ZAIDI YA 2,000 WAFANYA MTIHANI WAO WA KUHITIMU MASOMO YA KIPAIMARA KKKT-DMZV (Mwanza)*

Zaidi ya Wanafunzi 2,000 wamefanya Mtihani wao wa kuhitimu Elimu ya Kipaimara tarehe 05 Septemba, 2026 kupitia vituo 108.

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) hutoa Elimu hii ya Imani kwa Watoto/Vijana ili kuimarisha ufahamu wao juu ya Imani yao katika Kristo kwa miaka miwili.

KKKT - DMZV Kitengo cha Elimu ya Kikristo kilichopo chini ya Idara ya Uinjilisti, Misioni na Uwakili usimamia Utoaji wa Elimu ya Kipaimara kupitia Wachungaji, Wainjilisti na Wasaidizi wa Sharika.

Idara ya Uinjilisti, Misioni na Uwakili kupitia Kitengo cha Elimu ya Kikristo inawashukuru Wasimamizi wote 114 (Wachungaji na Wainjilisti) chini ya Wakuu wa Majimbo kwa usimamizi wao mzuri wa Mtihani huo uliofanyika.

Katibu Mkuu wa KKKT DMZV Bw. Joshua Kyelekule, akiwa na Mkuu wa Idara ya Mipango na Uwekezaji Bi. Joygrace Shoo na Mrati...
05/09/2026

Katibu Mkuu wa KKKT DMZV Bw. Joshua Kyelekule, akiwa na Mkuu wa Idara ya Mipango na Uwekezaji Bi. Joygrace Shoo na Mratibu wa EK Mchg. Malte Lei leo tarehe 05/09/2026 wameshiriki ibada ya kuweka vifaa vya uaskofu wakfu kwa ajili ya ibada ya kuwekwa wakfu Askofu Mteule Prince Kalisa wa Kanisa la Kilutheri Rwanda iliyofanyika St. Augustine Cathedaral Kigali Rwanda.

Leo tarehe 05/09/2026 Kamati (Bodi) ya Kituo cha Afya Nyakato kimefanya kikao chake cha Kikatiba. Kikao hiki kimepitia t...
05/09/2026

Leo tarehe 05/09/2026 Kamati (Bodi) ya Kituo cha Afya Nyakato kimefanya kikao chake cha Kikatiba. Kikao hiki kimepitia taarifa ya Utekelezaji ya miaka minne (2022-2025) na kupitisha Mpango Kazi wa miaka minne (2026-2029). Kikao kimefanyika katika ukumbi wa Charming Bungalows Hotel uliopo Nyakato Mwanza.

Mkuu wa Idara ya Jinsia na Maendeleo ya Jamii Mchg.Peweni Kikoti  leo tarehe 04.09.2026 amekutana na vijana 18 pamoja na...
04/09/2026

Mkuu wa Idara ya Jinsia na Maendeleo ya Jamii Mchg.Peweni Kikoti leo tarehe 04.09.2026 amekutana na vijana 18 pamoja na watoto 22 wa Usharika wa Nazareth Sumve kwa ajili ya semina ya Vijana.Katika semina hiyo somo lililofundishwa lilihusu CHANGAMOTO YA AFYA YA AKILI: Katika somo hilo mkazo ulikuwa:

Maana ya Afya ya Akili. Ni hali ya mtu kuwa na uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi sahihi na yanayostahili katika maisha. Au ni hali ya ustawi inayomwezesha mtu kwendana na hali ya maisha.Au ni hali ya ustawi kihisia,kisaikolojia na kijamii ambayo inaathiri utambuzi, mtazamo na tabia.Au ni hali ya ustawi ambapo mtu anatambua uwezo wake na anaweza kukabiliana na msongo katika maisha na anaweza kufanya kazi zenye tija na kwa ufanisi.

Maana ya Changamoto ya Afya ya Akili.
Ni hali inayovuruga ustawi wa kifikra,kihisia na kijamii wa mtu na kuathiri anavyofikiri, anavyohisi, anavyotenda na kukabiliana na maisha ya kila siku.
# Hali hii inajumuisha mabadiliko au matatizo yanayoathiri uwezo wa ubongo kudhibiti hisia, tabia na mahusiano kutokana na msongo wa mawazo (Stress) uliopitiliza,wasiwasi (anxiety) au hofu isiyo ya kawaida, pamoja na sonona ( depression).

Afya ya Akili kuingia changamoto inaanzia katika familia kwa kuwa ni msingi wa malezi bora na makuzi ya mtu mwenye utimamu katika kufikiri/kuwaza na kutenda.
Hivyo familia ina mchango katika kumfanya mtu awe na utimamu au la katika kufikiri/kuwaza na kutenda.

Semina itaendelea kwa tarehe 05.09.2026 na 06.09.2026.

Mkuu wa Idara ya Jinsia na Maendeleo ya Jamii Mchg. Peweni Kikoti ameongoza   Ibada ya Siku ya Bwana ya 13 baada ya Utat...
31/08/2026

Mkuu wa Idara ya Jinsia na Maendeleo ya Jamii Mchg. Peweni Kikoti ameongoza Ibada ya Siku ya Bwana ya 13 baada ya Utatu kwa ajili ya kuhitimisha Semina ya Wanawake wa Usharika wa Mazoezi Galilaya Nsumba iliyofanyika kwa siku 8 kuanzia tarehe 23.08.2026 hadi tarehe 30.08.2026 ikiwa ni hitimisho la maadhimisho ya Ibada ya Mwezi Agosti ambayo hufanyika kila mwaka kidayosisi (DMZV) kwa ajili kukumbuka Kuanzishwa kwa Kitengo cha Wanawake na Watoto - Dorcas.

Katika Ibada hiyo Mchg.Peweni Kikoti amewakumbusha wakristo kuishi maisha ya Unyenyekevu katika familia, Kanisa na Jamii ili Mungu aweze kuachilia baraka zake.

Aliendelea kusema kuwa mtu hawezi kuwa mnyenyekevu ikiwa anaishi na uchungu au maumivu moyoni mwake dawa pekee katika kuondoa uchungu moyoni ni kusamehe. Wakristo wanatakiwa kuitafuta furaha,amani na Upendo ili kudumisha umoja na mshikamano na kuepuka migogoro.
Aidha wazazi wanawajibu wa kuishi kwa mfano ili watoto wao wajifunze mema kutoka kwao.

Msaidizi wa Askofu Stephen L. John wa KKKT-DMZV leo tarehe 23/08/2026  amefungua mtaa wa Upendo Jojiro katika Jimbo la K...
23/08/2026

Msaidizi wa Askofu Stephen L. John wa KKKT-DMZV leo tarehe 23/08/2026 amefungua mtaa wa Upendo Jojiro katika Jimbo la Kaskazini Ngudu na kubatiza watu wazima 3, watoto 5 na kumpokea mkristo mtu mzima 1 toka dhehebu lingine.

Msaidizi wa Askofu Stephen Ling'hwa John wa KKKT-Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria tarehe 22 Agosti, 2026 ameshiriki k...
22/08/2026

Msaidizi wa Askofu Stephen Ling'hwa John wa KKKT-Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria tarehe 22 Agosti, 2026 ameshiriki kwa kutembelea Jumuiya ya Busulwe Mtaa wa Kiminza Usharika wa Malya.

Jumuiya hii wanahitaji la kununua kiwanja cha Kanisa.

Kwa yoyote atakaye guswa kushiriki sadaka yake anakaribishwa na Mungu ambariki, Akaunti Namba ni 0150355088301 CRDB ELCT ELVD GENERAL ADMIN.

Pia alipata kutembelea kiwanja cha Kanisa cha Jojiro ambacho wameanza kazi ya kufyatua tofari.

22/08/2026

Taarifa ya habari, iliyoonyesha uzinduzi wa mradi wa Maji Geita.

MRATIBU WA KITENGO CHA ELIMU YA KIKRISTO MCHG. MALTE LEI NA MWINJ. WILLIAM  MSOKWA WALIORATIBU  MAFUNZO YA UFUNDISHAJI E...
19/08/2026

MRATIBU WA KITENGO CHA ELIMU YA KIKRISTO MCHG. MALTE LEI NA MWINJ. WILLIAM MSOKWA WALIORATIBU MAFUNZO YA UFUNDISHAJI ELIMU YA KIKRISTO MASHULENI WAKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA WAINJILISTI KATIKA JIMBO LA MAGHARIBI NA MAGHARIBI KATI YALIYOFANYIKA KWA SIKU 3 TANGIA TAREHE 17- 19/08/2026 - USHARIKA WA MARTIN LUTHER NYANKUMBU- GEITA.

MSAIDIZI WA ASKOFU STEPHEN LING'HWA JOHN AZINDUA MRADI WA MAJI GEITAMsaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi Mashariki ya Ziw...
17/08/2026

MSAIDIZI WA ASKOFU STEPHEN LING'HWA JOHN AZINDUA MRADI WA MAJI GEITA

Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria Dean Stephen Ling'hwa John amezindua Mradi wa maji katika kijiji cha Nampalahala wilayani Bukombe mkoani Geita.

Akizindua mradi huo uliofadhiliwa na Kanisa la KKKT DMZV kwa ushirikiano na Shirika la Patnership Afrika la Nchini Ujerumani Msaidizi wa Askofu amesema uwepo wa mradi huo uwe chanzo cha kubadilisha uchumi wa watu wa eneo hilo na kulisaidia kanisa na iwe shamba darasa kwa wengine kujifunza zaidi.

Kwa upande wake Katibu wa DMZV Joshua Kyelekule amesema huu ni moja kati ya miradi mingi inayofanywa na Kanisa na lengo lao ni kushirikiana na Serikali kuendelea kutoa huduma kwa jamii katika maeneo mbalimbali huku akiiomba serikakali iwaunge mkono katika jitihada hizo.

Naye Mkuu wa Idara ya Huduma za Jamii kutoka DMZV Exaud Solomon amesema bado wanahitaji kuwa miradi mingi zaidi katika eneo hilo na maeneo mengine ili waweze kuisaidia jamii, kupunguza ukame na kutunza mazingira.

Nao wakazi wa eneo hilo wakiwemo washarika wa kanisa la KKKT mtaa wa nampalahala wamelishukuru kanisa kwa kuwapa mradi huo kwani utawakwamua kiichumi kwa kufanya kilimo ,ufugaji na shughuli nyingine za kibiashara huku wakiwataka wananchi kuwa walinzi wa miradi hiyo ili isiharibike.

Uzinduzi wa mradi huo umefanyika jumapili ya Agost 16 ukitanguliwa na ibada ambapo katika ibada hiyo wajumbe 7 walioteuliwa kusimamia mradi wa Maji waliingizwa kazini ili kuianza kazi yao.

Address

P. O. Box 423
Mwanza

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ELCT - ELVD posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to ELCT - ELVD:

Shortcuts

Share