Tumaini LETU

Tumaini LETU Kutangaza neno la MUNGU

10/03/2021

K**a Wanadamu tumeitwa na Mwokozi kwa ajili ya kuwaita watu wa BWANA. Barikiwa .

15/01/2021
07/08/2020

Ujumbe makini

25/06/2020

*TAARIFA KUHUSU MSIBA WA MWL SAMSON KIBASO*

1. Ibada ya kuaga mwili itafanyika siku ya Jumapili tarehe 28 Juni, saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni katika viwanja vya kanisa la waadventista wa Sabato Kurasini, Nyuma ya viwanja vya sabasaba maonyesho-DSM

2.Mwili utasafirishwa kwenda Musoma kwa mazishi siku ya Jumapili saa 10:00 jioni na mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne tarehe 30 Junvi.

3. Huduma za faraja kwa wafiwa zitaendelea nyumbani kwa Mwl Kibaso, maeneo ya Yombo Dovya hadi Jumaamosi tarehe 27 Juni, sambamba na hilo program za uimbaji kwa Kwaya na vikundi mbali mbali zitaendelea pia katika viwanja vya kanisa la Waadventista wa Sabato Kurasini Kila siku saa 8:00 mchana hadi saa 2:00 usiku na kutokea hapo Kwaya na vikundi vitapangwa kwa zamu kutoa huduma ya uimbaji Msibani.

Pr Keshi Malehiwa
Kurasini

USIJARIBU KUKOSA WIMBO HUU UTAKUBARIKI SANAusisahau ku subscribe
30/05/2020

USIJARIBU KUKOSA WIMBO HUU UTAKUBARIKI SANA
usisahau ku subscribe

Tazama wimbo kuhusu rehema ya mungu ilivyo ya ajbu

Kwa mafundisho ya kidini na nyimbo mbalimbali usikose kufuatilia kupitia youtube official account ya NelchannelNi hivi k...
15/05/2020

Kwa mafundisho ya kidini na nyimbo mbalimbali usikose kufuatilia kupitia youtube official account ya Nelchannel
Ni hivi karibuni!!!!!!!!
Usikoseeee

27/04/2020

Sasa mnaweza kufuatilia vipindi mbalimbali kupitia youtube .
Hivi karibuni.
Usikose!!!!!

14/04/2020

12 basi, tazama, nimefanya k**a ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu k**a wewe, wala baada yako hatainuka mtu k**a wewe.
1 Wafalme 3:12

21/03/2020

*KESHA LA ASUBUHI.*

Jumamosi, Machi 21,2020.

*NITAKUWA MKRISTO NYUMBANI.*

📖 *[Upendo] haukosi kuwa na adabu hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya.1 Wakorintho 13 : 5.*

✍️ *Mengi yanaweza kupatikana kwa kuishi kwa nidhamu nyumbani.... Hebu kila mmoja ayafanye maisha kuwa ya furaha kwa mwenzake kwa kadiri inavyowezekana. Kuwepo adabu katika maongezi. Dumisha umoja na upendo. Shetani hatakuwa na nguvu juu wale wanaojitawala kikamilifu nyumbani*

✍️ *Inatupasa kuwa na Roho wa Mungu, vinginevyo hatutakuwa na mwafaka nyumbani.... Inatupasa kujali sana upendo nyumbani, kwa kuwa nyumbani, ikiwa Roho wa Bwana yupo hapo, panakuwa mbingu ndogo.... Kitu chochote kinachoelekea kuharibu amani na umoja wa familia kisiendekezwe kamwe. Uungwana na upendo, roho ya kujali na uvumilivu, idumishwe. Pale mtu mmoja anapokosea, mwingine aoneshe uvumilivu wa Kikristo.*

✍️ *Yeyote anayeonesha roho ya upole, uvumilivu, na upendo atagundua kuwa roho ile ile itaoneshwa kwake.... Ikiwa Kristo ameumbika ndani, tumaini la utukufu, kunakuwa na umoja na upendo nyumbani. Kristo aliyeko ndani ya moyo wa mke anapatana na Kristo aliyeko ndani ya mume. Watakuwa wakijiandaa pamoja kuishi katika majumba ambayo Kristo alikwenda kuwaandalia wampendao.... Inapasa upendo wa kirafiki udumishwe daima kati ya mume na mke, wazazi na watoto, kaka na dada.... Ni wajibu wa kila mmoja katika familia kuwa na furaha, kuongea vizuri.*

✍️ *Nyumba ambayo ina upendo ndani yake, ambapo upendo unaelezwa kwa maneno, kwa mwonekano, na matendo, ndipo mahali ambapo malaika hupenda kuonekana na kuangaza kwa miale ya nuru ya utukufu… Inapasa upendo uonekane katika mwonekano na tabia na isikike katika sauti. Kujitawala kwa kila mmoja wa wanafamilia kutaifanya familia kufanana sana na paradiso.*

*MUNGU AKUBARIKI UNAPOTAFAKARI NENO LAKE.*
🙏🙏
UWE NA SABATO NJEMA.

Address

Mahina
Mwanza

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tumaini LETU posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share