22/11/2023
Kingdom Church Planting ni Nini?
Sisi ni Misheni ya wapanzi wa makanisa tunaojitolea. Tunapanda makanisa ya madhehebu mbalimbali yaliyo na njaa ya kuokoa nafsi na kueneza Ukristo wa kibiblia. Tunasali kwenye makanisa yetu na tunapanda makanisa ya madhehebu yetu na ya wengine.
Hivyo tunahitaji watumishi wanaoweza kujitolea katika kutimiza Agizo Kuu, kuanzisha makanisa, vyuo vya Biblia na huduma mbalimbali pamoja nasi.
Tunahitaji wainjilisti watakaohubiri Injili na kukusanya makundi mapya ili kuunda makanisa ya nyumbani, chini ya mti au mahali popote panapofaa kukutanika kwa kundi jipya lisilo na hekalu. Pia tunahitaji wachungaji watakaochunga haya makundi mapya. Kwa kweli wachungaji wa makundi mapya wanahitajika sana; makundi mapya hupatikana lakini hayana wachungaji. Wamishenari ni watumishi maalumu tunaowahitaji kufanya kazi hizo zote ndani ya taifa letu na mataifa mengine, kwenda kuanzisha makanisa na vyuo vya Biblia na taasisi za huduma za kijamii.
Watumishi wote ni vema k**a watakuja kwetu kufanya kazi pamoja nasi wakiwa wametumwa na makanisa au madhehebu yao kwa maana mzigo mkubwa utabebwa na makanisa/madhehebu yaliyowatuma. K**a kanisa lako halitumi watumishi na haliko tayari kufanya hivyo, sisi tunaweza kukushauri cha kufanya ili utimize wito wako mkuu wa kueneza Injili na kupanda makanisa. Kila mtu atafanya kazi ya Mungu ndani ya mazingira yake (dhehebu) au mazingira atakayoyapenda mwenyewe.
Pia ili kufanya watumishi wawe hodari katika Bwana, tunatoa semina na mafunzo ya Biblia kuhusu Uinjilisti, Kuanzisha Idara ya Uinjilisti/Utume (ngazi ya dhehebu), Upandaji wa Makanisa na Uchungaji wa Makanisa mapya. Hii inawafaa watumishi wote kutoka madhehebu yote yenye njaa ya kutimiza Agizo Kuu wakiwemo wainjilisti na viongozi wa makanisa na madhehebu, na pia watumishi chipukizi.
K**a unaweza kujitolea kumtumikia Mungu pamoja nasi karibu sana.
WhatsApp Namba 0756 008 855,
SMS/Piga namba 0788008855,
Laini Kuu namba 0694334556