Mkolani SDA central church

Mkolani SDA central church Bwana ni mwema watu wa baba
ukurasa huu umeundwa mahususi kutangaza jina la yesu kristo na kufanya watu wamjue Mungu tunae mwabudu kuwa ndio mweza wa yote.

Hivyo basi salimisha maisha yako kwa yesu hakika utalisi ufalme wa mbinguni.

DADA ANGU KABLA HUJAANZISHA MAHUSIANO NA MWANAUME HUU NDIO MGAWANYO WA WANAUME KURINGANA UMRI WAOLIONAO NA HULKA WALIZON...
10/09/2024

DADA ANGU KABLA HUJAANZISHA MAHUSIANO NA MWANAUME HUU NDIO MGAWANYO WA WANAUME KURINGANA UMRI WAOLIONAO NA HULKA WALIZONAZO

1. WANAUME wenye miaka 20-27 wengi hawako serious na ndoa au mahusiano yenye kesho labda wale wa vijijini. Kijijini vijana wengi huoa kwasababu k**a waongeze nguvu kazi ya familia, mahari mara nyingi zinatoka kwa wazazi sio zao (hawajazitesekea) lakini wanaume waliko mjini kwa 20-27 wengi ni wanafunzi na wanakimbizana na ndoto zao huwa si rahisi kuingia kwenye ndoa. Kwahiyo, ukianzisha naye mahusiano ni vigumu sana kukuoa kwasababu ana kiu na hofu ya MAISHA

Wanaume walioko kijijini mara nyingi hawayatazami maisha nje ya kulima na kuvuna zaidi wao wanatafuta kwa ajili ya muda uliopo si kwa ajili ya hatma zao njema. Kwahiyo dada angu mwanaume akiwa chini ya miaka 28 akiwa mjini ukianzisha mahusiano ni vigumu kuwaza ndoa kwake kwasababu anaona bado

2. WANAUME WA UMRI WA MIAKA 28-31 wengi huwa wameshapevuka na wameanza focus ya maisha anaweza akawa hana mafanikio ila angalau au ameshaona cha kufanya na utoto huwa umepungua zaidi labda awe hana dira yaani awe bado mgalatia au ameamua kuishi maisha ya KIGALATIA tu

Wengi wa 28-31 huwa si wanafunzi tena wamemaliza masomo wanajitafuta mtaani, wamepata pakushika, wanajimudu kwenye mambo yao muhimu na wanawaza kuanzisha mahusiano ya kudumu ili wasogee mbele. Wengi huwa hawajajipata sana ila huhitaji mahusiano yenye focus. Hawa watu huonekana wakorofi sana kwasababu wana uchungu na mafanikio hasa kwa mwanamke anayetaka bata au maisha ya anasa zaidi

3. WANAUME wa umri wa 32-38 wengi ni wanaume waliopitia mengi kupoteza, kuumizwa na kuumiza pia. Hawa huwa na mambo mawili kumpata mwanamke wa rika lake au linaondena na lake hawapendi vidada kwasababu wengi huwa wameumizwa sana na wadada wadangaji. Hawa wao nitafuta mwanamke aliyemaliza ujana k**a yeye na anayejielewa na aleyevuka hatua za UGALATIA.

4. WANAUME wenye miaka 40 na kuendelea hawa wao hutafuta mwanamke anayeweza kumheshimisha kuwa ana ndoa au familia baada ya kupigiwa kelele kwa nini haoi, kuchezea ujana sana, watoto aliozaa nje akitaka apate mtu wa kuwalea awakusanye.

Hapa kuna makundi mengi k**a ifuatavyo

A. Waliochelewa kuoa kwasababu ya utafutaji usiokoma au kusoma sana mpaka muda wa kuwa na familia ukataka kuwapa kisogo watu hawa wengi huwa wana changamoto zao kwasababu hawana uzoefu wa mahusiano wao hutaka mahusiano ya haraka sana na kuoana na kuzaa haraka kukimbiza na umri. Mwanamke akichelewa kumzalia huhaha sana na anaweza kuzaa nje ni mhitaji wa mtoto sana

B. Kundi jingine ni wale wanaokimbia ndoa zao baada ya kuvumilia sana wakaiachilua ili waoe waishi kwa amani baada ya kunyanyasika sana kwenye ndoa au mahusiano hayo ya awali huwa walishakiwa kwenye ndoa wakazikimbia

C. Kundi jingine ni wale wanaotaka kuongeza wake kwa matakwa yao baada ya kuona wamejipata kwenye maisha ya kuona wanahitaji kwasababu wamepata uzoefu wa ndoa nk. Kwahiyo huanzisha mahusiano na ndoa ya pili au zaidi kuringana na uhitaji wao

D. Kundi jingine ni wale waliofeli maisha wanatafuta kuelelewa wanatelekeza ndoa au mahusiano yao ya awali ili wakuelewe.

E. Wagane hili ni kundi linalohitaji mwanamke kwa ajili ya kumalizia uzee wao na kuondoa upweke yaani mwanaume akielekea uzeeni uhitaji wa mke unakuwa mkubwa sana ndio maana anaweza akaoa uzeeni ili apate faraja

WANAUME wa umri huu hutafuta single mother, vibinti vidogo wanavyoweza kuvilea muhimu viwazalie watoto hasa ambao wanatoka kwenye familia duni au wanawake wanaohitaji ndoa ambao hawachaguo mume

DADA ANGU HAYA NI MACHACHE USIYOYAJUA KWENYE UMRI WA WANAUME
By DaviiE

17/11/2022
 #Amen!ᎻᎪᏢᏢᎽ ᏢᎡᎬᏢᎪᎡᎪͲᏆϴΝ ᎠᎪᎽ!ᎬᏙᎬᎡᎽϴΝᎬ'Տ 🌎🙋🙏!
04/11/2022

#Amen!
ᎻᎪᏢᏢᎽ ᏢᎡᎬᏢᎪᎡᎪͲᏆϴΝ ᎠᎪᎽ!
ᎬᏙᎬᎡᎽϴΝᎬ'Տ 🌎🙋🙏!

04/11/2022

*KESHA LA ASUBUHI.*

Ijumaa, 04/11/2022.

*IBADA YA FAMILIA YA KILA SIKU HULETA MATOKEO YA THAMANI.*

*Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiliza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimilizia agano na rehema aliyowaapia baba zako. Kumbukumbu la Torati 7:12.*

▶️ Kwa sababu fulani baadhi ya wazazi hawapendi kuwapa watoto wao mafundisho ya kidini, na wanawaacha waokote katika shule ya Sabato maarifa ambayo ni haki na wajibu wao kuwapa. Wazazi k**a hao hushindwa kutimiza wajibu uliowekwa juu yao, ya kuwapa watoto wao elimu iliyo kamili. Mungu anawaagiza watu wake kuwalea watoto wao katika malezi na maonyo ya Bwana....

▶️ Wazazi, hebu mafundisho mnayowapa watoto wenu yawe rahisi, na mhakikishe kuwa yanaeleweka wazi. Masomo ambayo mnajifunza kutoka katika Neno mnapaswa kuyawasilisha kwa akili zao changa kwa uwazi kwamba hawawezi kushindwa kuyaelewa. Kwa masomo sahili kutoka katika Neno la Mungu na uzoefu wao wenyewe, mnaweza kuwafundisha jinsi ya kuyatiisha maisha yao katika kiwango cha juu kabisa. Hata katika utoto na ujana wanaweza kujifunza kuishi maisha ya uangalifu, yenye bidii ambayo yatatoa mavuno tele ya wema.

▶️ Katika kila nyumba ya Mkristo Mungu anapaswa kuheshimiwa kwa dhabihu za asubuhi na jioni za sala na sifa. Watoto wanapaswa kufundishwa kuheshimu na kuwa na kicho katika saa ya maombi. Ni jukumu la wazazi wa Kikristo, asubuhi na jioni, kwa maombi ya dhati na imani ya kudumu, kutengeneza uzio kuwazunguka watoto wao.

▶️ Katika kanisa la nyumbani watoto wanapaswa kujifunza kuomba na kumtegemea Mungu. Wafundishe kukariri sheria ya Mungu. Kuhusu amri Waisraeli waliagizwa: "Uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo" (Kumbukumbu la Torati 6:7).

▶️ Njoo kwa unyenyekevu, na moyo uliojaa upole, na kwa hisia za majaribu na hatari zilizo mbele yako mwenyewe na mbele ya watoto wako; kwa imani uwafunge madhabahuni, na ukisihi kwa ajili yao utunzaji wa Bwana. Waelekeze watoto jinsi ya kutoa maneno yao sahili ya sala. Waambie kwamba Mungu anafurahi kuwa wao wapate kumwita.

✍️ *Je! Bwana wa mbingu atapita kaya k**a hizo bila kuacha baraka yoyote pale? La kwa kweli. Malaika wanaohudumu watawalinda watoto ambao kwa jinsi hiyo wamewekwa wakfu kwa Mungu. Wanasikia kutolewa kwa sifa na sala ya imani, nao huyapeleka maombi hayo kwake Yeye ambaye anahudumu katika patakatifu kwa ajili ya watu Wake, naye hutoa stahili Zake kwa niaba yao. - Counsels to Parents, Teachers, and Students, 109, 110.*

*MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA.*
🙏🙏🙏🙏

30/10/2022

*KESHA LA ASUBUHI.*

Jumapili, 30/10/2022.

*HEWA SAFI NA ASILIA INAKUZA AFYA YA AKILI NA MWILI.*

*Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe; mche BWANA ukajiepushe na uovu. Itakuwa afya mwilini pako, na mafuta mifupani mwako. Zaburi 3:7, 8.*

✍️ Akili iliyoridhika, roho iliyochangamka, ni afya katika mwili na nguvu kwa roho. Hakuna kitu kinachosababisha sana ugonjwa k**a mfadhaiko, majonzi, na huzuni. Mfadhaiko wa akili ni mbaya sana....

✍️ Hewa, upepo mwanana, ni neema ya thamani ya mbinguni ambayo wote wanaweza kuwa nayo, itakubariki kwa ushawishi wake wa kutia moyo ikiwa hutakataa kuingia kwake. Ikaribishe, ipende, na itathibitika kuwa dawa ya thamani ya neva. Hewa lazima iwe katika mzunguko wa kila wakati ili iwe safi. Umuhimu wa hewa safi, ni kufanya damu kuzunguka kwa afya katika mfumo wote. Huburudisha mwili na huwa na kawaida ya kuufanya kuwa na nguvu na afya njema, wakati huo huo mvuto wake unaonekana waziwazi akilini, na kutoa kiwango maridhawa na utulivu. Inasisimua hamu ya kula, na hufanya usagaji wa chakula kuwa mkamilifu zaidi, na huleta usingizi mtamu na maridadi.

✍️ Madhara yanayotokana na kuishi katika vyumba vilivyofungwa, visivyo na hewa ya kutosha ni haya: Mfumo unakuwa dhaifu na usio na afya, mzunguko wa damu unashuka, damu hutembea kwa uvivu katika mfumo wote kwa sababu haijasafishwa na kuhuishwa na hewa safi, yenye kutia nguvu ya mbinguni....

✍️ Je, unaamini kwamba mwisho wa mambo yote umekaribia, kwamba matukio ya historia ya dunia hii yanakaribia mwisho kwa haraka? Ikiwa ndivyo, onesha imani yako kwa matendo yako....

✍️ *"Imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake." Ni wachache walio na imani hiyo ya kweli itendayo kazi kwa upendo na kuitakasa nafsi. Lakini wote wanaohesabiwa kuwa wanastahili uzima wa milele lazima wapate utimilifu wa kimaadili kwa huo. "Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona k**a alivyo. Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, k**a yeye alivyo mtakatifu." Hii ndiyo kazi iliyoko mbele yako, na huna muda mwingi kupita kiasi ikiwa unashiriki katika kazi hiyo kwa roho yako yote.-Testimonies for the Church 1:702-705.*

*MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA.*
🙏🙏🙏🙏

29/10/2022

KESHA LA ASUBUHI

JUMAMOSI, OKTOBA 29 2022

UWEZO WA KIMWILI NA KIAKILI UNAPASWA KUKUZWA

Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe. 1 Wakorintho 6:19.

📒 Afya ni hazina kubwa. Ni rasilimali adimu zaidi wanadamu wanayoweza kuwa nayo. Utajiri, heshima, au kujifunza hutafutwa kwa gharama, hata ikiwa ni kwa upotevu wa nguvu za afya. Hakuna hata moja ya mafanikio haya yanayoweza kuleta furaha ikiwa afya imepungukiwa. Ni dhambi mbaya sana kutumia vibaya afya ambayo Mungu ametupa. Kila matumizi mabaya ya afya hutudhoofisha maishani na hutufanya tuwe wapotezaji, hata k**a tutapata elimu ya namna gani....

📒 Umaskini, katika namna nyingi, ni baraka; kwani unazuia vijana na watoto kuharibiwa kwa kutojibidisha. Nguvu za kimwili na za kiakili zinapaswa kukuzwa na kuendelezwa ipasavyo. Utunzaji wa kwanza na wa kudumu wa wazazi unapaswa kuwa kwamba watoto wao wawe na maumbile thabiti, ili wawe wanaume na wanawake kamili. Haiwezekani kufikia mwonekano huu bila kufanya mazoezi ya mwili.

📒 Kwa ajili ya afya zao wenyewe za kimwili na maadili mema, watoto wanapaswa kufundishwa kufanya kazi, hata k**a hakuna uhitaji wa lazima. Ikiwa wangetaka kuwa na tabia safi na njema lazima wawe na nidhamu ya kazi iliyodhibitiwa vyema, ambayo itaifanya misuli yote kufanya kazi. Furaha ambayo watoto watakuwa nayo inayotokana na wao kuwa wenye manufaa, na katika kujikana nafsi ili kuwasaidia wengine, itakuwa ni furaha yenye afya zaidi ambayo wamewahi kuwa nayo....

📒 Kazi ya mikono haitazuia ukuzaji wa akili. La hasha. Faida zinazopatikana kwa kazi ya mikono zitamfanya mtu kuwa na uwiano mzuri na kuzuia akili kuchoshwa kwa kazi nyingi. Kufanya kazi kwa bidii kutaijia misuli na kutuliza ubongo uliochoka....

📒 Haihitaji kitu dhaifu, kisicho na msaada, kujionesha kwa mavazi, kujichekesha ovyo ili kuwa mwanamke. Mwili mzuri unahitajika kwa ajili ya akili nzuri. Utulivu wa kimwili na ujuzi wa vitendo wa kazi zote muhimu za kaya haziwezi kuwa vikwazo kwa akili iliyokuzwa vizuri; zote mbili ni muhimu sana kwa mwanamke.

📒 Nguvu zote za akili zinapaswa kutumiwa na kuendelezwa ili wanaume na wanawake wawe na akili zilizo na uwiano mzuri. Ulimwengu umejaa wanaume na wanawake wa upande mmoja ambao wamekuwa hivyo kwa sababu upande mmoja wa uwezo wao hukuzwa huku upande mwingine ukiwa umepungukiwa kwa kukosa utendaji....

🔘 Akili ya mwanadamu inahitaji kutumika. Ikiwa haifanyi kazi katika mwelekeo sahihi, itakuwa ikifanya kazi katika makosa. Na ili kuhifadhi uwiano wa akili, kazi na masomo vinapasa kuunganishwa mashuleni.-Testimonies for the Church 3:150-153.

MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA

27/10/2022

*KESHA LA ASUBUHI.*

Ijumaa, 28/10/2022.

*ANDAA LISHE BORA BILA MINOFU YA NYAMA.*

*Je! Hapana zeri katika Gileadi? Huko hakuna tabibu? Mbona, basi, haijarejea afya binti ya watu wangu? Yeremia 8:22.*

✍️ Wote wanajaribiwa na kuthibitishwa sasa. Tumebatizwa katika Kristo, na ikiwa tutatenda sehemu yetu kwa kujitenga na kila kitu ambacho kingetuvuta chini na kutufanya kuwa tusivyopaswa kuwa, tutapewa nguvu ya kukua ndani ya Kristo, ambaye ndiye kichwa chetu kilicho hai, nasi tutauona wokovu wa Mungu.

✍️ Ni pale tu tunapokuwa na weledi kuhusiana na kanuni za maisha yenye afya ndipo tunaweza kuamshwa kikamilifu ili tuweze kuona maovu yanayotokana na ulaji usiofaa. Wale ambao baada ya kuona makosa yao, wana ujasiri wa kubadili tabia zao, wataona kuwa mchakato wa matengenezo unahitaji mapambano na uvumilivu mwingi; lakini ladha sahihi zinapoundwa mara moja, watatambua kwamba matumizi ya chakula ambacho hapo awali walikiona kuwa hakina madhara yalikuwa yakiweka msingi wa kiungulia na magonjwa mengine polepole lakini kwa hakika.

✍️ Akina baba na akina mama, kesheni na kuomba. Jilindeni sana dhidi ya kutokuwa na kiasi kwa kila namna. Wafundisheni watoto wenu kanuni za kweli za matengenezo ya afya. Wafundisheni ni vitu gani waviepuke ili waweze kutunza afya. Tayari ghadhabu ya Mungu imeanza kupatilizwa kwa wana wa kuasi. Ni uhalifu gani, na dhambi za namna gani, na maovu ya namna gani, ambayo sasa yanafunuliwa kila upande! K**a watu tunapaswa kuwa waangalifu sana katika kuwalinda watoto wetu dhidi ya washirika waovu.

✍️ Juhudi kubwa zaidi zinapaswa kuwekwa ili kuelimisha watu katika kanuni za matengenezo ya afya. Shule za upishi zapasa kuanzishwa, na mafundisho ya nyumba kwa nyumba yanapasa kutolewa katika utaalam wa kupika chakula kizima. Wazee na vijana wanapaswa kujifunza jinsi ya kupika kwa urahisi zaidi. Popote ambapo ukweli unatolewa, watu wanapaswa kufundishwa jinsi ya kutayarisha chakula kwa njia sahili lakini yenye kuvutia. Wanapaswa kuoneshwa kwamba lishe bora inaweza kutolewa bila matumizi ya nyama ya wanyama....

✍️ *Busara na umakini mwingi vitumike katika kuandaa chakula chenye lishe ili kuchukua mahali pa kile ambacho hapo awali kilikuwa chakula cha wale wanaojifunza kuwa warekebishaji afya. Imani kwa Mungu, bidii ya kusudi, na nia ya kusaidiana itahitajika. Mlo usio na vipengele sahihi vya lishe huleta aibu juu ya sababu ya matengenezo ya afya. Sisi ni watu tunaofikwa na mauti, na lazima tujipatie chakula ambacho kitaupa mwili lishe ifaayo.-The Review and Herald, March 3, 1910.*

*MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA.*
🙏🙏🙏🙏

14/10/2022

CHANGAMOTO ZINAZOKUPATA PIA BABA YAKO WA MBIGUNI ANAJUA USIJALI WALA USIOGOPE YEYE YUPO POMOJA NAWE HADI MWISHO. zaburi 23:4

07/10/2022

Nawatakia Maandalizi Mema ya Sabato takatifu ya BWANA.

07/10/2022

*KESHA LA ASUBUHI.*

Ijumaa, 07/10/2022.

*AFYA NJEMA INAHITAJIKA ILI KUPATA MAFANIKIO.*

*Nami nitawatafuta waliopotea, nitawarudisha waliofukuzwa, nitawafunga waliovunjika, nitawatia nguvu wagonjwa; nao wanono na wenye nguvu nitawaharibu; nitawalisha hukumu. Ezekieli 34:16.*

✍️ Kwa kuwa akili na roho huonyeshwa kupitia mwili, nguvu za kiakili na kiroho zinategemea kwa kiwango kikubwa nguvu za kimwili na shughuli; chochote kinachokuza afya ya kimwili kinakuza maendeleo ya akili yenye nguvu na tabia yenye busara. Bila kuwa na afya nzuri hakuna mtu anaweza kuelewa kwa uwazi kabisa au kutimiza kikamilifu wajibu wake yeye mwenyewe, kwa watu wengine, au kwa Muumba. Hivyo basi afya inapaswa kulindwa kwa uaminifu k**a vile tabia inavyolindwa. Ujuzi wa fiziolojia na usafi unapaswa kuwa msingi wa juhudi zote za elimu.

✍️ Ingawa ukweli wa fiziolojia sasa unaeleweka kwa ujumla, kuna kutojali kwa kutisha kuhusiana na kanuni za afya. Hata kwa wale ambao wana ufahamu wa kanuni hizi, kuna wachache wanaozifanyia kazi. Mwelekeo au mhemko hufuatwa kwa upofu kana kwamba uhai ulitawaliwa na bahati tu badala ya sheria mahsusi na zisizobadilika.

✍️ Vijana, katika uzuri na wepesi wa maisha, wanatambua kidogo tu thamani ya nguvu zao nyingi. Hazina ya thamani kuliko dhahabu, muhimu zaidi kuliko kujifunza au cheo au utajiri zinachukuliwa kuwa za kawaida! Jinsi zinavyotumiwa vibaya! Ni wanaume na wanawake wangapi, huharibu afya zao katika kupigania utajiri au mamlaka, huanguka tu pasipo msaada, wanapokaribia kufikia lengo la shauku yao, huku wengine, wakiwa na ustahimilivu wa hali ya juu zaidi wa kimwili, wakishika tuzo iliyotamaniwa! Kupitia hali za ugonjwa, k**a matokeo ya kupuuza sheria za afya, ni wangapi wameongozwa katika mazoea maovu, hata kupoteza kila tumaini la ulimwengu huu na ujao!

✍️ Katika somo la fiziolojia, wanafunzi wanapaswa kuongozwa kuona thamani ya nguvu ya mwili na namna inavyoweza kuhifadhiwa na kuendelezwa kiasi cha kuchangia kwa kiwango cha juu kwenye mafanikio katika mapambano makubwa ya maisha.

✍️ *Watoto wanapaswa kufundishwa mapema, kwa urahisi, masomo rahisi, kanuni za fiziolojia na usafi.... Wanapaswa kuelewa umuhimu wa kujikinga na magonjwa kwa kuhifadhi nguvu za kila kiungo na pia wafundishwe jinsi ya kukabiliana na magonjwa na ajali za kawaida. Kila shule inapaswa kutoa maelekezo ya fiziolojia na usafi, na, kwa namna inayowezekana, kunapaswa kutolewa vifaa kwa ajili ya kuonesha kwa vitendo muundo, matumizi na utunzaji wa mwili.*

*MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA.*
🙏🙏🙏🙏

06/10/2022

*Wale wanaokwenda kuweka shida zao binafsi mbele ya wengine bora wangebaki nyumbani kusali, kusalimisha mapenzi yao potovu kwa Mungu, kuanguka juu ya Mwamba na kuvunjwa, kufa kwa nafsi zao ili Yesu apate kuwafanya vyombo vya heshima. Ukosefu wa adabu, dakika ya mzaha, neno moja gumu, lisilo la kufikiri, litaharibu sifa yako, na linaweza kufunga mlango wa mioyo usiweze kuifikia kamwe.*

Ellen G. White, The Adventist Home uk.38.
✍️✍️✍️✍️

30/09/2022

*KESHA LA ASUBUHI.*

Ijumaa, 30/09/2022.

*KILA MUUMINI ASAIDIE KUENEZA INJILI.*

*Basi Yesu akawaambia tena akasema, "Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima. Yohana 8:12.*

✍️ Wale wanaomfuata Yesu watakuwa watenda kazi pamoja na Mungu. Hawatatembea gizani, bali wataipata njia ya kweli ambapo Yesu, aliye nuru ya ulimwengu, huongoza njia; na wanapokunja hatua zao kuelekea Sayuni, wakisogea kwa imani, watapata uzoefu angavu katika mambo ya Mungu. Utume wa Kristo unaofahamika kidogo mno, unaeleweka kwa ufinyu mno, uliomwita kutoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu hadi kwenye fumbo la madhabahu ya msalaba wa Kalivari, utaifungua akili zaidi na zaidi, na itaonekana kuwa katika kafara ya Kristo hupatikana chemichemi na kanuni ya kila utume mwingine wa upendo. Ni upendo wa Kristo ambao umekuwa kichocheo cha kila mfanyakazi wa kweli wa Kimishenari katika miji, mijini, katika barabara kuu na njia za dunia.

✍️ Kanisa limepangwa duniani kwa kusudi la umishenari, na ni muhimu sana kuwa kila muumini binafsi wa kanisa awe mfanyakazi mwaminifu pamoja na Mungu, akijazwa na Roho, akiwa na fikra za Kristo, aliyekamilishwa katika huruma ya Yesu Kristo, na hivyo basi akitimia kila juhudi kulingana na uwezo wake aliopewa katika uokoaji wa roho. Kristo anataka kuwa kila mtu ambaye angependa kuitwa kwa jina Lake afanye kazi Yake kuwa ya kwanza na ya juu kabisa, na kushirikiana bila ubinafsi na wajumbe wa mbinguni katika kuwaokoa wale wanaoangamia ambao Kristo aliwafia.

✍️ *Kutumia vibaya nyenzo au mvuto au mtaji wowote wa akili au mwili ukiokabidhiwa ni kumwibia Mungu au kuuibia ulimwengu; kwa maana ni kuzigeuza nguvu kuwa njia nyingine zaidi ya ile ambayo Mungu alipanga kuwa zinapaswa kusonga mbele kwa ajili ya wokovu wa ulimwengu. Kristo alipokuwa hapa duniani, aliwatuma wanafunzi Wake kuutangaza ufalme wa Mungu katika uyahudi yote, na katika mfano huu alifunua waziwazi kuwa ni jukumu la watu Wake wakati wote kutoa kwa wengine elimu waliyonayo ya njia, ya uzima, na ya kweli. Katika kazi zake zote Yesu alitafuta kufundisha kanisa Lake kwa ajili ya kazi ya umishenari, na idadi yao ilipoongezeka, utume wao ungeenea, hadi hatimaye ujumbe wa injili ungezunguka ulimwengu kupitia huduma zao.*

*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*
🙏🙏🙏🙏

Address

Mkolani
Mwanza
MKOLANI

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mkolani SDA central church posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Mkolani SDA central church:

Share