Kingdom Bible School of Evangelism KBSOE

Kingdom Bible School of Evangelism KBSOE Training and supporting evangelists, missionaries and church leaders.

Heri ya mwaka mpya 2026
03/01/2026

Heri ya mwaka mpya 2026

12/12/2024
23/02/2024

Karibu katika masomo ya uinjilisti.
Tuma Jina, namba yako ya simu na mahali ulipo kwenda 0788008855

Join our classes today. We offer courses in Swahili and English through our satelite Bible School centres found in local...
31/01/2024

Join our classes today. We offer courses in Swahili and English through our satelite Bible School centres found in local churches. Please leave your WhatsApp Number in a comment if you wish to join training.

Many Christians from different countries in Asia and Africa are benefitting from School of Evangelism trainings. Tanzani...
30/01/2024

Many Christians from different countries in Asia and Africa are benefitting from School of Evangelism trainings. Tanzania is inclusive.

MUNGU AMEAHIDI KWAMBA ATASIKIA NA KUTUJIBU MAOMBI YETU. A. Mungu husikia na kujibu maombi yetu k**a tutakaa ndani yake n...
21/01/2024

MUNGU AMEAHIDI KWAMBA ATASIKIA NA KUTUJIBU MAOMBI YETU.

A. Mungu husikia na kujibu maombi yetu k**a tutakaa ndani yake na maneno yake kukaa ndani yetu – Yh. 15:7.

B. Mungu ametuahidi kutuonyesha mambo makubwa na magumu k**a tutamwita – Yer. 33:3.

C. Mungu huyaheshimu maombi yetu tunapomwomba kwa jina la Yesu – Yh. :14:14.

D. Mungu ameahidi kumponya na kumwokoa kila atakayeliitia jina lake – Yoe. 2:32, Mdo. 2:21.

E. Mungu hujibu maombi ya mwenye haki akiomba kwa bidii – Zab. 24:3-4, 1 Yh. 3:22, Yak. 5:16.

SOMO: KANISA NI MWILI WA KRISTO NA KRISTO NI KICHWA CHAKE UTANGULIZIYesu ana mwili mmoja tu, na haugawanyiki. Yesu ni ki...
29/12/2023

SOMO: KANISA NI MWILI WA KRISTO NA KRISTO NI KICHWA CHAKE

UTANGULIZI
Yesu ana mwili mmoja tu, na haugawanyiki. Yesu ni kichwa cha huo mwili, na ametoa nguvu kubwa na urithi wenye utukufu kwao walio ndani ya mwili wake.
Tunahitaji kuelewa ni nani walio viungo vya huu mwili mmoja, ndipo kwamba tutaweza kuwa na ushirika mkamilifu na nguvu za Yesu Kristo katika maisha yetu.
Kiungo cha mwili huwa hai na chenye nguvu tu pale kinapokuwa kimeungana na viungo vingine (mwili); hii ina maana kwamba, tutakuwa hai na wenye nguvu za Yesu ikiwa tutadumu katika ushirika na wengine walio katika Kristo. Hii ni sawa na tawi linapokuwa hai na kuzaa matunda kwa sababu limeshik**ana na shina. Hupaswi kujitenga na ushirika wa kanisa lako, wala umoja wa kanisa, wala kukiacha kichwa, yaani Kristo, ambaye ni mzizi na shina lako pia – Yh. 15:1-8.

I. KWELI YA MAANDIKO
A. Waefeso 1:18 – Mungu ametoa urithi wa utukufu wake kwa watakatifu.
B. Waefeso 1:19-20 – Ametoa nguvu za uweza wake zisizo za kawaida kwetu tuaminio.
C. .Waefeso 1:21 – Yesu Kristo ni kichwa kwa kila kitu kwa ajili ya Kanisa
D. Waefeso 1:23 – Kanisa ni mwili wa Yesu Kristo.

II. MAFUNDISHO

A. Mungu ametoa urithi wa utajiri wa utukufu wake kwa watakatifu.
1. Mungu ametuita kupitia tumaini la ufufuo wa wafu – Efe. 1:18, 1 Kor. 15:1-4.
2. Mungu ametupatia urithi na nguvu zilizo katika Yesu aliyefufuka – Efe. 1:18, Yud. 1:1.

B. Mungu hudhihirisha uweza na Nguvu zake kwa njia ya imani.
1. Zipo kwa ajili yao waaminio – Efe. 1:19, Mdo. 26:18.
2. Zilidhihirishwa kwetu katika ufufuo wa Yesu Kristo – Efe. 1:20, Flp. 3:8-11.
3. Zinapatikana kwa wote walio waaminifu kwa Yesu – Efe. 1:20 na 23.

C. Mungu alimfanya Yesu kuwa kichwa cha kanisa.
1. K**a kichwa, Yesu ameketi mkono wa kuume katika kiti cha Mungu Baba – Efe. 1:20, 1 Pet. 3:22).
2. K**a kichwa, Yesu amepewa mamlaka yote mbinguni na duniani – Efe. 1:21, Mt. 28:18, Yh. 1:1-3.
3. Yesu ni kichwa chetu na anatawala vitu vyote kwa ajili yetu – Efe. 1:22, Kol. 1:16-20.

D. Mungu amemfanya Yesu kuwa mwili (Kanisa ni mwili wa Yesu Kristo) – Efe. 1:23, 1 Kor. 12:13.
1. Yesu katika uhai wake duniani alikuwa na mwili na Roho ndani yake – Mt. 4:1
2. Alipokwenda mbinguni alimtuma Roho wake kuja kukaa ndani ya miili yetu – Mdo. 2
3. Roho wa Yesu anakaa ndani yetu ili tufanyike mwili wa Yesu – 1 Kor. 3:16-17
4. Tumefanyika mwili wa Kristo duniani – Efe. 5:23-27

III. MATUMIZI

A. Mungu anataka Kanisa tumpe utukufu – Efe. 3:10.
1. Urithi wetu na tumaini letu la milele linapatikana katika Kanisa – Efe. 1:18).
2. Tafuta kuwa sehemu ya Kanisa ili ufanyike kiungo katika mwili wa Kristo – Flp. 3:8-11.

B. Kanisa ni familia ya Mungu iliyoitwa kutoka ulimwengu uliopotea kwa njia ya Injili – Rm. 1:16, 1 Kor. 1:21, Yh. 20:31.
1. Mungu huzidisha watu katika Kanisa pale wanapoonyesha imani Kwake – Mdo. 2:47, 1 Kor. 12:13.
2. Wote walioitii Injili ni viungo vya mwili, yaani ni sehemu ya Kanisa – Mdo. 5:32.

C. Tunza muunganiko wako kwenye Kanisa (mwili).
1. K**a unataka kuendelea kuwa hai katika Yesu Kristo – Rm. 6:17-18
2. K**a unataka kumzalia Mungu matunda – Yh. 15:1-14.

D. Kamwe usishirikiane wala kuungwa na walimu wa uongo au manabii wa uongo.
1. Ambao wanakataa kumkiri Yesu k**a Bwana na Mwokozi wao – Yh. 5:39-40.
2. Ambao wanaukataa ujumbe wetu wa Injili ya wokovu na nguvu zake zinazopatikana kwa njia ya imani katika msalaba, yaani kifo, kuzikwa na kufufuka kwa Yesu Kristo - 2 Yh. 1:6-11);
3. Ambao wanazikana nguvu za jina la Yesu na kutumia nguvu na miujiza ya uongo – Mdo. 4:12
4. Ambao wanajitukuza wenyewe kwa wenyewe na utukufu wa Mungu hawautafuti – Yh. 5:41-44

E. Si kila kitu kiingizwacho na wanadamu katika Mwili wa Kristo kwamba mwamini atakikubali - taz. Rm. 13-15.

IV. AYA YA KUKARIRI: Waefeso 1:22-23

Ujumbe wowote wa Injili lazima ujenge msingi wake kwenye upendo wa Mungu, msalaba na Yesu aliyefufuka.Jesus was crucifie...
15/08/2023

Ujumbe wowote wa Injili lazima ujenge msingi wake kwenye upendo wa Mungu, msalaba na Yesu aliyefufuka.
Jesus was crucified to crucify satan and sin on our place so that whoever hears His message of the Cross and believes must be saved.

Address

Nyakato
Mwanza

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00

Telephone

+255788008855

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kingdom Bible School of Evangelism KBSOE posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Kingdom Bible School of Evangelism KBSOE:

Share