Baptist Church_Bonde la Uzima

Baptist Church_Bonde la Uzima SIRI YA BWANA IKO KWAO WAMCHAO

Karibu katika Mkutano mkubwa wa injili  mkoani Kagera. Nguvu ya Mungu itaonekana kwa watu wote kwa kufunguliwa vifungo n...
06/09/2023

Karibu katika Mkutano mkubwa wa injili mkoani Kagera. Nguvu ya Mungu itaonekana kwa watu wote kwa kufunguliwa vifungo na magonjwa bila kusahau kuwaleta watu kwa yesu ili wapate wokovu.

Mchungaji Amos Mandilindi atahudumu mkutano huu ambao utakuwa ni wa siku tatu. Pia kwaya ya kanisa la Baptist kayenze itakuwa ikihudumu kwa njia ya nyimbo ikishirikiana na kwaya zingine nyingi zinazopatikana mkoa wa Kagera

Watu wote tunawakaribisha sana

Baptist Kayenze Choir (KBC) wakihudumu Kwenye ibaada moja ya jumapili na aliyeko mkono wa kulia ni mchungaji kiongozi wa...
02/09/2022

Baptist Kayenze Choir (KBC) wakihudumu Kwenye ibaada moja ya jumapili na aliyeko mkono wa kulia ni mchungaji kiongozi wa kanisa, Pastor Amos Mandilindi

27/08/2022
Mkutano mkubwa wa Vijana
23/08/2022

Mkutano mkubwa wa Vijana

Karibu kanisa la Baptist Kayenze
12/08/2022

Karibu kanisa la Baptist Kayenze

DOKEZO WAPENDWA. HAKUNA KUAKILISHANA KWENDA MBINGUNI AU JEHANAMU: 1KOR 15:29 Au je, Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu wa...
02/05/2022

DOKEZO WAPENDWA. HAKUNA KUAKILISHANA KWENDA MBINGUNI AU JEHANAMU: 1KOR 15:29 Au je, Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu watafanyaje? K**a wafu hawafufuliwi kamwe, kwa nini kubatizwa kwa ajili yao? Mstari huu mtume Paulo alikuwa anasahihisha mafundisho potofu ya viongozi wa dini za Kiyahudi.Zilizowafundisha waumini wao kuwa mtu aliye hai anaweza kutenda jambo jema la Kiimani Likamsaidia mtu aliyekufa Dhambini yaani bila kumwamini Yesu, mfano kubatizwa badala yake, kutoa sadaka, kufunga na kumwombea, nk. Waambieni hakuna biashara k**a hiyo kuna wengine ukimhubiria anakwambia Mch si Family yangu inakuja kusali Wananiwakilisha we weeee! Ongeza na hii EZEKIELI 32:24 Elamu yuko huko, na watu wake wote jamii, pande zote za kaburi lake, wote pia wameuawa, wameanguka kwa upanga, walioshuka Hali hawana tohara (Hawakumwamini Yesu) ......nao wamechukua aibu yao, pamoja nao washukao shimoni. CHUKUA TAHADHARI MAPEMA TENA NI LEO

Shalom watu wa MUNGU ......Leo tuzungumzie vita vya kiroho ni vyema kwanza sisi tuliye mwamini YESU KRISTO tuwe na maari...
01/05/2022

Shalom watu wa MUNGU ......
Leo tuzungumzie vita vya kiroho ni vyema kwanza sisi tuliye mwamini YESU KRISTO tuwe na maarifa ya kutosha juu ya KRSTO YESU maana YEYE ndiye kiongozi wetu katika mapambano yote ya kiroho hususani vita vya rohoni ametuachia ROHO MTAKATIFU katika kutusaidia katika mapambano hayo ya kiroho na ndiyo maana paulo mtume amethibitisha hili kwa kusema na watakatifu walioko efeso kwa kuwaeleza kabla ya kupambana vita vya kiroho ni vyema kumfahamu MUNGU kwanza kwa kuwa na maarifa ya kutosha juu yake Waefeso 6:10 na baada ya hapo mshirikishe katika vita uliyonavyo naye atakuonesha namna ya kupigana hiyo vita na siyo kwenda kupigana wewe k**a wewe ni rahisi sana kuangushwa maana unatumia akili zako.Ni vyema umpe MUNGU nafasi ya katika mapambano hayo.Na ndiyo maana mtume Paulo amesisitiza kwanza katika kumfahamu MUNGU kwanza na ndipo mapambano yanafuata waefeso 6:10, 11-15.

DOKEZO. JIFUNZE KUMSIKILIZA KILA MTU HATA K**A UNAMZIDI, UMRI, ELIMU, MALI, CHEO, NK. waziri mmoja wa maliasiri alitembe...
01/05/2022

DOKEZO. JIFUNZE KUMSIKILIZA KILA MTU HATA K**A UNAMZIDI, UMRI, ELIMU, MALI, CHEO, NK. waziri mmoja wa maliasiri alitembelea mradi wa Nyuki, getini mlinzi akamwambia kipindi hiki haturuhusu mtu yeyote kuingia ndani. Waziri kwa hasira akaona amedharirishwa akamwambia mlinzi kwani wewe hunijui mimi nani eti? Akatoa vitambulisho, mlinzi akaogopa kufukuzwa kazi akafungua geti haraka waziri akaingia.Baada ya robo saa hivi mlinzi akasikia humo ndani mwano na kilio waziri anamwita mrinzi njoo unisaidie nyuki wamenivamia, MLINZI AKAMWAMBIA MHESHIMIWA WAONYESHE KITAMBULISHO YAWEZEKANA NYUKI HAWAKUJUI ETI. baada ya saa moja ndipo mlinzi akaingia akamkuta waziri amezimia akamkimbiza hospital. USIKU MWEMAA WATAKATIFU WA MUNGU

Yeremia 17:1-2 DHAMBI YA YUDA IMEANDIKWA KWA KALAMU YA CHUMA, NA KWA NCHA YA ALMASI, IMECHORWA KATIKA KIBAO CHA MOYO WAO...
26/04/2022

Yeremia 17:1-2 DHAMBI YA YUDA IMEANDIKWA KWA KALAMU YA CHUMA, NA KWA NCHA YA ALMASI, IMECHORWA KATIKA KIBAO CHA MOYO WAO, NA KATIKA PEMBE ZA MADHABAHU ZENU. Wapendwa mstari huu usihusishwe kabisa na Yuda msaliti wa Yesu ni vitu viwili tofauti Kabisaa. Wanaoongelewa hapa ni k**a taifa ambao ibada ya mungu baali ilikuwa sehemu ya maisha yao toka moyoni mwao nakumwacha Mungu wa Kweli. Hata watoto walipokuwa wakizaliwa tu walifundishwa baali ndio mungu wao na aliwatoa hadi utumwani. Jambo hili liliumiza Sana moyo wa Mungu wa kweli, Mungu aliona dawa ya kuiondoa hii Ibada ya baali kwenye mioyo yao iliyoonekana k**a imeandikwa kwa kalamu ya chuma dawa ni kuwaondoa kwenye nchi yake takatifu na kupelekwa uhamishoni Babeli. Nini cha kujifunza Tunachokifanya mbele ya watoto wetu au wadogo zetu au kuwaambia, kuwaelekeza kinajengeka mioyoni mwao Mungu huchukizwa Tuweni makini Mungu asitutupe mbali nae utumwani

24/04/2022

Mwanzo 2:18 FAIDA YA KUJIKOSOA. mara ya kwanza Mungu anajikosoa katika kazi yake ya Uumbaji nimeshangaa Sana. Mwanzoni kila alichokiumba alipokiangalia alijisifia nakusema ni chema, Ndipo baadae ameniambia kuwa (1)Adamu kupata mke mzuri Hawa ni baada ya Mungu kujikosoa, ndio maana mimi nawe Leo tupo duniani. Wengi tumeshindwa kuendelea kufanikiwa sababu hatuko tayari kujikosoa ktk maamuzi ya Kwanza, Ndoa nyingi zimevunjika sababu mume au mke kukataa kujikosoa kuwa ila hiki nilichokifanya kwa mwanzangu sio Vema. Mwana mpotevu alipopigika alijikosoa akasema sikufanya jambo zuri mbele za Mungu na kwa baba yangu akarudi kusawazisha, mpendwa ebu usiku huu mruhusu Roho mtakatifu apite moyoni ruhusu Kujikosoa

Pastor Mandilindi

Ibaada ya kesho jumapili
16/04/2022

Ibaada ya kesho jumapili

Kanisa la Baptist Kayenze linawatakia  heri ya siku ya Ijumaa kuu
15/04/2022

Kanisa la Baptist Kayenze linawatakia heri ya siku ya Ijumaa kuu

Address

KAYENZE
Mwanza

Telephone

+255765984288

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Baptist Church_Bonde la Uzima posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share