19/07/2022
NENO LA HEKIMA
LEO, tunapenda kuongea TENA na WAAJIRIWA. Iwe ni serikalini, kwenye sekta binafsi nk. K**a ulipitwa na post yetu ya kwanza kuhusu waajiriwa pitia post za nyuma ina kichwa WAAJIRIWA.
UNAJUA, shida kubwa ya waajiriwa ni kwamba wengi bado hamjajua kwamba hapo mlipo mnamtumikia Mungu na mmesimama k**a mawakili wake. Wengi sana wanatilia maanani mwisho wa mwezi tu. Lakini tunakwambia kabisa, ukibadili mtazamo na kujua kwamba hapo ulipo wewe ni mwakilishi wa Mungu, kuna mambo mengi sana mazuri yatatokea kwenye maisha yako na kuna mambo mengi sana mabaya utaepuka.
Tito 2: 9 - 10
Watumwa na wawatii bwana zao, wakiwapendeza katika mambo yote; wasiwe wenye kujibu, wasiwe WAIBAJI; bali wauonyeshe UAMINIFU mwema wote, ili wayapambe mafundisho ya Mwokozi wetu Mungu katika mambo yote.
NINYI waajiriwa wengi wenu sio WAAMINIFU na hamna uchungu kabisa na MALI za ofisi. Mnazitumia tu vile mpendavyo na wala hakiwaumizi. Kuna watu mnabeba tu vifaa mbalimbali kutoka maofisini yani k**a vile ni vyenu. Bahasha, kalamu, office pins, karatasi wengine mpaka stapler na punch machines, huo ni wizi.
Wengine mna-print mambo yenu binafsi kutumia printer za ofisi, wino wa ofisi, karatasi za ofisi bila huruma. Mambo yenu binafsi sijui network marketing report, wengine application letters na CVs za kwenda kuapply kazi sehemu nyingine mnaprint hapo hapo. Wengine upuuzi puuzi tu. Hivi wewe umeajiriwa na mshahara unalipwa, kwanini usiwe mwaminifu tu nenda stationery print lipa.
Wengine wana misuse tu, unaweza kuhitaji page moja tu ya kwanza, lakini unaprint page zote 7, halafu zile 6 zote zinaishia kwenye dustbin. Au document moja una print mara 3, kwanini usiwe mwangalifu? Jamani hata k**a ofisi sio yako hivi husikii uchungu hata kidogo wewe mwakilishi wa Mungu? Unamwakilishaje Mungu kwa wizi na kukosa uaminifu?
Wengine mnabeba mpaka toilet papers. Yani wewe unabeba chochote kinachobebeka. Wengine mnafanya kazi store yani ninyi ndio wakati wote mnaangalia namna ya kuiba vitu.