KMT Vision 2034

KMT Vision 2034 Kanisa la Mennonite Tanzania (KMT) with a 15 years (2018-2033) goal to win 1,000,000 NEW SOULS to Christ, through Business for Mission.

22/02/2019

Mennonite Theological College of Eastern Africa and Kanisa la Mennonite Tanzania (Country Office) are looking for an Information Technology Specialist. Duties of an information technology specialist can include network management, software development and database administration. IT specialists may also provide technical support to employees of the Mennonite Theological College and Country Office of the Mennonite Church both located in Bukiroba, Nyabange township of Butiama District in Tanzania and train non-technical workers on the computer application and information systems. He/She may design systems and assess the effectiveness of technology resources already in use or new systems that are being implemented. Additionally, he/she will determine the practicality of changes and modification of systems. Interested Christian young men and women can apply to The General Secretary, KMT Box 1040 Musoma, Tanzania through [email protected]. International Volunteers are highly encouraged to apply.

Boanza la watoto chini ya miaka 15 waliokutana katika kusakata soka na kupokea mafundisho ya ujana kabla ya kurudi mashu...
06/01/2019

Boanza la watoto chini ya miaka 15 waliokutana katika kusakata soka na kupokea mafundisho ya ujana kabla ya kurudi mashuleni baada ya likizo yao kuisha. Tulitumia nafasi hii kuwafundsha Amani na Haki, Nidhamu, Heshima na Bidii ya Masomo ili kuwawezesha kufiki malengo yao

BACK TO SCHOOL BONANZA - NYANTIRA DAR ES SALAAM JANUARY 5, 2019
06/01/2019

BACK TO SCHOOL BONANZA - NYANTIRA DAR ES SALAAM JANUARY 5, 2019

01/01/2019

MKESHA WA MWAKA MPYA; KMT Dayosisi ya Mashariki, Sinza, Dar es Salaam:
Usiku wa jana tumekesha kwa nyimbo za kusifu na kuabudu tukiongozwa na kwaya za KMT Upanga, Sinza, Tegeta, Nyantira na Praise Team.
Askofu Nelson Kisare Mwenyekiti wa Dayosisi ya Mashariki akitoa NENO la ufunguzi aliwaasa Kanisa la Mennonite kuwapa vijana uhuru wa kumwabudu Mungu bila kuigeuza Biblia na maagizo ya Maandiko Matakatifu, maana dunia inabadilika lakini Biblia haibadiliki. Aliwaasa vijana kuepuka kuibeba dunia na mambo yake na kuyaleta Kanisani bali walibebe Kanisa na kulipeleka duniani. Imani ya Kikristo igeuze utamaduni, mila na desturi za dunia na si kinyume chake.
Mchungaji Juma Aguttu (Katibu wa Afya Hospitali ya Shirati) alinena ujumbe wa mkesha kupitia Yoshua 4:1-8 uliobeba MAWE 12 ambayo ni Kanuni 12 za kutembelea mwaka 2019 ili kufikia malengo ya kila mmoja na Kanisa na hata Taifa. 1. Mungu ni Mwanzo wa kila kitu. 2.Kutenda HAKI 3. Kuutegemea Ufalme uliokamilika wa UTATU MT. 4. Beba Silaha za vita 5. Ng'ang'ania usikate tamaa 6. Tambua roho ya uharibifu uikabili 7. Ufalme utatekwa na wenye BIDII 8. Mwanzo mpya 2019. 9. Shukuruni kwa kila jambo 10. Baraka hutoka kwa BWANA 11. Beba MAONO yako 12. Kulea watoto wairithi kazi ya Bwana.
Kanisa lilitoa sadaka ya kwanza (MALIMBUKO) ya mwaka 2019 kisha Kanisa tuliomba maombi ya Shukrani ya 2018, Kuweka wakfu mwaka 2019, Kuombea Umoja wa Kanisa, Uamusho na Kumpokea Roho Mtakatifu, pamoja na maombi ya Kuutafuta Ufalme wa Mungu ili tufunguliwe mipenyo ya mafanikio 2019.
Mchungaji Magasi Mkuu wa Jimbo la KMT Sinza, aliwashukuru wote waliojitoa kuuandaa mkesha huu wa aina yake uliokutanisha waumini wengi wa Dar es Salaam.
Katibu Mkuu KMT Baraza, Mch John Wambura katika kufunga Mkesha huu aliwakumbusha Vijana wa KMT kuwarudisha vijana wenzao waliohamia makanisa mengine na huduma za watu binafsi kuwa warudi maana huku kwetu nako kumenoga sasa. Alikumbusha Kanisa juu ya Dira yetu "Vision 2034" na kuwataka Vijana kuweka alama kwa kushiriki utekelezaji wake. Aliwahimiza vijana wa Mashariki kumsaidia Askofu kwenda Ruvuma mkoa wa Kuenea unaoratibiwa na dayosisi hii. Aliwakumbusha Kanisa kuwa Mwezi May 2019 tutaadhimisha WEEK YA KMT mkoani dodoma Dayosisi ya Kati, hivyo aliwataka waumini kujiandaa kushiriki. Pamoja na hayo alikumbusha Kanisa kuwa Mwaka 2021 kutakuwa na Mkutano wa Wamennonite Duniani (MWC) utakaofanyika Indonesia. Aliwaomba kanisa kujipanga kushiriki na hasa msisitizo ni kwa uwakilishi wa Team ya Praise & Worship ya KMT ipate kushiriki.
Mwisho Askofu Kisare Alitangaza kuwa kuanzia sasa Mkesha huu utakuwa ni sehemu ya matukio katika kalenda ya Dayosisi ya Mashariki na utazunguka majimbo yote. HONGERA KMT SINZA IMEWEZEKANA KWA MARA YA PILI KUWA NA MKESHA MKUBWA WENYE MGUSO WA AINA YAKE.

Address

Nyabange
Musoma
255

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when KMT Vision 2034 posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share