Efatha Church Mara

Efatha Church Mara Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Efatha Church Mara, Religious organisation, bweri stand, Musoma.

03/08/2026

NGUVU INA MIPAKA LAKINI SI IMANI

Apostle & Prophet Josephat Elias Mwingira

Unataka kuona matokeo?
endelea kumwamini Mungu ushindi wako upo karibu.

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 2/08/2026KANISA LA EFATHA MAKUTANO (ZONE YA KYESWA)MCHUNGAJI CHRISTOPHERSOMO: IMANIWaebrania 11...
03/08/2026

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 2/08/2026
KANISA LA EFATHA MAKUTANO (ZONE YA KYESWA)

MCHUNGAJI CHRISTOPHER

SOMO: IMANI

Waebrania 11:1
"Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana."

Imani nini?
Imani chanzo chake ni kusikia. Imani uliyoibeba leo katika Wokovu ni ya muhimu sana kuzidi vitu vingine vyoote, imani uliyonayo leo ni chanzo cha wengine kuokolewa kupitia wewe.

Kwa imani, kupitia Yesu sisi tumeokolewa tumekombolewa na kuwekwa mbali na uovu na laana za huko tulikozaliwa kimwili.

Wakolosai 1:13-14
"Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;
ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;"

Unapookolewa kutoka nguvu za yule adui, na kuingizwa katika Pendo lake, dhambi ya aina yoyote ile inawekwa mbali nawewe.

Madhara ya Dhambi.

-Dhambi inamweka mtu gerezani ambako hajui nilini atakuwa nje ya gereza. Adui anapopata nafasi ndani ya mtu humbebesha mzigo ambao kwa akili ya kawaida ni ngumu na huwezi kujikoa.

Lakini unapobeba maamuzi ya kukimbilia kwa Yesu, anakutua mzigo na kukuweka mbali na dhambi, na laana ambazo si sehemu ya Wokovu wako.

Dhambi inapokaa kwa mtu inamfanya awe mnyonge, dhaifu na kukosa ujasili na nguvu ya kufanya mambo kwa amani. Unapohamia kwa Yesu, anakukomboa na kukuweka mbali na mateso ambayo awali ulikuwa huwezi.

Tambua hapo ulipo umesamehewa na kuwekwa huru, tangu sikuile Yesu alivyopanda pale Msalabani/Goligota dhambi zako ziliondolewa na kuwekwa Huru.

27/07/2026
Zaburi 86:7-8"Ee BWANA, uyasikie maombi yangu; Uisikilize sauti ya dua zangu. Siku ya mateso yangu nitakuita, Kwa maana ...
26/07/2026

Zaburi 86:7-8
"Ee BWANA, uyasikie maombi yangu;
Uisikilize sauti ya dua zangu. Siku ya mateso yangu nitakuita,
Kwa maana utaniitikia."

Pichani: Ni Ubarikio wa watoto wa Efatha, Wakiwekwa wakfu na Mtume Michael Meela, Pamoja ma  Mtume Vick Temu.Katika ibad...
26/07/2026

Pichani: Ni Ubarikio wa watoto wa Efatha, Wakiwekwa wakfu na Mtume Michael Meela, Pamoja ma Mtume Vick Temu.
Katika ibada ya leo, Julai 26, 2026. Katika Kanisa la Efatha Bweri (Musoma)

26/07/2026

Anaitwa Askofu Advela, Anapenda kumshukuru Mungu, kwa Ukuu wake na matendo yake Makuu aliyomtendea kwa namna ya tofauti kabisa tangu alipookoka 2017 katika Utumishi wake ndani ya Efatha...

26/07/2026

Anaitwa Bernadetha Francis, anapenda Kumshukuru Mungu kwa matendo makuu Mungu wa Efatha aliyomtendea katika Utumishi wake.

13/05/2026

IBADA YA KUSHUGULIKIA MISINGI YA KUZALIWA

SIKU YA PILI YA KUFUNGA NA KUOMBAKatika siku hii ya pili, chagua njia ya haki, jitenge na yale yasiyompendeza Mungu na u...
02/05/2026

SIKU YA PILI YA KUFUNGA NA KUOMBA

Katika siku hii ya pili, chagua njia ya haki, jitenge na yale yasiyompendeza Mungu na utembee katika mapenzi yake. Kaa karibu na Neno lake, maana hapo ndipo nguvu yako ilipo.

Zaburi 1:1 “Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha."

NAIBARIKI JUMAMOSI YANGU BWANA ni Nuru yangu na Wokovu wangu, BWANA ni Ngome ya Uzima wangu, Nimhofu nani? Watenda mabay...
02/05/2026

NAIBARIKI JUMAMOSI YANGU

BWANA ni Nuru yangu na Wokovu wangu, BWANA ni Ngome ya Uzima wangu, Nimhofu nani? Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka.

Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa.

Haleluya, YESU ni Mzuri. Jumamosi yangu Imebarikiwa na

Address

Bweri Stand
Musoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Efatha Church Mara posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share