30/08/2026
4. Neno linaponya na kukomboa;
Zaburi 107:20 “Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao.”
Katika Neno kuna uponyaji na ukombozi, hivyo katika hali yoyote uliyonayo Neno linaweza kukutoa, k**a unaumwa Neno linaweza kukuponya, k**a umefungwa Neno ni ukombozi wako, kamwe hauwezi kufa katika mateso maana ukiwa na Neno linakukomboa na kukuponya. Kwa namna unavyokula Neno ndivyo unapata nguvu.
5. Neno ni uzima wako; Zaburi 16:11 “Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele.” Neno la Mungu linakuongoza katika uzima wako kamwe hautapotea.
6. Neno ni silaha yako; Waebrania 4:12 “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.”
Mtu anayelifahamu Neno anajua mambo mengi: Waefeso 6:13 “Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.” Neno la Mungu ni siraha kuu hapa duniani na hii ndiyo siraha ambayo ibilisi anaiogopa sana kuliko maombi unayoomba. Kwa sababu unapoomba unaiambia mbingu itende kwa ajili yako lakini unapotendea kazi neno wewe unakuwa ndiye mtendaji mkuu.
7. Neno ni maji ya uzima; linaondoa kiu, mashaka, hofu na hali ya kutokuamini; neno lipo ili kusababisha uwe mtendaji mkuu katika ufalme wa Mungu.
Ufunuo 22:17 “Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.” Neno k**a maji kazi yake ni kutoa mashaka yako, hofu, uovu wote na linakutakasa. Neno linapokuja kwako linakutakasa na kukufanya uwe mtakatifu.
8. Isaya 11:2 “Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana;” 10 “Na itakuwa katika siku hiyo, shina la Yese lisimamalo kuwa ishara kwa kabila za watu, yeye ndiye ambaye mataifa watamtafuta; na mahali pake pa kupumzikia patakuwa na utukufu.”
Kanuni hizi za Imani zilimfanya Musa aamuru watu kuzingatia amri hizi na Neno la Mungu; Kumbu kumbu 28:1-2 “Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako.”
Unapoelewa nadharia hii inakupeleka katika Imani, unapozingatia kusikia Neno ndivyo Mungu anakupandisha cheo na kukuinua atakutoa nafasi ya chini na kukupeleka nafasi ya juu.
©Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira