09/08/2026
KUNDI LA WANAWAKE LILILOONGOZANA KATIKA KABURI KWENDA KUMPAKA BWANA YESU MAFUTA:
Ni wakina nani hao? Luka 24:9-10 “Wakaondoka kaburini, wakarudi; wakawaarifu wale kumi na mmoja na wengine wote habari za mambo hayo yote. Nao ni Mariamu Magdalene, na Yoana, na Mariamu mamaye Yakobo, na wale wanawake wengine waliokuwa pamoja nao;”
Pale wanaume walipokuwa wamejawa hofu lakini hawa wanawake waliamka asubuhi na mapema wakaenda kumpaka Yesu mafuta, hawakuuliza wanaume wako wapi, bali waliamka na kwenda moja kwa moja kwa Bwana wao.
MWANAMKE WA EFATHA:
Wewe mwanamke wa Efatha onesha upendo wako kwa Kristo mwokozi wako;
Luka 23:28 “Yesu akawageukia, akasema, Enyi binti za Yerusalemu, msinililie mimi, bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu.” Nakuita wewe mwanamke wa Efatha, k**a biblia isemavyo kuwa wanawake ni jeshi kubwa, onesheni hivyo.
Wagalatia 6:7-8 “Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.”
Kile utakachoenda kufanya mbele za Baba yako wa mbinguni usifanye katika mwili bali katika roho maana katika mwili utavuna uharibifu lakini katika roho utavuna uzima wa milele kwako na wa kizazi chako.
© MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA