Efatha Church Kilimanjaro

Efatha Church Kilimanjaro Welcome to the OFFICIAL facebook account of EFATHA Church Kilimanjaro | Healing & Deliverance by the blood of JESUS.

.

  Hii  jioni
07/09/2026

Hii
jioni

06/09/2026

2,Kuonyesha pendo: (kumfanya Mungu kuwa wa kwanza)Mithali 8:17"17]Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bid...
06/09/2026

2,Kuonyesha pendo: (kumfanya Mungu kuwa wa kwanza)

Mithali 8:17"17]Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona."
i)Pendo limebeba uzima.:
K**a unafanya biashara
ii)endo limebeba maongezeko: kwa kadri unavyo mpenda Mungu Mungu atakuongeza pendo haikubali ubaki k**a ulivyo kuwa . Nikatika pendo tunaongezeka
iii)Pendo limebeba furaha: na furaha ni nguvu kwa ajili ya pendo unajikuta una furaha ni katika pendo Kuna furaha na Ile furaha inakupa kupita sehemu ambayo mtu mwingine hapiti. Furaha ni nguvu ya Mungu unayo mvusha mtu kwenye magumu
iv)Pendo limebeba nguvu ya kuondoa aibu:unapo mpenda Mungu aibu yako inaondoka.

3.Zingatie maisha ya ibada

Kwa kujua mambo manne(4)
i.Matakatifu ya Mungu
ii.Hayo ya Siku zote
iii.Yaliyo najisi
iv.Yaliyo safi

Mambo ya Walawi 10:10 [10]kisha, mpate kupambanua kati ya yaliyo matakatifu na hayo yaliyo ya siku zote, na kati ya yaliyo najisi na hayo yaliyo safi;

1.unapozingatia matakatifu ya Mungu, kwa kuwekeza akili yako, nguvu na moyo wako mbingu inakuana kuwa unajitambua.

Acha kisafi kiwe kisafi usikichanganye na kitu najisi,
unapozingatia hayo mbingu inakua wazi kwako na yale yaliyo kuwa hayawezekani yanawezekana yale yaliyo kuwa magumu yanakuwa mepesi.

Mtu wa ibada ni mtatua changamoto zinazo jitokeza.
Maisha ya mtu wa ibada ni maisha ya kutatua changamoto.

UKOMBOZI ni kwamtu anayezingatia ibada maana mbingu inamuona yeye k**a yeye. Ukombozi unapatikana kwa mtu aliye kubali na kutii.

Isaya 1:19"19]K**a mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; "

Unaweza kuhisi ile nguvu lakini hakuna unachoweza kufanya
unakuta una ngome ambayo inakunyima kuona ile nguvu ya Mungu ikifanya kazi ndani yako.

Kwa kadri unapokubali na kutii ndivyo unavyowezeshwa kuwa raia wa mbinguni na ukisha kuwa raia kamili wa mbinguni vile ya mbinguni vinakuwa vya kwako.
Baraka Lyimo
la Efatha Kilimanjaro

Ibada ya Jumapili Tarehe Sept 06_2026Kanisa la Efatha Kilimanjaro Sayuni-Moshi KDC Mhubiri:Mchungaji Baraka Lyimo Mada: ...
06/09/2026

Ibada ya Jumapili Tarehe Sept 06_2026
Kanisa la Efatha Kilimanjaro Sayuni-Moshi KDC
Mhubiri:Mchungaji Baraka Lyimo
Mada: Ukombozi

Ukombozi ni nini?
Ni mchakato wa kumtoa mtu sehemu moja kwenda sehemu nyingine. UKOMBOZI sio tukio la siku moja ni mchakato kwa kadri unavyo chukua hatua ndipo unapokombolewa.

Mtu ni wa mtu aliyeamua kutoka sehemu alipo.

ILI UPATE UKOMBOZI
1. Kujua kutaka kweli
Hakuna ukombozi bila kujua kweli ya neno la Mungu, yawezekana eneo lako la uchumi akili afya nllimek**atwa lakini unapojua ukweli unakombolewa.

Ili apate ukombozi lazima achague kujua kweli na kweli ni Neno la Mungu na kwa kadri unavyo msikiliza mtumishi wa Mungu na kutendea kazi ndipo unaijua kweli.
Kweli inaleta ufahamu kwa kadri unavyo fahamu vitu ndivyo unajua na hauwi mjinga tena.

Yohana8:32Yohana 8:32"[32]tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru."

Kanisani ni sehemu pekee ambayo Mungu ameruhusu hekima yake itolewe. Kanisa ni sehemu pekee ambapo kuna hekima ya Kristo inafunuliwa kwa walioridhiwa.
i)Kweli imebeba maajabu, yasiyo wezekana kwa wanadamu kwa Mungu yanawezekana
ii)Kweli imebeba nguvu:kwa kadri unavyo jua kweli inabeba nguvu inayovua vazi la ujinga la hasara nguvu ya Mungu ikija ikikaa moyoni inakusukumq kugeza maisha yako kuwa viwango vingine.na wakati watu wanakufatilia wanaanza kuona maajabu ya Mungu
iii)Kweli imebeba maumivu:Kuna maumivu kwenye kweli kweli kwasababu inasjuhulika na wewe sio watu Kuna wakati utasikia maumivu kwasababu Ina shughulika na wewe.unapo kibali kweli Kuna baadhi ya tabia lazima zingolewe na mwili lazima upate maumivu lakini baada ya hapo utapata furaha na utaketi na wakuu.usipo yakubali

iv)Kweli inakaa moyo na akili
Unapo ipokea iruhusu ikae moyoni na akilini usiiache ikae masikioni iruhusu ingie kwenye akili ikafanye makazi moyoni ili ikusukume kufanya vitu vya viwango vya juu.

06/09/2026
Highlights Sunday Service Sept 06_2026
06/09/2026

Highlights Sunday Service Sept 06_2026

KINACHOSABABISHA MTU ASIKOMBOLEWE1. Dhambi, inazaa uovu na hapa kuna nguvu inayosababisha usifanye chochote. Kuna kitu k...
06/09/2026

KINACHOSABABISHA MTU ASIKOMBOLEWE

1. Dhambi, inazaa uovu na hapa kuna nguvu inayosababisha usifanye chochote. Kuna kitu kinachosababisha uwe k**a watu wa ukoo wako.

NAFASI 5 ambazo wakuu wa giza wanazitumia kwenye familia yako ili ushindwe kupata ukombozi.
i) Familia inakulazimisha kuishi kawa wao
ii) Ukoo " "
iii) Kabila " "
iv) Taifa, " "
v) Kimataifa, kuna nguvu ambayo inazuia jambo kufanyika.

UNAWEZAJE KUTUNZA VITU AMBAVYO MUNGU AMEKUPA

Unatunza kwa kusikia fundisho na kulikumbatia moyoni na akilini mwako litakustawisha.

Kumbukumbu la Torati 28:1"1]Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;"

1. Bidii, unapokua na bidii ya kusikia na kutunza inakupa wewe kuongezeka.

2. Kwa kufuata kile Mungu anasema
i.Hekima ya kutunza fedha na vitu.
ii.Unaipanda k**a mbegu ili izalishe
iv.Unatunza kwa kujali.

NAMNA YA KUSHUGHILIKA NA ZILE NAFASI 5 ZA FAMILIA YAKO

1. Ufahamu
2. Kuchukua hatua/ Kufanya
3. Kukubali na kutii Mungu anachosema.
4. Maombi, na hii ni kwa ajili ya kurahisisha kuelekea u ukombozi wako.

Baraka Lyimo
la Efatha Kilimanjaro

AKILI YA MTU IKIKOMBOLEWA1. Anaanza kuona vitu ambavyo wengine hawaoni, katikati ya umasikini, kushindwa na kadhalika.. ...
06/09/2026

AKILI YA MTU IKIKOMBOLEWA
1. Anaanza kuona vitu ambavyo wengine hawaoni, katikati ya umasikini, kushindwa na kadhalika.. akili itakufanya ushinde hayo yote.

2. Inasababisha changamko la kweli, anaishi maisha ya uhakika kwa maana kuna sababu fulani ya hekima inakuhakikishia una ubaadae mwema.

3. Inakupa kuishi katika nguvu ya Mungu, inakupa utajiri haijalishi uko katika mazingira gani na siku hadi siku unaendelea kubadilika.

4. Inabeba ubora ( Roho ya ubora) unaanza kuwa mtu unayevutia fedha, vitu mbalimbali maana vyote vinaenda kwa mtu mwenye akili iliyokombolewa. Hafanyi vitu visivyo na ubora, anaweka vitu katika mpangilio mzuri.

UKOMBOZI ENEO LA AFYA
Ili Mungu amtumie mtu lazima awe na afya njema. Lazima afya yako ikombolewe ihame kwenye magonjwa yanayotesa familia yako.
Maendeleo yoyote aliyonayo mtu ni matokeo ya afya njema.

UKOMBOZI ENEO LA UCHUMI
Unapokua umekombolewa katika uchumi utaweza kumtangaza Mungu. Lazima kanisa liwe huru kwenye eneo la uchumi.

Kuna watu kwenye familia zao wamewekewa mipaka ya kumiliki kiasi fulani cha fedha.
Kwanini tunatakiwa tuwe na fedha?

Mathayo 6:9"9]Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,"

1.Mimi nawewe tukiwa na fedha jina la Yesu linatukuzwa maana alivyo baba ndivyo alivyo mwana.

2. Ili kufanya mazingira ya huku duniani yawe k**a mbinguni. Lazima uwe na fedha ili uishi katika mazingira mazuri na inawezekana. Fedha ni mtumishi wako anatakiwa akutumikie.

3.Ili kurahisisha mambo.

UKOMBOZI WA MAZINGIRA
Mazingira yako lazima yakombolewe kwa sababu yanasababisha majibu. Lazima uyatiishe yakusikilize ukiita fedha inakuja. Mazingira yakiwa hayajakombolewa yatakua yanapingana na wewe.

Ikishakombolewa Akili, afya, uchumi na mazingira yako hakuna kitu kitakachotishia maisha yako.

Mhubiri: Mchungaji Baraka Lyimo
Mada : UKOMBOZI

MKESHA wa Ukombozi na Uponyaji Tarehe 04_09_2026.Kanisa la Efatha Kilimanjaro Sayuni Moshi-KDC Mhubiri: Mchungaji Baraka...
06/09/2026

MKESHA wa Ukombozi na Uponyaji Tarehe 04_09_2026.
Kanisa la Efatha Kilimanjaro Sayuni Moshi-KDC
Mhubiri: Mchungaji Baraka Lyimo
Mada : UKOMBOZI

Ukombozi ni mchakato wa kumtoa mtu kutoka mahali kwenda mahali, huo mchakato unapofanyika ndio Ukombozi.

Ukombozi sio jambo la mara Moja ni mchakato ambao unaendelea na mtu aliyeamua kutoka sehemu Moja kwenda nyingine.

Kuna watu wengine hawajaamua kupata ukombozi bado ndio maana wanaendelea kuteseka.

Ukombozi ni safari ya mtu kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Wakolosai 1:13"13]Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;"

Wokovu ni jambo la siku moja yaani kumpokea Yesu akae ndani ya moyo wako na hapo wewe unakua umempata Yesu, Lakini Ukombozi ni wewe umpate Yesu.

Ukombozi ni kutoka hapo ulipo na kwenda pale Yesu alipo.

Mtu yeyote anayetaka ukombozi ni lazima kupata kwanza ukombozi wa akili. K**a hutaruhusu akili yako kufahamu ukweli.

Eneo ambalo watu wengi wamek**atwa ni akili, na shetani akishak**ata akili yako anakumaliza. Akili ikishakombolewa inaruhusu mambo mengi ya faida kufanyika.

Address

Efatha Church Kilimanjaro
Moshi
1058

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Efatha Church Kilimanjaro posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share